Mei 09, 2012
Wazalishaji wengi wamekuwa wakifunga maduka yao mjini Kenya kwa sababu ya gharama kubwa za nishati na uzembe katika bandari ya Mombasa, miongoni mwa manung’uniko mengine, ambayo baadhi ya wenye viwanda wanasema yanatishia ushindani wa Kenya.
“Wakati umefika kwa serikali kushughulikia suala la nishati, miundombinu na urasimu ili kupunguza gharama za kibiashara nchini Kenya,” alisema Betty Maina, mtendaji mkuu wa Jumuiya ya Wazalishaji wa Kenya, kikundi cha ushawishi cha wenye viwanda.
Maina alisema kuwa wazalisshaji wamejiondosha kwa sababu ni gharama sana kufanya biashara nchini Kenya, katika hali zote, uzalishaji na usafirishaji.
“Muda inaochukua kutoa mizigo katika bandari ya Mombasa na usafirishaji kuelekea sehemu husika kunaathiri uzalishaji kwa idadi kubwa ya kampuni za uzalishaji. Bado kuna suala la kushughulikia makaratasi, kunakosababisha ucheleweshaji wa kutoa mizigo, na kwa hivyo kufanya iwe vigumu kupata mizigo yako toka bandarini kwa wakati,” alisema.
Baadhi ya makampuni yamehamia sehemu nyingine za bara yakiwemo Colgate-Palmolive, Reckitt Benckiser na Cadbury, ambayo imehamisha sehemu kubwa ya shughuli zake za utengenezaji wake wa chokoleti kuelekea Afrika Kusini.
Mwezi Aprili, Benki ya Dunia ilitoa taarifa ya uchunguzi wa kurahisisha ufanyaji wa biashara, iliyoonesha kuwa licha ya uimarishaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo Kenya ilionekana kupoteza uwezo wake wa ushindani kwa nchi kama vile Afrika Kusini, Misri, Mauritius na Rwanda.
Ripoti hiyo inasema hadhi ya Kenya ilishuka kutoka nafasi ya 98 mwaka 2011 hadi 109 mwaka 2012, katika uchunguzi wa kiuchumi wa nchi 183. Kwa nchi za Afrika Mashariki, Rwanda ilishika nafasi ya 45, Uganda ya 123, Tanzania ya 127 na Burundi 169. Nchi hizi zote zilionesha ama kuimarika au kubakia katika nafasi zao zile zile.
Ripoti hiyo inalaumu gharama za nishati, miundombinu mibovu na kusuasua kwa mchakato wa kisheria katika kutatua migogoro ya biashara kama sababu za kushuka kwa Kenya.
“Kiwango cha juu cha bei za umeme tayari zimeleta athari hasi kwa sekta ya uzalishaji nchini,” Maina alisema. “Jambo hili kinyume chake kinaumiza ushindani wetu katika soko la kimataifa, kwa vile bidhaa zinazozalishwa nchini zinakuwa na bei ya juu kuliko zile zinazozalishwa katika nchi zenye ushindani.”
Mamlaka ya Bandari ya Kenya (KPA) inasema matatizo ya kujazana mizigo na ucheleweshwaji bandarini yanashughulikiwa.
“Tunakabiliwa na changamoto nyingi za kiutendaji, ambazo zinashughulikiwa kwa msaada wa washirika wa maendeleo na sekta binafsi wakati tunafanyiakazi ufumbuzi wa muda mrefu,” Mkuu wa mawasiliano wa shirika Bernad Osero aliiambia Sabahi.
Alisema serikali imewekeza shilingi bilioni 10 (sawa na dola za Kimarekani 120) kwa upanuzi wa bandari na uwezo wa utendaji, ikiwa ni pamoja na kazi za upakuaji, ujenzi wa pahali pa kufungia gati, na kuboresha teknolojia ya habari na mawasiliano. Haya yatakamilishwa na ujenzi wa bandari ya Lamu iliyopendekezwa, na kuzinduliwa na Raisi Mwai Kibaki mwezi Machi.
Zaidi ya hayo, serikali ilizindua mradi mwezi Januari ili kuongeza ufanisi na uwezo wa bandari ya Mombasa.
Serikali pia inasema sekta ya nishati imejengwa upya ili kukidhi ipasavyo mahitaji ya viwanda na watumiaji wa meme majumbani.
“Serikali inazishughulikia changamoto hizo kupitia upanuzi wa haraka wa uwezo wa umeme na kupandisha hadhi mitandao ya utoaji na usamabazaji na kuongeza uwekezaji katika vyanzo vya nishati mbadala,” msemaji wa serikali Alfred Mutua aliiambia Sabahi.
Mwezi uliopita, serikali ilitia saini makubaliano na kampuni ya Kichina ili kuipatia Kenya umeme rahisi kutokana na umemejoto wa ardhini.
Kampuni ya Unilever Group, yenye makao yake Uingereza na ambayo ina maslahi mengi ya uzalishaji nchini Kenya, ilikutana na Waziri Mkuu Raila Odinga hapo mwezi Aprili kuiomba serikali kuingilia kati baadhi ya changamoto za kibiashara zinazoikabili jamii.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Unilever Paul Polman, hata hivyo, alimhakikishia Odinga kuwa kampuni yake haitahamisha kiwanda chake kutoka Kenya, licha ya kupanda kwa gharama.
"Kinyume chake, tunawekeza sana katika uvumbuzi, shughuli za kuimarisha soko, uwezo wa uzalishaji, teknolojia, uwezo wa kufanya kazi, kusambaza miundombinu na uimarishaji wa vipaji," Polman alisema.
Naye Jonathan Chifalu, meneja wa mawasiliano katika Eneo la Ushughulikiaji Usafirishaji, alisema idadi kubwa ya makampuni katika eneo hilo, lililoko kama kilomita 10 kutoka Nairobi, yalipata hasara ya shilingi mioni 20 (dola 240,000) mwezi Aprili kutokana na kukatika kwa umeme, kulikodumu siku tatu mfululizo.
"[Makampuni] yalilazimika kutumia majenerata ya dharura ambayo ni ghali sana kuyaendesha," aliiambia Sabahi.
Vile vile, kampuni ya Orata International, Ltd., ya uzalishaji wa chakula cha mifugo ilioko katika wilaya ya viwanda mjini Nairobi, ilisema ilipoteza zaidi ya shilingi milioni 3 (dola 36,00) baina ya mwezi machi na Aprili kutokana na kukatikakatika kwa umeme.
"Ni shida sana kuendesha biashara kukiwa na ukatikaji wa umeme mfululizo ambapo hakuna yeyote aliyetuelezea juu ya suala hilo kabla," Meneja utawala wa Orata Lyadi Orata aliiambia Sabahi.
Ushirika wa Sekta Binafsi wa kenya (KEPSA) unasema utaratibu mkubwa sana wa kupata kibali cha biashara kunawavunja moyo wawekezaji.
"Sababu kubwa Rwanda iko mbele ya Kenya ni kwa sababu ni nchi pekee katika kanda hii ambayo imeweka mfumo wa kutoa huduma sehemu moja ambao unafanyakazi kweli," Mwenyekiti wa KEPSA aliiambia Sabahi.
Obath asema Kenya inahitaji kufanya marekebisho ya mfumo wa sheria ili kutoa maamuzi ya masuala yanayohusiana na mizozo ya kibiashara.
Licha ya changamoto za kukatika kwa umeme mara kwa mara na mzigo mkubwa wa urasimu unaowekwa katika sekta ya biashara, bado kuna mwonekano hasi, anasema Aly Khan Satchu, mchambuzi wa sekta ya uwekezaji inayoibuka jijini Nairobi.
Aliiambia Sabahi kuwa ukuaji umekuwa ukikwamishwa katika sekta ambayo inategemea zaidi nishati, lakini idadi kubwa ya makampuni yasiyokuwa ya uzalishaji yanaendelea kujiandikisha kwa kasi kubwa.
Kisichovutia ni sekta inayotumia nishati kwa wingi. Kuna idadi kubwa ya makampuni ya kimataifa yaliyoko Kenya, kwa mfano, katika teknolojia ya habari na mawasiliano, kama vile Visa, MasterCard na mengineyo," Satchu alisema.
"Hata hivyo, ikiwa serikali haitalishughukia tatizo la nisharti ambalo linazorota, mipango ya maendeleo ya Dira ya 2030 inaweza isilete matunda, alisema.
"Gharama kubwa ya umeme haikubaliki hata kidogo, Maana yake ni kuwa hatuko kiushindani ulimwenguni linapokuja suala la uzalishaji." alisema.
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
Sampuli ya DNA iliyochukuliwa kwenye mswaki uliokuwemo kwenye begi lililokuwa na risasi lililopat...
Wakenya kumi na wasaba wameshtakiwa kwa kuvunja amani, kufanya ghasia na ukatili dhidi ya wanyama...
Al-Shabaab imedai kuhusika na urushwaji wa makombora kwenye kasri ya rais mjini Mogadishu siku ya...
Wanajeshi wa Uganda wa Kikosi Namba 9+ wanarudi nyumbani baada ya kukamilisha miezi 13 ya ziara y...
Kikosi cha polisi cha Kenya kitaanza uhakiki wa kina wa maofisa mwezi ujao, kikianza na kusaili w...
Ujambazi ulizuiwa katika ofisi za usalama za Wells Fargo huko Mombasa ulisababisha kifo cha watu ...
Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliahidi msaada wa nchi yake katika kipindi cha ujenzi mpya wa ...
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Vyanzo vya nishati mbadala vinaweza kusaidia kutatua matatizo mengine ya kimazingira ya eneo. Eneo hili linakabiliwa na kukua kwa haraka viwango vya uharibifu wa hali ya hewa ikiambatana na kuzorota kwa ubora wa maisha. Kwa sasa eneo hilo linakabiliwa na kiwango cha pili cha juu duniani cha uharibifu wa hali ya hewa. Pia, vyanzo vya nishati mbadala vinaweza kupunguza kiwango cha mafuta na gesi katika uzalishaji wa umeme katika maeneo. Na kwa hivyo kutumia fursa ya viwango hivi kwa maeneo husika kuna faida. Ikiwa nishati mbadala zinaweza kuchukua nafasi ya mafuta na gesi ambayo sasa zinatumika katika uzalishaji umeme, kutakuwepo na viwango vya ziada kwa ajili ya usafirishaji na matumizi kwa faida kubwa.
Huu ndio ukweli kuwa makampuni ya utengenezaji yanafunga operesheni zake kutokana na matatizo ya kimazingira. Hata hivyo, tatizo linaweza kuwa ni usimamizi mbaya wa mtaji wa kazi, kama vile kiwanda cha karatasi Wabuye, kilianguka kwa sababu ya usimamizi mbaya wa mtaji wa kazi.