Mei 14, 2012
Wito wa kuwataka al-Shabaab kuendelea kupigana nchini Somalia uliotolewa na Ayman al-Zawahiri, kiongozi wa al-Qaida, ni jaribio la kuwapa moyo wapiganaji waliochanganyikiwa wasio na uhakika kuhusu hatima ya uhusiano wao na al-Qaeda, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na usalama wasema.
Katika video iliyorekodiwa na kutolewa Ijumaa (tarehe 11 Mei), al-Zawahir aliwataka washirika wa al-Qaida kupuuza juhudi za kuweka amani za kimataifa na kutumia mbinu za vita vya msituni dhidi ya majeshi ya maeneo nchini Somalia.
Muda wa kutolewa ujumbe huo, ambao umekuja baada ya kutolewa kwa nyaraka zilizogunduliwa katika maficho ya Osama bin Laden huko Pakistan, unaonesha kuwa al-Zawahir pia alitaka macho ya watu yaelekee kwengine na sio kwenye barua zilizoandikwa na bin Laden zilizoonesha mahusiano ya kulazimishwa baina ya kiongozi wa zamani wa al-Qaeda na al-Shabaab, wachambuzi wasema.
“Muda uliochaguliwa uko wazi,” anasema mchambuzi wa siasa Osman Mahmoud. “Al-Zawahiri alikuwa najaribu watu waelekeze macho kwengine kutoka maelezo ya kutia shauku katika nyaraka kama vile kashifa na mahusiano ya kulazimishwa baina ya vikundi viwili hivyo.”
Katika barua iliyoandikwa tarehe 7 Agosti, 2010, kiongozi wa zamani wa al-Qaida alimvunja moyo kiongozi wa al-Shabaab Mukhtar Abu al-Zubayr asitangaze wazi wazi ushirika na kikundi cha al-Qaeda, kwa kusema kuwa kuweka hadharani uhusiano na al-Qaeda ungewavunja moyo wafanya biashara wa Kiarabu katika kuwasaidia Wasomali na kungetengua uhusiano baina ya wanamgambo na watu wa Somalia.
“Ni wazi kuwa lengo la kiongozi wa al-Qaeda katika video hii iliyokusudiwa al-Shabaab lilikuwa ni kuondosha hofu na kupunguza mivutano na kuvunjika moyo kulikosababishwa na makala za bin Laden,” Omar Dahir, mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi na Mijadala cha Mogadishu, aliiambia sabahi. “Pia alikuwa anatafuta kuhakikisha kuwa mahusiano baina ya al-Qaida na al-Shabaab ni mazuri.”
Al-Zawahiri alikuwa anatafuta “kuwapa moyo wanachama wa al-Shabaab, ambao karibuni wamekumbwa na kupooza kwa matokeo ya operesheni zao kutokana na kampeni za kijeshi dhidi yao”, Dahir alisema.
Katika video hiyo, al-Zawahiri aliwataka al-Shabaab kuendelea na mapigano na wasiogope mashambulio ya angani. Akiwahutubia “simba wa Uislamu wa Somalia”, aliwauliza, “Mtafanya nini? Mtaiacha dhamana yenu ya kidini na kujisalimisha kwa dhuluma na kuungana nao na kwa hivyo, kujipeleka wenyewe katika ghadhabu ya muumba wenu?”
Akaongeza, “Wapigeni katika mtindo wa vita vya msituni ili kuwamaliza, kuwa angamiza na kuwalipua.”
Al-Zawahiri anailewa vyema hali ya udhaifu wa kijeshi ya al-Shabaab, ambapo ndio sababu kwa nini anajaribu kuwatia moyo, alisema mchambuzi wa siasa Abdirahman Hussein.
“Video hii mpya iliyotolewa na al-Zawahir kuwahutumia al-Shabaab hakuja kwa kushitukiza. Kilicho wazi ni kuwa kiongozi wa al-Qaeda anajaribu tena kuwapa moyo wapiganaji wa al-Shabaab ili kikundi kiweze kunyanyuka tena,” aliiambia Sabahi.
“Ujumbe huu unatoa kwa al-Zawahiri katika wakati ambapo al-Shabaab wamekuwa wakikabiliwa na mengi, mikwamo katika uwanja wa mapambano pamoja na uwezo wao kijeshi uliopungua,” Hussein alisema. “Al-Zawahiri anawataka al-Shabaab kutumia mbinu za vita vya msituni si kingine bali kiashirio kuwa anaifahamu hali ya kijeshi ya al-Shabaab na mikwamo mikubwa iliyokikumba kikundi hicho. Kwa sababu hii, anajaribu kuwatia moyo warejeshe operesheni zao za kigaidi kwa sababu hataki kuona kikundi kinakufa muda mfupi baada ya kujiunga na al-Qaeda.”
Huu ni ujumbe wa pili katika video kwa kikundi hiki tangu alipotangaza muungano rasmi wa al-Shabaab na al-Qaeda hapo mwezi Februari.
"Hotuba ya al-Zawahiri haina maana yoyote kwetu,” alisema Ahmed Mo'allim Fiqi, mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Somalia. “Tunauchukulia ujumbe huu kutoka [al-Zawahiri] kwa wafuasi wake nchini Somalia (al-Shabaab) si lolote bali jaribio la woga kutoka kwa kiongozi aliyechanganyikiwa.”
Katika taarifa iliyotolewa na Redio Mogadishu, ambayo ni redio rasmi ya Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia, Fiqi alisema, “Al-Shabaab na al-Qaeda ndio adui pekee wa watu wa Somalia.”
Aliuliza, “Al-Qaeda na al-Shabaab wamewapa nini watu wa Somalia zaidi ya vifo, uharibifu na umwagaji damu wa watu wasio na hatia?”
Fiqi alisema vikosi vya Somallia, kwa msaada wa watu wa Somalia, “tuna nia ya kuwasaka al-Shabaab na al-Qaeda mpaka watoke Somalia”.
Alitoa wito kwa wapiganaji wa al-Shabaab kuweka silaha zao chini na kujiunga na mchakato wa amani. Pia aliwataka wawaombe radhi watu wa Somalia ambao wamedhurika kutokana na vitendo vyao.
“Matendo yaliyofanywa na wafuasi wa al-Qaeda nchini Somalia ni bahati mbaya na kinyume na misingi na maadili ya Kiislamu,” alisema.
Al-Zawahiri anataka kuharibu maisha ya Wasomali ambao wamekuwa wakiteseka kwa umasikini na vita kwa zaidi ya miaka 20, alisema Aadan Abdullahi Mohammed, mchambuzi wa masuala ya usalama na kanali mstaafu kutoka jeshi la Somalia. Alisema kiongozi wa al-Qaeda anawataka wafuasi wake kukandamiza juhudi za amani za mitaa na kikanda nchini Somalia.
“Uchochezi huu wa al-Zawahiri ni bahati mbaya. Angetaka aturejeshe, kwa mara nyingine tena, katika vita, vurugu na kutokuwepo kwa utulivu,“ Mohammed aliiambia Sabahi.
“Watu wenye msimamo mkali wanaweza kujaribu kuanzisha mashambulizi ya kigaidi kama njia ya kuitikia wito wa al-Zawahiri, na ndio sababu vikosi vya usalama vinapaswa kuimarisha tahadhari katika viwango vyote,” alisema.
Mohammed aliwataka watu wa Somalia kulaani na kukataa uchochezi huu wa kiongozi wa al-Qaeda. “Somalia haitaki kumwaga damu zaidi ya watu wake wasio na hatia na pia hatuhitaji upande mmoja uchochee upande mwengine. Tunachotaka ni amani, utulivu na kuunga mkono juhudi za amani nchini mwetu,” alisema.
Mohammed alimshutumu kiongozi wa al-Qaeda kwa kuingilia mambo ya nchi yake. “Tunamtaka kiongozi wa al-Qaeda kutoingilia masuala yetu. Wasomali wanaelewa vyema hatima yao na ya nchi yao, na al-Zawahiri hana haki ya kukutukana.”
Ibrahim Abdullahi, mwandishi wa habari na mwandishi alliyejikita katika masuala ya vikundi vya Waislamu wenye misimamo mikali, alisema ujumbe wa video ya al-Zawahiri itakuwa na athari ndogo nchini Somalia.
"Kwa sasa al-Shabaab wako katika hatua isiyotia wivu na ya mashaka kutokana na kushindwa mfululizo kunapotokea siku hadi siku," Abdullahi aliiambia Sabahi. “Vikosi vya kijeshi vya Somalia na washirika wao wa Ethiopia, Kenya na AMISOM wamezidi kukaza kitanzi dhidi ya kikundi hiki na bila ya shaka watakimaliza tu.”
Abdullahi aliongeza, “Al-Qaeda kwa sasa hawawezi kutoa msaada kwa al-Shabaab nchini Somalia, kwa sababu wamepoozeshwa nchini Iraki, Afghanistani, Yemeni na Pakistani, sembuse Somalia iliyo mbali, ambayo iko mbali kutoka kituo cha al-Qaeda.
Kwa sababu hii, ujumbe wa al-Zawahiri ni kutumia vyombo vya habari tu na njia ya kuwafanya watu waelekeze macho kwengine kutoka kile kilichomo katika nyaraka za bin Laden,” alisema.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
zawahiri tafadhali wachana na watu wa Somalia wenyewe.
waaaaa runtiis al zawahiri waa in gaalada lala dagaa lamaa meel kasta oo ay dunida ka joogaan cadaan iyo madowba waa in lagu jahaadaa
Bado hamjachelewa kuamka. Kwa muda mrefu mmekuwa mkidanganywa na al-Qaeda na al-Shabaab ambapo wanaofaidika ni watu wachache kwa gharama za maisha yao.