Wataalamu wanaorejea nchini kusaidia kufufua uchumi wa Somalia

Na Mahmoud Mohamed huko jijini Mogadishu

Mei 15, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kurejea kwa wataalamu wa Somalia kumechangia kustawisha biashara na kufufua uchumi wa ndani na elimu katika nchi hii.

  • Hoteli mpya inayomilikiwa na wataalamu wa Kisomali waliorejea iko katika ujenzi huko wilaya ya Hodan ya Mogadishu. [Mahmoud Mohamed/Sabahi]

    Hoteli mpya inayomilikiwa na wataalamu wa Kisomali waliorejea iko katika ujenzi huko wilaya ya Hodan ya Mogadishu. [Mahmoud Mohamed/Sabahi]

  • Nyumba katika Wilaya ya Waabari ya Mogadishu imejengwa tena baada ya mmiliki wake kurejea nyumbani kutoka nchi za ng’ambo. [Na Mahmoud Mohamed/Sabahi]

    Nyumba katika Wilaya ya Waabari ya Mogadishu imejengwa tena baada ya mmiliki wake kurejea nyumbani kutoka nchi za ng’ambo. [Na Mahmoud Mohamed/Sabahi]

Maofisa wa ndani na wataalamu walisema kurejea kwa wingi kwa Wasomali kutoka katika nchi mbalimbali ni ishara ya uboreshaji wa hali ya usalama katika nchi hii.

“Nilikuwa dereva wa teksi huko Minnesota kwa miaka mitano, lakini niliamua kurudi Mogadishu,” alisema Ahmed Abdullahi, mwenye umri wa miaka 37, ambaye alirejea miezi michache iliyopita akitokea Marekani. "Kukombolewa kwa Mogadishu kutoka kwa waasi kumenipa matumaini ya kurudi nyumbani.”

“Mwanzoni, nilikuwa naogopa kurudi Mogadishu kwa sababu niliambiwa kuwa Mogadishu ni sehemu ya hatari. Watu walikuwa wakizumgumzia kuhusu mauaji na kwa sehemu kubwa kukosekana kwa usalama, lakini kuondolewa kwa al-Shabaab jijini Mogadishu kulinipa matumaini," aliiambia Sabahi.

Abdullahi alisema kuwa wakati akirejea, alikuta mji mkuu huo kuwa tofauti kabisa na kile alichokuwa akiambiwa. “Haukuwa tena sehemu ya hatari ambayo watu walikuwa wakiuzungumzia,” alisema. “Niliwakuta wakazi wa Mogadishu wakijishughulisha kwa maisha mazuri ya baadaye. Pia, athari za mapigano zinaishia taratibu katika mji huu. Nina furaha kurudi Mogadishu na ninafikiri kuwa maisha hapa ni mazuri kuliko mahali pengine popote.”

Abdullahi alisema kuwa anafikiria kuwarejesha watoto wake Mogadishu ili waweze kujifunza lugha hii na kuzoea utamaduni wa Kisomali.

Wataalamu wa Kisomali wanatimiza jukumu muhimu katika ujenzi upya

Toka al Shabaab walipoondolewa Mogadishu mwaka uliopita, idadi ya Wasomali wanaorudi kutoka nje imeonekana kuongezeka kwani hali ya kawaida inarudi katika maisha ya kila siku.

Mahmoud Omar, mwenye umri wa miaka 48 alirudi Mogadishu mwishoni mwa mwaka uliopita baada ya kuishi Uingereza kwa miaka mingi.

Aliiambia Sabahi kuwa kurudi kwa wataalamu wa Somalia kunawarejesha wakiwa na utajiri wa uzoefu, akiba na ujuzi walioupata wakati wakiishi nje ya nchi. Hii inawapa fursa kutimiza jukumu katika jitihada za ujenzi upya wa nchi hii.

