Magonjwa yatishia mazao ya mahindi nchini Kenya

Na Sargajan Bin Kadii, Nairobi

Juni 08, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Maradhi mabaya kabisa unatishia mashamba ya mahindi nchini Kenya na yanaweza kupelekea upungufu mkubwa wa chakula hicho kikuu, wameonya wataalamu wa kilimo na wakulima.

  • Mkulima akiyaanika kwa jua mavuno yake ya mahindi karibu na Narok mwaka 2011. Kiasi ya wakulima 300,000 wameathirika na maradhi ya mahindi ya lethal necrosis mwaka huu. [Tony Karumba/AFP]

    Mkulima akiyaanika kwa jua mavuno yake ya mahindi karibu na Narok mwaka 2011. Kiasi ya wakulima 300,000 wameathirika na maradhi ya mahindi ya lethal necrosis mwaka huu. [Tony Karumba/AFP]

Kwa mujibu wa wizara ya kilimo, maradhi hayo yanayofahamika kama maize lethal necrosis yaligunduliwa kwa mara ya kwanza na wakulima katika majimbo ya Nyanza na Bonde la Ufa. Maradhi hayo huenezwa kwa hewa na husababisha miti kudumaa, kukauka na kufa wakati ikitoa maua.

Wizara hiyo inakisia kwamba kiasi ya wakulima 300,000, ambao walizalisha magunia milioni 3.5 ya kilo 90 mwaka jana, wameathirika na maradhi haya mwaka huu.

“Kuna haja ya hatua za haraka kuchukuliwa ili kuzuia kutapakaa kwa maradhi haya katika maghala ya chakula ya taifa kama vile Kaskazini ya Bonde la Ufa,” alisema mwenyekiti mtendaji wa Jumuiya ya Wakulima wa Nafaka, David Nyameino. “Hilo likitokezea, nchi itakuwa kwenye hatari ya kuwa na upungufu wa mahindi kwa mwaka ujao. Kwa kuwa mahindi ndicho chakula kikuu kwa Wakenya wengi, hili litakuwa sawa na upungufu wa chakula katika kiwango cha taifa.”

Nyameino alisema serikali na mashirika ya binafsi ya utafiti lazima waingize fedha zao na kuchangia kwenye utafiti ili kuwalinda wakulima dhidi ya kupoteza zaidi na kuhakikisha usalama wa chakula nchini unabakia kama ulivyo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo na Idara ya Takwimu ya Taifa ya nchi hiyo, utumiaji wa mahindi nchini Kenya umepanda sana katika kipindi cha miaka kumi ijayo. Wakenya walikula magunia milioni 23 ya mahindi na walizalisha magunia milioni 26, hivyo wakawa na ziada. Lakini mwaka 2011, Wakenya walitumia magunia milioni 43 ya mahindi na kuzalisha magunia milioni 30 tu, hali inayoonesha kuwa uzalishaji haukwenda sambamba na mahitaji. Upungufu wa magunia milioni 13 umefidiwa na mahindi yanayoingizwa kutoka nje.

Mwezi Machi, Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, alionya kwamba Kenya itakuwa imesaza akiba yake ya mahindi kufikia mwezi Julai, sakisema kwamba nchi hiyo lazima iruhusu uingizaji wa chakula ili kukidhi mahitaji yake ya chakula. Wataalamu na wakulima wameitaka serikali kuwezesha utafiti zaidi wa zao hilo na mahitaji ya udongo, na pia matumizi ya kiwango bora cha bidhaa za kilimo kama vile mbolea na mbegu zinazohimili magonjwa.

"Hali ya sasa inahitaji kuchukuliwa kwa umuhimu mkubwa zaidi na serikali kuliko hivi tunavyoshuhudia hivi sasa, ambapo maafisa wa kilimo wanatembelea mashamba bila ya kutoa suluhisho muafaka,” alisema Poltas Nyanchama, mkulima wa mahindi kutoka Mradi wa Makazi ya Kineni huko Nyanza.

Nyanchama alisema upungufu wa mahindi umekuwa suala la usalama wa taifa. “Hali hii ya sasa tayari inasababisha wasiwasi kwenye soko, ambapo bei ya mfuko wa kilo mbili za unga wa mahindi inafikia hadi shilingi 120 (dola 1.42 za Kimarekani) kutoka shilingi 100 mwezi Januari,” aliiambia Sabahi.

Baada ya kuwekeza zaidi ya shilingi 200,000 (dola 2,370) katika shamba lake la mahindi la ekari 10, Nyanchama alisema pesa yake sasa itapotea kwa vile mazao hayo hayawezi kutumika kuwalisha wanyama kutokana na maradhi.

“Tumeshauriwa aidha kuizika au kuichoma shehena, kwa kuwa kumekuwa na taarifa ya kufa kwa ngombe baada ya kuzila,” alisema. “Hatujui shamba lipi la kwanza liliathirika, lakini mahindi kwenye mashamba ya kila mkulima kwenye eneo hili yameathiriwa vibaya sana -- majani yanageuka kuwa ya njano badala ya kijani kama inavyotakiwa na baadae mmea mzima ukafufa katika kipindi cha wiki chache.”

Kutatua tatizo hilo wakati huu ambao tunatafuta suluhu ya kudumu, Wizara ya Kilimo imewashauri wakulima kutumia mbegu ambazo zimewekwa dawa za kuzuia magonjwa na wadudu kuzishambulia na ambazo zimethibitishwa. Wametakiwa kuacha kupanda mazao kwenye maeneo yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara, pamoja na kupanda mazao wakati usiokuwa wakiangazi au ukame. Wakati huo mazao huwa katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa zaidi.

Uchunguzi wa awali uliofanywa na kituo cha Afya ya Mimea cha Kenya unaonyesha kuwa ugonjwa huo unaoshambulia mahindi ulianzia katika shamba moja lililoko Taveta kwenye mim wa Pwani mwaka 2011.

"Ingawa tumeshagundua magonjwa hayo, bado tunaufahamu mdogo wa namna ya kuutibu. Mpaka saa, tunafanya uchunguzi zaidi ihara zake ili tuweze kutafuta dawa," alisema Johnson Irungu, afisa wa Kurugenzi ya Udhibiti wa Mazao katika Wizara ya Kilimo. "Tumeunda tume ya pamoja na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Egerton na Kituo cha Kimataifa cha Uboreshaji wa Mahindi ambayo karibuni itapata ufumbuzi."

Irungu aliiambia Sabahi vielelezo vya mazao yaliyoathiriwa vilipelekwa Uingereza mwezi Mei kwa uchunguzi zaidi. Alisema asilimia 40 mpaka 40 ya mahindi yaliyopandwa katika maeneo ya mikoa ya Bonde la Ufa na Nyanza yameathiriwa na magonjwa.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Saddallah Ali
    June 9, 2012 @ 09:18:54PM

    Serikali ya Kenya inafanya kila inachoweza kuona inajitosheleza kwa chakula ifikapo mwaka 2030. Ili iweze kufikia hilo inahitaji kusaidia shughuli za kilimo na mkulima katika nchi. Kuna njia mbalimbali ambazo kilimo kinaweza kuongezeka nchini Kenya ili kuhakikisha ghala la chakula kimejaa. Njia ya kwanza, serikali inaweza kuwapatia wakulima mbegu za kisasa na mbolea wakati wa msimu wa kupanda unapokaribia. Serikali pia inaweza kuhakikisha bei za zana za kilimo ni rahisi kupatikana na kwa bei ya chini, kuhakikisha kuwa mbegu na mbolea zipo tayari wakati wowote. Serikali ya Kenya pia inawezakuja na mpango ambapo inaweza kununua mazao ya kilimo kutoka kwa wakulima kwa bei ya juu. Hii itawahamasisha wakulima kupanda zaidi na kuwa na hamu katika uzalishaji wa mazao ya kilimo. Kama serikali ya Kenya inaweza kufanya hayo hapo juu hivyo itaweza kuona ghala la chakula kimejaa ndani ya muda mfupi.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo