Zawadi zaongeza mgogoro wa ndani miongoni mwa al-Shabaab, wachambuzi asema

Na Mahmoud Mohamed jijini Mogadishu

Juni 11, 2012

  • 5 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Makundi ya Somalia yalikaribisha vyema kujumuishwa kwa viongozi saba wa ngazi ya juu wa al-Shabaab wanaoshirikiana na al-Qaeda katika orodha ya wanaotakiwa sana na Marekani, ambao wanatoa mamilioni ya dola kwa taarifa zitakazosababisha kujua walipo chini ya Zawadi kwa Programu ya Sheria.

Marekani ilitangaza tarehe 7 Juni kwamba itatoa Dola za Kimarekani hadi milioni 33 kubadilishana na taarifa zinazohusiana na mahali walipo viongozi saba waandamizi wa al-Shabaab.

Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia (TFG) ilisema zawadi ya fedha taslimu ilikuwa hatua muhimu kuzuia fursa yoyote ya magaidi kutoroka vyombo vya sheria.

Kiasi kikubwa kilitolewa kwa mwazilishi wa kundi hilo, Ahmed Abdi aw-Mohamed, anayejulikana kama Ahmed Godane au Mukhtar Abu al-Zubair, na Idara ya Dola ya Marekani kutoa zawadi ya dola za Kimarekani milioni 7 kwa taarifa za mahali alipo.

TFG ilisema Godane anahusika na mauaji ya raia wasio na hatia nchini kote Somalia, ikwa ni pamoja na mfululizo wa mashambulio ya kigaidi ambayo yalifanywa na al-Shabaab nchi jirani”.

Dola za Kimarekani milioni 5 zaidi zilitolewa kwa wanachama wengine wa al-Shabaab: Ibrahim Haji Jama, Fuad Mohamed Khalaf, Bashir Mohamed Mahamoud na Mukhtar Robow.

Dola za Kimarekani hadi milioni 3 zilitolewa kwa Zakariya Ismail Ahmed Hersi na Abdullahi Yare.

Marekani iliorodhesha al-Shabaab kama asasi ya kigaidi mwaka 2008, lakini hii ni mara ya kwanza imejumuisha viongozi wa harakati hizo katika Mpango wake wa Zawadi kwa Sheria.

Viongozi wa Somalia walisema zawadi ya Marekani inaendana na zawadi ya serikali ya Somalia iliyotangazwa Aprili kwamba inatoa motisha ya fedha taslimu hadi dola 500 kwa raia ambao watatoa taarifa ambayo itasababisha kuuawa au kukamatwa kwa wanaoiendesha al-Shabaab.

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Somalia Mohamed Ali Atoosh alisema zawadi iliyotolewa na Marekani itasaidia mapambano dhidi ya al-Shabaab nchini Somalia.

"Serikali ya Somalia inakaribisha hatua mpya ya serikali ya Marekani, ambayo inaendana na zawadi zilizotolewa na serikali ya mpito,” Atoosh aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba al-Shabaab inaleta tishio la utulivu Somalia na mashariki mwa Afrika yote.

Washiriki wa serikali ya Somalia, wanamgambo wa Ahlu Sunna wal Jamaa (ASWJ) pia inakaribisha uamuzi wa zawadi.

"Zawadi hii ya Marekani ni hatua nzuri katika kupambana na al-Shabaab,” Sheikh Abdulqadir Soomow, msemaji wa Baraza Kuu la ASWJ, aliiambia Sabahi.

"Zawadi iliyowekwa kwa viongozi waandamizi wa al-Shabaab inaweza kuleta woga miongoni mwa viongozi wanaotafutwa na kuleta mgogoro wa kujiamini ndani ya vyeo vya mtandao huo,” alisema. “Hii inaweza kusababisha kusambaratika kwa uongozi wake, ambao hadi sasa, unatafutwa na watafikiria tu kujificha na kuzuia mtandao wao kujitokeza hadharani ili kuepuka kutambuliwa na raia.”

Soomow alisema viongozi wa al-Shabaab watakuwa na wasiwasi usiokuwa na kikomo -- hata kwa walinzi wao na washirika wengine wa harakati -- kwani huduma za kiintelijensia zinajaribu kupenyeza katika ngazi zao.

"Tunakusudia kuwalenga viongozi wa al-Shabaab kama hatua ya msingi kwa sababu kuwaua viongozi wao kutakuwa na madhara makubwa katika mshikamano wa kuendeleza zoezi hili," alisema.

