Aprili 25, 2012
Tanzania, Msumbiji na Afrika Kusini walifanya operesheni ya pamoja ya kupambana na uharamia wiki iliyopita, ambayo ilipelekea kukamatwa kwa maharamia 12 waliokuwa wakilenga kuziteka meli za mafuta katika Bahari ya Hindi.
Afisa wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Majini la Tanzania, Kanali Abdallah Mwemnjudi, aliiambia Sabahi kuwa operesheni hiyo ya pamoja ilifanyika siku ya Jumatano (tarehe 18 Aprili) baada ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupokea taarifa kutoka washirika wao katika masuala ya usalama.
Tangu Tanzania ianzishe operesheni za kupambana na uharamia hapo mwaka 2010, imeshawakamata maharamia 35, lakini hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa operesheni ya pamoja, alisema Mwemnjudi.
“Tulipopokea taarifa hizo, tuliwaarifu wenzetu kutoka Afrika Kusini na Msumbiji. Pia tulituma ujumbe kwa kikosi cha kupambana na uharamia cha Umoja wa nchi za Ulaya kilichoko Pembe ya Afrika,” alisema Mwemnjudi. “Hispania ilituma meli yao ya kivita mara moja na kwa pamoja tukawavamia maharamia wa Kisomali.”
Mwemnjudi alisema maharamia hao walikamatwa katika boti mbili tofauti. Vikosi vya usalama viliwaokoa mateka wa Sri Lanka, kukamata bunduki tatu na kiasi ya risasi elfu moja na ngazi ya kupandia kwenye meli.
Alisema maharamia hao walikuwa wamewakamata mateka wao kwa kipindi cha miezi sita. “Mateka walikuwa dhaifu kwa sababu walikuwa wakipata chakula kidogo…lengo kubwa [la maharamia] lilikuwa ni kuteka meli za utaffiti wa mafuta zilizoko Mtwara kwa nia ya kupata fidia,” aliiambia Sabahi.
Maharamia saba wa Kisomali walikamatwa katika eneo hilo hilo karibu na Mtwara mwaka jana. Kwa mujibu wa Mwemnjudi, maharamia hao walisema walikuwa wakilenga meli zilizokuwa zinatafuta mafuta zinazomilikiwa na kampuni ya mafuta ya Brazil, Petrobras.
Mwezi Januari, Tanzania ilisaini mkataba na Msumbiji na Afrika Kusini juu ya kuwa na vikosi vya pamoja na kuyaruhusu mataifa hayo kuwafukuza maharamia kutoka kwenye mipaka yao ya baharini.
Mwemnjudi alisema kwamba kabla ya makubaliano, maharamia walikuwa wakilindwa na sheria za kimataifa za bahari, ambazo haziruhusu vikosi vya kijeshi kuvuka mipaka ya majini wakati wakiwafukuza maharamia.
Chini ya makubaliano hayo, maharamia waliojiweka nje ya fukwe za Afrika Kusini au Msumbiji wanaweza kufukuzwa hadi kwenye bahari ya Tanzania bila ya kutoa tahadhari na pia kinyume chake. Juu ya hayo, nchi zilizosaini makubaliano hayo wanatumiana taarifa za kiusalama na kufanya mafunzo ya pamoja kuzisawazisha operesheni zao, alisema Mwemnjudi.
Alisema kwa sasa Tanzania inafanya mazungumzo na Kenya ili kusaini makubaliano hayo.
JWTZ pia linafanya kazi na Umoja wa nchi za Ulaya, India, China na nchi nyingíne kwa kubadilishana taarifa.
“Zamani wakati [maharamia] wakiikamata meli, tunabakia kama wakando tu. Lakini sasa, katika matukio matatu tofauti, India imewavamia maharamia katika meli zilizotekwa na hili limewatia khofu maharamia hao,” alisema Mwemnjudi. “Bahari ya Hindi sasa iko salama zaidi ikilinganishwa na mwanzo.”
Msaidizi Mkuu wa Polisi, Fortunatus Musilimu, ambaye anaongoza Kamanda ya Polisi wa Majini, aliiambia Sabahi kwamba polisi itawahoji watuhumiwa hao. “Tuliwapokea jana na sasa ni jukumu letu kama polisi kufanya uchunguzi ili kutambua uhusiano na kiwango chao cha ushiriki,” alisema.
Alisema baada ya uchunguzi kukamilika, washukiwa watapelekwa mahakamani kukabiliana na mashitaka dhidi yao.
Martine Nyambele, meneja wa uendeshaji wa LAZ Tanzania Limited, kampuni inayoshughulikia bidhaa zinazoingia kwenye bandari ya Dar es Salaam, alisema kwamba tangu Tanzania ianze operesheni hiyo ya pamoja, uingizaji na usafirishaji wa bidhaa umeongezeka kwa asilimia 60.
Nyambele alisema asilimia 60 ya biashara bandarini hapo inahusu mataifa jirani yasiyo na mpaka wa bahari ikiwa ni Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi na Zambia. Kabla ya makubaliano hayo, harakati za kiharamia zilikuwa zikiathiri kiwango cha bidhaa ambacho nchi hizo zilipitishia nchini Tanzania.
“Uharamia ulipoongezeka, gharama za bima na usafirishaji mizigo zilipanda juu sana,” Nyambele aliiambia Sabahi. “Hatari ilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba wengi walisimamisha biashara zao, lakini sasa wamerudi kwenye shughuli zao."
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
maharamia wakikamtwa wapigwe risasi hakna haja ya kuwafuga magerezani
Ili kikundi kuingia bahari kuu na kuteka meli, huhitaji kudhuru na kuua yeyote anayepingana na amri zao. Vingi vya vikundi hivi vinachukua fursa ya kutofuata kwao sheria na kuchukua mapato yote ya wizi wanayotaka na kuondoka nayo. Kwa mapato hayo ya wizi, ambayo hawakuyafanyia kazi, wanaweza kuyatumia watakavyo, kama vile kugharamia vikundi vingine vya kigaidi kama vyao.
Uharamia na ugaidi vinahusiana kwa karibu hasa kukiwa na hali za uharamia zaidi na zaidi zinazoripotiwa hasa katika Pembe ya Afrika. Tunachokijua kwa uhakika, ni ukweli kuwa kikundi hicho huwa na nguvu na kuweza kugharimia vitendo vyake vingi vya kigaidi. Ni kwa matumizi ya ugaidi tu na biashara nyingine haramu ndio vikundi hivi vya kigaidi huweza kudumu. Kuna nyakati ambapo vikundi hivi hulazimika kuja nchi kavu, na kukamata watu mateka, kwa lengo la kutaka pesa za kikombolea kutoka nchi za mateka wao.
Kuna uharamia mwingi Afrika na unaathiri bara zima hasa nchi za Afrika ya Mashariki. Kumekuwepo na kesi za meli kutekwa nyara katika bahari kuu wakati zinapoelekea nchi za Afrika ya Mashariki katika Bahari ya Hindi. Jambo hili limezua mtafaruku duniani kote na nchi nyingi za magharibi zinaogopa kufanya biashara na nchi hizi.
Hii ni mbaya kwa uchumi wa nchi hizi. Nchi za Kiafrika zinahitaji kufanyakazi pamoja kuwang’oa maharamia wote, hatua ya kwanza ikiwa ni kutokutoa pesa za ugombozi kwa magaidi, hili huwa linawahamasisha na kuwafanya wawe na jeuri zaidi. Kitu kingine ni kwa nchi za Kiafrika kulinda baharí zao na kuhakikisha kuwa meli zinazoelekea sehemu fulani hazibughudhiwi zinapopita kwenye baharí zao. Pia kuwepo na adhabu kali kwa yeyote atakayekamatwa anafanya viendo vya uharamia. Kwa njia hizi, nchi za Kiafrika zitaweza kuzuia uharamia ambao umeenea sana.