Yemeni yapokea idadi ya kuvunja rekodi ya wakimbizi kutoka Pembe ya Afrika

Faisal Darem huko Sanaa alichangia katika ripoti hii

Mei 24, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Idadi ya kuvunja rekodi wahamiaji wanaokimbia ukame, hali mbaya ya uchumi na hali ya usalama isiyo na utulivu katika Pembe ya Afrika wanafikia Yemeni, wakiweka mzigo mkubwa katika nchi ambayo inasongwa na matatizo yake yenyewe ya wakimbizi wa ndani.

  • Wakimbizi wa Somalia wakishuka kwenye gari katika kituo cha mapokezi cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huko Yemeni katika mji wa Ahwar, kilometa 230 kutoka bandari ya Aden ya Bahari Nyekundu, mwaka 2008. Miaka michache iliyopita, wakimbizi 750,000 na wahamiaji walifika Yemeni.[Khaled Fazaa/AFP]

    Wakimbizi wa Somalia wakishuka kwenye gari katika kituo cha mapokezi cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huko Yemeni katika mji wa Ahwar, kilometa 230 kutoka bandari ya Aden ya Bahari Nyekundu, mwaka 2008. Miaka michache iliyopita, wakimbizi 750,000 na wahamiaji walifika Yemeni.[Khaled Fazaa/AFP]

  • Wakimbizi wa Kisomali wamekaa Yemeni zaidi ya miongo miwili iliyopita. Wengi wameanzisha biashara kama mgahawa hiyo huko Sanaa. [Faisal Darem/Sabahi]

    Wakimbizi wa Kisomali wamekaa Yemeni zaidi ya miongo miwili iliyopita. Wengi wameanzisha biashara kama mgahawa hiyo huko Sanaa. [Faisal Darem/Sabahi]

Katika kipindi cha miezi minne iliyopita, watu 43,000 walisafiri kutoka Ethiopia na Somalia, ikilinganishwa na watu 30,000 kwa kipindi kilichofanana cha mwaka uliopita, kwa mujibu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Umoja wa Mataifa kwa wakimbizi (UNHCR) alisema hali hiyo inatokana na kuibuka kwa hali isiyo na usalama na usafirishaji watu katika kanda hiyo.

“Wale wote walioamua kufanya safari ya kuvuka wamejiweka wenyewe kwenye hatari kubwa na janga katika kila hatua ya safari yao,” msemaji wa UNHCR Andrej Mahecic aliwaambia waandishi wa habari huko Geneva tarehe 18 Mei. “Wanakumbana na viwango vya kutisha vya unyanyasaji na vurugu za wafanya magendo, pamoja na ukamataji wa kushtukiza na kuwekwa kizuizini, mipaka iliyofungwa na kulazimika kurudi, usafirishaji watu, ukosefu wa malazi, maji, chakula au msaada wa matibabu.”

“Wale wanaofanya safari hufika wakiwa wamechoka, wana sikia kiu, wana utapiamlo na hali ya mshtuko,” Mahecic alisema.

Ni hapo tarehe 2 Aprili tu wakimbizi wa Kisomali 2,144 na 1,147 wa Ethiopia waliwasili katika pwani za Yemeni, taarifa hizi ni kutokana na Kituo cha Habari cha Yemeni, shirika linaloendeshwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemeni.

Serikali ya Yemeni ilisema mwezi huu kwamba idadi ya wakimbizi wa Kisomali nchini Yemeni imefikia milioni 2 tangu kuanza kwa vita vya Wasomali mapema miaka ya 1990.

Yemeni yakumbwa na tatizo loa la watu wanaokimbia makazi yao

Zaidi ya uingiaji kwa wingi wa wakimbizi, Yemeni inakabiliwa na changamoto zake za kukosa makazi nchini. Kuna watu 470,000 ambao wameandikishwa kukosa makazi nchini Yemeni, pamoja na watu wa ziada wanaokadiriwa kuwa 95,000 ambao bado hawajaandikishwa, kwa mujibu wa UNHCR.

UNHCR mwaka huu iliomba Dola za Kimarekani milioni 60 kushughulikia mahitaji ya kibinadamu ya wakimbizi na watu waliokosa makazi nchini Yemeni. Hadi sasa, wakala walisema wamepokea moja ya tatu ya fedha hizo.

Waziri wa Mambo ya ndani wa Yemeni alieleza wasiwasi wake kuhusu uingiaji wa wakimbizi wanaokuja kutoka Pembe ya Afrika.

"Wakimbizi kutoka Somalia na Pembe ya Afrika wameipa changamoto Serikali ya Yemeni, hususan katika suala la usalama, kwani baadhi yao wanajiunga na makundi ya uhalifu au vikundi vya kutumia silaha ambavyo vinafanya vurugu dhidi ya serikali," Kanali Mohammed al-Qaidi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani, aliiambia Sabahi.

Viongozi wa Yemeni pia wanafikiria kwamba harakati ya al-Shabaab walioshirikiana na al-Qaeda wanatuma wapiganaji wa Somalia kujiunga na upiganaji wa al-Qaida dhidi ya jeshi. Mwezi Machi Wizara ya Mambo ya Ndani iliwalaumu al-Shabaab kuwapeleka wapiganaji 300 huko Yemeni.

Makamo Waziri wa Mambo ya Nje Ali Muthana Hassan alisema Yemeni inapokea wakimbizi wakati huohuo watu wake wamekosa makazi nchini kutokana na migogoro na ugomvi kati ya serikali na al-Qaeda katika baadhi ya majimbo.

"Idadi ya wakimbizi na wahamiaji ambao wamekuja Yemeni kwa miaka michache iliyopita imefikia 750,000, ambao wameibebesha mzigo nchi, ambayo inakabiliwa na hali ngumu ya uchumi na usalama hususan baada ya matukio ya mwaka jana," Hassan alisema katika mkutano wa kimataifa wa wizara kuhusu "Wakimbizi katika Dunia ya Kiislamu" uliofanyika tarehe 11-12 Mei huko Turkmenistan.

Hassan alisema Yemeni imejiunga na mkataba wa kimataifa na mikataba inayolinda hali ya wakimbizi, hususan Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1951 na Mkataba wa mwaka 1967 unaohusu Hali za Wakimbizi.

Wakimbizi wa Somali wakosa ari ya kurejea nyumbani

Wakimbizi wengi wanaoingia nchini Yemeni hawana hamu ya kurejea nyumbani katika siku za hivi karibuni, hivyo kuiongezea mzigo serikali ya Yemeni.

Hussain Abdi Mohammed, mwenye umri wa miaka 30, alikuja Yemeni kinyume cha sheria miaka minne iliyopita akikimbia vita na njaa nchini Somalia. Kwa sasa anafanya kazi katika mgahawa wa Somalia maeneo ya Safia katikati ya mji mkuu.

Alisema anaendeleza mawasiliano na familia yake iliyoko Somalia na anatamani angewaleta Yemeni kuungana nao. Aliiambia Sabahi anatamani kubakia nchini Yemeni hadi hali itakapoboresha nchini Somalia.

Bashir Omar pia alikuja Yemeni kinyume cha sheria na kuishi katika jimbo la Taiz. Hawezi kuongea Kiarabu vizuri na anawategemea Wasomali wenzake kumsaidia kukabiliana na kikwazo cha lugha.

Hata kama hawezi kutafuta ajira na anatakiwa kutegemea ujira wa mke wake anayefanya kazi za nyumbani ili kuwalisha watoto wao watatu, alisema kwamba anatamani kuishi Yemeni kwa maisha yake yote yaliyobaki.

Vivyo hivyo, Ismail Abd Haras, mwenye umri wa miaka 69, alikimbilia Yemeni miaka mitano iliyopita wakati familia yake yote ilipouawa isipokuwa watoto wake wawili ambao majaaliwa yao hajui chochote.

Haras hawezi kabisa kuongea Kiarabu na hana mahali pake mwenyewe. Ana ndoto za siku moja kuwapata watoto wake wawili wa kiume na kuishi maisha yake yote nchini Yemeni kwa sababu alisema kuna usalama na hakuna vurugu.

Wakimbizi ni changamoto ya maendeleo nchini Yemeni

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mchumi wa Yemeni Rafiq al-Qudsi, wakimbizi wanapatiwa elimu na huduma za afya katika majengo ya serikali bila ya malipo yoyote. Pia kuna shule maalumu kwa wakimbizi ambapo serikali inabeba gharama zote, kama vile mishahara ya walimu, utunzaji majengo na huduma.

Zaidi ya hayo, serikali imeweka vituo vya afya maalumu kwa wakimbizi, ambao pia wanaweza kupata huduma kutoka vituo vingine vya serikali. Al-Qudsi anasema idadi kubwa ya wakimbizi imesababisha gharama za hali ya juu kwa uchumi wa Yemen.

Taha al-Fasil, mshauri kwa Wizara ya Viwanda na Biashara, alisema wakimbizi wamekuwa changamoto kwa maendeleo nchini Yemeni. “Wanashindana na raia katika kupata huduma, wakati wanakuwa na athari hasi kwa biashara na mzigo kwa nguvukazi ya Yemen katika kuunguza mishahara,” alisema.

"Urefu wa mwambao wa Yemen, ikijumuisha mfumo mbaya wa usimamizi, inafanya Yemeni kuwa kitovu cha wakimbizi wanaokuja kutoka Pembe ya Afrika, hasa kutoka Somalia,” alisema ali-Faisal.

Profesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Sanaa Mohammed al-Maytami aliiambia Sabahi kuwa misaada ya kigeni kwa ini kidogo sana, ukilinganisha na dhamana inazobeba. Mgao wa misaada kwa raia wa Yemeni unakadiriwa kuwa dola 12 kwa mwaka, wakati mtu mmoja anayeishi Afghanistan anapata dola 118 kwa mwaka, alisema.

Jumuiya ya kimataifa [ina wajibu] wa kuisaidia Yemeni, ambayo inakabiliwa na changamoto kubwa, hasa katika kipindi hiki,” alisema.

”Yemeni ina upungufu wa rasilimali, kwa hivyo wakimbizi wanatoa shinikizo kwa wakazi wenyeji ambao wanazihitaji sana rasilimali hizo,” alisema al-Maytami. “Baadhi ya mashirika ya kimataifa hutoa sadaka kwa wakimbizi moja kwa moja na sio kwa serikali, ambayo ingepaswa kusaidiwa kwa ukarimu na jumuiya ya kimataifa.”

Al-Maytami alisema tafiti zinaonesha kuwa serikali ya Yemeni inatumia kiasi cha dola 2,300 kwa mwaka kwa kila mkimbizi. “Hiki ni kiwango sawa na inachotumia serikali kwa kila raia kwa ajili ya huduma za msingi kama vile afya, elimu na huduma nyingine,” alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(1)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Abdi Ahmed
    June 12, 2012 @ 06:48:46AM

    Watu wa Somalia wamehusika katika miongo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha mamilioni kukosa makazi, ambao wanakimbia vita. Hii imesababisha wakimbizi katika nchi jirani kama Kenya na Tanzania. Kuna njia mbalimbali ambazo serikali ya Somalia na nchi nyingine zinaweza kusaidia wakimbizi kujenga maisha yao tena. Serikali na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali yanaweza kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha kwamba wakimbizi wanapata mahali pa kuishi na chakula. Wakimbizi pia wanahitaji matibabu na huduma za kijamii katika kambi wanamoishi. Serikali hizi na mashirika mengine ya nje lazima yatoe ulinzi kwa wakimbizi katika kambi kwa sababu wanakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wapiganaji. Njia nyingine yenye faida sana ni kuwasaidia kujipatia maisha yao kwa kuwapatia kazi fulani ya kufanya. Kuna baadhi ya maeneo ya Somalia ambayo kwa kiasi zina utulivu na wakimbizi wanaotaka kurudi nyumbani lazima wasaidiwe kusafiri salama kurudi Somalia ambapo wanaweza kuanza kujenga upya maisha yao.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo