Kiongozi wa Al-Shabaab awaomba msamaha Wasomali

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Mei 22, 2012

  • 112 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Ali Mohamed Hussein, aliyekuwa kiongozi wa al-Shabaab katika eneo la Banadir, amesema wiki iliyopita kwamba yuko tayari kulikana kundi hilo na kujitenga nalo, hatua ambayo wachambuzi wanatarajia itazidisha mgawanyiko ndani ya kundi hilo.

  • Aliyekuwa kamanda wa al-Shabaab Mohamed Sheikh Abdullahi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mwaka 2009 kuhusiana na sababu zilizompelekea kujiengua kutoka kundi hilo. Matukio ya hivi karibuni ya kushindwa kwa kundi hilo yamepelekea baadhi ya viongozi wa al-Shabaab kuliacha kundi hilo. [Yasuyoshi Chiba/AFP]

    Aliyekuwa kamanda wa al-Shabaab Mohamed Sheikh Abdullahi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mwaka 2009 kuhusiana na sababu zilizompelekea kujiengua kutoka kundi hilo. Matukio ya hivi karibuni ya kushindwa kwa kundi hilo yamepelekea baadhi ya viongozi wa al-Shabaab kuliacha kundi hilo. [Yasuyoshi Chiba/AFP]

Hussein amewaomba msamaha wakaazi wa Mogadishu na watu wote wa Somalia ambao wameathirika na matendo ya al-Shabaab wakati wa uongozi wake, imeripoti Redio Mogadishu inayoendeshwa na serikali hapo Alhamisi (tarehe 17 Mei).

Hussein, ambae bado yuko mafichoni na hajajiunga rasmi na serikali ya Somalia, amesema angependa wananchi wampatie taarifa kwa wale aliowakosa ili kuweza kuwakabili na kuwaomba msamaha.

"Kama ningekuwa na fursa, ningeliukabili umma na kuilaani al-Shabaab hadharani,” amesema. "Ningeweza pia kuwaomba watu msamaha. Nipo tayari kufanya hivyo kama nitapata fursa ya kuomba radhi.”

Maoni ya Hussein yanakuja kukiwa na mgogoro wa kutoaminiana miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab kulikosababishwa na shinikizo kubwa la serikali ya Somalia na vikosi vya AMISOM, wachambuzi wanasema.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Muhyadin Ahmed amesema tamko la Hussein ni "maendeleo yasiyotarajiwa" katika historia ya al-Shabaab. “Hii ni mara ya kwanza ambapo kiongozi mwandamizi wa al-Shabaab ameeleza kuwa tayari kwake kuuomba radhi umma na kutaka kusamehewa,” Ahmed aliiambia Sabahi.

Ameongeza kwa kusema kwamba Hussein kuwa tayari kujiondoa kutoka al-Shabaab kunaashiria kuchukizwa kwake na mashambulizi ya "kishenzi” yanayofanywa na kundi hilo dhidi ya raia.

"Tamko la Hussein linaweza kuwa ishara kwamba [Hussein] anataka kuliacha mkono kundi hilo na kujisalimisha kwa serikali, akiitumia fursa ya msamaha uliotolewa kwa wanamgambo wa al-Shabaab ambao kwa hiari zao watajisalimisha,” alisema Ahmed. “Kama Hussein ataamua kujiunga na mpango wa amani na kuachana na unyanyasaji, hiyo itakuwa ni hatua ya kishujaa itakayohamasisha viongozi wengine wa al-Shabaab, hasa wale wenye msimamo wa wastani, kufuata njia hii kabla muda haujawapita.”

Tangu serikali ya Somalia kutangaza msamaha, wapiganaji kadhaa wa al-Shabaab wamejiengua na kujisalimisha kwa maafisa wa serikali.

Ahmed ameeleza kwamba kundi la al-Shabaab linakaribia hatua ya kupigana wenyewe kwa wenyewe kutokana na kutoelewana kwa viongozi wao, hasa baina ya wale wenye msimamo mkali na wale wa wastani.

"Kiongozi wa al-Shabaab [Mukhtar Abu al-Zubayr, ambae pia anajulikana kama] Ahmed Godane atapigana kufa kupona ili kuwakandamiza wapinzani wake na kuepusha kusambaratika kwa safu kuu ya uongozi wa kundi hilo,” alisema Ahmed. “ Kwa viongozi wenye msimamo wa kati miongoni mwa wapinzani wake, wao watapigana ili kujitenga na kuunda kundi jipya au kujiunga na serikali.”

Ahmed amesema kupigwa marufuku kwa vyama vya siasa kulikotangazwa na Godane hapo Machi katika maeneo yaliyo chini ya usimamizi wake kumewakasirisha viongozi wa kundi hilo kama Sheikh Hassan Dahir Aweys na Sheikh Mukhtar Robow, anayejulikana pia kwa jina la Abu Mansur.

Osman Yusuf, mchambuzi wa masuala ya kisiasa anayefuatilia mwenendo wa al-Shabaab amesema pia kwamba al-Shabaab inakabiliwa na mpasuko mkubwa na kutoelewana miongoni mwa viongozi wake.

"Kumekuwa na dalili na maendeleo makubwa yanayoashiria kuongezeka kwa tofauti miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab,” aliiambia Sabahi.

Yusuf amesema ridhaa ya Hussein ya kujitoa katika kundi la al-Shabaab inaashiria kuwepo kwa mgogoro wa kutoaminiana miongoni mwa viongozi wa kundi hilo ambao wanaonekana kukataa tamaa kutokana na kushindwa kijeshi hivi karibuni kumetoa shinikizo kubwa kwa kikundi. "Tangu al-Shabaab kutangaza kujiunga na al-Qaeda hapo Februari tofauti zimeibuka kwa kiasi kikubwa na kupelekea kuwepo kwa mgogoro baina ya viongozi wa al-Shabaab,” alisema Yusuf.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na Profesa wa Chuo Kikuu Mohamed Hassa ameiambia Sabahi kuwa hali ya kutokuwepo kwa utulivu katika uongozi wa al-Shabaab kumekuwa dhahiri hasa baada ya mpiganaji wa kundi hilo asiye na asilia ya Kisomali Omar Hammami, anayejulikana pia kwa jina la Abu Mansour al-Amriki, aliyekamatwa mwezi wa Machi baada ya kutoa rikodi anayosikika akisema alihofia maisha yake kwa sababu za tofauti za kimikakati na kifikra miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab.

"Tofauti hizi zimechochewa na kiongozi mkuu wa al-Shabaab Sheikh Hassan Dahir Aweys kuwakosoa hadharani viongozi wengine. Kisha ikafuatia ukosoaji kutoka kwa Ali Mohamed Hussein, ambako kunaashiria kiwango cha mgogoro wa kutoaminiana miongoni mwa viongozi hao,” alisema Hassan. “Tunatarajia kuwaona viongozi wengi zaidi wa al-Shabaab kupingana na kamanda wao.”

Hassan ametoa wito kwa serikali ya mpito na wananchi kwa jumla Kufanya kazi pamoja na kuwakaribisha viongozi na wapiganaji walioihama al-Shabaab na ambao wako tayari kujisalimisha kwa serikali. Amesema watu hao wanahitaji kupatiwa ulinzi na hifadhi ili kuwahamasisha wengine kuachana na al-Shabaab na kujiunga na mpango wa amani.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 135)

Dislike_icon(24)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • tuuute calas dacasbeen
    September 11, 2012 @ 04:41:31AM

    Mtu huyu anafaa kusamehewa kwa sababu imetajwa katika Injili (Biblia): “Watu wote waliotenda dhambi na wakashindwa kuwafikia makafiri, Mungu aliwataka wawafikie. Mungu ni Mungu ambaye anasamehe na ikiwa damu yetu ni nyekundu kama damu, Mungu ana uwezo wa kuisafisha na kuifanya nyeupe kama barafu. Kwa vile Mungu husamehe kama hivyo, kwa nini binadamu hawamsamehe mtu huyu ambaye dhambi yake iko wazi?

  • wa kutisha
    June 26, 2012 @ 04:18:30AM

    Yule alie tayari kuachana na Al Shabab asamehewe kama anakubali kuachana kwa dhati na si janja tu baada ya kuona upepo wa mabadiliko hasa baada ya kuona dalili dhahiri za kushindwa vita

  • Simon Maina
    June 21, 2012 @ 06:51:48AM

    Inashangaza kuona kuwa Al-Shabaab wanathubutu kutoa maoni. MAGAIDI kamwe hawawatawali watu. Mimi ni Mkenya na nisingependa al-Shabaab kusikia hili. JESHI LA ULINZI LA KENYA halina nia mbaya na Somalia kwa hali yoyote. Tulikuja tu baada ya wapuuzi waliokuja na kufanya uhalifu katika nchi yetu. Ni hivyo tu. Tayari mmeanza kupoteza vita na kinachofuatia ni kuanguka kwa Kismayu kwa wazalendo wa kweli wa Somalia. Jirani yetu, ulisema Wakenya watateseka ndani ya Somalia. Kuanzia sasa hivi ni Wasomali wa kweli ambao wanashinda vita kwa msaada wa mapigano ya Wakenya. Endeleeni kupigana mpaka tutakapowatoa nje. Tunahitaji tu kukubalika kwa watu halisi wa Somalia ambao wanataka amani na utulivu kwa kuwaponda wapuuzi hawa. KWA NJIA YA MUNGU TUNAKUJA KULETA AMANI NCHINI SOMALIA!! Ifikapo mwezi wa Agosti, Waomali watajitawala wao wenyewe na kunywa maji juu ya makaburi ya magaidi. Na mnathubutu kutaja utakatifu wakati mnaendesha ugaidi? Jehanamu utakwenda.

  • clement ngetich
    June 21, 2012 @ 02:41:27AM

    Msameheeni.

  • Blasto maina
    June 20, 2012 @ 11:14:23PM

    Kaka na dada wa Somalia mmebakia katika taifa lililoshindwa kwa miaka mingi tangu utawala wa Said Barre. Ninawaombeeni ili kuuonesha ulimwengu kuwa sasa inatosha na mnahitaji serikali ili kuweza kwenda sambamba na ulimwengu wote.

  • Amat M. Omar
    June 20, 2012 @ 07:52:58PM

    Mwacheni ajitokeze mbele na kujisalimisha kwa viongozi ili kuomba msamaha kwa wale aliowakosea, ikiwa kweli yuko tayari kusamehewa au kushitakiwa.

  • samsoty
    June 20, 2012 @ 10:32:55AM

    Heshima, nyinyi ni wapiganaji kweli, kwa hivyo hao wanaojiita al-Shabaab lazima waachane na kikundi...furahia, tunawakaribisha katika jamii yetu ya amani.

  • sayfull islaam
    June 20, 2012 @ 10:32:46AM

    Habari gani nyote! Kwa fikira zangu kwanza tunahitaji amani na viongozi wa al-Shabaab wanataka wasamehewe kwa sababu ni watu wangu na ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka, siku moja Somalia itakuwa na amani – Mungu akipenda...

  • brian ogwenoh
    June 20, 2012 @ 07:44:01AM

    Nimefurahi sana kusikia sauti hiyo ya kujisalimisha, Hatimaye inatoa nafasi ndogo ya kuishi na kutumia nyezo zenye kiwango katika nchi zao.

  • Dominic
    June 20, 2012 @ 06:17:59AM

    Inakuwaje iwapo mtoto anakulenga jiwe na unajaribu kuficha kichwa chako mchangani na kujidai hakukutokea chochote? Wanaanza tena mchezo wao, wameshaua na kujeruhi wengi, kwa hiyo tuongozwe na jicho kwa jicho bila ya kuangalia nyuma.

  • DENNIS KIRIMI
    June 20, 2012 @ 05:11:54AM

    MSAMAHA UNAENDA PAMOJA NA HAKI. NAFIKIRI WASOMALI WOTE WENYE AKILI WATATABASAMU IKIWA BILA KICHEKO WALA KUMSAMEHE MARA TU ATAKAPOTIWA KITANZI. ANA HUZUNI KIASI GANI IKIWA HAWEZI KUWAREJESHA WALE WANANCHI WASIO NA HATIA WALIOTESEKA NA KUFA KATIKA UTAWALA WAKE. AMECHELEWA SANA KWA HATUA HIYO.

  • Christopher J. Ayo
    June 19, 2012 @ 09:06:49AM

    Siku zote Mungu ni Mungu wa vitu ambavyo ni vigumu kwa binadamu, nani anajua Mungu atafanya mambo mapya kwa Somalia. Tuendelee kusali kwa ajili yao. Mungu ni mwaminifu na atazigusa nyoyo za watu wote na siku moja Somalia itakuwa huru kutoka vita vya kila siku.

  • elvis nyakreal
    June 19, 2012 @ 02:14:48AM

    Ikiwa utaikosoa au la, huu ndio ukweli, al-Shabaab wanapigana vita wanavyoshindwa.

  • isaq
    June 16, 2012 @ 02:42:04PM

    Hata kama mtawalaani hamuwezi kufanya chochote kwa sababu al-Shabaab ni jeshi la Mungu. Nyinyi ni Wakristo na karibuni mtakufa, Mungu akipenda, nchi itakuwa yetu. Hatutawauliza Wakristo wa Kenya tunataka kufanya nini katika nchi yetu.

  • kemboi
    June 15, 2012 @ 01:32:45AM

    Hili halishawishi sana, angejisalimisha baadaye kulipa matendo yake.

