Mei 15, 2012
Baraza la Mitihani la Kenya (KNEC) limetunga rasimu mpya ya sheria ambayo itafanya udanganyifu kwenye mitihani ya taifa kuwa uhalifu, baada ya tuhuma za udanganyifu mkubwa uliosababisha kufutwa kwa matokeo ya karibuni wanafunzi 3,000 mwaka huu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa KNEC, Paul Wasanga, alisema Waziri wa Elimu Mutula Kilonzo aliuwasilisha msaada huo bungeni mwezi Aprili na wabunge wanatarajiwa kujadili marekebisho yoyote na kuupigia kura kuwa sheria mwaka huu.
“Hadi sasa serikali haijawahi kumshitaki hata mtu mmoja kwa udanganyifu kwenye mitihani ya taifa. Tabia hii imekuwa ikiongezeka kwa miaka mitano iliyopita kwa hivyo sasa tunakuja na hatua kali,” Wasanga aliiambia Sabahi
Wanafunzi wa Kenya wanatakiwa kufanya mtihani wa taifa wa Cheti cha Elimu ya Sekondari mwishoni mwa mwaka wao wanne wa sekondari ili kupata vyeti vya kuhitimu, ambapo bila ya vyeti hivyo hawawezi kuomba kazi au kuendelea na elimu ya chuo kikuu.
Chini ya sheria hiyo inayopendekezwa sasa, wadanganyifu watazuiwa kufanya mitihani kwa kipindi cha hadi miaka mitatu. Wao na washirika wao wanaweza kufungwa hadi miaka 10 jela na faini ya shilingi milioni 2 za Kenya (dola 24,000), alisema Wasanga.
Watu wanaovujisha mitihani au sehemu ya karatasi za mitihani na vifaa vyake atakabiliwa na adhabu ya hadi miaka mitano jela na faini ya hadi shilingi milioni 1 (dola 12,000). Mtu yeyote atakayegunduliwa wakati au kabla ya mtihani na sehemu ya mtihani atashitakiwa.
Pamoja na hayo, wafanyaji mitihani wanaojisajili kwa majina bandia na wale waliowaruhusu wanafunzi kufanya mitihani kwa majina yao wataweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka miwili jela na faini ya shilingi milioni 1.
“Tunatarajia kwamba sheria hii itapitishwa kwa haraka mwaka huu kudhibiti wadanganyifu na washirika wao,” alisema Wasanga.
Mwezi Februari, KNEC ilifuta matokea ya wanafunzi 2,927 kwa sababu ya kukiukwa kwa taratibu na tuhuma za udanganyifu mkubwa. Kwa mujibu wa baraza hilo, kati yao matukio 1,694 ya uvunjaji wa taratibu za mitihani yaliyotokea kwenye Jimbo la Kaskazini Mashariki.
Ushirikiano kati ya wanafunzi, walimu na watu wengine uliwezesha udanganyifu na uingizaji wa visaidizi vya mitihani katika vyumba vya mitihani vilikuwa chanzo cha tatizo, alisema Wasanga. Alisema ukiukwaji wa taratibu ulionekana wakati wa mitihani na wasimamizi.
Wanafunzi ambao mitihani yao imefutwa hawataweza kuendelea mbali hadi alama zao zitakapopatikana kihalali, alisema.
Mohamed Bunow Korane, mtafiti katika Jihan Foundation, ambayo inafadhili elimu kwa wasichana mjini Garissa, alisema mengi zaidi yanahitaji kufanywa kuhakikisha kuwa jimbo hilo halikabiliwi tena na ufutaji mkubwa wa matokeo ya mitihani, ikiwemo kutoa vifaa zaidi kwa shule.
Alisema vifaa visivyofaa katika skuli nyingi kwenye mkoa huo husababisha wanafunzi kutumia pamoja vifaa vya maabara hata wakati wa mitihani ya taifa.
“Mitihani ya sayansi kwa kawaida inafanyika kwenye maabara za shule na wasimamizi wa mitihani wanaona wanafunzi wakitumia vifaa pamoja kwenye maabara na kuhitimisha ni mpango wa kuwasaidia wanafunzi kudanganya,” Korane aliiambia Sabahi.
Kufutwa kwa mitihani kulichochea maandamano na vikao vya kijamii katika mkoa huo.
Sasa wanafunzi wanasubiri matokeo ya uchunguzi unaoendelea kuhusu matokeo ya mitihani ya taifa kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge juu ya Elimu. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, David Koech, aliiambia Sabahi kwamba kamati yake bado inakusanya ripoti na itahakiki ugunduzi na mapendekezo yake bungeni hivi karibuni.
Uchunguzi huo uliagizwa baada ya viongozi waliochaguliwa kuwakilisha jimbo hilo wakiongozwa na mbunge wa Dujis, Aden Bare Duale, kulalamikia ufutwaji wa matokeo na kupeleka hoja bungeni ya kutaka bunge liuhakiki mtihani upya. Spika Kenneth Marende aliagiza uchunguzi huo hapo mwezi Aprili.
Mohammed Affey, mteule wa chama Orange Democratic Movement katika moja ya viti 12 vya ubunge vitakavyojazwa kwa uteuzi wa chama, aliiambia Sabahi kwamba udanganyifu unaweza kutokea, lakini akashuku uhakika wa ugunduzi wa KNEC.
Pia wanafunzi, walimu na wazazi walisema walishtushwa kwamba mkoa wao ulivunja rikodi ya idadi kubwa ya vitendo vya uvunjifu wa taratibu mwaka jana, na kuzua masuala dhidi ya ripoti ya ugunduzi wa KNEC katika kikao na kamati ya Bunge mjini Garissa hapo tarehe 13 Aprili.
Hussein Abdi Muhumed, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 kutoka Garissa ambaye matokeo yake ya mtihani yalifutwa, amesema jambo hilo limemuathiri sana. Ufutwaji wa matokeo yake, alisema, unamaanisha hawezi kuendelea kwenda chuo kikuu au kutafuta kazi.
“Baada ya matokeo yangu kufutwa, nilijihisi nimeangamizwa”, aliiambia kamati ya Bunge katika kikao chake kwenye ukumbi wa Boys Town Secondary School.
Mzazi Adan Ibrahim Ahmed aliiambia kamati hiyo kwamba mkoa haujawahi kufanya vyema kwenye mitihani ya taifa kwa miaka 40 sasa na akawataka maafisa kuipa alama tena mitihani iliyofutwa.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji