Juni 04, 2012
Wachambuzi wa Somalia na maofisa walipokea vyema matokeo ya mkutano wa Istanbul kuhusu Somalia baada ya kumalizika hapo Ijumaa (tarehe 1 Juni) huko Uturuki.
Wachambuzi walisema kuwa wana matumaini na upigaji hatua wa mkutano huo ambao unaweza kuiweka Somalia katika njia sahihi ya ujengaji wa hatima ya baadaye.
Mkutano huo, ambao mada yake kuu ilikuwa "Kutayarisha Hatima ya Somalia: Malengo hadi mwaka 2015", ulitoa taarifa inayosisitiza umoja wa Somalia na umuhimu wa mazungumzo na uwazi katika uteuzi wa wajumbe wapya wa serikali. Waliohudhuria walitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa fedha na msaada katika kipindi cha baada ya mpito kujenga miundombinu ya Somalia.
Wajumbe wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho (TFG), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, na wawakilishi kutoka nchi 57 na mashirika ya kimataifa 11 waliohudhuria mkutano huo wa siku mbili.
Washiriki walitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendeleza msaada wake kwa ujenzi na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kutosha kwa vikosi vya usalama vya Somalia, likiwemo Jeshi la polisi la taifa, jeshi la majini, ulinzi wa pwani na mashirika ya ujasusi. Mkutano huo ulitoa wito kwa wasomali kuacha vurugu na kufanya kazi pamoja ndani ya mpango wa katiba na kusaidia mchakato uliopo wa siasa, Mpango Mkuu huo, mchakato wa usuluhishi wa Somalia na kujenga dola hiyo.
Serikali ya Somalia ilisema katika taarifa siku ya Jumamosi kuwa inakaribisha vyema matokeo ya mkutano wa Istanbul, yaliyobainisha uchumi wake, usalama na athari za kisiasa.
"Kwa kushughulikia masuala ya kiuchumi na umaskini uliokithiri, watu wa Somalia watakuwa na fursa mpya za kazi – ambazo zingeweza kuwa mbadala katika vurugu – hususan kwa vijana," waraka ulisema.
"Jumuiya ya kimataifa ina wajibu mkubwa wa kutimiza nchini Somalia, hususan kutoa misaada ya muhimu ya kuanzisha jeshi la kitaalamu na majeshi ya polisi ambayo yatawajibika katika kuendeleza usalama wa nchi," TFG ilisema.
"Wanajeshi wa Somalia pamoja na msaada wa AMISOM nchini Somalia wamefanya mabadiliko makubwa katika suala la usalama, [na]wametekeleza mpango wa uthabiti wa nchi kwa kiwango kikubwa [ambao] umefikisha katika ukombozi wa maeneo mengine mapya kutoka kwa kikundi cha magaidi wa al-Shabaab."
Kuhusu suala la siasa, serikali imerudia kusema uwajibikaji wake katika ratiba ya kumalizika kwa kipindi cha mpito mwezi Agosti, kama ilivyoahidiwa na wadau katika mkutano huko Addis Ababa tarehe 23 Mei.
Watu wa Somali wameona maendeleo makubwa kwa miezi nane iliyopita, ikiwa ni pamoja na kipindi kirefu cha amani jijini ambacho kimeboresha biashara na jitihada za ujenzi mpya," waraka ulisema, ukihitimisha kwamba, "serikali itaendeleza mashambulizi yake dhidi ya magaidi kwani inaendeleza kwa al-Qaeda waliobaki wakizunguka kusini na kati mwa Somalia."
Mchambuzi wa masuala ya siasa Ahmed Abdirazaq aliiambia Sabahi kwamba Mkutano wa Istanbul ulikuwa "ni fursa nzuri kwa serikali na watu wa Somalia".
Mkutano huu umekuja kwa wakati mwafaka kutokana na hatua ambayo Somalia yenyewe imefikia," alisema. "Maandalizi yanaendelea kwaajili ya kumaliza kipindi cha mpito mwezi Agosti, kwaajili ya kufuata katiba mpya, uundaji wa bunge jipya la Somalia, uchaguzi wa Rais mpya na uundaji wa serikali mpya."
Abdirazaq alisema ana matumaini kwamba uamuzi uliofanyika huko Istanbul unatekelezwa, "kwa hiyo kutoa fursa halisi na ambayo haijawahi kutokea kwa Somalia".
"Mkutano wa Istanbul umeonyesha kwamba dunia sasa iko tayari kuendelea kuisaidia Somalia na kutatua suala hili ambalo limekuwa likiachwa kwa zaidi ya miongo miwili," alisema. "Mkutano pia umehakikisha tena msaada wa kimataifa kwa Somalia baada ya shauku kubwa iliyopunguzwa kuhusiana na suala hili."
Mwandishi na mwanaharakati wa kisiasa Abdiwahab Ahmed Ali alisema matakwa ya kimataifa katika suala la Somalia ni kiashiria cha jinsi ilivyo muhimu kwa uthabiti wa Somalia kwa ajili ya eneo na dunia.
"Mikutano iliyofanyika London, Istanbul na Rome (mikutano ya kukutana na vikundi vya kimataifa) yote ilionyesha kwamba dunia inataka kuijenga upya Somalia kwani tatizo la Somalia sio la kwake peke yake," aliiambia Sabahi. "Badala yake ni tatizo la nchi na ngazi ya kimataifa ambalo linaacha madhara ya amani na usalama wa nchi na dunia kwa sababu ya kuwepo kwa ugaidi na uharamia nchini Somalia."
Alitoa wito kwa viongozi wa Somalia kuitumia fursa hii, ambayo inaweza isitokee tena. "Ninadhani mkutano huu unatoa fursa ya kihistoria kuleta matumaini mapya kwa Somalia," alisema.
Mohammed Abdullahi, mchambuzi wa masuala ya kisiasa anayeishi Mogadishu, alisema anatumaini Mkutano wa Istanbul unawakilisha "kuanza kwa mwisho wa tatizo la Somalia".
"Baada ya miezi mingine miwili, Somalia inatarajiwa kuwa na katiba mpya, kipindi cha mpito kinaisha na serikali mpya inakabidhiwa kipindi kilichopo cha mpito," alisema. "Ninaamini kwamba maendeleo katika hatua ijayo yataiweka Somalia katika njia sahihi."
Abdullahi aliiambia Sabahi matokeo ya mkutano ni "ushindi mkubwa kwa watu wa Somalia".
Tamko la mwisho la Mkutano wa Istanbul lilisisitiza kwamba kuisha kwa mgogoro wa Somalia kupo mikononi mwa Wasomali wenyewe na kwamba jumuiya ya kimataifa inaweza tu kutoa msaada kwa kile ambacho Wasomali wataamua.
Hassan al-Bisri Sheikh Abdulqadir, mkuu wa Kituo cha Masuala ya Afrika ya Mashariki na Vyombo vya Habari cha Mogadishu, alisema Uturuki hivi karibuni imechukua mfululizo wa hatua za kisiasa na za kibinadamu ili kusaidia kuinyanyua Somalia toka mizozo inayokabiliana nayo hivyo sasa.
“Uturuki inakuwa mshirika na mshughulikiaji imara wa masuala ya Somalia na ilikuwa nchi ya mwanzo kubwa kutoa msaada wa kibinadamu kupunguza athari za ukame na njaa iliyoikumba Somalia mwaka jana, aliiambia Sabahi.
Abdulqadir alisema Uturuki ina shika nafasi muhimu huko Somalia.
“Wakati Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, akifuatana na mke wake na mawaziri wake muhimu, aliamua kuitembelea Mogadishu mwezi Agosti uliopita, ziara hiyo iliimarisha heshima ya juhudi za Uturuki nchini Somalia kwa njia ambayo haikuwahi kutokea" alisema. "Uturuki inatekeleza miradi kadhaa ya maendeleo ili kuijenga upya Somalia, ikiwemo ujenzi wa barabara na hospitali na ufunguzi wa shule mpya. Uturuki pia imetoa mamia ya misaada ya masomo ya chuo kikuu kwa wanafunzi wa Somalia kusoma Uturuki.”
Profesa wa chuo kikuu, Mukhtar Hussein, alisema jukumu ya Uturuki ni pekee na “imekuja wakati uwajibikaji wa Uislamu na nchi za Kiarabu katika kukabiliana na mzozo wa Somalia ni mdogo sana”.
“Ankara kwa sasa inaongoza ari zilizolengwa kujenga dira moja inayokubalika na jumuiya ya kimataifa kwa Somalia ili kujenga upya nchi na kuwaruhusu Wasomali waweze kujitegemea,” alisema. “Uturuki pia imekuwa na nafasi ya kuzileta pamoja mawazo yanayotofautiana ya vikundi mbalimbali vya Wasomali."
Baada ya kushindwa kwa mkutano wao wa Mogadishu, viongozi wa makabila walisafirishwa kwa ndege hadi Istanbul mwezi uliopita kwa gharama za serikali ya Uturuki kwa ajili ya vikao vya kutatua migogoro.
Hasan Ozturk, mmoja wa wataalamu maarufu wa Kiafrika katika jumuiya ya washauri mabingwa wa Bilgesam ya Ankara, alisema nafasi ya Uturuki nchini Somalia ni ya kisiasa, lakini haina kikomo.
"Wazee kutoka koo za Somali wanatafuta dalali ambaye atawashawishi wazee wengine kukubaliana na makubaliano ya hatimaye na ambao hawatapendelea upande wowote,” alisema. “Mzozo wa sasa wa kuaminiana upo Somalia na unaweza kushindwa na kuwepo na upande wa tatu kama vile Uturuki ambayo tayari imeshaweka misingi ya kuaminiana huko.”
Ozturk alisema, hata hivyo, Uturuki haiwezi pekee kutatua matatizo ya Somalia.
“Katika taarifa ya mwisho ya mkutano wa Somalia, ilisemekana kuwa jumuiya ya kimataifa lazima izisukume pande zinazohusika kufikia makubaliano. Hata hivyo, taarifa hiyo inasisitiza kuwa hatua zinazofaa lazima zichukuliwe dhidi ya zile zinazozuia maendeleo. Katika hili, lazima mtu ajiulize swali: Ikiwa inaonekana kuwa upande mmoja unazuia maendeleo, Uturuki itaweza kufanya nini? Kwa bahati mbaya, sio sana," alisema, na kuongeza kuwa Uturuki itaweza kusaidia kuandaa hatima ya Somalia, lakini sio kuchukua dhamana kubwa kiasi hicho.
"[Uturuki] ingejitahidi kutoa matokeo mazuri, lakini Uturuki isibakie kuwa mtendaji mwenye maamuzi yote,” alisema. “Suala hili linahitaji mashirikiano ya kimataifa."
Menekse Tokyay alichangia akiripoti kutoka Istanbul.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Somaliland
Nafikiria kuwa Somaliland ni mojawapo wa eneo zuri zaidi la Somalia.
Naamini mikutano zaidi na zaidi itafanyika nchini Somalia ili kukuza uhusiano na mataifa mengine ya Afrika na dunia nzima.
Ninakubali, lakini hali ya sasa kule hakuna ukabila tena. Naamini kuwa siku zote kuna maslahi binafsi ya viongozi ambao wanatumia ukabila au umakundi kama silaha, lakini tufikirie kuwa Somalia imekosa uongozi unaoweza kuja na ahadi inayosema jumuiya ya kimataifa inataka nini kutoka kwetu hasa wadau wanaojihusisha na masuala ya kisiasa ya Somalia kama vile Ethiopia, Misri, Saudia, Ulaya, China, Uturuki na Marekani. Naamini kuwa hakuna yeyote duniani anayekupa chakula cha bure bila kuwa na maslahi yake, lakini kutokana na upungufu wa usambazaji wa mafuta duniani ambapo Wachina na Wamagharibi wanahakikisha kunapatikana mafuta kutoka vyanzo vyovyote barani Afrika, inaonekana kama kila mtu anataka kunyakua uwezo mkubwa wa nyenzo za mafuta na madini nchini Somalia. Kwa bahati mbaya baadhi ya nchi jirani zinadai kuwa Somalia lazima iwe na utulivu, lakini kinyume chake wanavipa silaha baadhi ya vikundi vya Kiislamu ili kusababisha hali kutokuwepo kwa utulivu huo kwa muda mrefu ili wao wawe wanatafuta mafuta. Kwa vyovyote vile, kuna mgombea yeyote anayeweza kufahamu nini nchi zenye nguvu zinatafuta nchini Somalia? Natumai hakuna, kwa sababu kila mmoja anafikiria kuhusu sera zilizopitwa na wakati zisizo na maslahi ya kibiashara kwa kusema kuwa Wamisri wanachotaka kutoka Somalia ni kuitumia Somalia kama chanzo cha vurugu na Ethiopia, kwa hivyo hayo ndiyo maslahi ya Somalia katika eneo hili; Ethiopia inataka kuhakikisha kuwa uongozi dhaifu unaotegemea mfumo wao; Marekani wanataka kuona na kusubiri kumuona mtu wakisema Jambo! Najua unataka mafuta.
Somalia inapaswa kuwa na umoja na watu wa Somalia wanapaswa kujifunza kutoka kwa majanga ya zamani waliyopitia. Wanapaswa kuelewa kwamba ukabila hauwezi kujenga taifa. Wanapaswa kutambua kuwa mataifa yanajengwa na wananchi wao na nafasi ya kujenga nchi upya haiji mara kwa mara.
Nadhani mkutano huu utazaa matunda yanayolika