  • Raypatrick
    June 14, 2012 @ 03:10:01AM

    Hussein apewe fursa ya kuomba radhi. Serikali ya Somalia ichukue muda na kumkaribisha Hussein ili kusaidia kuwachakaza al-Shabaab huko Kismayo.

  • MAHAMOUD
    June 12, 2012 @ 01:15:54PM

    Kwa maoni yangu, nadhani tahariri hii si sahihi na wala haikuandikwa na mwandishi wa habari. Ina sarufi mbaya na mpangilio mbaya wa maneno. Ningependa kuwaomba wale waliaondika makala hii kushauriana na waandishi wa habari wakati wa kuandika makala, ili kuvutia wasomaji. Asanteni wote. Imeandikwa na...........

  • ishwaaq.m.c
    June 12, 2012 @ 03:37:45AM

    Mimi ni msichana wa Somalia na ningependa kuwaomba mumsamehe mtu huyo kama aliomba msamaha.

  • Mwana wa millongo
    June 11, 2012 @ 07:44:04AM

    Ni kweli kwamba mtu anapofikia hatua ya kuomba msamaha inamaanisha amekiri, laini kwa hao sidhani kama wanahitaji kusamehewa hata mmoja, mimi binafsi hakuna kinachoniuma kama kuharibu jina la UISLAM hilo pekee halihitaji mtu asamehewe.

  • Al- Shabaab
    June 11, 2012 @ 01:35:04AM

    Hasira ya Mungu iwashukie hawa wasio Waislamu ambao wamekutana hapa kuwasema vibaya wapiganaji wa vita vitakatifu.

  • Abdalla
    June 10, 2012 @ 04:16:26PM

    Ni mwongo mkubwa huyu!

  • mohamed hassan
    June 9, 2012 @ 07:00:26PM

    Ni nafuu kubwa sana kwa raia wa Somalia. Mimi ni mtoto wa Somalia ambaye nchi yake imeharibiwa kwa vita vya kikabila na kisiasa visivyokwisha. Wakati wa makosa ya mahakama chini ya utawala wa raisi wa sasa wa Somalia, tulikuwa na ndoto kuwa amani imekuja kiasi kwamba maisha yetu yalikuwa huru lakini ndoto hizo zilikatishwa na serikali ya Ethiopia, na sasa al-Shabaab wamekuja kutaka samahani. Bora kuwasamehe na atakayechukua nafasi yake ashauriwe kutoa msamaha. Vita hivi si vya jihadi bali maslahi binafsi. Kugawangika kwao ni ushindi kwa raia wa Somalia. Ninamuomba Mwenyezi Mungu kuwa vita hivi vya Somalia vimalizike ili tupumzike kama raia wengine. Watu wengi wamekuwa wakimbizi katika nchi nyingine. Mwenyezi Mungu nitakabalie dua zangu.

  • SAMWEL.H
    June 9, 2012 @ 08:13:42AM

    NI MUDA MZURI KWA VIONGOZI WENGINE WA AL-SHABAAB KUOMBA RADHI KWA YOTE WALIYOFANYA HATA KAMA WATAKAA KTK GEREZA MAALUM KWA MREFU KWA KUOGOPA KUDHURIWA.HAKUNA ASIYESAMEHEWA HATA KM UMEFANYA MADHAMBI MAKUBWA,KINACHOHITAJIKA NI KUKIRI MADHAMBI YK. VITABU VYA DINI VINATUANGIZA.WASOMALI MWOMBENI MUNGU KWA AMANI YA TAIFA LENU,JIRANI ZENU TUNASIKITIKA KWA TAABU NA SHIDA MNAZOPATA.MUNGU ATAWASAIDIA.AMEN.

  • DENNIS
    June 8, 2012 @ 05:28:38AM

    Hiki ni kiwango cha juu cha unafiki. Kwa nini anataka kujisalimisha sasa? Kwa sababu amezingirwa? Kwa sababu hakuna njia ya kutorokea? Wakati alipokuwa anawaagiza vijana wake kuua, hakujua kwamba huo ulikuwa uhalifu ambao mwishoni angelipa? Uongozi wote wa kundi hili lazima kunyongwa na sio kusamehewa.Kwa nini wanajificha nyuma ya Uislam na kuua? Kwa nini wanatumia Uislamu huo huo ili kujiokoa? Kwa nini wanaogopa kifo leo na bado wanatumia mabomu ya kujitoa muhanga na kuwaua watoto wasio na hatia? Ni jamii hiyo hiyo waliyokuwa wakiiua ambayo leo itawaua wao. Ni siku ya adhabu kwa ajili ya uongozi wote wa kundi hili.

  • Future President
    June 8, 2012 @ 01:08:16AM

    Kijana huyu anazo habari nyingi ambazo idara ya intelijensia inazihitaji. Mbaneni, mpate habari baadaye mfanyeni alipe kwa maovu waliyosababisha yeye na watu wake dhidi ya binadamu.

  • benard
    June 7, 2012 @ 03:58:42AM

    Hatua nzuri, endeleeni!

  • elmi
    June 6, 2012 @ 10:50:34AM

    Haki haiwezi kupatikana katika ulimwengu huu. Kwa vyovyote vile, askari wa al-Shabaab hawana makosa bali viongozi wao lazima waadhibiwe kwa sababu nasikia askari hawa huwa wanapewa madawa vya kulevya. Hata kuwaadhibu viongozi wao ndio kutaleta haki kwa mtu mmoja na sio kwa kila mtu. Mungu akipenda tutaona matokeo yake.

  • Brenda Serem
    June 6, 2012 @ 02:43:44AM

    Haishawishi.

  • Bernard Odali Alema
    June 5, 2012 @ 04:49:36AM

    Somalia imeteseka na Mungu amesikia dua zao na amezijibu. Hussein aachane na kikundi hiki na kurejea kwa Mungu, atasamehewa.

  • محيي الدين الشيخ عبد الرحمن محمد
    June 5, 2012 @ 03:50:50AM

    Nafikiri wazo hili linaonesha wazi kuwa wameshashindwa kabisa. Na hii ndio sababu tunatakiwa tuwahurumie na kuwasamehe, kwa sababu msamaha unaweza kuwazuia na vitendo kama hivyo.

  • Alfa alfa
    June 5, 2012 @ 02:42:11AM

    Al-Shabaab? Hakuna kusamehewa daima…endeleeni kuwabana, tayari wameshasababisha mateso mengi kwa Afrika ya Mashariki na ya Kati yote. Hussein anajaribu kujifanya mjanja – jiulizeni wenyewe, si kwa sababu ya shinikizo wanalopata, angeomba msamaha? Hapana hata kidogo. Wanyongwe tu!

  • hussein
    June 5, 2012 @ 02:01:19AM

    Wale wanaojuta na kuomba msamaha wasamehewe ikiwa ni wakweli katika matendo yao lakini waliobakia waletwe mbele ya sheria.

  • Denis
    June 4, 2012 @ 12:56:20PM

    Mimi ni Mkristo na msamaha ni kitu muhimu sana hata hivyo, Yesu alisema, “utavuna ulichopanda.” Ikiwa ulipanda kifo utavuna vitisho, vipi aweze kuvuna amani? OmBeni msamaha na mtapata kutoka kwa watu na Mungu, lakini bado kwa njia yoyote ile utalazimika kulipa kutokana na matendo yako mabaya kabla ya kufa…hivyo ndivyo haki inavyotolewa. Mungu anaweza kutoa aina yake ya haki (ikiwa watu watamsamehe, na kumwachia Mungu kila kitu), au sheria nayo ina aina yake ya kutoa haki (ikiwa wahalifu wanaungama, hupunguziwa adhabu. Ikiwa watakimbia na kukamatwa, hupata adhabu kali) – Mbwa ni mbwa daima.

  • jonah ngetich
    June 4, 2012 @ 08:15:58AM

    Hiyo ni hatua nzuri kwa Hussein, natumai wengine wataiga mfano wake mzuri.

  • Washingtone Onyango
    June 3, 2012 @ 06:46:09PM

    Hapaswi kusamehewa. Utajuaje kama si misheni ya hali ya juu ili kuharibu serikali ya mpito na taifa zima lililosambaratika. Nafikiri kijana huyu anafanya mzaha, inaweza kuwa anajaribu kujigeuza, na kuja kuanzisha mashambulizi mengine nchini Somalia. Ni bahati mbaya kwa al-Shabaab kwa sababu ikiwa walijua kuwa kuua ni dhambi kwa nini walifanya hivyo? Itabidi wakabiliane na matokeo yake. Hakuna kusamehewa.

  • maurice otieno apondi
    June 3, 2012 @ 09:14:32AM

    Hii ni imani kubwa kutoka moyoni. Binadamu hana uwezo wa kujenga imani. Muamini Mwenyezi Mungu mpaka uhisi maovu yako na baadaye ndio uombe msamaha kutoka kwa watu ambao huko nyuma uliwakosea. Kwa kiongozi huyu, ni Mwenyezi Mungu tu wa kumsamehe ambapo yeye anasamehe madhambi madogo na makubwa.

  • haji khalif
    June 3, 2012 @ 09:05:06AM

    Ooo Mungu wangu...Mwenyezi Mungu amsamehe kijana huyu, asiombe msamaha kwa vyombo vya habari bali kwa wale aliowatendea maovu. Nimekuwa nikiisubiri siku kama hii...Nadhani wameona kile alichofanyiwa Mubarak.

  • asad ismaaciil aadan
    June 3, 2012 @ 03:41:47AM

    Hii inaonesha kuwa al-Shabaab wameshang’olewa nchini na hili tatizo limeshamalizwa Somalia moja kwa moja. Al-Shabaab wanaweza tu kupigana kwa njia ya vita vya msituni lakini intelijensia ya serikali iko tayari kuwazuia.

  • WILLIAM
    June 3, 2012 @ 01:01:00AM

    Ndio, wasameheni, lakini serikali ya Somalia isigawane nao chochote katika uongozi. Na lazima sheria ufuate mkondo wake. Kwa kijeshi siku za mbele watasababisha matatizo ikiwa watapata nafasi za uongozi serikalini, sababu ni kuwa wametoa mafunzo kwa watu wanaowaunga mkono.

  • musya ngei
    June 2, 2012 @ 11:06:14AM

    Hapana, sio kweli. Msameheni kwa hatari yenu wenyewe. Mwacheni akabiliane na matokea.

  • ADAMS MAKORI
    June 1, 2012 @ 08:24:47AM

    HILI NDILO TULILOKUWA TUNASUBIRI KWA KILA WAKATI WA KOSA NA TUKO TAYARI KUMSAMEHE LAKINI KWA MASHARTI.

  • zuhuur
    June 1, 2012 @ 06:52:09AM

    Mimi ni mwanamke wa Kisomali na ningependa mumsamehe huyo mtu kwa vile mlivyoahidi kwa watu kwa sababu yeye ni raia wa Somalia anayekiri makosa kwa maovu aliyotenda.

  • WAFULA HENRY SIMIYU
    June 1, 2012 @ 05:52:43AM

    Hapaswi kusamehewa kwa sababu ya maafa ambayo Somalia imeyapata wakati wa utawala wake na kwa kuongezea, atakuwa anakejeli anaposema ni kwa ajili ya kufanya madhara zaidi kwa wananchi wasio na hatia. Serikali ya Somalia muangalieni vyema mtu huyu.

  • مبارك جامع عبدالله
    June 1, 2012 @ 04:31:06AM

    Watumishi wa Mungu mwogopeni Mungu na mjuwe kuwa kesho mtakuwa mikononi mwake. "Na wanao waliodhulumu watakuja kujua ni aina gani ya malipo watalipwa.” – [al-Shu'ra': 227]. Amani inakuja Somalia. Wananchi wote washirikiane na kuungana ili kujenga taifa lao. Amani kwa Somalia… Amani kwa Somalia…

  • DOUGLAS MUKUNGA
    June 1, 2012 @ 02:55:10AM

    Nafikiri jamaa huyu hafanyi mzaha wala kupiga kijembe kwa kusema maneno hayo. Natumai anakusudia katika maneno yake kwa hivyo anastahiki kusamehewa. Ningependa kuwahamasisha watu wa Somalia kutafuta amani, kukuza mapatano na kupendana wao kwa wao, na kwa kufanya hivyo wataiendeleza nchi yao kwa uzalendo. Nadhani wangeelewa kuwa watu wameanzisha njia yao ya kutatua mizozo tangu enzi za asili za vita vya misituni hadi kufikia maelewano.

  • kemboi peter
    May 31, 2012 @ 09:52:31AM

    Hakuna kurudi nyuma hakuna kujisalimisha kwa wahuni wa al-Shabaab.

  • Ali Abdallah Ali
    May 31, 2012 @ 08:51:52AM

    Hawa ni ndugu zetu Waislamu...ingawaje matendo yao siyo tuliyofunzwa katika kitabu chetu cha Kuran hata (Menyezi Mungu) anasamehe, sisi ni nani hata TUSIMSAMEHE!

  • wahome jackson
    May 31, 2012 @ 06:53:29AM

    Je, huu hauwezi kuwa ni mtego? Kama ambavyo baadhi ya viongozi wetu wanasema ambapo katika ukweli wenyewe hasa wanasaidia makundi haramu ..... Hebu fikiria mara mbili juu ya hilo.

