Mei 23, 2012
Riadha Kenya (AK), chombo kinachoshughulika na riadha nchini, kinapanga kuandaa mfululizo wa mashindano ya mbio ndefu mapema mwaka ujao ili kuibua vipaji vilivyojificha katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki.
Mwenyekiti wa AK Isaiah Kiplagat alisema hii ni mara ya kwanza kwa tukio kubwa la riadha kama hili kuanzishwa mkoani. Alisema AK inataka kuinua mwamko wa riadha katika mkoa na inatumai kuwa baadhi ya wanariadha wa juu watakuja kukuza mchezo huo.
Ili kuusaidia mkoa kufikia uwezo wake kamili, AK imewapa mafunzo makocha 15, Kiplagat alisema.
“Tumekuwa tukituma timu za Kenya katika mashindano ya kimataifa, lakini inavunja moyo kuwa mwaka baada ya mwaka, hakuna yeyote kutoka mkoa huu anayeshiriki – hata katika mashindano ya kitaifa,” aliiambia Sabahi.
Kiplagat alisema mpaka sasa, imekuwa vigumu kupata wafadhili wa michezo katika eneo. Mashirika kadhaa ikiwa ni pamoja na Benki ya Taifa ya Kenya, Benki ya Biashara ya Kenya na Safaricom, zimekubali kufadhili mfululizo wa mashindano katika mkoa, tukio kubwa katika hayo litafanyika Wajir.
Dickens Olewe, mchambuzi wa masuala ya michezo wa Nairobi, aliiambia Sabahi kuwa wafadhili wenye uwezo mkubwa hapo mwanzo walikuwa wanasita kuwekeza katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki kwa sababu ya marejesho hasi ya fedha zao walizotarajia.
Makampuni binafsi, yanayofadhili matukio kama hayo ili kutangaza biashara zao na kuufikia umma wao, waligundua kuwa mkoa hauvutii kifedha, na hivyo kuathiri fursa za matukio ya michezo kufanyika katika mkoa, alisema.
"Katika miaka ya nyuma, watu waliepuka kuwekezaji wa mali na kufanya biashara katika mkoa huu kwa sababu ya kukosekana usalama,” alisema. “Kwa sasa, mkoa uko salama kabisa na tunashuhudia mashirika yakijishughulisha katika njia kadhaa za kuwajibika katika jamii, kama vile kufadhili elimu, kuunga mkono sekta ya afya na sasa michezo.”
“Michezo inaweza kuwa kitu kikubwa kitakachofuatwa katika mkoa na makampuni yanajua yanaweza kupata faida kutokana nayo,” Olewe alisema.
Riadha Kenya inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi milioni 30 (dola za Kimarekani 375,000) katika mashindano yatakayodumu kwa mwezi mmoja. Kiplagat alisema zawadi zitatolewa katika mbio za mita 800, mita 1,500, mita 5,000 na mita 10,000.
Kiplagat alisema wakazi wengi wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki walikuwa wanaihusisha riadha na Mkoa wa Rift Valley kwa sababu wanariadha wao wanang’ara katika matukio ya michezo ya kitaifa na kimataifa.
Lakini hali hiyo ilianza kubadilika kwa kasi mwezi Oktoba mwaka jana pale Muingereza mwenye asili ya Somalia, Mo Farah, alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya mita 5,000 na medali ya fedha katika mbio za mita 10,000 katika Mashindano ya Riadha ya Dunia huko Daegu, Korea Kusini. Kiplagat alisema Farah mara nyingi hufanya mazoezi nchini Kenya na mafanikio yake yanaweza kutumiwa katika kukuza michezo katika mkoa.
Ammey Abdi Salah, mwenye umri wa miaka 25 na mkazi wa Garissa, alisema kuwa hakuwahi kuifikiria michezo ya riadha mpaka mwaka jana. Hakukuwa na watu wa michezo alioweza kuwahusisha nayo na hakukuwa na utiaji moyo wowote katika uwanja huo, alisema.
“Sikufikiria daima kuwa Somalia inaweza kushinda dhahabu,” Salah, Mkenya mwenye asili ya Somalia aliiambia Sabahi. Hali hii imebadilika baada ya ushindi wa Farah. “Nimekuwa nikifanya mazoezi katika viwanja vya kukimbia tangu mwezi wa Januari na marafiki zangu, ambao miaka ya nyuma walikuwa wanacheka wazo hilo. Tuligundua kuwa tunaweza kuendesha maisha kwa kukimbia,” alisema. “Nimetiwa moyo.”
Mjumbe wa AK katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki Hassan Omar Abdullahi alisema idadi kubwa ya wakazi wa mkoa ni Wakenya wenye asili ya Somalia, ambao wana mahusiano na Wasomali ulimwenguni kote, ambao mafanikio yao yanaweza kuwa ushawishi chanya katika eneo hilo.
“Katika miaka mitatu au mitano ijayo, ni imani yetu kuwa riadha itakubalika katika eneo hili,” alisema.
Abdullahi alisema kuwa kukosekana kwa nyenzo zinazofaa kufundishia na kiwango cha juu cha joto vinaweza kuwa ni changamoto, huu ni wakati muafaka wa kuamsha ari ya michezo katika eneo hili, linalojulikana kwa watu wake wazima na wanaovumilia.
John Muindi, afisa katika Wizara ya Masuala ya Vijana na Michezo, alisema serikali inaichukulia michezo kwa umakini kama njia ya kujipatia riziki na fahari kwa raia.
Alisema michezo ni chaguo zuri la kukuza uchumi katika eneo. Ambao unategemea sana ufugaji wa wanyama, ambao mara nyingi huathirika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na maradhi. Mkoa umeshuhudia uti wa mgongo wa uchumi wake, mifugo, kufa kutokana na ukame wa mara kwa mara, na wakazi lazima wajishughulishe na michezo kama njia nyingine ya kujipatia riziki, Muindi alisema.
“Inasikitisha kuwa mkoa umechelewa kuigundua michezo, lakini itafanya kila iwezalo kuwafikia wengine, hasa katika Mikoa ya Rift Valley na Nyanza, ambayo imepiga hatua kubwa katika michezo,” aliiambia Sabahi.
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Mimi kwa kweli ninathamini juhudi zao kwa kutumia vyema vipaji vya watu wanaodhihakiwa kama wageni, al-Shabab (kundi la kigaidi lililopo Somalia) na serikali yao wenyewe na wananchi wengine kutokana na maeneo yao kijiografia na uhusiano wao wa kikabila na Somalia. Niaminini kwa vile mimi ni kijana kutoka eneo hili, kuna uwezekano mkubwa wa kuwatumia vyema vijana kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na kwa nchi pia. Vile vile ninawaomba wakurugenzi wasiwe na kikomo kwa msaada wao katika riadha tu, wakati mpira wa miguu na maigizo ni miongoni mwa maeneo mengine yanayopaswa kuwezeshwa. Asanteni.
Mnatarajia vipi eneo litafanya vizuri wakati masomo ya elimu ya mazoezi ya viungo ni masomo tu katika ratiba ya NEP? Na ni tangu lini wanariadha wa Garissa wanapewa mafunzo au kuteuliwa katika mashindano ya Wajir kutoka tarehe 28 Mei 2012.