Somaliland, Chuo kikuu cha Ufaransa waingia ubia kuendeleza maeneo ya akiolojia

Na Barkh Barkhad Dahir, Hargeisa

Aprili 30, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Serikali ya Somaliland na wajumbe kutoka chuo kikuu cha Paul-Valery huko Ufaransa wanafanya makubaliano kuhusu mradi wa kuendeleza maeneo ya akiolojia huko Somaliland.

  • Mwamba wa kale uliotiwa rangi umepamba mapango katika Laas Geel huko Somaliland, nyumbani kwa waafrika wanaojulikana kuwa wa  mwanzo na sanaa ya mwamba wa zamani za kale. [Tony Karumba /AFP]

    Mwamba wa kale uliotiwa rangi umepamba mapango katika Laas Geel huko Somaliland, nyumbani kwa waafrika wanaojulikana kuwa wa mwanzo na sanaa ya mwamba wa zamani za kale. [Tony Karumba /AFP]

Ubia ulianza mwaka 2002 wakati mtaalamu wa akiolojia wa Ufaransa alipofanya mazungumzo na Wizara ya Utalii na kukubaliana kufanya utafiti na kuendeleza maeneo ya akiolojia mahali vyombo vya kale vilipochimbiwa, waziri wa Biashara, Viwanda na Utalii wa Somaliland Abdirizak Khalif Ahmed aliiambia Sabahi.

Ahmed alisema wataalamu walishaanza utafiti wao huko Laas Geel, karibu na wilaya ya Dacar Budhuq, takribani kilometa 70 mashariki mwa Hargeisa. Waziri huyo alisema siku za karibuni sana watatangaza eneo lingine la akiolojia linaloitwa Dhagax Kure, kati ya wilaya ya Hergeisa na Gabiley.

“Tuna matumaini ya kupata msaada zaidi kwenye eneo lingine lililo huko wilaya ya Sheekh ya mkoa wa Saahil linaloitwa Firdowz, ambalo huonyesha mji wa zamani uliofukiwa, ambao tunaamini bado haujaguswa pamoja na maeneo mengine ya kihistoria kama vile mlima Daallo katika mkoa wa Sanaag,” Ahmed alisema.

“Laas Geel na Dhagax Kure ni maeneo mawili muhimu sana, lakini Wizara imeshasajili maeneo 139 tofauti ya kihistoria ambayo yanajumuisha msikiti wa Qiblatayn, visiwa vya Sacadadiin, maeneo yanayosawiri miji ya zamani iliyofukiwa,” Ahmed alisema.

Serikali imetoa ulinzi katika maeneo yote nchini kote Somaliland , ambapo mengi yapo mikoa ya Maroodi jeex na Sanaag, alisema Mohamed Abdi, ambaye anafanya kazi katika Idara ya Utalii na Akiolojia huko Somaliland.

Ali alisema ubia na chuo kikuu cha Ufaransa unaweza kutangaza fursa mpya kwa watalii kutembelea Somaliland. Zaidi ya hayo , vyuo vikuu vingine vinaweza pia kuvutiwa katika uendelezaji wa maeneo haya, ambayo yanaweza kusaia kukuza uchumi wa Somaliland, alisema.

Baadhi ya vyombo vya kale vilivyopatikana katika maeneo haya ni pamoja na vitu vilivyotengenezwa kwa mawe, vyombo, picha zilizopakwa rangi, vitu vilivyo katika maandiko na maumbo vimebakia, waziri alisema. “Baada ya kuingiza katika katalogi vyombo vya kale, inakadiriwa kuwa na vitu vya [miaka ya kale] zaidi ya miaka 2,500," Ahmed alisema. “Ni uthibitisho wa kutunza utamaduni huo waliokuwa nao."

Ahmed aliimbia Sabahi kuwa toka eneo la Lees Geel lilipofunguliwa 2002 kati ya watalii 50 hadi 60 wanakuja kwenye eneo hili kila mwezi. Hata hivyo mambo mengi yanahitaji kufanywa kuendeleza zaidi maeneo ya akiolojia na kuvutia zaidi watalii, alisema.

Kusaidia utalii, huduma mbalimbali ni lazima viendelezwe ikiwemo ujenzi wa migahawa, kuboresha barabara na kuwezesha usafirishaji kufikia kwenye maeneo hayo, lakini serikali haiwezi kumudu kutekeleza miradi hiyo peke yake, Ahmed alisema. “Kama tutapata msaada wa baadhi ya vitu hivi, tunaamini itasaidia uchumi wa Somaliland kwa kiasi kikubwa," alisema.

Mnamo Aprili, wanaakiolojia walijumuishwa katika mradi huu kukamilisha uingizaji katika katalogi ya kitabu utafiti wao na matokeo ya utafiti. Nakala mia tano za kitabu zilitolewa kwa serikali ya Somaliland kusaidia kuongeza uelewa na kuhamasisha utalii katika maeneo haya, Ahmed alisema.

Abdirahman Osman Aden wa taasisi ya Beder ya Utafiti na Maendeleo huko Hergeisa aliimbia Sabahi kuwa kama maeneo haya yataendelezwa kwa ajili ya utalii, yatazalisha mapato mengi kwa Somaliland na kuvutia wawekezaji wa nje.

Aden alisema mawazo mawili muhimu kwa wawekezaji ni uwezo wa mapato ya muda mrefu kwenye uwekezaji na iwapo hali ya maeneo haya kama vile amani na utulivu, ni ya kufaa kwa matokeo chanya.

“Ninaamini [maeneo hayo] yatavutia uwekezaji wa nje,” Aden alisema, akiongezea kuwa Somaliland itaweza kutoa hali nzuri kwa wawekezaji waliovutiwa.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 10)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Osman
    May 8, 2012 @ 02:58:32PM

    Nimefurahi sana kusikia habari kama hii. Hiki ni kitu ambacho Wasomali wanaweza kujivunia na ni ishara ya wazi kuwa Wasomalia wananakili sifa yao kuu iliyopotea. Ningependa kuipongeza serikali ya Somaliland.

  • abshir askar
    May 3, 2012 @ 05:09:00PM

    Bila ya shaka, mapango haya huko Laas Geel litavutia watalii wengi kutoka ulimwenguni, ni muhimu pia kwa umuhimu wa kihistoria na kiakiolojia kama zilivyo sehemu nyingine katika Pembe ya Afrika karibu na Las Geel.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo