Red_arrow

Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |

Wanawake wasaidia kulinda usalama jijini Mogadishu

Na Adnan Hussein, Mogadishu

Mei 11, 2012

  • 65 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Jeshi la polisi la Somalia limewajumuisha maafisa wa polisi wanawake ili kusaidia kuleta amani na utulivu na kuiwezesha Serikali ya Mpito ya Shirikisho kukabidhi serikali ya kuchaguliwa mwezi Agosti.

  • Maofisa wanawake ndani ya jeshi la polisi wakifanya gwaride kuelekea adhimisho ya makabidhiano kwa vifaa vilivyotolewa na serikali ya Japani mwaka huu ili kusaidia kulijenga upya jeshi la polisi la Mogadishu. [Na Stuart Price/AU-UN IST/AFP]

    Maofisa wanawake ndani ya jeshi la polisi wakifanya gwaride kuelekea adhimisho ya makabidhiano kwa vifaa vilivyotolewa na serikali ya Japani mwaka huu ili kusaidia kulijenga upya jeshi la polisi la Mogadishu. [Na Stuart Price/AU-UN IST/AFP]

  • Vikosi vya usalama vya wanawake na wanaume wakifanya kazi kwa pamoja huko Mogadishu, katika picha siku ya Ijumaa (tarehe 11 Mei). [Adnan Hussein/Sabahi]

    Vikosi vya usalama vya wanawake na wanaume wakifanya kazi kwa pamoja huko Mogadishu, katika picha siku ya Ijumaa (tarehe 11 Mei). [Adnan Hussein/Sabahi]

Kamanda wa Polisi Somalia Sharif Sheikhuna Meh aliiambia Sabahi kuwa polisi imewapatia mafunzo wanawake 1,800 tangu mwanzo mwa mwaka 2011. Alisema serikali ya mpito imefungua milango kwa wanawake kujiunga na jeshi na polisi kama njia ya kuvunja ukimya na woga unaosababishwa na washirika wa al-Qaeda, al-Shabaab.

Meh alisema kuwa wanawake vijana wamekuwa wakijiunga na jeshi kwa wingi na vituo vya mafunzo vya polisi ili kuwa maofisa, wanaopata mshahara wa dola za Kimarekani 200 kwa mwezi. Licha ya kuwa kazi ya polisi ni hatari nchini Somalia, imekuwa kazi inayochaguliwa na wanawake walio tayari kujitolea ili kuleta usalama nchini mwao, alisema.

Maafisa wa polisi wanawake sasa wanaweza kuonekana katika mitaa ya Mogadishu, kwenye majengo ya serikali, kwenye magari ya kijeshi yenye silaha, katika doria za polisi na katika polisi wanaongoza usalama barabarani, mambo ambayo hakuna hata moja kati yao lilikuwa linawezekana huko nyuma.

Kanali mstaafu Mohammed Osman Jilieo alisema wanawake wamekuwa na hamu ya kuitumikia nchi yao na kulinda utulivu na usalama wa watu wa Somalia.

Jilieo alisema mipango ya mauaji kutoka Waislamu wenye msimamo mkali na kukataa kwa familia zao kulitumiwa ili kuwazuia wanawake wasijiunga na vikosi vya jeshi na polisi, kwa vile iliaminika kuwa kunaweza kuwabadilisha imani na mila zao.

Ili kuweza kufuzu kujiunga na jeshi, wanawake wanapitia katika mafunzo magumu katika kambi ndani na nje ya Somalia.

Jenerali Hussain Mukhtar Afrah, kamanda wa polisi wa Somalia maarufu katika kuongoza vita vilivyoanzishwa na Muungano wa Mahakama za Kiislamu mwaka 2006, aliiambia Sabahi kuwa polisi inawafunza wanawake katika vyuo vya Mogadishu vilivyoko katika kijiji cha Armo, karibu na Bosaso.

Alisema juhudi za kuimarisha polisi wenyeji kunatoa fursa ya kupunguza mzigo wa askari katika misheni ya Umoja wa Afrika ya kulinda amani.

Afrah alitoa wito kwa watu wa Somalia kuendelea kuisaidia serikali ya mpito kwa kuwaruhusu mabinti wao kujiunga na jeshi la usalama kama njia ya kupunguza vurugu na kumaliza utawala wa watu wenye itikadi kali katika maeneo ya katikati na kusini mwa nchi.

Fatima Osman, mwenye umri wa miaka 24, alimaliza mafunzo yake katika kituo cha polisi Manyani huko Mombasa, Kenya, na amekuwa akifanyakazi kama afisa ya polisi kwa miezi minne sasa.

Osman aliiambia Sabahi kuwa anafurahia kuitumikia nchi yake na watu wake. Alisema anataka kusaidia kurejesha utulivu na kuuweka muundo wa serikali utakaomruhusu kila mtu kuishi kwa amani.

Alisema wanawake vijana kama yeye mwenyewe walianza kujiunga na polisi na jeshi kwa wingi mwaka jana, wakati Serikali ya Somalia na vikosi vya washirika vilipowafukuza al-Shabaab kutoka kambi zao mjini Mogadishu.

Kanali Abdullah Shinoo, kamanda wa kikosi cha ulinzi wa raisi huko Villa Mogadishu, aliiambia Sabahi kuwa kuwaingiza wanawake katika vikosi vya usalama kunasaidia upekuaji wa majumbani na kuwapekua wanawake katika sehemu za umma.

“Baadhi ya wahalifu hujificha nyuma ya wanawake,” Shimo alisema. “Wanamgambo wa al-Shabaab na wafanya biashara za madawa ya kulevya hutumia wanawake wa majumbani mwao kuficha silaha na bidhaa zao, na matokeo yake, operesheni za kuwakagua huishia kushindwa.

Habiba Ahmed, mwenye umri wa miaka 22, anafanyakazi kama afisa ya polisi katika kituo cha Upekuzi cha Afgoye katika eneo la kuingilia mjini Mogadishu. Wapanda pikipiki kutoka upande ulipokuwa kambi ya al-Shabaab ya Elasha Biyaha na Afgoye wanapekuliwa katika kituo cha upekuzi kabla ya kuingia mjini.

Ahmed huwa anawapekua wanawake ili kuhakikisha kuwa hawapiti na silaha au milipuko. Askari wa kiume wa vikosi vya usalama hufanya idadi kubwa ya upekuzi wa vyombo na abiria.

“Ninajihesabu kama shujaa kwa sababu nimezuia operesheni nyingi za wanawake wanaosafiri kutoka maeneo yanayodhibitiwa na al-Shabaab kuelekea Mogadishu,” Ahmed alisema. “Niliweza kufichua mashambulizi ya kujitoa muhanga na magendo ya silaha kuingia katika soko la Bakara katika operesheni iliyovilenga vikosi vya usalama."

Ahmed alisema uamuzi wake wa kujiunga na vikosi vya usalama ni wake binafsi.

“Bado ninapambana na kung’oa ugaidi uliomuua kaka yangu katika mji wa mwambao wa Merca. Alishutumiwa kufanya upelelezi kwa ajili ya vikosi vya serikali kwa sababu alikuwa mwanafunzi, na hakuweza kusherehekea miaka yake 20 ya kuzaliwa,” alisema. “Tulilazimika kuuhama mji, na kwa sababu hizi, niliamua kujiunga na polisi ili niwezi kuwa shujaa wa kuwawinda maadui wa amani.”

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 70)

Dislike_icon(11)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Edward # 195
    July 30, 2012 @ 03:50:10PM

    Sikuwahi kujua kuwa hili ni suala linaloweza kuchunguzwa. Bwana Kamishna nifikirie mimi kesho tarehe 31/07 kwa ajili ya kunisikiliza , kwa sababu nimefanya juhudi ya kujifunza zaidi kuhusu Somali. Kwa kweli wanawake ni nuru ya maisha ya wanaume.

  • faddy
    July 26, 2012 @ 03:38:25AM

    behind a succesful man there must be a woman otherwise kidole kimoja hakistiri chawa.

  • Janet Wanjiku
    July 24, 2012 @ 05:09:54AM

    Wanawake wa Somalia katika jeshi na polisi!! Hongera. Al-Shabaab angalieni sana: chaguo lenu zuri zaidi ni kujiunga na juhudi za amani katika nchi yenu na mchague amani, upendo, mapatano na maendeleo badala ya itikadi. Hatuwezi kula itikadi na kila mtu nchini Somalia anahitaji kuuungana mkono na mama na dada zao ambao wamepinga mila na kuyaweka maisha yao mbele ili kurejesha amani kwa nchi hii inayopendeza. Hongera mabibi, hongera, Mungu yupo pamoja nanyi. Endeleeni, Endeleeni, Endeleeni.

  • ck
    June 6, 2012 @ 04:46:17AM

    Wanahitajika watu milioni moja kujenga heshima nzuri, lakini anahitajika mpuuzi mmoja tu kuharibu kila wengine walijenga…Lucky Philip Dube. Wanawake ni nguzo ya amani na tendo hili la kujitolea la wanawake wa Somalia litaipa Somalia sura tofauti. Endelee… jengeni taifa lenu kwa faida ya watoto wenu na watoto wa watoto wenu. Si kazi rahisi, inafanyika. Mwisho, sauti za watoto wanaolia zitachukuliwa nafasi na sauti za vicheko. Kwa al-Shabaab, hawajui kile wanachokifanya kwa nchi yao.

  • john cherutich
    June 4, 2012 @ 10:09:08AM

    Ninapenda mafanikio ya AMISOM na jeshi la Somalia. Ikiwa hawakuchunguzwa, al-Shabaab wanaweza kujichanganyisha na watu hapo baadaye na kuanza tena uhalifu dhidi ya binadamu.

  • 33881
    June 4, 2012 @ 09:34:37AM

    Nadhani ni kazi kubwa na ya kishujaa ya vijana hawa kukubali kazi ngumu kama hii.

  • Bilal Al-Somali
    June 2, 2012 @ 07:57:41PM

    Nzuri sana. Inshaallah mtasafisha hatari.

  • Paul Adhoch
    June 2, 2012 @ 11:57:45AM

    Wanawake wakubwa wa Somalia. Ninawapongeza..

  • Geoffrey muricho
    June 1, 2012 @ 09:36:06AM

    Asanteni wanawake wa Somalia. Ninawaheshimu.

  • MWIKA T
    May 31, 2012 @ 08:41:42AM

    Hongera mabibi wenye uwezo nchini kwa kazi nzuri ya kujiunga na uaskari kwa adui yenu. Ooo Mwenyezi Mungu, washushie Baraka zako. Wajaalie al-Shabaab wang’olewe ili amani, upendo na utulivu vitawale. Hongera tena na tena.

  • connie juma
    May 30, 2012 @ 12:05:40PM

    Vidole juu kwa wanawake wazalendo wa Somalia na ni sifa kwao kuwa katika jeshi la polisi.

  • stanley
    May 30, 2012 @ 11:22:38AM

    Makala hii imeandikwa vizuri, kwa kuwa wanawake wa Somalia wameweza kujitolea kuleta utulivu katika nchi yao kama njia ya kuendeleza kazi za kuvunja mgongo majumbani kwao kwa usalama wa taifa lao "Ninawaheshimu na endeleeni." Magaidi wengi hujificha nyuma ya wanawake. Wakati umefika kwa wao kujisalimisha.

  • abdul
    May 30, 2012 @ 08:07:03AM

    Endeleeni, mabibi zangu.

  • caroline oundo
    May 30, 2012 @ 03:35:25AM

    Ninawasalimu na kuwapongeza wanawake wa Somalia, Mungu akubarikini. Asanteni. Caroline

  • Shila
    May 29, 2012 @ 10:45:54AM

    Ni nzuri sana, tunaipenda hiyo hapa nchini Kenya. Ni vizuri kuwa kuna kiwango fulani cha busara nchini Somalia. Tunataka Somalia istawi tena. Wasichana jasiri. Songeni mbele! Songeni mbele! Songeni mbele! Songeni mbele!

  • evans omega
    May 29, 2012 @ 05:57:05AM

    Vidole juu kwa wanawake wa Somalia

  • Isaac Karimi
    May 28, 2012 @ 06:07:42AM

    Heko wanawake wa Somalia, hili ni jambo kubwa. Lazima muwe chombo cha amani ambayo dunia imekuwa ikisubiri kwa miaka mingi. Mungu awabariki na endeleeni na moyo wenu.

  • VICTOR LAGAT
    May 28, 2012 @ 04:58:55AM

    Wanawake ni mama/wazazi wetu, kama walivyo wanaume. Tunawataka watuunge mkono au kuliunga mkono taifa. Wapeni nafasi sawa ya kuchangia maendeleo ya taifa. Piganieni haki zenu. Tunawaunga mkono. Kila la heri.

  • tiberius kisiangani
    May 28, 2012 @ 01:13:58AM

    Ni vizuri kwa wanawake kupigana na kufa kwa ajili ya taifa lao. Hongera wanawake wa Somalia.

  • thomas kerongo
    May 27, 2012 @ 01:17:39PM

    Hongera kwa wanawake wetu wa Somalia kwa uwajibikaji wao katika kumaliza janga la nchi yao. Hongera.

  • barrack
    May 27, 2012 @ 05:05:49AM

    Wanawake wa Somalia, ninawaamkia na kuwapongeza.

  • mwangij
    May 27, 2012 @ 01:01:45AM

    Wanawake wana kila haki ya kuongoza dhamira hii. Ni wao wanaovumilia ghadhabu za vita kwa vile hawawezi kukimbia bila ya watoto wao. Wanawake pia wana ushawishi na mvuto. Wao ndio suluhisho. HONGERA mabibi, unganeni na okoeni nchi yenu.

  • W. MWANGI
    May 26, 2012 @ 10:40:18AM

    Hiyo ni hatua ya kuwa na wanawake katika ujenzi wa taifa na pia kuhubiri amani kwa jamii yote ya Somalia. Haya ni mapambazuko kwa nchi hii na pia kuonesha kuwa wanawake wa nchi hii sio tu wanaweza kuitumikia nchi bali pia kuiongoza. MUNGU, TUNAKUOMBA UIKOMBOE SOMALIA KUPITIA MAJESHI YETU.

  • njuni james
    May 25, 2012 @ 08:19:28AM

    Wanawake kwa kweli ni watu wanaofaa kuituliza Somalia na nchi nyingine yoyote ulimwenguni. Hongera kwa wazo hilo!

  • joseph mwandairo
    May 25, 2012 @ 05:40:39AM

    Hiyo ni hatua mbele kwa majirani na ndugu zetu wa Somalia, kuweni na amani kwenu ni lazima wanawake washirike....Mapambano Yanaendelea!

  • obbyero erick
    May 25, 2012 @ 03:31:16AM

    Anachoweza kukifanya mwanaume, mwanamke anaweza kukifanya bora zaidi!

  • abdifatah mohamed
    May 24, 2012 @ 03:23:48PM

    Wau! Hii inatia moyo. Nimefurahi kuona mama zetu wanashiriki katika amani ya nchi yetu na wako tayari kusafisha uchafu toka nchini mwetu.

  • ali omar
    May 24, 2012 @ 08:54:12AM

    Hongera kwa wanawake ambao wanaendelea kulinda amani kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa ajili ya jamii na tunathamini sana juhudi zao.

  • Joram Odima
    May 24, 2012 @ 06:20:25AM

    Hiyo ni sifa kubwa sana kwa serikali ya Somalia na kwa wanawake ambao wamebaini kuwa usalama wao unawategemea wao. Waafrika wengine wanapaswa kuiga utamaduni huu.

  • issadhin
    May 23, 2012 @ 12:43:03PM

    Kazi nzuri sana wanawake wa Somalia. Mungu akipenda atawasaidia katika kila kitu wanachokifanya.

  • fuad musa
    May 22, 2012 @ 07:56:47AM

    WAKATI WA AMANI UMEFIKA, TUIEPUSHE NA ITIKADI CHAFU. BAADHI YA WATOTO HAWAJUI NENO AMANI MAANA YAKE NINI...KAMBI ZA WAKIMBIZI HAZIKUKUSUDIWA WASOMALI PEKE YAO.

  • regina
    May 22, 2012 @ 07:40:32AM

    Heshima kwa dada zetu.

  • John W. Kang'ethe
    May 22, 2012 @ 05:43:34AM

    Hongera wanawake wa Somalia. Esther katika Biblia, Mariamu Dada wa Musa miongoni mwa wengine, ni mashujaa wa zamani. Wanawake wa Somalia wapewe na naamini watachukua nafasi ambayo ni haki yao katika jamii yao na kujenga kile ambacho wanaume wameshindwa na daima watashindwa kufikia uongozi wa kweli usio na uchoyo. Mungu ibariki Somalia, Mungu wabariki wanawake wa Somalia na Mungumbariki mwandishi wa makala hii nzuri.

  • Omwansa Lionel
    May 22, 2012 @ 01:08:57AM

    Kazi nzuri Somalia kwa kuwashirikisha wanawake katika kurejesha amani nchini. Pia wahamasisheni na kuwashirikisha vijana. Ninawatakieni mafanikio katika kila jitihada mnazozifanya.

  • victor nyami
    May 21, 2012 @ 07:16:38AM

    Ni wazo zuri sana kwa Somaliland kuwaruhusu wale wenye nyoyo nzuri kujiunga na jeshi, wanaelewa uchungu wa kuzaa watoto. Ninawapenda kwa sababu wao ni walinzi wetu wa kwanza. Karibuni mtakuwa na amani lakini watumieni kama mama na dada zetu halali. Kila la heri.

  • cabdishakuur
    May 21, 2012 @ 04:21:13AM

    Ninakataa kwa nguvu zote wanawake kuwa polisi au mambo yanayohusiana na hayo kwa sababu wanaweza kudhurika haraka.

  • Brian Mandela
    May 21, 2012 @ 03:41:07AM

    Wanachoweza kufanya wanaume na wanawake wanaweza kukifanya. Yote yanaanza na sisi. Wanawake wa Somalia wameanzisha jambo zuri na naamini halitakuwa bure. Hongera! Maadui wa amani lazima wang’olewe moja kwa moja.

  • Filsan Abdillahi
    May 21, 2012 @ 03:06:42AM

    Kazi nzuri dada zangu. Mwenyezi Mungu akipenda tutakuwa na amani nchini Somalia karibuni. Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kusubiri.

  • Felisiah Nelly
    May 20, 2012 @ 11:29:50AM

    Ili mtu awe mkamilifu lazima awepo mwanamke. Wanawake wanajulikana kama walinda amani kwa sababu kila panapokuwepo na vita wao ndio wakaanza kuathirika. Kwa hivyo ili Wasomali wawe na amani lazima mwanamke ahusike. Hongera wanawake wa Somalia na Mwenyezi Mungu atawajaalieni ushujaa wa kutosha ili kuwaangusha al-Shabaab.

  • fredrick muoki
    May 20, 2012 @ 07:36:57AM

    Mshikamano hufanikiwa...

  • Bryceson L Nassari
    May 19, 2012 @ 07:22:50AM

    Kuwaruhusu vijana wa kike kujiunga na Polisi na Jeshi la Ulinzi ni njia ya kuiokoa nchi ya Somalia. Kwa muda mrefu wanawake wa Somalia kwa sababu za kimila na imani za kidini walikuwa hawapewi fursa ya kuilinda nchi yao. Kwa sasa haitawasaidia wanawake na watoto waliokwishafariki. Kwa hivyo wanawake ni wazuri katika kuilinda jamii hasa wanawake na watoto. Ninaunga mkono programu hii.

  • pm macharria
    May 19, 2012 @ 04:50:22AM

    Wanaweza kwa sababu Mwenyezi Mungu yuko pamoja nao, kwa hivyo wanawake, msirudi nyuma.

  • vincrent lex
    May 19, 2012 @ 04:17:47AM

    Hii ni hatua nzuri ya kuleta amani, ni mwanamke tu anayejua maumivu ya umwagaji damu yalivyo.

  • martin mutethia
    May 18, 2012 @ 10:50:54AM

    Anachoweza kufanya mwanamme na mwanamke anakiweza.

  • Joel Nandwa
    May 18, 2012 @ 08:40:53AM

    Somalia iliyoungana italeta amani na utulivu inayositahiki. Hili halitawafaidisha wao tu bali pia zitafaidika nchi inazoizunguka na ulimwengu kwa jumla. Hongera kwa wanawake ambao wapo kutimiza ndoto hii.

  • Rose
    May 18, 2012 @ 08:37:29AM

    Hongera wanawake wa Somalia. Ni watu pekee wanaoweza kusaidia kuleta amani nchini mwao. Wanaoteseka kwanza ni wanawake na watoto wakati wa migogoro. Tunamuomba Mwenyezi Mungu kuwasaidia na kuwapa nguvu. Amani nchini Somalia maana yake ni amani kwa Afrika.

  • prince tasher
    May 18, 2012 @ 04:04:49AM

    Nafikiri ni mfano mzuri kwa wananwake wengine ulimwenguni na ningependa kuwapongeza wanawake wa Somalia kwa ujasiri na motisha yao. Mwenyezi Mungu awalinde katika misheni yenu.

  • mutheu muoki
    May 18, 2012 @ 02:36:59AM

    Ndio, ninachoweza kusema ni kuwa wanawake wanapata wanachostahiki na kama alivyosema mmoja kabla, inapaswa wapewe nafasi nyingi za uongozi. Hongera mabibi wa Somalia.

  • Amat M. Omar
    May 17, 2012 @ 01:13:48PM

    Kwa nini kusema uongo? Wanawake wanajulikana kuwa ni watu wa amani ulimwenguni kote. Kwa kweli wanawake wa Somalia ndio walioathiriwa zaidi katika vita hivi visivyo maana. Ninamuomba Mwenyezi Mungu kuwapa ujasiri na nguvu ili kupambana na wahalifu hawa.

  • Peter Titi
    May 17, 2012 @ 11:30:51AM

    Nimefurahi kusoma kuwa Wanawake wa Kiislamu wa Somalia wanaweza kusaidia kuwang'oa al-Shabaab. Endeleeni akina dada na karibuni hivi nchi yenu itakombolewa kutoka kwa majambazi wa al-Shabaab.

  • domy
    May 17, 2012 @ 10:27:37AM

    Ndio, mazingira ya amani ndiyo tunayohitaji.

  • David Sikuku
    May 17, 2012 @ 09:15:01AM

    Asanteni sana dada wa Somalia ambao ni walinda amani ya taifa. Ifanyeni Somalia kuwa taifa la amani sio taifa la vita. Tunawaombeeni kwa Mwenyezi Mungu awape nguvu ya kulishughulikia suala la ugaidi. Tuko nyuma yenu.

  • MWANGI
    May 17, 2012 @ 08:44:05AM

    NIMEIPENDA MAKALA HII, NI NZURI SANA.

  • kuthur Moha
    May 17, 2012 @ 05:47:20AM

    Nafikiri al-Shabaab wangeingia katika aina Fulani ya mazungumzo na ‘serikali’ au ‘utawala’ wa sasa wa Somalia kwa vile nawao pia ni Wasomali, kwa ajili ya amani itawale nchini. Visa visivyokwisha vitaleta mateso yasiyosemeka kwa watu wa Somalia ambao sasa ni wakimbizi wasiotakiwa popote kwa sababu dunia ‘imechoka’ nao. Wasomali, ambao huko nyuma walikuwa watu wanaojivunia, sasa wamekuwa waombaji na wavushaji magendo na watu wachache wanawaamini kwa sababu ya ‘viwango vyao vidogo vya elimu.’ Wasomali wanapaswa kuchukua hatua kubwa ya amani na nchi yao itaweza tena kuwa taifa kubwa la mashariki ya Afrika lenye kauli ya kuheshimika katika masuala ya Afrika.

  • hamse
    May 17, 2012 @ 04:13:33AM

    Sifa ziende kwa Mwenyezi Mungu. Nimefurahi sana kuona amani inarejea Somalia baada ya juhudi zilizofanywa na Wasomali ambao kwa muda mrefu walikuwa wahanga wa majanga. Itakuwa bahati mbaya kwa kikundi chochote cha Somalia kupingana na urejeshaji amani nchini. Wasomali inawabidi wapate somo kutokana na matatizo wanayokabiliana nayo kwa muda mrefu na kuwa makini na amani na mafanikio ya nchi. Watu wa eneo la kusini mwa Somalia inawabidi kuwasiliana na kujifunza kutoka kwa watu wa Somaliland ambao walijipanga wenyewe na kuweka mfumo wao wa serikali ya kikanda baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini. Ni Somalia ambayo leo inahitaji msaada kutoka Somaliland lakini Somaliland haihitaji msaada wowote kutoka Somalia. Ninamuomba Mungu kuwasaidia Wasomali kufahamu maslahi yao. Amin.

  • Prophetess Catherine njeri gichinga
    May 17, 2012 @ 03:53:48AM

    Inaonesha kama Mungu aliwaumba wanawake wawe viumbe imara…wanawake ni viongozi na waendeshaji wazuri…nasikitika nina watoto wa kiume, lakini nafikiri wanaume katika uongozi wameshindwa ulimwenguni kote. Wameshindwa kwa Mungu Muumbwa wao!!! Hii ni ishara nzuri kutoka peponi, ambapo wanawake wako tayari kuwa walinzi wa amani katika Somalia iliyoteketea...Ninaomba kuwa karibuni sana sisi kama Wakenya tutaweza kutembelea Somalia kama watalii siku moja...Faidini amani!! Yesu awabariki!!

  • Wadani
    May 17, 2012 @ 02:50:44AM

    Ni mapema sana kutabiri kuwa al-Shabaab wamedhoofika na kuwa busara na amani inaingia. Pamoja na udhaifu wa al-Shabaab, hao walio mbadala ni dhaifu zaidi. Serikali kuishi katika hali ya kusaidiwa, na wanawake kujiunga na vikosi hakutabadili kitu. Tunachohitaji ni utawala bora na viongozi na makamanda wawajibikaji. Hawa askari wa kukodiwa wanaoitwa (PS), ambapo wale wanaojiita viongozi katika TFG hawawezi kujibu na kuzingatia mikataba yao, hilo linaloitwa bunge ni chombo kilichokufa, na mawaziri wachoyo walioko kule kwa maslahi yao binafsi, askari wa AMISOM kutoka nchi mbaya zaidi za Afrika hawawezi hata kuzisaidia nchi zao kwa kurejea katika maisha ya kawaida wao wenyewe na bado wanapewa fursa zote na jumuiya ya kimataifa.

  • indes eddy
    May 17, 2012 @ 02:25:53AM

    Usawa lazima uheshimiwe. Hongera wanawake wetu.

  • Joseph Kimondo
    May 17, 2012 @ 01:59:23AM

    Hakika. Somalia inakomaa. Wanawake ni watu na kwa kweli wanatumikia kwa utendaji mkubwa.

  • joe kam
    May 16, 2012 @ 12:22:53PM

    Hongera kwa wanawake wa Somalia kwa kujitolea na kukubali changamoto hii ya kulinda nchi yao kutokana na ugaidi. Nafikiri watakuwa mashujaa wetu na mama wa Somalia na ulimwengu kwa jumla.

  • Kimario Ngalai
    May 15, 2012 @ 07:00:51AM

    Hongera sana dada yangu kwa ushujaa ulionesha

  • Ali Abdirahmaan hashi
    May 14, 2012 @ 08:19:15AM

    Kwa maoni yangu, nafikiri al-Shabaab wamedhoofika na hawana nguvu ilizokuwa nazo mwaka jana. Kwa hivyo, ningependa kuiomba serikali na umma kwa jumla kuanzisha mkakati bora zaidi wa kuwamaliza wanachama wa kikundi hiki nchini.

  • MULEI MUSYOKI
    May 12, 2012 @ 10:08:21AM

    Ni vyema kuwa tuna busara kidogo Somalia. Waacheni wanawake wachukue nafasi sio tu katika jeshi lakini kokote kule mwanaume anakoenda. Huku kupigana nchini Somalia kulianza wakati nikiwa mdogo na sasa mimi ni mzee, na bado hamjachoka kupiga watu wenu. Tafadhaleni acheni vita na anzeni kujenga nchi yenu. Kuweni kama majirani zenu. Wao wako na amani. Tumuombe Mungu atuletee malaika wa amani nchini Somalia ili matatizo haya yamalizike.

  • chef mogotu
    May 12, 2012 @ 07:02:45AM

    Tunachohitaji ni amani tu, hii inaweza kupunguza matatizo. Na hao al-Shabaab waache kutishia vikosi.

  • Johan Ras
    May 11, 2012 @ 09:51:34PM

    Nzuri sana. Wanawake ni lazima watumike sawa na wanaume katika nyanja zote za kuzuia uhalifu na kupambana na ugaidi. Wao pia ni mama ambao wana athari kubwa kwa watoto wao. Hawa ni walinda amani wa kweli.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, katiba ya Kenya inapaswa kurekebishwa ili kulipa baraza jipya la Seneti madaraka zaidi?

Angalia matokeo