Mei 22, 2012
Kuongezeka kwa kodi za uagizaji na bei za mafuta huko Somaliland kunafikisha hadi wateja, wakati serikali ya eneo hilo inasema inajaribu kupunguza mzigo kwa kukabiliana na ushindani wa soko.
Mkurugenzi wa biashara katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Utalii Aden Elmi Ahmed alisema bei za mafuta zimeongezeka kutokana na migogoro katika baadhi ya sehemu ulimwenguni na vitendo vya maharamia katika eneo.
“Hata hivyo, kuna vikwazo vingi [ambavyo vimepelekea kuongezeka kwa bei za mafuta], tunaamini kuwa wanaomiliki biashara wataongeza faida ya ziada kwa bei, ambazo zinakuwa mzigo kwa wateja,” Ahmed aliiambia Sabahi. “Wamiliki wa biashara wanaruhusiwa kufaidika kutokana na ongezeko la bei za mafuta, lakini tunawaomba wasiibebeshe jamii mzigo mkubwa.”
Akielezea kupanda kwa bei za mafuta, Ahmed alisema kuwa wizara yake inafuata uchumi wa soko huru na inaruhusu ushindani wa kibiashara. "Tunamruhusu kila mtu ambaye anaweza kuagiza mafuta kutoka kokote ulimwenguni,” alisema.
Ahmed alisema serikali inajaribu kushughulikia athari za ongezeko la bei za mafuta kwa wateja. “Ikiwa bei za mafuta hazitapungua, serikali itapaswa kuangalia kodi zilizowekwa katika mafuta yaliyoagizwa,” aliiambia Sabahi.
Abdiaziz Gahnug, anayemiliki kituo cha mafuta huko Hargeisa, aliiambia Sabahi wiki iliyopita kuwa bei ya diseli ilikuwa dola 215 kwa pipa, ikilinganishwa na dola 167 mwezi Machi, na pipa la petrol ni dola 209, ikilinganishwa na dola 197 mwezi Machi.
“Bei ya mafuta imepanda kwa kiwango cha kihistoria kilichowekwa mwaka 2007, na bei zake za soko ziko karibu na bei za siku hizo,” alisema Hassan Mohamed Egeh, meneja wa Red Sea Petroleum Company.
Egeh alielezea kupanda kwa gharama kunachangiwa na uharamia, machafuko nchini Libya, vikwazo vilivyowekewa Irani, kutokuwepo kwa utulivu huko Bahrain na uzalishaji mdogo huko Iraki.
Serikali ya Somaliland mwaka jana iliongeza kodi inayokusanywa kutoka mafuta yanayoagizwa kutoka nchi za Ghuba. Serikali inatoza kodi ya kiasi cha dola 12.18 kwa pipa la diseli, kutoka dola 11.60 mwaka 2010, na kodi kwa pipa la petroli kwa dola 15.60, ikilinganishwa na dola 14, Egeh alisema.
Katika mwezi uliopita, Red Sea Petroleum Company, Hass Petroleum na SOM Petroleum zilinunua meli ili kuepukana na gharama kubwa za kukodi meli kutoka makampuni ya kigeni, Egeh alisema.
“Kampuni nyingi za petrol za Somaliland zilinunua meli zao baada ya kukabiliwa na vikwazo vya kukodi meli kutokana na hofu ya kutekwa nyara na maharamia. Matatizo ya kukodi meli za kigeni sasa yameondoka na tunajisikia kupata nafuu,” Egeh alisema, na kuongoza kuwa kampuni yake ilinunua meli mbili.
“Kampuni zina uwezo wa kuagiza mafuta kutoka popote wanapotaka kwa sababu wanazo meli zao wenyewe na hawana hofu ya maharamia, au kukodi meli za kigeni ambazo zinaweka aina fulani ya masharti,” Egeh alisema.
Kupanda kwa bei za mafuta pia kunaathiri gharama za maisha kwa wateja.
Daud Ibrahim Ali, mwenye umri wa miaka 27 na dereva wa basi huko Hargeisa, aliiambia Sabahi kuwa anasafirisha watu 270 mpaka 300 kwenda kazini kila siku, pamoja na wanafunzi 40 anaowapeleka shule na kuwarejesha makwao.
Ali alisema mabasi yana wajibu mkubwa kwa watu wa Hargeisa, ambao mara nyingi wanahitaji mfumo wa usafirishaji wa umma kwenda katika shughuli zao za maisha za kila siku.
Hussein Ahmed Mohamoud, mwenyekiti wa jumuiya ya wamiliki wa mabasi huko Hargeisa ambayo inawakilisha mabasi 800 binafsi, alisema kupanda kwa bei za mafuta zimeathiri sana shughuli za kila siku za mabasi.
Alisema serikali inapaswa kupunguza kodi za uagizaji mafuta ili kupunguza gharama za usafirishaji kwa wananchi.
Kikwazo kikubwa kinachotukabili sasa ni ongezeko la bei za mafuta, kwa hivyo tuna hali mbili akilini mwetu – ama kuacha kuendesha au kuongeza nauli za mabasi,” Mohamoud aliiambia Sabahi.
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Tuna mfumko mkubwa wa bei nchini na hii inaathiri mahitaji ya kujikimu. Uchumi unaanguka, tunapaswa kufanya chochote, uvumbuzi ni lazima.
Sio bei ya mafuta tu iliyopanda bali kwa jumla kuna mfumko wa bei katika uchumi nchini. Ikiwa serikali inashindwa kufanya lolote kuhusu mfumko wa bei, hili litakuwa na athari hasi kwa uchumi nchini ambao mwanzo ulikuwa dhaifu.