“Kwa hakika, baadhi wameshaanzisha miradi mbalimbali, kama vile benki za biashara na viwanda vidogo vidogo, wakati wengine wanajihusisha na miradi ya maendeleo, kama vile kujenga shule na hospitali,” alisema.

Omari alitoa wito kwa wafanyabiashara wa Kisomali wanaoishi nje ya nchi kurudi na kuwa sehemu ya jitihada za ujenzi upya. "Taifa linajengwa na raia wake lenyewe na ujenzi wa nchi hii ni jukumu la kila mmoja na kila raia wa Kisomali, ndani ya nchi au nje ya nchi,” alisema.

Malyuun Hassan, mwenye umri wa miaka 36, alirudi Mogadishu baada ya kuishi huko Bristol Uingereza kwa miaka 14.

“Nimerudi Mogadishu kwa sababu nilihisi kutamani kurudi nyumbani,” aliiambia Sabahi. “ Kuwaacha marafiki zetu nyuma na kuwa mbali na nyumbani ni vitu ambayo tulivikosa sana wakati tukiishi nje ya nchi. Tulikosa sana kuwaona marafiki zetu, sehemu tunayoikumbuka na marafiki zetu wa zamani, na bila shaka, hali ya hewa nzuri ya Somalia. Kwa sababu hizi, niliamua kurudi nyumbani pamoja na kusikia kuwa kuna uboreshaji mkubwa wa hali ya usalama.”

Hassan alisema wengi wa marafiki zake huko Bristol wanafunganya masanduku yao ya nguo kurudi nyumbani iwapo hali ya usalama itaendelea kuimarika.

Abdirazaq Mohammed, mfanyabiashara ambaye kwa sasa amerejea kutoka Kenya, alisema yeye na baadhi ya wenzake wameamua kujenga hoteli kubwa huko Mogadishu.

"Mimi na wenzangu tulikuwa na biashara jijini Nairobi, lakini tumeamua kuja Mogadishu baada ya kusikia kwamba hali ya hapa imebadilika," alisema. "Hatufikirii kuhusu faida na hasara lakini badala yake tunajisikia kwamba tunawajibu katika taifa wa kushiriki katika ujenzi mpya wa nchi hii."

"Baada ya miaka kadhaa ya uharibifu, matumaini ni makubwa kwamba mafanikio yatarejea Mogadishu hivi karibuni," alisema, hueleza kwamba kuna ukuaji wa ujenzi huko Mogadishu, kwani watu wamerejea kujenga tena makazi yao.

Somalia yafaidika na utaalamu wa jumuiya ya wahamiaji

Profesa wa Uchumi Abdullahi Farah alisema wahamiaji wana utajiri wa ujuzi, sifa na mtaji walioupata walipokuwa wakiishi nchi za ng’ambo.

"Wasomali waliorejea kutoka uhamishoni wanaweza kufanya kazi kubwa ya kuinua uchumi wa nchi pamoja na kuamsha elimu nchini," Farah aliiambia Sabahi. "Wataalamu kutoka nje wana uwezo wa kuwekeza nchini na kufanya kazi ya kujenga taasisi muhimu na miundombinu ambayo nchi hiyo inaihitaji sana."

Farah alisema jamii iliyokuwa ugenini imekuwa na uwezo wa kukamilisha mengi nchini Somalia kwa miaka 20 iliyopita.

"Walikuwa muhimu katika jitihada za kusaidia kwa kutuma misaada kwa watu walioathirika katika maeneo ambayo mawakala wa kutoa misaada hawakuweza kufika," alisema. "Walikuwa wapiganaji wa kweli wa maisha ya nchi hii, kwani walifanya kazi muhimu katika jitihada za maendeleo na kushiriki katika kukarabati miundombinu ya nchi, ambayo iliharibiwa vibaya. Walijenga shule, hospitali na hata vyuo vikuu."

"Nchi hii imeharibiwa vibaya na sisi wenyewe Wasomali, na hivyo tunapaswa kufanya kazi pamoja kuijenga, kwa sababu hakuna mtu mwingine atakayetujengea," alisema Farah.

Msemaji wa Serikali ya Somalia Abdirahman Omar Osman alisema kuimarishwa kwa usalama ni kitu cha msingi kwa ajili ya kurejea kwa wataalamu wa Kisomali walioko nje.

"Serikali ya Mpito ya Shirikisho imefanya jitihada kubwa za kurejesha msimamo katika hali yake, utawala wa sheria na heshima nchini," aliiambia Sabahi. " Leo, Mogadishu ni mahali salama na jitihada nyingine kubwa zinaendelea kulijenga jiji hili."

Osman alisema serikali imeweka mazingira sahihi ya wataalamu kutoka nje kurejea katika nchi yao na kushiriki katika ujenzi wake mpya. Alisema Waziri Mkuu Abdiweli Mohammed Ali amesafiri hadi Ulaya, Marekani na nchi nyingine za karibu kuwatia moyo Wasomali wanaoishi katika nchi hizo kurejea nyumbani.

Uwekezaji unaleta amani na msimamo kwa Somalia

Baadhi ya Wasomali waliorejea nyumbani, hususani wale wenye shahada za vyuo vikuu, wamechaguliwa kushiriki katika siasa, wakati wengine wamechagua kujihusisha na uwekezaji na fursa za elimu.

Hussain Abdulqadir, mfanyabiashara aliyerejea kutoka Kanada mwaka huu, anasema kuna fursa nyingi kwa Wasomali wote wanaoishi nchi za ugenini kurejea nyumbani na kuweka miradi ya uwekezaji.

"Kwa sasa ninafikiria kuweka mradi wa uwekezaji jijini Mogadishu," aliiambia Sabahi. "Nipo katika mchakato wa kuchunguza uwezekano wa kujenga mtambo wa kusafishia maji baada ya kugundua jinsi wananchi wanavyopata shida kutokana na ukosefu wa maji safi."

"Uwekezaji unaleta amani na msimamo katika nchi kwa sababu unaleta ajira kwa vijana, watu wasiokuwa na ajira ambao wangeshawishika kuwachukua maofisa wa ajira katika jeshi la mgambo," Abdulqadir alisema. "Tunapaswa kuionyesha dunia kwamba Somalia sio mahali pa vita na uharibifu tena na kwamba kuna upande mwingine wa maisha hapa."

Abdulqadir alisema miradi ya uwekezaji ya wataalamu wa Somalia waliokuwa wakiishi nje ingewatia moyo wageni kuwekeza. "Kama kuna usalama na utulivu nchini, uwekezaji wa wenyeji na wageni utaingia kwa wingi. Wawekezaji wanasubiri kurejea kwa utulivu," alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 17)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Mariam
    January 28, 2013 @ 01:04:49AM

    Ni nzuri sana kujua kuwa taifa letu linaimarika.

  • Abdi Osman
    August 8, 2012 @ 03:47:15AM

    Ndugu zangu, ujenzi wa majengo mapya bila ya kutatua masuala ya usafi kwa jumla nchini, hakutatusaidia kupata mabadiliko mengi yanayohitajika. Lazima jamii kwa jumla kuwa safi kwa sababu usafi ni kitu muhimu sana kwa taswira ya nchi. Ikiwa hakuna usafi, vitu vyengine vitakavyojengwa havitakuwa na thamani. Kwa sababu hii, Wasomali kutoka uhamishoni wanaorejea nchini lazima walinganishe baina ya usafi wa nchi wanazoishi sasa na ule wa mji wetu mkuu. Pia wafikiri namna gani tunaweza kufanya kuhusu masuala yanayohusiana na usafi na kuifanya jamii kushindana katika masuala ya usafi. Dini yetu inatufundisha kuwa usafi ni nusu ya imani. Asante sana. Abdi Osman.

  • axmed jaamac cali
    May 16, 2012 @ 09:20:23AM

    Kwa maoni yangu, nafikiri tulipiga hatua muhimu sana.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo