Kuipoteza Afgoye ni pigo kubwa kwa al-Shabaab

Na Mahmoud Mohammed, Mogadishu

Mei 29, 2012

  • 54 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kwa al-Shabaab kuipoteza Afgoye, ngome muhimu kwao, kutakuwa na athari kubwa na mbaya sana kwa kundi hilo linalojihusisha na mtandao wa al-Qaeda, wasema wachambuzi.

Vikosi vya serikali ya Somalia na vile vya Umoja wa Afrika, (AMISOM) vilichukuwa udhibiti wa Afgoye hapo Ijumaa (tarehe 25 Mei) baada ya siku tatu za kampeni ya kijeshi.

"Al-Shabaab wameshindwa vibaya na ushindi huu wa wazi kwa upande wa vikosi vya serikali na vya AMISOM mjini Afgoye ni pigo kubwa kwa kundi hilo; ambalo kamwe haliwezi kupona,” mchambuzi wa mambo ya siasa, kanali mstaafu Osman Aden, aliiambia Sabahi.

Aden alisema kuichukua Afgoye, iliyo umbali wa kilomita 30 kutoka Mogadishu, kutavirahisishia vikosi vya majeshi ya washirika kuilinda barabara kuu kati ya Afgoye na Baidoa. “Itawezesha pia upatikanaji wa misaada ya kibinaadamu kwa wakaazi walio kando ya barabara hiyo muhimu baina ya Afgoye na mji mkuu,” alisema.

Noor Yusif, mchambuzi wa masuala ya siasa na mtaalamu wa harakati za Kiislamu nchini Somalia, alisema: “Mafanikio ya Jeshi la Taifa la Somalia ya kuutoa mji wa Afgoye kutoka mikononi mwa al-Shabaab, kwa msaada wa AMISOM, ni hatua muhimu ya kijeshi, kuchukua ngome ya mwisho ya waasi karibu na Mogadishu.”

Yusif alisema al-Shabaab imedhoofidshwa tangu kuingia majeshi ya Kenya na Ethiopia nchini hapo mwaka jana. “Operesheni za kijeshi za majeshi ya pamoja na ya kieneo zimeudhoofisha uwezo wa kijeshi wa al-Shabaab,” aliiambia Sabahi. “Kuukomboa mji wa Afgoye bila ya upinzani mkubwa ni alama kwamba al-Shabaab inaporomoka na kwamba sasa haina tena uwezo wa kukabiliana na opesheni ya kjeshi dhidi yake.”

Kuziba njia ya usambazaji kwa wapiganaji wa al-Shabaab

Afgoye imekuwa ngome ya al-Shabaab kwa miaka mitatu na mafanikio makubwa kwa vikosi vya AMISOM tangu kuingia kwake Somalia mwaka 2007.

“Mji wa Afgoye ilikuwa ngome madhubuti ya waasi wa Kiislamu kwa sababu upo kwenye barabara muhimu, ikiuunganisha na mji mkuu, Mogadishu na sehemu za magharibi na kusini za Somalia,” alisema mchambuzi wa masuala ya kisiasa Ahmed Omar. “Ilikuwa ni ngome ya pili muhimu kwa al-Shabaab baada ya mji wa Kismayo.”

“Ushindi huu uliopatikana na majeshi ya Somalia na AMISOM mjini Afgoye ni mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya al-Shabaab. Inawakilisha mwanzo wa mwisho wa harakati ya al-Shabaab,” aliiambia Sabahi.

“Kwa kuchukuwa udhibiti wa Afgoye, vikosi vya Umoja wa Afrika na vya serikali sasa vinaweza kuchukua udhibiti kamili wa njia kuu inayounganisha mikoa kusini na magharibi na mji mkuu.” Alisema ushindi huo utawakatia al-Shabaab njia zao za kusambazia vifaa vya kijeshi na mafao wapiganaji wa al-Shabaab.

“Kuichukuwa Afgoye kutoka mikononi mwa waasi kunaelezea kushindwa tena kwa al-Shabaab, ambayo imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kijeshi kutokana na kampeni ya vikosi vya washirika katika maeneo ya kati na kusini,” alisema.

Usalama wa Mogadishu

Wachambuzi wanasema “Operesheni Shabelle Huru" ambayo ilipelekea kuanguka mwa mji wa Afgoye inadhamiria kusaidia kuimarisha usalama mjini Mogadishu, ambao umo kwenye matayarisho ya mkutano wa kwanza wa Bunge la Taifa la Katiba utakaofanyika hivi karibuni.

“Kampeni hii inachangia katika kuuweka salama mji mkuu, Mogadishu, ambao unajitayarisha kwa mkutano wa Bunge la Katiba ambao utaidhinisha katiba mpya na kutayarisha uchaguzi wa Bunge na Rais utakaofanyika tarehe 20 Agosti mwaka huu,” mchambuzi wa masuala ya siasa Abdul Fattah Osman aliiambia Sabahi.

Kudhibiti mji wa Afgoye kutaimarisha usalama karibu na al-Shabaab na kutawanyima wanamgambo hao wa siasa kali fursa ya kufanya mashambulizi dhidi ya Mogadishu kutokea mji wa Afgoye. Hatua hii itaviruhusu pia vikosi vya usalama kuwashinda al-Shabaab na washirika wake wa al-Qaeda nchini Somalia,” aliongeza.

Al-Shabaab wakimbia

Kujiondoa kwa al-Shabaab katika mji wa Afgoye bila ya upinzani mkali kunafuatia mtiririko wa kushindwa kwao, ikiwemo kujitoa katika maeneo yao mjini Mogadishu mwezi Agosti na kuucha kwao mji wa Baidoa mikononi mwa vikosi vya Ethiopia na Somalia hapo mwezi Februari.

Jenerali Abdi Kareem Yusif Dhagabadan, mkuu wa majeshi ya Somalia na kamanda wa operesheni dhidi ya al-Shabaab, aliahidi kuendelea na operesheni za kijeshi.

"Bado hatujakuwa na udhibiti kamili wa Afgoye na tutaendelea kuwawinda waasi hadi tutakapoweza kuwaponda magaidi wote waliokuwa wakaidi,” aliiambia Sabahi. “Operesheni hizi za kijeshi zitasimama baada tu ya kuwamaliza wote.”

"Wanamgambo wana nafasi ya mwisho ya kujisalimisha,” alisema Dhagabadan, akiwataka wapiganaji wa al-Shabaab kujipeleka mwenyewe kwa vikosi vya serikali.

Luteni Jenerali Andrew Guti wa AMISOM aliiambia Sabahi kwamba al-Shabaab inakimbia. “Waasi wanashindwa vita na wanapoteza matumaini,” aliiambia Sabahi. “Wanakimbia na vikosi vya washirika vinapiga hatua kubwa".

“Operesheni hii ilipangwa vyema na hatua zote za tahadhari zilichukuliwa kuepusha maafa kwa raia,” alisema. Kwa kuikamata ngome ya Afgoye, misaada ya kibinadamu inaweza sasa kufikishwa kwa watu 400,000 wanaoishi kwenye eneo hilo, kwani al-Shabaab alikuwa wamepiga marufuku mashirika ya misaada kuyasaidia makundi yaliyoathirika na yaliyo kwenye mazingira magumu.

Al-Shabaab yakataa kushindwa

Al-Shabaab ilisema kwamba iliondoka kwenye mji wa Afgoye kwa makusudi baada ya vikosi vya Umoja wa Afrika kuingia kwenye mji huo na vifaru.

“Mujahidina walitumia mbinu ya kujiondoa kwenye baadhi ya maeneo, lakini hiyo haimaanishi kushindwa,” alisema Abdiaziz Abu Musab, msemaji wa operesheni za kijeshi za al-Shabaab. “Tutaendelea kupigana na bila shaka tutashinda. Vifaru vya AMISOM havitutishi."

Maofisa wa usalama waliiambia Sabahi kwamba taarifa za al-Shabaab si chochote zaidi ya jaribio la kuinua morali ya wapiganaji wao wanaorudi nyuma.