  • HENRY ROP
    May 31, 2012 @ 06:11:26AM

    Wakati vita vitakapomaliza tutasamehe vifo vyetu. Mungu huleta vita ili pawepo na amani. Somalia karibuni itarejea katika ramani ya dunia. Ninawapenda Waislamu wanaomuogopa wakati watakaporudi tutaweza kuiga mila na bidii zao kwa ajili ya Mungu na watoto wetu kujifunza sayansi ya atomiki katika chuo kikuu cha Mogadishu na Rashid Al Abdullah ataweza kuvua samaki katika ziwa Victoria na kukaa jioni na Maria NA MUNGU ATATABASAMU JUU YA UUMBAJI WAKE WA KUSHANGAZA.

  • ishmael
    May 31, 2012 @ 05:07:56AM

    Tunamshukuru Mungu kwa hatua hii nzuri.

  • marytheuri
    May 31, 2012 @ 02:46:35AM

    Hii inaweza kuwa ni sababu ya kushambulia watu wasio na hatia.

  • catherine kinyanjui
    May 30, 2012 @ 10:23:37AM

    Nina imani kubwa kuwa huku ni kuchezeana akili. Tulikwishazoea unafiki wa watu hawa, MUNGU awasamehe makosa yao.

  • kaka
    May 30, 2012 @ 10:06:04AM

    Hili ni ombi la nusu kwa nusu. Kitatokea nini wakati wakishaasi kutoka kikundi fulani? Vingi vya vikundi hivi vina viapo vya maisha, kwa hivyo kama unamsamehe muasi mmoja wengine wanaweza kulipiza kisasi kwa kusajili wengine zaidi na kushambulia kuliko walivyofanya kabla. Ina utata kidogo.

  • Riziki
    May 30, 2012 @ 09:10:48AM

    Mfumo wa kimataifa ufikirie juu ya athari kwa jamii kabla ya kusamehewa. Akili zetu lazima ziwe zimejengwa vyema juu ya jinsi watakavyoifanya kazi hii kwa vile wao wanafanyakazi katika mtandao kama wahusika kwenye mahusiano ya kimataifa.

  • NDAMBUKI
    May 30, 2012 @ 07:37:21AM

    MSAMAHA UNARUHUSIWA KAMA UNATOKA MOYONI MOJA KWA MOJA, KUNDI HILI HALIJUI KAMA AMANI ITAWAWEZESHA KUPATA UTAJIRI ZAIDI KULIKO WANAVYOFIKIRIA. HIVI SI VITA VITAKATIFU KAMA WANAVYODAI, NI VITA VYA RASILIMALI AMBAZO WANAWEZA KUFURAHIA KUKIWA NA AMANI IKIWA WATAWEKA CHINI BUNDUKI NA MABOMU, MWENYEZI MUNGU, ZUNGUMZA NA VIJANA HAWA WA AJABU WA KIKE NA WAKIUME.

  • GERALD
    May 30, 2012 @ 07:34:40AM

    Akisamehewa au la, wakati wa al-Shabaab ni mdogo sana.............. kazi nzuri askari wa AMISOM!

  • peter m
    May 30, 2012 @ 06:32:21AM

    Amani iwe kwa kaka na dada zetu wa Somalia.

  • arafat
    May 30, 2012 @ 03:15:17AM

    Huyo mtu aliyejisalimisha ni mnafiki, ikiwa sio jasusi. Huyo ahukumiwe kifo. Hivi ni vita visivyokwisha ambavyo vinaendelea ulimwenguni kote na ni vita baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu kwa msaada wa wanafiki. Kila Muislamu anaelewa mkile kinachowasibu waislamu wenzetu kule Palestina. Kila Muislamu ana wajibu wa kushiriki katika vita vitakatifu vya kuwang’oa wasiokuwa Waislamu na viongozi wao wanaoutawala ulimwengu. Al-Shabaab wana wajibu wa kutekeleza kazi hii ya lazima katika Afrika ya Mashariki na itafanikiwa, Mwenyezi Mungu akipenda. Watu maarufu watakaoondoka katika kikundi hiki ni wawili au watatu ambao hawana ujuzi wa kijeshi. Tunapigana kwa faida ya dini na dini inayotokana na Mwenyezi Mungu. Hatupigani kwa ajili ya Mungu kwa sababu Abuu-Mansuur au Somalia bali kwa sababu ya wajibu wetu kwa Mwenyezi Mungu. Mtume wetu Mohammad bin Abdullahi (Amani Iwe Juu yake) mwanzo alikuwa Muislamu pekee ulimwenguni na wengine hakuwa Waislamu lakini unaweza kuona vipi Waislamu walivyoenea ulimwenguni leo. Ikiwa watu watano tu watabakia katika al-Shabaab bila ya jeshi, nina hakika bado watakuwa wanamtumikia Mwenyezi Mungu kama alivyoamrisha katika Kuran na watashinda vita kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anaangalia dhamira zetu na sio kile tulicho na uwezo nacho. Al-Shabaab hawatadhoofika kwa mtu huyo aliyeasi. Ikiwa al-Zubeir anaasi kutoka katika kikundi, atahukumiwa kifo kama ambavyo wasiokuwa Waislamu wengine au wanafiki, lakini kwa kadiri ninavyoelewa kuhusu imani yake imara kwa Mwenyezi Mungu, hilo halitatokea, Mwenyezi Mungu akipenda. Ninaitakia mafanikio al-Shabaab na kiongozi wao, Abu-Zubeir.

  • Edwin Nateminya
    May 29, 2012 @ 12:00:03PM

    Msamaha ni muhimu na ninamuunga mkono yeyote anayeuomba. Vijana hawa wanaoomba msamaha wangesamehewa na kupelekwa katika vituo vya kuwarekebisha ama mabwenini kwa angalau mwaka mmoja. Kwa njia hii serikali itakuwa na uwezo wa kuamua kiwango gani wamerekebishika kwa ajili ya ushiriki wao katika masuala ya kijamii.

  • JUMA RODGERS
    May 29, 2012 @ 11:31:58AM

    HUYU KIJANA ANATAKA MSAMAHA NA KUKUBALIKA KATIKA JAMII.

  • Okoth Valentine
    May 29, 2012 @ 08:17:31AM

    Inaweza kuwa njia ya kujaribu kutushawishi tupunguze shinikizo juu yao lakini hiyo haiwezi kufanya kazi.

  • MERCY
    May 29, 2012 @ 08:14:11AM

    HUSSEIN WEWE NI SHUJAA. BINADAMU WOTE NI NDUGU. HAKUNA HAJA YA VITA, VINAWAATHIRI WANAWAKE NA WATOTO.

  • musili
    May 29, 2012 @ 05:38:23AM

    Haya ni maoni yangu: huyu mtu angesamehewa na kuingizwa katika serikali ya mpito kwa sababu tayari anayo maarifa juu ya "kikundi" hivyo wamtumie kama nyenzo kwa habari zaidi. Pia angewekwa katika kikosi cha mapambano kila ambapo kuna misheni inafanywa dhidi ya al-Shabaab ili kujaribu ombi lake la msamaha kwa vile hakuna yeyote anayefahamu hasa ikiwa inatoka moyoni mwake. Ikiwa atapigana vikali dhidi ya wenzake wa zamani ndipo kila mtu atakubali ni hatua ya maana.

  • LINUS HAJI
    May 29, 2012 @ 05:02:58AM

    MIE SIPENDI VITA KWA NDUGUZE,TUSHIRIKIANE KUJENGA JAMII YETU YA KISLAMU BADALA YA VITA,NIMEWASAMEHE MIE,INSHALLAH LATULAHI.

  • Sylvanus Kishao
    May 29, 2012 @ 05:01:11AM

    Wasomali ni watu imara na wafanyakazi na wajasiriamali hodari, msisahau. Natumai kwa dhati na ninaomba AMANI itakuja Somalia LEO. Sikutarajia kuwa Somalia ni nchi nzuri kiasi kile! Angalieni tu ukubwa wa wafanyakazi wa K.D.F. kwenye fukwe za Rasi Kamboni Wakati amani itakaporejea Somalia, ninaona mamilioni ya watalii wakijazana katika nchi ile. ENYI WAFANYABIASHARA WA SOMALIA MLIOKO UHAMISHONI, mnaisoma habari hii?

  • Aisha Adam
    May 29, 2012 @ 03:58:15AM

    Hii ni hatua ya kijasiri iliyochukuliwa na kiongozi huyo. Itakuwa bora iwapo wengine wakamfuata ili kuondokana na mapambano ambayo yamedumu kwa miongo kadhaa, wakati ambao hatuishi katika utulivu.

  • KOSSY
    May 29, 2012 @ 03:48:44AM

    MSAMAHA MAANA YAKE NI KUJITOLEA KWA HIARI KWA VIONGOZI NA KUKABILI KILA ADHABU WATAKAYOKUMBANA NAYO.

  • qoran
    May 29, 2012 @ 03:19:44AM

    Wao ndio sio Waislamu wanaotuvamia katika eneo letu na tunahitaji kupambana nao.

  • fuaad
    May 29, 2012 @ 02:33:36AM

    Kwa maoni yangu, nadhani, wanahitaji kuadhibiwa kwa makosa waliyofanya dhidi ya jamii. Ni makafiri wanaojisingizia kuwa ni Waislamu na wanahitaji kushughulikiwa kwa njia ile ile wanayodai washughulikiwe watu wasiokuwa Waislamu. Mimi nimefurahi kuhusu kuparaganyika kwa Al-Shabaab ambao ni maadui wakubwa wa jumuiya ya Wasomali. Wasomali ambao walikimbia kutokana na matatizo yao wamekufa baharini wakiwa njiani kuelekea Libya na Italia. Ni wao ambao walifanya Wasomali wachukuliwe kama ni watumwa nje ya nchi. Ni pengine wapi katika dunia hii utaona watu wanachinjwa kama wanyama?

  • william
    May 29, 2012 @ 02:21:08AM

    Ninaipenda hiyo. Al-Shabaab waungane na serikali ili kuijenga Somalia. Waelewe kuwa vita vimekwisha na hakuna tena cha kupigania.

  • tom ogweno
    May 28, 2012 @ 04:31:31PM

    Endeleeni Waislamu wenzangu. Mwenyezi Mungu ni mkubwa.

  • Elizama kibe kore
    May 28, 2012 @ 07:06:15AM

    it is unfortunate for al shabaab co3 if they knew that killing was a sin why do they do, they should pay the consequences, there4 i reject peace talks with the group to prevent them from comofleging.i there4 stand on my words (time is now).mtoto akililia wembe mpe.

  • Joseph Omemo
    May 28, 2012 @ 06:13:16AM

    Kikundi chote kilipaswa kutawanywa mara tu KDF walipoingia Somalia! Ni hatua ya busara, na karibuni kikundi kizima kitatawanyika. Naamini Somalia inataka amani.

  • Gordon Odhiambo
    May 28, 2012 @ 05:09:43AM

    Msamaha lazima uende sambamba na kuungama.

  • Weru
    May 28, 2012 @ 04:53:25AM

    Mwenyezi Mungu huwasamehe wale wanamuomba msamaha lakini vitendo vina maana zaidi kuliko maneno. Kwa nini mtu anafanya makosa lakini baadaye anaogopa haki, kwani haki inamuweka mtu huru kutokana na ufungwa wa dunia yenye giza. Muombe msamaha Mwenyezi Mungu na njoo ukabiliane na sheria, omba msamaha na uonje dawa ile ile ya watenda maovu. Kwa nini uogope haki sasa na bado uliwakatalia wengine haki? Usingeweza kuwalaumu wengine na tayari umeshagundua kuwa uhuru una gharama kubwa na ndio maana unamuamini Mwenyezi Mungu, na bado unaogopa ukweli na hutubu kwa matendo yako. Asante Weru

  • Warfar Neyo
    May 27, 2012 @ 03:47:03PM

    Hussein anapaswa kusamehewa. Sote tunatenda madhambi na husamehewa, kwa nini isiwe hivyo kwa Hussein? Dhambi ni dhambi na amekubali kuwa amekosa, ikiwa hatutamsamehe tutahitakiwa siku ya malipo. Sikubaliani na kumuua kama wengine wanavyodai. Na wao pia hawako safi, tumwache Mungu afanye kazi yake ya kumhukumu. Baada ya yote yuko tayari kujisalimisha mwenyewe na bado KDF na AMISOM hawataki kufanya hilo. Hili ni dhidi ya maadili ya haki za binadamu, ndiyo, lakini hili lingefanywa baada uchunguzi wa kina na kuthibitisha kuwa hafanyi propaganda ili aweze kupanga mikakati mengine baada ya pigo la Afgoye. Wakristo nchini Kenya wameteseka sana kwa sababu ya mashambulizi ya kigaidi. Watoto na wanawake wasio na hatia wamepoteza maisha yao. Kitu kizuri kwa Wakristo ni kuwa daima hawalipizi kisasi, mafunzo yao yanawafundisha kukipeleka kila kitu katika maombi kwa Mungu. Machozi waliyomwaga mbele ya Mungu yao yanatosha na al-Shabaab watalipa katika njia inayoumiza kabisa. Waislamu, tumsamehe Hussein, ni mkweli …kwa kufanya hivyo kuna mwanga mwisho wa shimo kwa kuwepo kwa Somalia nzuri. Tuamini na kuokoa uwepo wake.

  • SIMION
    May 27, 2012 @ 06:35:34AM

    Msamaha ungetolewa kwa wale wanauomba kwa dhati, hata hivyo mimi ninaumia kwa sababu kijana wangu anaonekana kuwa kipofu kwa askari wa AMISOM wanaomzunguka. Vipi kuhusu kusogea karibu na Makao Makuu ya Serikali kwa bidii?

  • a_rahmaan mohamed a_laahi
    May 27, 2012 @ 05:10:00AM

    Mimi ni raia wa Somalia ambaye naishi katika nchi hii. Ningependa kuomba kwa Mungu kutuongoza njia iliyonyooka, Mungu akipenda. (Mungu anawapenda waumini wake wa kweli ambao wameokoka.) Mungu atufanye sisi kuwa miongoni mwa wale ambao atawalipa Pepo yake, Amina, Mungu akipenda.

  • steven mokaya
    May 26, 2012 @ 03:01:37PM

    Yeyote anayeomba msamaha anastahiki kusamehewa, ikiwa anaomba msamaha huo kwa dhati kutoka moyoni.

  • Oyatsi
    May 26, 2012 @ 12:46:25PM

    UPDF itawaangamiza, iwapo mpuuzi huyu atasamehewa au hatasamehewa.

  • songo
    May 26, 2012 @ 10:17:30AM

    Mtajuaje kuwa hii si misheni ya hali ya juu yenye nia ya kuharibu serikali ya mpito na taifa lote ambalo mwanzo lilisambaratika lakini kwa dhamiri na kutoa ufukara wake milele. Hawa ni kondoo waliovaa ngozi za mbwa mwitu wanasubiri wakati wa kuwaita wenzake waje kufanya mashambulizi kwa wakati muafaka, ndio kusema, baada ya kuondoka kwa vikosi vya AMISOM (kikwazo), itakuwa rahisi kwao kuwashughulikia maadui zao. MIMI SIAMINI CHOCHOTE

  • peter
    May 26, 2012 @ 08:35:08AM

    Hii ni hatua ya kuachana na kikundi cha kigaidi na vitendo vyao kwa baadhi ya viongozi wao; ni hatua mbele katika mchakato wa amani kwa watu wa Somalia.

  • maxamed c/laahi xasan
    May 26, 2012 @ 06:18:38AM

    Kujisalimisha na kuomba msaada kwa jamii ya Somalia kuliletwa kwa kuona watu ndani ya meli waliyokuwemo, wakijitosa wenyewe baharini kabla ya kukamatwa.

  • faruoqdah
    May 26, 2012 @ 02:18:45AM

    Mwenyezi Mungu amuongoze kutoka gizani kwenda kwenye mwangaza. Ndugu zetu Waislamu wamekuwa na wakati mgumu nchini Somalia. Tushukuru kwa jina la Mwenyezi Mungu.

  • FRANKLIN
    May 25, 2012 @ 10:10:19PM

    Tutumai kuwa ni mkweli katika maneno yake.

  • thekenyandude
    May 25, 2012 @ 12:22:28PM

    Kazi iko kwa serikali ya Somalia kuonana na kijana huyu kwa tahadhari. Njia watakayomshughulikia itashawishi mazingira huko mbele kwa wengine kuasi. Chukueni mfano kutoka kwa “uasi” wa askari doria wa Ethiopia aliyejiunga na al-Shabaab. Alipokelewa vyema na naamini akiwa njiani kwenda mstari wa mbele kuchinjwa. Chai ni Kismayo.

  • ALPHONCE MUSYIMI
    May 25, 2012 @ 12:00:11PM

    Msamaha, ikiwa utaombwa kwa moyo safi na ahadi unaweza kuwa njia nzuri ya kutatua mzozo wa Somalia kwa vile hii inatoa nafasi ya masikilizano na mshikamano wa watu wa Somalia. Yule aliojuta na washirika wao waondolewe Somalia wapelekwe nchi nyingine salama ambako wataungama na baadaye yaombwe makundi kadhaa ya Somalia yajisalimishe na kuungana na wengine katika taifa la Somalia lililoungana.

  • a.moody
    May 25, 2012 @ 10:59:47AM

    Hii ni propaganda inayoenezwa na Marekani na washirika wao katika Afrika ya Mashariki.

  • Hussein Mohamed Mohamood
    May 25, 2012 @ 10:44:31AM

    Makosa ni sehemu ya maisha ya binadamu. Kufanya makosa si kosa bali tunapaswa kusoma kutokana na makosa yetu. Tusisahau makosa tuliyofanya huko nyuma ili tusiruhusu wengine kurudia makosa hayo hayo. Tusikose shukurani kwa Mwenyezi Mungu; ambaye ametupa neema kama vile chakula tunachokula, hewa tunayovuta na kupumua, nguvu ya kuona vitu na hisia nyingine. Tumwombe Mwenyezi Mungu atusamehe kwa madhambi yetu tuliyofanya kabla. Kwa maoni yangu, nafikiri tunapaswa kumkaribisha mtu au kikundi chochote kilicho tayari kutubu madhambi yao waliyofanya dhidi ya watu wengine. Ulimwengu umeumbwa kwa kusameheana. Kulipiza kisasi kwa watenda maovu na kukosekana na msamaha kutasababisha madhara zaidi kuliko mema. Tukishindwa kuwasamehe wanachama wa al-Shabaab, maana yake ni kuwa wataendelea kuwa wapinzani mpaka watakapokufa, jambo ambalo litakuwa kikwazo cha kurejesha amani nchini Somalia. Asante sana Hussein. Kila la heri.

  • AGESA AGANI DAVID
    May 25, 2012 @ 09:50:09AM

    Hii ni ishara nyingine ya nyakati za mwisho. Biblia imesema kuwa wa mwanzo ndiye huwa wa mwisho. Hakikisheni kuwa hampitwi na watu kama hao. Ndugu zangu, acheni na kikundi cha shetani na mrejee kwa Yesu na mjitayarishe kwa vile BWANA ANAREJEA.

  • bethu makani
    May 25, 2012 @ 09:02:45AM

    Pengine anajaribu kujigeuza tu na kufanya mashambulizi mengine nchini Somalia. Kuweni waangalifu na njama zake.

  • Said HashimRashid
    May 25, 2012 @ 07:50:02AM

    Kama Mwafrika niliye karibu sana na Somalia ninakerwa sana na kile kinachoendelea kule. Kenya imekuwa nchi pekee ambayo imekuwa rafiki wa karibu wa watu wa Somalia. mateso yao yametuathiri pia na ninaomba kuona amani katika eneo hili. MUNGU waongoze wawe na maisha mema. Watu wa kule ni wafanyakazi hodari ikiwa watatulia; sisi pia tunanufaika kutokana na uhodari wa kazi.

  • Peter Kingori
    May 25, 2012 @ 06:44:31AM

    Mimi kama Mkenya ningependa kuwaomba ndugu zetu wa Somalia kuungana na kuwajali wanawake na watoto wa Somalia. Nimefanya kazi Somalia kwa muda wa miaka mitatu na kwa kweli ninaomba amani ipatikane hivi sasa na tutakuja hapa kwa matembezi ya kirafiki na kama watalii na sio kuwasaidieni katika hali ya vita. Tafadhaleni ndugu zetu, unganeni na acheni kupigana. Mwenyezi Mungu amewapeni utajiri mwingi hata mafuta na ikiwa hamkuungana wageni watauchukua. Hebu fikirieni ni kiasi gani cha samaki mmepoteza kwa mashirika ya kigeni yanayovua visivyo halali katika maeneo yenu ya mwambao kwa sababu hamna serikali ya kuyalinda. Ninaomba amani kwa ajili ya Somalia.

  • zeitun
    May 25, 2012 @ 05:57:54AM

    Wangesamehewa, hakuna mkamilifu.

  • Peter Odhiambo
    May 25, 2012 @ 05:09:57AM

    Wapiganaji wa al-Shabaab wangetumia nguvu zao kwa kuijenga nchi yao badala ya kupigana vita hivi vya umwagaji damu ambavyo hatimaye vinawaathiri watoto. Lazima waelewe kuwa vita havilipi. Ikiwa kweli wanauijali Somalia, LAZIMA waweke chini bunduki na maguruneti yao SASA na sio kesho.

  • susan karwitha Tembo
    May 25, 2012 @ 02:37:25AM

    Huyu asamehewe kwa sababu Biblia takatifu inasema, "kwa wale waliotenda dhambi na kukosea fahari ya Mungu, Mungu anasamehe. Hata kama dhambi zetu zitakuwa nyekundu kama damu, ataziosha na kuwa nyeupe kama theluji," Bwana anasema. Binadamu ni nani wa kutomsamehe mtu huyu ambaye ameungama dhambi zake?

  • Mambo
    May 25, 2012 @ 12:42:00AM

    Ni habari njema lakini ninawahakikishia kuwa huu niunafiki tu!

  • ABDULLAHI MOHAMED
    May 24, 2012 @ 05:37:26PM

    Kusema kwa uwazi, tunapaswa kuwasamehe wale wanaoomba msamaha kwa sababu huko ndiko iliko hatima yetu na la kujiuliza ni vipi tunaweza kufanya na sio kwa nini ilitokea. Mungu aijaalie amani nchi yetu.

  • MOES
    May 24, 2012 @ 12:12:20PM

    Hii inatia moyo; ina maana vita vimeshindwa. Asante KDF kwa ujasiri wao wa kumkamata ng'ombe mapembe. Ningependa kuwaomba waasi wengine kulikubali neno hili KUJISALIMISHA.

  • Abu Omar
    May 24, 2012 @ 10:57:11AM

    ACHENI UONGO NA UOZO WA KUANDIKA HABARI ZISIZO NA UKWELI, HIVI MNAJUA REDIO MUGDISHO? NA PROPAGANDA ZAO ? BASI MUANDIKE HABARI KUTOKA REDIO ANDALUS NAZO TUZIJUE MNAPO NUKUU HABARI!

  • lakironnie
    May 24, 2012 @ 08:04:25AM

    Siwezi kuamini hili. Wanajaribu wasamehewe wakati wanafanya shughuli isiyo halali.

  • nalosh
    May 24, 2012 @ 07:10:51AM

    Watu wa Somalia na ulimwengu wamsamehe pale tu baada ya kuvunja kikundi na kuwalipa fidia wahanga. Lazima aeleze kwa nini kikundi hiki kilianzishwa.

  • Bismark Langat
    May 24, 2012 @ 04:40:23AM

    Vyema, ikiwa hali iko hivyo kwa uongozi wa al-Shabaab hiyo ni ishara inayoonesha kuwa wameshindwa, lakini nashangaa kwa sababu inaweza kuwa wanapanga mchezo ili watu wawahurumie. Tujuwe kuwa al-Shabaab ni kikundi cha kihalifu ambacho lazima kishughulikiwe ipasavyo kwa gharama yoyote. Tuelewe kuwa kikundi hiki kimeua raia wengi na hakiwezi kulipa kwa yote kilichofanya.

  • isige kevin
    May 24, 2012 @ 03:33:24AM

    Ikiwa tu wataapa kutoibuka tena, katiba ifuatwe na hatua za kufaa zichukuliwe; ikiwa itamaanisha msamaha, ni sawa tu.

  • sayid axmed dini
    May 23, 2012 @ 12:05:56PM

    Sidhani kama ni jambo zuri kwa sababu kutahatarisha maisha ya Hussein.

  • safwaan
    May 23, 2012 @ 12:02:55PM

    Huyu angeuliwa kwa sababu amejisalimisha baada ya kuua Waislamu wengi na lilikuwa suala la wakati kabla hajakamatwa. Ningeomba apigwe risasi hadharani.

  • eva
    May 23, 2012 @ 09:13:46AM

    Hawapaswi kusamehewa hata kidogo lakini wanapaswa kusalimu amri na kulipa hasara zote walizosababisha.

  • fathe
    May 23, 2012 @ 07:42:28AM

    Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Wasomali waungane kwa ajili ya amani na utulivu katika Pembe ya Africa. Wageni wataondoka kwa sababu maslahi yao binafsi yatazuiwa na umoja wa watu.

  • qarandoon
    May 23, 2012 @ 04:33:50AM

    Huyu ni mnafiki, kwa hivyo hastahiki kusamehewa. Yeyote atakayejulikana kuwa ni mwanachama wa al-Shabaab lazima ahukumiwe kifo. Wanataka msahamaha sasa baada ya kuona wamedhoofika. Vipi wanatarajia wapewe msamaha na wale waliowachinja watu wao? Vipi wanatarajia wasamehewe na wale waliowaulia ndugu zao? Kama ningetakiwa kuwahukumu wanafiki hawa mahakamani, ningesema wakatwe vipande vipande.

  • PASTOR PATRICK
    May 23, 2012 @ 02:50:48AM

    Al-Shabaab wanapaswa kuhamasishwa kuacha vurugu na kuungana na serikali ya Somalia ili kujenga nchi yenye amani kwa vizazi vijavyo...Mungu hapendi umwagaji damu...Amani inakuja na wananchi wote waungane ili kuijenga upya nchi...AMANI KWA SOMALIA...AMANI KWA SOMALIA.

  • walter onduso
    May 23, 2012 @ 02:39:38AM

    Ndio, iko haja ya kusamehe kwa sababu sote ni binadaamu kwa hivyo tuna madhambi.

  • buru
    May 23, 2012 @ 12:02:29AM

    Nimeipenda hii, ninawatia moyo viongozi wengine wa al-Shabaab ambao wana nia ya kuasi. Kwa serikali ya Somalia, tafadhali timizeni ahadi yenu ya kuwalinda wale walioasi kutoka al-Shabaab. Amani nchini Somalia ni amani kwa nchi nyingine za Afrika ya Mashariki.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo