Mei 06, 2012
Barua kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda Osama bin Laden kwa kiongozi wa al-Shabaab Mukhtar Abu al-Zubayr imethibitisha kwa maandishi kukataa ombi la al-Zubayr la umoja rasmi.
Barua hiyo ya tarehe 17 Agosti, ni sehemu ya nyaraka 17 zilizogundulika wakati wa shambulio la Abottabad huko Pakistani ambalo lilisababisha kifo cha bin Laden Mei 2011.
Mrithi wa bin Laden, Ayman al-Zawahiri alitangaza al-Shabaab kuungana na al-Qaeda Februari 2012. Muungano huo unaaminika kuleta mgawanyo ndani ya vyeo vya al-Shabaab, ikiwa ni pamoja na uasi wa wazi na kukosa kuungwa mkono na umma kufuatia operesheni zinazowalenga raia.
Katika barua hiyo, bin Laden alimkatisha tamaa al-Zubayr, anayejulikana pia kama Ahmed Godane, kutotamka wazi kuwa Somalia ni nchi inayoongozwa na Kiongozi wa Kisilamu. Pia alimshauri kuendeleza uratibu na al-Qaeda kwa siri, na kurejelea uhusiano kati ya makundi hayo mawili kuwa “uhusiano wa kindugu wa Kiislamu”:
Tumepokea barua yako ya ukarimu na nilikuwa na furaha kusoma kilichokuwa kimeandikwa kwenye barua hiyo kuhusu vikundi vya jihadi vilivyoungana pamoja kuungana nawe; pia kuhusu baadhi ya masuala yaliyotokea ambayo yanaibua mijadala ya masuala muhimu mawili: suala la kutamka wazi dola hiyo na suala la kuungana na ndugu.
Nimeona kuwa kunapaswa kuwepo na dola ya kiislamu inayofanya kazi kanadharia kwa chinichini lakini pasipo kutamka katika vyombo vya habari au kuithibitisha kwa maandishi yoyote, ili kuepuka kuvuja kwa nyaraka hizi kwa maadui – lazima itokea kwa sababu zozote zile.
Haya ni maoni yangu, lakini wewe uko uwanjani na unaona uhalisia; lolote unaloliona na kulishuhudia kwa kuona, ambapo watu waliokuwa hawako huko hawayaoni. Kwa hiyo utalinganisha kati ya faida na hasara kuhusiana na suala la kutangaza au kutotangaza uanzishaji wa nchi ya Kiislamu; ikiwa utaamua kutoa tangazo, mimi kama ninavyooana, itakubidi utangazo kwa jina la Jumuiya ya Kiislamu la Somalia, na mkuu wake kuitwa Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Somalia.
Sasa, kuhusiana na suala la umoja, ninaona kwamba wajibu huu utapaswa kufanyika kwa uhalali na kupitia ujumbe wa siri usiotangazwa, kwa kusambaza jambo hili kwa watu wa Somalia, bila ya tangazo rasmi kutoka kwa afisa yeyote wa upande wenu au wetu, kwamba umoja umefanyika. Na hili litabaki kuwa ni suala pamoja na ndugu wa upande wenu ikiwa wataulizwa kuhusu uhusiano wao na al-Qaeda. [Watasema] kwamba kuna uhusiano na al-Qaeda ambao utakuwa ni uhusiano wa undugu wa Kiislamu bila ya kukataa au kukubali.
Bin Laden pia alisema uhusiano wa wazi na al-Qaeda utakatisha tamaa wafanyabiashara wa Kiarabu kuwasaidia Wasomali na utapunguza uhusiano kati ya wapambanaji na watu wa Somalia:
Baadhi ya Waislamu wa Somalia wanateseka kutoka na umasiki mkubwa na ukosefu wa lishe kwa sababu ya vita vinavyoendelea nchini kwao; mimi nimeamua, kutumia moja ya taarifa zangu, kuwashinikiza wafanya biashara katika nchi za Rasi ya uarabuni kuunga mkono kikamilifu na miradi muhimu ya maendeleo ambayo haina gharama sana; tulijaribu jambo kama hili huko Sudan. Kwa hivyo, kwa kutokuwa na mujahidina walioungana waziwazi na al-Qaida, wafanyabiashara hao watakaokuwa tayari kuwasaidia nf¡dugu zao wa Somalia, na watu watakuwa pamoja na mujahidina.
Barua ya Bin Laden pia ilitoa mwanga wa onyo dhidi ya al-Shabaab kusababisha mapambano na majeruhi wa Kiislamu wakipanga mashambulizi dhidi ya majeshi ya Umoja wa Mataifa:
Kuhusiana na shambulio lenu dhidi ya Majeshi ya Afrika lazima mjipange vizuri kupunguza [uharibifu] kwa Waislamu katika mashambulio makubwa dhidi ya Soko la Bakara.
Pengine operesheni zenu dhidi yao zitapaswa kuwa wakati wa kuwasili au kuondoka katika uwanja wa ndege na bila ya kufanya shambulio lolote dhidi ya makao makuu yao, isipokuwa operesheni hizo zikiwa kubwa au kupitia njia za ardhini zitakazowasaidia kufika katikati ya ngome; na kwa wakati shambulio la nje. Tunaamini kwamba mnapitia suala hili na Mungu awawezeshe na kuwabariki kwa ufanisi dhidi ya malengo yenu.
Katika dalili za kutokubaliana kwa ndani kuhusu uhusiano wa al-Qaeda na wafuasi wake, barua nyingine, iliaminika kuandikwa na al-Zawahiri mwezi Desemba 2010 na kutolewa kama sehemu ya nyaraka 17, alimsihi bin Laden kuzingatia tena nafasi yake kuhusiana na kuibuka kwa al-Shabaab.
Naona kuwa ni muhimu sana kwa al-Qaeda kuthibitisha na kukubali uhusiano wake na washirika wake, ili kuwa ukweli uliothibitika; hakuna maana ya kukataa. Kwa hiyo, tafadhali zingatia tena mawazo yako ya kutothibitisha uhusiano na ndugu wa Somalia ili kutosukumwa baadaye kutangaza kutohusiana nao au na wengine.
Wizara ya Usafiri wa Anga ya mkoa wa Somaliland siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni) iliikataza ndege...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata makamu wanne wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Ma...
Watu wenye silaha kwenye Kaunti ya Wajir walimuua polisi mmoja wa akiba wa Kenya siku ya Jumanne ...
Japan inaipa Tanzania dola milioni 49 (shilingi bilioni 80.4) kama msaada na mkopo kwa ajili ya k...
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo yeye pekee yake amewateua na kuwapangia kazi maafisa wa...
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne ilimkubalia Makamu wa Rais wa Kenya Willia...
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Kwa maoni yangu, ninaona kuwa itikadi ya marehemu kiongozi wa Kiislamu, Osama bin Laden, ni sahihi na ninaiunga mkono.