“Baada ya kupoteza mji wa Afgoye, al-Shabaab inajaribu kuinua morali ya wapiganaji wao walioondoka kwenye maeneo yanayoshikiliwa na vikosi vya washirika, na kuelekea maeneo ya vijijini kwenye miji ya kusini,” alisema Mohammed Abdi Qadir, afisa katika Jeshi la Taifa la Somalia.

Huku wakimbizi wa ndani wakikimbia, mashirika ya misaada yaomba walindwe

Misafara mirefu ya magari na mabasi yanayowasafirisha wakimbizi imekuwa ikielekea Mogadishu. Hapo Alhamis na Ijumaa, eneo hilo lilishuhudia misafara mikubwa kutoka Eilasha na ushoroba wa Afgoye, wakitafuta usalama.

Operesheni ya kuikomboa Shabelle imezilazimisha familia kadhaa kuziacha nyumba zao za muda licha ya AMISOM na serikali ya Somalia zimewataka wabakie majumbani mwao.

Kambi ya Afgoye imekuwa makaazi ya muda kwa kiasi ya wakimbizi 400,000 wa ndani ambao waliziacha nyumba zao mjini Mogadishu na maeneo mengine katika miaka iliyopita kukimbia mapigano na ukame.

Fartuun Ahmed aliiambia Sabahi alikimbia na watoto wake wanane kutoka Eilasha. “Hatuwezi kukaa hapa tena kwa sababu mabomu yanatuangukia na sauti za bunduki ziko kila upande,” alisema. “Watu wanaogopa.”

Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinaadamu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) nchini Somalia, Dk. Mohammed Noor Jaal, alizionya pande zinazohusika kuwalinda wakimbizi wa ndani wa Ushoroba wa Afgoye.

“Tunamtaka kila mmoja kuchukua hatua za tahadhari kuzuia majeruhi au maafa kwa raia na wakimbizi wa ndani,” aliiambia Sabahi.

Alisema mashirika ya misaada na washirika wa OIC wanafanya kazi ya kupeleka misaada ya kibinaadamu kwa wakimbizi hao waliokimbia mapigano.

Umoja wa Mataifa pia umezitaka pande zote kuruhusu misaada kamili ya kibinaadamu kwa watu wenye uhitaji kwenye Ushoroba wa Afgoye.

“Ambapo tunaendelea kutokuwa na upande wowote wa michakato ya kisiasa na kijeshi, wafanyakazi wa huduma za kibinadamu wanaratibu shughuli za kuhakikisha kuwa msaada wa haraka unapatikana kwa raia walioathirika vibaya na harakati za kijeshi katika ushoroba huo,” alisema Mratibu wa Masuala ya Binaadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Mark Bowden, hapo Jumanne.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 80)

Dislike_icon(22)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • abdull
    October 11, 2012 @ 05:55:17AM

    Tuviunge mkono vikosi vya Kenya, kwa kweli wanafanya kazi nzuri. Na ninasema hongera:.............tuwang'oe al-Shabaab kutoka ardhi ya Somalia.

  • baashe cadde
    June 19, 2012 @ 01:36:27AM

    Amani iwe juu yenu. Mimi ni mzee mwenye uzoefu lakini nyinyi vijana hamna watu wenye uzoefu miongoni mwenu. Ningependa kuwaambieni kuwa nchi iko chini ya koloni. Ikiwa mnadhani siko sahihi, oneni jinsi nchi ilivyozingirwa. Msiwaangalie al-Shabaab tu lakini hatima ya Somalia. Sahauni juu ya al-Shabaab kwa sababu hawa ni Wasomali na fikirini ikiwa mko tayari kuiweka nchi katika mikono ya maadui zenu. Ninauzoefu wa ukoloni wa Waingereza, Wataliana, Waethiopia n.k. ambao hawako tayari kuwaona Wasomali wanaungana na kurejesha amani nchini. Fikirini kwa kina na mtulize vichwa vyenu.

  • xamar cadey
    June 16, 2012 @ 04:27:09AM

    Somaliland? Nyota katika Afrika ya Mashariki? Iko wapi hiyo?

  • muuna cabdi raxmaan hasan
    June 14, 2012 @ 06:30:23AM

    Mimi nahisi kwamba suala hilo ni tofauti na kile ambacho kinasemwa. Ni kweli kuwa wamefanya uhalifu dhidi ya watu wa Somalia na pia ni kweli kwamba wanasambaratika, lakini sidhani kwamba walishindwa na Jeshi la Ulinzi la Kenya na siungi mkono hatua ya kuleta Jeshi la Kenya mjini Mogadishu na Baidoa. Kama mnapendekeza waje, basi ni kama kuwadai malipo kwa kazi ambayo hawawezi kuitekeleza. Juu ya suala la wale wanaojisalimisha wenyewe kwa serikali, ningependa kusema kwamba si wote walioasi kutoka kwa Al-Shabaab ni wahalifu na miongoni mwao ni wale ambao tulikuwa tunawatumikia Al-Shabaab kwa nguvu. Wahalifu wanaweza kujulikana na kutofautishwa kutoka kwa wale ambao si wahalifu kwa njia ya uchunguzi. Ningependa kuwaomba Al-Shabaab kuisaidia serikali katika kurejesha amani na utulivu katika nchi kwa sababu walishindwa kufikia chochote kwa muda wa miaka saba waliyokuwa wanatawala nchini.

  • warsame
    June 14, 2012 @ 02:48:13AM

    Mtoto wa Godane bado anatamba na hakukamatwa. Mwana wa haramu huyu kutoka ukoo wa Hawiye lazima apelekwe mahakama ya sheria kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

  • Alla Yaqaan
    June 13, 2012 @ 10:29:18AM

    Angalieni jibu hili katika hali ya shairi: Mimi sikuuza dini yangu kwa ajili ya kujenga ghorofa jehanamu, mimi sithamini dunia kwa kulinganisha na akhera. Jana mlishirikiana na adui zangu, jana, mlimuunga mkono adui yangu wakati mimi nilipowashinda. Nyinyi mliwahifadhi mbwa na nguruwe wakati mimi nilipokuwa nikiwafukuza. Sikuwafuateni nyuma katika nyumba zenu, wakati mlipomficha kutoka kwangu, wala sikupotea kutoka njia ya haki ya Mungu katika dini maalum. Darood Ismail haelewi mashimo yaliyochimbwa kwa ajili yake, amegundua hilo baada ya kuwa katika mashimo hayo kwa miaka. Ninyi watu mnapaswa kusikiliza ushauri wangu ili kuepuka majanga au msitilie maanani kile ninachowaambia. Ushauri wangu unaweza kuwasaidia wale tu walio na busara na wala sio wapumbavu. Hamuwezi kusaidiwa na wasio Waislamu, kama mtawakaribisha, mtaangushwa na wasiokuwa Waislamu mnaowakaribisha. Msijisahau kwa fedha wanayowapeni, watawafanyeni watumwa na kuwatumieni kama punda. Nitaweza kufanyieni nini kama mtanitahadharisha baada ya kuwa tayari wamekwenda mbali zaidi ya Adari na IImay kwa sababu tayari wameshachukuwa mashamba huko.

  • Alle yaqaan
    June 13, 2012 @ 09:53:25AM

    Ni heshima ya Mungu ambayo walijaaliwa wale waliokuwa kabla yetu na Mungu anaweza kufanya kila kitu.

  • gul
    June 12, 2012 @ 03:29:57PM

    Wanauliza habari mpya ni ipi? Habari mbaya pia ni habari. Kwa hiyo ikiwa habari mpya ni watu kukutakia mema, maana yake wewe ni mwema na ikiwa wanakutakia mabaya, wewe ni mbaya. Ndivyo ilivyo. Wakati utaamua kama walikuwa wema au la.

  • WANYONYI EVANS
    June 12, 2012 @ 03:45:35AM

    ALSHABAAB MMESHAFANYA UHARIBIFU WA KUTOSHA.REJEENI KATIKA FAHAMU ZENU NA KUSAIDIA KUJENGA UPYA NCHI YENU.

  • hamze
    June 11, 2012 @ 10:40:48AM

    Kuna matumaini mazuri ya maendeleo katika Afrika Mashariki isipokuwa Somalia lakini Somaliland ndio nyota.

  • hamze
    June 11, 2012 @ 10:35:24AM

    Somaliland ni nchi bora mpya katika Afrika Mashariki. Kila mtu lazima ajivunie.

  • PHINIAS
    June 7, 2012 @ 07:36:46AM

    HA! TAYARI WAMESHINDWA.NINI ZAIDI?

  • KOL
    June 7, 2012 @ 03:51:02AM

    IKIWA MNAFIKIRI KUWA KILA MTU ANAWEZA KUIONGOZA SOMALIA, BORA MNGEFIKIRIA TENA. CHUKUENI MFANO WA KILE SHEIKH ANACHOFANYA SASA.

  • Evans Chirchir
    June 6, 2012 @ 01:50:27AM

    Heshima kwa timu yetu ya Ulinzi ya Kenya. Hili litakumbukwa katika historia yetu

  • chelangat
    June 5, 2012 @ 09:23:33AM

    Kuna wakati kwa kila kitu, na ni wazi kuwa wakati wa al-Shabaab imefika. Ama wabadilike na kusalimu amri au wasafiri kwenda bahari kuu ambako wanatoka. Hata huko, tutakuwa nyuma yao. Hongera askari wetu shujaa waliothubutu kuota juu ya jirani yetu mwenye amani.

  • FYATTY FONDO MEN
    June 4, 2012 @ 08:59:03AM

    Wow! Watu hawa hawatanii licha ya vitisho tunavyowatia, hawataacha mpaka mtu wa mwisho aliye hai. Watu hawa wapo kwa ajili yao wenyewe katika uwanja wa vita na hawaogopi kufa.

  • David Muga
    June 4, 2012 @ 08:49:05AM

    Kampeni za kijeshi zinazofanywa na maafisa wa serikali ya Kenya inaacha mengi. Nilisema tangu mwanzo kuwa Serikali ya Kenya ilitaka kampeni ya kijeshi iendelee kwa muda mrefu, kwa sababu zisizojulikana kijeshi. Mwisho itathibitika kwa serikali ya Kenya kuwa kuchelewesha huko kumesababisha gharama zaidi kwa nyenzo za kibinadamu na fedha, ambazo zisingetokea kama wangewasafisha al-Shabaab kutoka Kismayu mapema. Kuiteka Kismayu kungefanyika mapema zaidi. Ingekuwa operesheni ya ghafla ya kijeshi na waasi kuondoka katika ushoroba kuelekea Kismayo. Kungekuwa na upinzani mdogo kutoka kwa adui. Lakini sasa tumewazingira al-Shabaab ili kuwakimbizia Kismayu. Kikundi cha watu kilichochanganyikiwa kama hiki kinahitaji jeshi lenye mafunzo maalumu na zana nyepesi ili kukifukuza kikundi kilichochanganyikiwa kama hiki. Kwa kweli kwa kila askari mmoja aliyechanganyikiwa wanahitaji askari 25 kumtoa ndani ya nyumba yake na pengine kusababisha kifo au vifo vya watu. Ikiwa Jeshi la Kenya nchini Somalia lingeanza kampeni ya kuiteka Kismayo, tungepelekea al-Shabaab kuyeyuka katika misitu mikali, na hapo ingekuwa rahisi kuwafuata huko msituni na kuwakamata bila ya kuhatarisha maisha. Lakini sasa hali iko tofauti kabisa. Itaigharimu Serikali ya Kenya pesa nyingi na nyenzo za kibinadamu ambazo zingeweza kutumika pahali pengine.

  • Daniel Githinji
    June 4, 2012 @ 08:31:03AM

    Punda anayekata roho hupiga mateke kwa sana na kile tunachokiona katika siku za karibuni ni matokeo yale yale. Wakenya wasipotee imani na vikosi vyetu. Tunakwenda kuwaombea bila ya kujali chochote na pia tutashughulikia usalama wetu sehemu nyingine. Mungu Ibariki Kenya.

  • SORE GEORGE LIGABO
    June 4, 2012 @ 07:21:27AM

    KAZI NZURI YA JESHI LA KENYA. WAENDELEE NA MOYO HUO HUO KWA SABABU AMANI NI KITU MUHIMU SANA KATIKA ENEO HILO.

  • Lothar
    June 4, 2012 @ 07:17:43AM

    Hongera askarI wema nyote. Muangamizeni adui moja kwa moja.

  • kithinji Godfrey
    June 4, 2012 @ 07:15:32AM

    Wenye silaha zaidi watashinda na wale wenye ukweli watashinda, lakini moto utamwendea yule yule anayetenda maovu.

  • abel ojwang'
    June 4, 2012 @ 05:05:24AM

    Hongera AMISOM, hakuwezi kuwa na amani kukiwa na al-Shabaab nchini Somalia. Kwa hivyo ninaiomba AMISOM kuendelea ili tuweze kuwa na serikali nchini Somalia.

  • catherene mutua
    June 4, 2012 @ 04:04:56AM

    Hongera vikosi vya ulinzi vinavyofanyakazi Somalia. Juhudi zenu hazitakuwa bure. "Vita ni vya Bwana lakini mafanikio ni yenu", na ikiwa Mungu yuko pamoja nanyi, al-Shabaab ni nani wao wa kuwa dhidi yenu? Ninamuomba Mungu awape busara za kutosha na nguvu zakufikia lengo. Al-Shabaab walishindwa kitambo, walifikia hadi ya kuvua sare zao na kusaini kushindwa kabisa. "MWISHO WA ENZI YA AL-SHABAAB". Shukurani kwa Mwenye Enzi Mungu ambako nguvu zetu zinatoka, ametufikisha mbali hadi huku.

  • Bernice Kagame
    June 4, 2012 @ 03:40:01AM

    Hii inafurahisha kuwaona watu wa Somalia kuwa na amani. Kitawezaje kikundi kidogo kuichafua nchi. Hawa wanapaswa kusafishwa moja kwa moja. Hawana imani kwa watu wengine, ni wachoyo. Wasafisheni. Waacheni wale majani. Furaha Furaha kwa KDF. Hongera Somalia. Hongera Wakenya. Bernice Kageme.

  • Abdirashid
    June 4, 2012 @ 03:36:46AM

    Kitu pekee tulikuwa tunataka ni amani itawale, lakini UA isiwamalize raia wasio na hatia kwa kisingizio cha kupambana na al-Shabaab. Ujumbe wangu kwa UA ni kuwa wawasafishe katika majengo ya maficho yao na kuwapeleka mbele ya sheria.

  • KARANJOZ
    June 3, 2012 @ 05:11:28PM

    AR-SHABAB WAKIFALIKI NAOMBA SERIKALI ITUJENGE BARARA TWENDI TURIME HUKO SOMARI NA TUNJENGE MAPROTI HUKO KAMA VIRE WAO WAMENJENGA HUKU KWETU E-SIRI.

  • KENITO
    June 3, 2012 @ 05:06:30PM

    MWENYEZI MUNGU ALIBARIKI JESHI LA KENYA KWA KAZI YAO NZURI SANA. NINAIPENDA NCHI YANGU YA KENYA.

  • james
    June 3, 2012 @ 03:37:00PM

    Nimeshangaa kuwa watu 13 hawakupenda bandiko hili. Hawa ni al-Shabaab? Kwa vyovyote vile, al-Shabaab waache kupigana vita hivi kwa sababu wanachofanya ni kuua wananchi wa Wasomalia tu wasio na hatia bila sababu yoyote. Al-Shabaab wanaendelea kudai kuwa wamerejea nyuma kutoka miji iliyochukuliwa na majeshi ya AMISOM. Huko ni kushindwa, iwe kurudi nyuma au kwa jina lolote wanalotaka kuliita, ni kushindwa na wameshashindwa!

  • GITHINJI
    June 3, 2012 @ 03:16:14PM

    NI UWEZO WA MUNGU.

  • J. Njiru
    June 3, 2012 @ 02:39:27PM

    Ni ushahidi wa uwezo wa Mungu dhidi ya waovu.

  • MARANGA OSORO DENIS
    June 3, 2012 @ 09:50:40AM

    Hayo ni mateke ya mwisho kwa farasi anayekata roho. Kuondoka kwao Afgoye ni ishara ya wazi ya kushindwa. Tunakuja Kismayo, tusubirini au jisalimisheni kwa amani. Hongera AMISOM.

  • WAMPS
    June 2, 2012 @ 12:46:46PM

    KAZI NZURI, ENDELEENI.

  • frederick mutua
    June 2, 2012 @ 10:14:50AM

    Watu hawa wanahitaji elimu nyingi na sala kwa ajili yao ili wajielewe wenyewe na kuishi kama binadamu. Ninatoa wito kwa ulimwengu kuwasaidia watu wa Somalia katika elimu na amani.

  • MUUYI
    June 2, 2012 @ 10:05:05AM

    Ndiyo, tunahitaji amani katika Afrika ya Mashariki

  • ELIZABETH MUTHEU MUTUKU
    June 2, 2012 @ 08:42:55AM

    AL-SHABAAB, HAMNA KITU CHA KUFANYA? REJEENI KATIKA AKILI ZENU, MUNGU HAKUWAUMBI ILI MUWE WAUWAJI. ANA MIPANGO MIZURI KWA AJILI YA MAISHA YENU. TAFADHALENI MUSIWAUE WAKENYA. KUMBUKENI MNAPASWA KUSALIMU AMRI AU MTAUONA UFALME WA SHETANI. KUMBUKENI NYINYI AL-SHABAAB NI WATOTO WA SHETANI NA BABA YENU NI MKOSAJI TU.

  • Appolo Alluma
    June 2, 2012 @ 08:06:24AM

    Hongera AMISOM, endelezeni kuweka shinikizo.

  • paul nginya
    June 2, 2012 @ 07:15:39AM

    Hongera kwa askari wetu wenye juhudi na ndio maana natamani ningekuwa mmoja wao.

  • Al-Xaq
    June 2, 2012 @ 01:23:27AM

    Nyote mnakosea ukweli kwa hivyo njooni muonje ukweli, kwa vile Somalia tunavyofaidi mazingira ya amani...bila ya milio ya bunduki kutoka kwa Harakat Al-Mujahidini Al-Shabaab sasa Afgoye na miji mengine ambayo ilivamiwa na majeshi ya kikoloni iliyokumbwa na uporaji, ubakaji na mauaji ya watu wasio na hatia hasa wanawake na watoto. Mmeshawahi kusikia al-Shabaab wamembaka msichana? Hapana, mmeshawahi kusikia al-Shabaab wamepora mali? Hapana, lakini wakati askari wa kukodiwa wa Marekani walipokuja mjini raia wengi waliteseka kutokana na kufedheheshwa, kwa wajinga wale na kutambia wao ni wataalamu. Sio wataalamu, hawajui chochote kuhusu Somalia. Al-Shabaab walipata ushindi kwa vile walifanikiwa katika nyoyo za jamii ya Kiislamu ya Somalia bila ya kujali kama walipoteza miji. Cha muhimu ni nani alibakia kwa ajili ya miji ile. Ni kwa ajili ya watumwa wa Uganda na majeshi ya Burundi (askari wa kukodiwa) au al-Shabaab (Wasomalia)?

  • Stevo
    June 1, 2012 @ 03:43:24PM

    Watu hawa ni mashetani. Wasomali wengi wanateseka nchini Kenya na katika makambi mengine kwa sababu ya uroho wa al-Shabaab...au vyovyote wanavyojiita wenyewe...

  • yaasir
    June 1, 2012 @ 01:39:50PM

    Mimi ni Msomali na mzalendo ninayependa nchi yangu na watu wake. Siwezi kuishi nje ya nchi yangu, Somalia. Ningependa kumwomba Mungu arejeshe amani na utulivu katika nchi yangu na kutupa ahueni ya majangwa ambayo yanatokea nchini mwangu. Mzozo wa Somalia unahitaji wanasiasa wenye uzoefu ambao wanaoweza kujenga mfumo wa utawala ambao utatatua mzozo huu wa muda mrefu. Asanteni sana nyote.

  • JAMES KARANJA
    June 1, 2012 @ 11:02:49AM

    Al-Shabaab, pumzikeni kwa amani. karibuni Somalia itakombolewa kikamilifu. Mjisalimishe tu. Kama hamuwezi kuwapiga, unganeni nao.

  • Gerald
    June 1, 2012 @ 07:46:49AM

    Kwa Menyezi Mungu kila kitu kinawezekana...muwekeni mbele Mwenyezi Mungu katika kila kitu. Sisi si washindi lakini zaidi ya hayo yeye anakwenda kabla yetu katika njia ya mhimili wa moto.

  • jeremiah
    June 1, 2012 @ 05:56:46AM

    Waelewe kuwa wakati wao umekwisha.

  • Patrick
    June 1, 2012 @ 05:32:03AM

    Hongera kaka na majirani zangu huko Somalia, tutaomba pamoja.

  • Albanus Mutie
    May 31, 2012 @ 01:48:31PM

    Ni hatua mbele kuelekea kupatikana kwa amani ya kudumu katika eneo hili. Waislamu wenye itikadi kali wamekuwa wakiitumia isivyopaswa dini ya Kiislamu ili kusababisha maafa na wamewalemaza wengi. Tuwaunge mkono watu wote wa AMISOM hasa wa KDF yetu wenyewe. Ninawaungeni mkono.

  • sammy Ndirangu
    May 31, 2012 @ 09:09:40AM

    Heko, Heko mashujaa wetu. Ninawapogeza, fanyeni mnavyoweza. Tunasali kwa ajili yenu. Endeleeni, Endeleeni, Endeleeni----

  • ndambuki
    May 31, 2012 @ 07:16:04AM

    Al-Shaabab lazima wajisalimisha tu kwa sababu watashindwa vita moja kwa moja na wengi watakufa ikiwa ni pamoja na wananchi wasio na hatia. Ni nini malengo yenu Al-Shaabab? Je, hamjui kuwa Mwenyezi Mungu haruhusu kumwaga damu isiyo na hatia? AMISOM na vikosi vingine lazima vitawapondeni bila ya huruma wale ambao hawajisalimishi.

  • levy ogechi
    May 31, 2012 @ 05:45:18AM

    Hizi habari mpya ni nzuri. Endeleeni!

  • Benson Waweru
    May 31, 2012 @ 03:27:22AM

    Wasafisheni. Tunawakaribisha Somalia kwa moyo safi katika nchi za Afrika ya Mashariki kwa sababu itakuwa chanzo cha malisho ya majani kwa wanyama kwa nchi wanachama wa Afrika ya Mashariki. Hongera kwa watu wetu mashujaa ambao wanawasakama al-Shabaab.

  • VITALIS
    May 31, 2012 @ 02:26:56AM

    SAWA, SIO MBAYA

  • maarshaal
    May 30, 2012 @ 02:03:36PM

    Natarajia kuwa al-Shabaab watatolewa nje ya maeneo wanayoyadhibiti ndani ya Somalia. Mungu akipenda. Ikiwa mmoja yeyote miongoni mwao atakamatwa, basi aadhibiwe kwa namna ile ile waliyokuwa wakiwaadhibu wengine kwa sababu wao ndio walioanza kwenda kinyume na njia ya Mungu. Ninawatakia nakama iwashukie al-Shabaab kwa vile wamefanya ukiukaji mubwa wa haki za binadamu dhidi ya Wasomali.

  • GERALD
    May 30, 2012 @ 06:39:32AM

    WAUWENI WANYAMA HAO WOTE!!!!!!!!!

  • [email protected]
    May 30, 2012 @ 05:04:34AM

    Muda mkubwa wamekuwa wakizuia barabara nyingi lakini sasa na wao ni waathirika wa vizuizi vya barabarani. KKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKK. Hata Rais Sharif aliepukana kifo kutokana na mwenye sharafa. KKKKKKKKKKKKK.

  • maturi geoffrey
    May 30, 2012 @ 04:27:53AM

    Hiyo ni nzuri kwa watu kufurahia hali ya amani ... bila ya milio ya bunduki ... Bwana ibariki nchi ....

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo