Juni 05, 2012
Vikosi vya Serikali ya Mpito ya Somalia (TFG) vikiungwa mkono na majeshi ya Kenya vimeanza operesheni kubwa ya kuelekea kwenye mji wa pwani wa Kismayo, mji mkuu wa mkoa wa Lower Juba ulio kusini mwa Somalia.
Kuuchukuwa mji huo wa bandari kutoka mikononi mwa al-Shabaab kutakata ufadhili kwa kundi hilo linalonasibishwa na al-Qaeda, ambalo linauchukulia mji wa Kismayo kama kitovu chake cha kifedha.
Wasafiri wanaoitumia barabara inayounganisha miji ya Afmadow na Kismayo waliiambia Sabahi kwamba majeshi ya Somalia na Kenya wameendelea kusonga mbele kuelekea mji mdogo wa Bulo Haji, magharibi ya Kismayo, huku vikosi vya TFG vikiripotiwa kuwa umbali wa kilomita 110 kutoka mji huo wa bandari.
“Magaidi wako kwenye kitanda chao cha mwisho cha mauti na dakika ya mwisho inakaribia,” alisema Mahmoud Dahir Farah, msemaji wa vikosi vya Somalia katika mkoa wa Lower Juba. “Tutapigana nao mpaka wasalimu amri au waihame nchi yetu.”
“Tunajitayarisha kwa mashambulizi na kuwazuia kuingia kwenye msitu wa kusini, ambao tangu mwaka 2007 wameutumia kama sehemu ya kujifichia na sasa baada ya kufukuzwa kwenye mji wa Mogadishu na sehem nyengine za nchi,” Farah aliiambia Sabahi. “Haiwezekani kwao kupata mahala pa kujificha na tutawashinda kwa sababu tuna rehema za Mwenyezi Mungu na uungwaji mkono kutoka kwenye miji na kwa wanavijiji.”
Habari zisizothibitishwa za vyombo vya habari zinasema kuwa viongozi wa al-Shabaab wanaanza kuuhama mji wa Kismayo wakati majeshi ya Somalia na washirika yakisonga mbele. Redio RBC ya Somalia iliripoti hapo Jumanne (tarehe 5 Juni) kwamba makamanda kadhaa wa al-Shabaab wameonekana wakiuhama mji huo.
Hivi karibuni al-Shabaab waliutelekeza mji wa Afmadow, ulio umbali wa kilomita 114 kaskazini mwa Kismayo, bila ya kuleta upinzani wowote. Mji huo ulio nyumbani kwa maelfu ya watu ni kituo muhimu cha kibiashara kwa vijiji kadhaa vya karibu na una barabara unayoiunganisha na Kismayo na Buale.
Mkaazi mmoja wa Afmadow, Dhayib Aato, aliiambia Sabahi kwamba al-Shabaab ni kama samaki na watu wa Somalia ni kama bahari kubwa iliyochafuka. Alisema watu wamekataa kutoa hifadhi kwa al-Shabaab kwa sababu kundi hilo limeharibu miundombinu ya nchi na kuuwa wasomi, masheikh, wanafunzi na waandishi wa habari wa Kisomali kukidhi matakwa ya wahalifu waliojitolea kwa ajili ya fujo ulimwenguni kote.
Mkaazi mwengine wa Afmadow, Mohammed Nur, aliiambia Sabahi kwamba al-Shabaab imemwaga damu ya Waislamu, kuvunja imani ya Uislamu, ambayo inataka pawepo uvumilivu na kusameheana na kuacha ghasia, wasiwasi na chuki.
Mwanajeshi wa Kisomali aliyepo mjini Afmadow, Abdi Abukar, alisema al-Shabaab haifahamu maana halisi ya jihadi.
“Ikiwa kweli ni mujahidina, kwa nini wakawa wanakimbia medani ya vita baada ya mapambano? Mara kadhaa tunawaona wakikimbia bila ya hata kukusanya maiti na majeruhi wao,” aliiambia Sabahi. “Kwa ukweli hasa, ni woga na wanajizuia kupambana uso kwa macho na wanapendelea kurushiana makombora na mizinga huku wakijaribu kuchukua madaraka kwa mtutu wa bunduki.”
Wachambuzi wamekuwa wakirejea kueleza kila mara kwamba kundi hilo linalojiambatanisha na al-Qaeda linaelekea kuporomoka, huku wapiganaji wake wakipoteza moyo wa mapambano mbele mapigo mfululizo kutoka majeshi ya Somalia na vikosi washirika na pia wakikabiliwa na kuzorota kwa ufadhili wa kifedha kwao. Kundi moja la makamanda wa al-Shabaab wanaunga harakati ya pembeni kushauriana na TFG, kamanda wa al-Shabaab aliiambia Sabahi.
Ndani ya kipindi cha wiki mbili zilizopita, al-Shabaab wamepoteza mji wa Afgoye kwenye mkoa wa Lower Shabelle na Afmadow katika mkoa wa Lower Juba. Sasa kundi hilo linarudi kwenye upiganaji wa msituni na mbinu za kushambulia na kukimbia, jambo ambalo linaweza kumaanisha mwisho wa operesheni za kigaidi za al-Qaeda katika Pembe ya Afrika, wanasema wachambuzi.
Wapiganaji wa al-Shabaab wanakabiliwa na mapigano katika gome zao zilizobakia huku wanajeshi wa Somalia wakielekea katika mkoa wa Lower Juba kutokea Gedo na Middle Juba, huku majeshi ya washirika yaliyo kwenye miji ya Mogadishu na Afgoye yakijitayarisha kuushambulia mkoa wa Middle Shabelle.
Ahmed Mohammed Islan, kiongozi wa wanamgambo wanaoiunga mkono serikali katika Ras Kiamboni, aliiambia Sabahi kwamba vikosi vya washirika vitasonga mbele kuuchukua mji wa Kismayo katika mkoa wa Lower Juba na miji ya Buale na Jilib katika mkoa wa Middle Juba.
Huku vikosi vya washirika vikiwakaribia wapiganaji wa al-Shabaab, baadhi ya wapiganaji hao wamejisaliisha kwa serikali ya mpito, Aadan Hirsi, msemaji wa jeshi la Somalia mjini Gedo aliiambia Sabahi.
“Kundi lililojitenga kutoka al-Shabaab limejisalisha kwetu,” alisema. “Kundi hilo linajumuisha wapiganaji 20 wenye silaha zikiwemo bunduki na gari la kubebea makombora. Walipokelewa katika mji wa Beled Hawo baada ya kunyang’anywa silaha, ikiwa ni hatua ya mwanzo ya kuwatayarisha na kuwaingiza kwenye jamii katika kituo maalum kwa ajili ya raia walioachana na wapiganaji wenye siasa kali.”
“Wapiganaji wengine wa al-Shabaab bado wana nafasi ya kujisalimisha kabla ya vikosi vyetu havijachukuwa udhibiti wa miji yote iliyo sehemu ya mkoa huu, ikiwemo Bortobo na Baardheere," alisema Hirsi. “Tutatekeleza mpango kamili wa mashambulizi kuchukuwa udhibiti wa maeneo mapya.”
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
maoni yangu ni kuwa kenya ni makafiri,na serikali ya somalia ni makafiri,amison ni makafiri,marekani ni makafiri na wote,sasa Ali shabab ni waislamu wanaotaka Quran itawale na makafiri hawataki na wanataka akili zao zitawale na waweke pombe na makanisa sisi waislamu tutawaunga mkono mpaka mwisho ama waislamu tufe au wao wafe.
Angalau Jeshi la Ulinzi la Kenya linaweza na litafanya nchini Somalia ni kuwasafisha al-Shabaab. Ni kizazi cha walemavu ambacho lazima kifutwe ikiwa hawakujisalimisha na kujigeuza kuwa kikundi kinachoishi na wengine kwa amani.
Kwa kweli al-Shabaab hawana nafasi. Tulijaribu kuwaambia lakini sasa wanajifunza kwa haraka kuwa Wakenya si watu waoga kama Wamarekani. Kiatu cha KDF kupigwa kwenye meno ya al-Shabaab. Watakiona...
Huu ni ushindi uliokuwa unasubiriwa muda mrefu.
Ningetamani mabaki ya al-Shabaab wangejua mdundo tunaocheza ukoje, bila ya kujali itachukua muda gani ambapo sielewi. Tutawachuna ngozi na kuwafanya kama vile walivyowafanya wengine. Wajisalimishe na kuijenga upya nchi yao.
Jifanye kama uko dhaifu na kuchochea machafuko ili kumpa moyo adui. Wakati wa kushambulia, jidai unajiondoa, na wakati wa kujiondoa, rejea na kushambulia, baadaye jitokeze bila ya kutarajiwa na KUMPONDAPONDA adui yako. Mchezo umekwisha kwa al-Shabaab. Jitayarisheni kukutana Muumba wenu! Amani kwa Somalia, Heshima kwa KDF.
Al-Shabaab kama mnaipenda nchi yenu na Wasomali, basi tafadhali acheni mapambano kwa sababu kamwe hamtashinda vita hii. Ikiwa ni zaidi ya askari 20,000, watu wa AMISOM hulipwa vizuri na morali wao uko juu, hamuwezi kushinda. Jisalimisheni na kuanza kujenga nchi yenu.
Hii ni kama muziki kwa Wasomali ambao wanaopenda amani na wale wote wanaothamini amani ya Mungu katika eneo letu. Mungu awape askari wa TFG na KDF ushindi bila ya vifo na majeruhi yoyote.
Ninaandika kutoka Kenya nikiwa si Muislamu wala Mkristo. Mimi ninafuata jadi za Afrika tu lakini ninafurahi kwamba amani inakuja kwa ndugu zangu wa Somalia na kwamba Wasomali wenyewe wanaongoza katika kutafuta. Utoaji wenu wa taarifa haupendelei na ni sahihi kiasi kwamba unaaminika hapa! Tafadhali Somalia msiruhusu nafasi hii kuwapita. Mimi ni mwalimu wa shule ya sekondari kijijini Kenya na ninafundisha wavulana wengi wa Somalia wasio na makazi. Wanaonekana wamejawa na matumaini. Kibichii Kemboi - Baringo.
Al-Shabaab wanapaswa kuheshimu damu ya ndugu zao.
Napenda al-Shabaab wasambaratike kabisa kwa sababu wametenda ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya jumuiya ya Somalia. Kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab kinasambaratika kwa kiwango cha kasi kwa sababu jamii imegeuka dhidi yao kwa ajili ya mauaji ya wanachama wa jumuiya, kati yao wakiwemo wanafunzi, wataalamu na wakuu wa kidini wa Somalia.
Asanteni kikosi cha Sabahi kwa kutujulisha kwa wakati juu ya vita vya Somalia. Ninafurahia utoaji wenu nzuri wa habari, Mungu akijalie maisha marefu kikosi cha Sabahi.