Kuongeza shinikizo kwa al-Shabaab

Wachambuzi walisema zawadi iliyotolewa na serikali za Marekani na Somalia itaongeza shinikizo kwa al-Shabaab wakati ambapo ushindi muhimu dhidi ya zoezi hili umekamilika kupitia operesheni za kijeshi.

"Zawadi hii mpya inaweza kuongeza shinikizo kwa al-Shabaab, ambao wamekabiliwa na mashambulizi katika maficho yao kadhaa na Somalia ya Kusini," Ismail Abdullahi, mchambuzi wa masuala ya kisiasa anayeishi Mogadishu aliiambia Sabahi.

"Kuanzia sasa na kuendelea, viongozi wanaotafutwa wanatakiwa kutazama mabega yao na wote wanaowazunguka wakati wote. Watatakiwa kujificha mbali na macho ya watu na wale waliopo katika huduma za kiintelijensia," alisema. "Hata kama zoezi hili halitawezesha kuwakamata viongozi wa al-Shabaab siku zijazo, kuwaongezea shinikizo al-Shabaab ni jambo la msingi katika mkakati unaotaka kuangamiza zoezi hilo kama jeshi."

Abdullahi alisema baadhi ya ishara za udhaifu na migawanyo vimeibuka ndani ya al-Shabaab. Taarifa za wiki iliyopita zilionyesha kwamba viongozi wa al-Shabaab wanalikimbia jiji la Kismayo, ambayo ni ngome yao kuu ya mwisho.

Abdirahman Mahmoud, mchambuzi na mtafiti wa makundi yenye msimamo mkali, alisema zawadi inaweza ikasababisha washirika wa al-Shabaab kuwasaliti viongozi wao ili kupata fedha zilizotangazwa.

"Kumekuwa na hali ya tuhuma na migogoro ya kujiamini ambako kumeruhusu[mizunguko ya ndani] ya al-Shabaab na zawadi hii mpya, kwa maoni yangu ndiyo pekee itakayozidisha mogogoro huu wa ndani katika awamu ijayo," Mahmoud aliiambia Sabahi.

"Sitashangaa kuibuka kwa mawakala zaidi watakaotaka kufaidika na fursa hii au, angalau baadhi ya watendaji wa al-Shabaab----hususani viongozi wa ngazi ya chini--- watatekeleza na kutoa taarifa za viongozi wanaotafutwa ili kupata zawadi hiyo ya Dola za Kimarekani," alisema.

Mahmoud alisifia matumizi ya zawadi ya fedha katika kubadilishana na ukamataji wa viongozi muhimu wa al-Shabaab, akiita ni njia nzuri ya kuwahimiza wale wote wenye taarifa kujitokeza.

"Zawadi hii kubwa iliyotolewa na Marekani itawahimiza wale wenye taarifa kuhusiana na maficho ya viongozi wa al-Shabaab wanaotafutwa kujitokeza," alisema.

Al-Shabaab waidharau zawadi

Al-Shabaab wapuuza zawadi lililotolewa na Marekani na kuahidi kuwa wataendelea na mapigano.

“Makafiri ambao wanaelewa ni nani viongozi wazuri wa Kiislamu – na hiyo ndiyo sababu pesa zinatolewa ili wajulikane walipo,” taarifa iliyochapishwa katika tovuti yenye mafungamano na kikundi ilisema, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. “Wakati baadhi ya viongozi wa mujahidina tayari wameshauliwa na mipango kama hiyo, wengine wanaendelea na jihadi.”

Fuad Mohamed Khalaf, mmoja wa viongozi wa al-Shabaab ambaye kichwa chake kimewekewa dau la dola milioni 5, aliidhihaki zawadi ya marekani kwa kukamatwa kwake. “Ninakuhakikishia kuwa aina hii ya mambo karne hayatatuzuia tusiendelee na vita vitakatifu dhidi yao,” alisema katika kipindi cha redio kilichotangazwa tarehe 9 Juni.

“Tangu mwaka 2006, al-Shabaab imekuwa ikidai kuhusika na ulipuaji mabomu kadhaa ya kujitoa muhanga – ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya katikati na kaskazini ya Somalia na katika mji mkuu, Mogadishu,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema katika taarifa yake ya tarehe 7 Juni. “Kikundi kinawajibika kwa mauaji ya maelfu ya raia wa Somalia, wanaharakati wa Somalia, wafanyakazi wa kimataifa wa misaada, waandishi wa habari na walinda amani wa Umoja wa Afrika.”

Taarifa hiyo ilisema al-Shabaab pia walishambulia nchi jirani ya Uganda na kutishia kushambulia maslahi ya Marekani, Kenya na Burundi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 14)

Dislike_icon(5)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • mamoud ali
    June 20, 2012 @ 02:47:19PM

    Al-Shabaab wanadhoofika kila siku na kushindwa kwao dhahiri katika miezi ijayo, vikosi vinavyopigana na wapiganaji wanasonga ili kuikamata miji yao yote ya ngome na hivi karibuni tu askari wa AMISON waliuteka mji mmoja mkubwa wa ngome. Pia wamewaua viongozi mbalimbali na wapiganaji katika vita. Ngome pekee ya al-Shabaab ni Kismayu na askari wote wa AMISON wanazunguka kwenye ngome muhimu na mara tu watakapoiteka Kismayu kutoka kwa magaidi, al-Shabaab hawatakuwa na mahali pa kukimbilia au kujificha. Kikundi cha kigaidi kimezidiwa kwa kiwango cha juu mno kwa sababu askari ambao wanapigana na farasi ni zaidi ya askari 11,000.

  • mujaahid soomaaliyeed
    June 17, 2012 @ 09:18:13AM

    Ninawahofia nyinyi kwa kufanyakazi na wale wasio Waislamu na mnaeneza chuki waliyoipandikiza miongoni mwa ndugu zao lakini sisi tutawakamateni kwa kuhusika na hicho mnachofanya.

  • KAYSE JAAMAC XIRSI
    June 13, 2012 @ 04:52:25AM

    Ningependa kusema kwamba watu tulioonyeshwa wanapaswa kuadhibiwa namna hiyo.

  • Hussein Mumin
    June 12, 2012 @ 07:00:32AM

    Al-Shabaab ni dhamana wa kukataa misaada ya wafadhili isifike sehemu zilizoathiriwa zaidi na kupelekea vifo vya maelfu na mateso kwa watu wa Somalia. Al-Shabaab pia ni dhamana ya utekaji nyara meli katika Bahari ya Hindi.

  • somalilander
    June 12, 2012 @ 04:26:50AM

    Hii hailinganishwi na dini, haki za binadamu na utamaduni wa Wasomali. Kama Wasomali kutoka kusini mnawindwa kwa makosa mliofanya dhidi ya watu wenu ikiwa ni pamoja na viongozi wenu wa kisiasa na kidini kuanzia utawala uliolaaniwa wa Siyad Bare hadi sasa. Aliidhihaki dini ya Kiislamu na masula yote ya haki yaliyohusika nayo, na nyote mnajua kuwa aliua viongozi wa kidini waliokuwa wanaiongoza jamii katika njia sahihi mbele ya macho ya Wasomali na hakuna yeyote aliyelizungumza. Serikali yake pia iliwaangamiza watu wa kaskazini ya Somlaia bila ya sababu. Baada ya hapo nchi ilikamatwa na mabwana wa vita ambao pia waliuwa watu wengi bila ya sababu. Baada ya kutenda maovu yote haya kwa kupingana na dini, sasa mnatumia dini kwa maslahi binafsi na kutafsiri vibaya kitabu kitukufu. Mnawaua watu kwa kuwachinja kama wanyama, kuwapiga mawe mpaka kufa na wengine kuwalemaza kwa kuwakata mikono yao kwa jina la Sharia ya Kiislamu ambayo sio kweli lakini mmeitafsiri vibaya ili kukidhi maslahi yenu. Kwa niaba ya Somaliland ningependa kuwaomba kufanya yafuatayo: 1. Mtubu kwa Mungu kwa makosa mliyofanya. 2. Kuacha kukiuka haki za watu. 3. Fuatilieni utamaduni unaokubalika uliopotea na ikiwa mtapigana, basi piganeni kwa njia zinazokubaliwa kimataifa. Acheni kuwachinja kama wanyama watoto na wanawake wasio na hatia. Ningependa kuwaomba al-Shabaab kuacha kuua watu kwa jina la kupigana na wasiokuwa Waislamu na muende kupigana na wasiokuwa Waislamu huko waliko

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo