Mei 16, 2012
Sabahi inaendelea kuchapisha madondoo na uchambuzi wa nyaraka 17 zilizogunduliwa wakati wa mashambulizi ya Abbottabad huko Pakistani yaliyopelekea kuuliwa kwa Osama bin Laden mwezi Mei 2011.
Nyaraka hizo zimo katika mfumo wa barua za elektroniki au barua za maandishi zilizoandikwa kati ya Septemba 2006 na Aprili 2011, na bin Laden au na viongozi wengine wa al-Qaeda.
Baadhi ya barua zinaonesha uhusiano wenye mvutano baina ya viongozi wa al-Qaida na washirika wao wa kikanda na washirika wao. Barua moja ilionesha ushahidi kwamba bin Laden alipinga ombi la al-Shabaab kujiunga na al-Qaeda. Nyaraka nyingine zinaonesha kuwa viongozi wengi walikuwa hawaridhishwi na vitendo vya al-Qaeda nchini Iraki na Talibani wa Pakistaní.
Nyaraka pia zinaonesha mgawanyiko mkubwa baina ya uongozi wa al-Qaeda na vikosi vilivyoko mapiganoni juu ya kuwalenga wananchi na kuanzisha vita dhidi ya malengo ya wenyeji.
Katika barua kwa mtu asiyejulikana mwishoni mwa mwezi Januari 2011, Adam Gadahn, msemaji wa al-Qaeda na mshauri wa vyombo vya habari, alikosoa mbinu za Taifa la Kiislamu la Iraki na Talibani wa Pakistani na aliisisitiza al-Qaeda kujiondoa hadharani kutoka makundi yote mawili.
Akitoa maoni juu ya shambulio la kanisa huko Baghdadi mwaka 2010 lililofanywa na Taifa la Kiislamu la Iraki, Gadahn aliandika:
"Shukurani zimwendee Mwenyezi Mungu, uko wapi msimamo wa Taifa la Kiislamu la Iraki kwa Wakristo, kutoka msimamo wa sheikh Osama katika hotuba yake (Suluhisho) miaka mitatu iliyopita?
Inashangaza, naapa mgogoro baina ya maelezo ya viongozi na wanazuoni wetu, na matendo ya wale wanaoshirikiana nao, au tusema: wale wanaojidai kuwafuata!
Sioni kikwazo chochote au tendo baya ikiwa kundi la al-Qaeda linatangaza kutoridhika kwake na tabia hii na tabia nyingine zinafanywa na wale wanaojiita Taifa la Kiislamu la Iraki bila amri kutoka kwa al-Qaeda na bila kuwasiliana na uongozi wa al-Qaeda…na kwamba maamuzi yao wenyewe yamesababisha mgawanyiko katika safu za mujahidina na wafuasi wao ndani na nje ya Iraki.
Huu ndio ufumbuzi pekee unaokikabili kikundi cha al-Qaeda. Vinginevyo hadhi yake itahujumiwa zaidi na zaidi kwa matokeo ya vitendo na maelezo ya kikundi hiki, kwa kutumia jina la kikundi chetu (kibarikiwe kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu).
Na miongoni mwa masuala yanayotia kinyaa – na hasa yanayokatazwa – ni kulenga misikiti kwa milipuko na silaha nyingine, kama yale yanayotokea nchini Afghanistani na Pakistaní na mara nyingine Iraki. Bado tunahitaji kuweka wazi uthibitisho wetu kwa Waislamu kabla ya kuweka wazi kwa Wazungu…”
Gadahn alitaja orodha kubwa ya mashambulizi ya Talibani wa Pakistani yaliyofanywa dhidi ya maeneo ya raia na misikiti na mashambulizi ya al-Shabaab nchini Somalia yaliyoua madaktari walikuwa wanahitimu kutoka shule ya uuguzi mjini Mogadishu.
"Hili ni tone tu katika mafuriko, na kidogo katika mengi, kama ninavyojaribu kushughulikia matukio ambayo nina hakika yanachangia kweli kwa mujahidina na wale wanaoshirikiana nao, au matukio ambayo ninaamini yanachangia sana. Vinginevyo orodha ni ndefu sana; pia, sikuzungumzia kuhusu matukio yanayohusiana na unyang’anyi, utekaji nyara na uhalifu mwengine unaofanywa na mafisadi hao.
Inaeleweka kuwa kuishambulia misikiti na kumwaga damu ya watu wasio na hatia kulijulikana katika historia kushirikishwa na vikundi viovu kabisa au na watu binafsi…Sasa, watu maarufu kwa vitendo kama hivyo ni wale wanaoshirikiana na wanajihadi na mujahidina, kama vile kikundi cha Hamas na cha Talibani huko Pakistani na Afghanistani!
Sina shaka kuwa yale yaliyokuwa yanatokea kwa kikundi cha jihadi katika nchi hizi si kwa bahati mbaya, lakini adhabu ya Mungu dhidi yetu kwa sababu ya madhambi na udhalimu wetu, au kwa sababu ya madhambi ya baadhi yetu na kimya kwetu sote…"
Katika sehemu inayoshughulikia mikakati ya vyombo vya habari vya al-Qaeda wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001, Gadahn alimtaka bin Laden na Ayman al-Zawahiri kukutana na waandishi wa habari wa kimataifa “kuelezea misheni zetu katika magazeti na vituo vyao” na kutoitegemea pekee Al-Jazeera na baraza “yanayotia kinyaa” ya wanajihadi.
"Kuitegemea Al-Jazeera pekee na baraza ya wanajihadi katika intaneti hakusaidii kitu. Al-Jazeera inaonekana kuweka masharti kama vituo, mashirika na magazeti mengine katika kuandika matangazo ya al-Qaeda, hasa kwa kujumuisha vitisho au kukubali kuhusika na tukio fulani. Ama kuhusu ujumbe kwa njia ya kidiplomasia, kama vile ujumbe mbili za sheikh kuhusu mafuriko [nchini Pakistani], [inachukuliwa] haifai kwa kuchapisha kwenye vyombo vyao, kwa vile huu ndio mwonekano wa al-Qaeda [wanaamini] hawafai kutokezwa mbele ya watu.
Ama kuhusu baraza ya wanajihadi, yanatia uchefuchefu kwa Waislamu wengi, au kuwazibwa. Pia yanaharibu sura ya al-Qaeda, kwa kuzingatia kile unachojua kuhusu ulokole na kauli kali zinazotumiwa na washirika wengi wa baraza haya. Pia wanaegemea upande mmoja kuhusu [Wasalafi] na sio Msalafi yeyote, lakini Wasalafi Wanajihadi tu. Usalafi ni mojawapo wa madhehebu miongoni mwa madhehebu ya Kiislamu, na Usalafi wa Wanajihadi ni madhebu ndani ya madhehebu madogo!”
Gadahn pia alimtaka bin Laden ajitokeze hadharani “kunyanyua mori” wa wanajihadi.
"Pia lazima tusisahau ndugu zetu mujahidina walioko mstari wa mbele ambao wako katika wakati mgumu na wanakabilia na majanga baada ya majanga. Na wao pia watafurahi kumuona tena sheikh. Kujitokeza tena hadharani kutanyanyua mori kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Ningefikiria kuwa ni vyema kwa sheikh kutoa hotuba ya video kwa mujahidina katika nyanja zote, kuwafariji, kuwataka wavumilie, kuthibitisha hatua hazo na kuwaongoza.”
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
Moto kwenye soko kubwa la Garissa uliharibu zaidi ya maduka 100 usiku wa Jumatatu (tarehe 17 Juni...
Waziri wa Umoja wa Kitaifa wa Djibouti Zahra Youssouf Kayad alisaini mikataba ya miradi miwili ye...
Kamati ya bajeti ya Bunge ya Kenya imekataa pendekezo la kununua ofisi mpya kwa aliyekuwa Rais Mw...
Moto ulifanya uharibifu mkubwa katika mji wa Balbala huko Djibouti siku ya Jumapili (tarehe 16 Ju...
Picha ambazo al-Shabaab ilizituma siku za Jumapili (tarehe 16 Juni) kwenye mtandao wa Twitter za ...
Polisi nchini Kenya walimuua mtuhumiwa wa ugaidi, Kassim Omolo Otemo, mjini Mombasa wakati uvamiz...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji