Aprili 23, 2012
Ukosefu wa uwajibikaji kutoka kwa viongozi wa kundi la wanamgambo wenye msimamo mkali la al-Shabaab kuhusu taarifa za kuuawa kwa mwanamgambo wa nje wa kundi hilo Omar Hammami katika mikono ya wafuasi wa kundi hilo unaweza kuwa umesababishwa na hali ya mkanganyiko iliyopo ndani ya kundi hilo kwa sasa, Mchambuzi mmoja aliiambia Sabahi.
Kuongezeka kwa ugawanyikaji ndani na vikwazo vya kijeshi vinavyolikwamisha kundi hilo vimesababisha kugawanyanyika kwa viongozi wa ngazi za juu wa kundi hilo lenye mafungamano na mtandao wa al-Qaeda.
Vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa vimekuwa vikitoa taarifa tangu tarehe 5 Aprili juu ya shutuma za mauaji ya Hammami, ambaye pia alijulikana kama Abu Mansour al-Amriki aliyekuwa mmoja katika ya viongozi maarufu wa kigeni wa kundi hilo. Kwa mujibu wa ripoti ambazo hazijathibitishwa, Hammami aliuawa kwa kukatwa kichwa kufuatia amri iliyotolewa na Kamanda wa kundi hilo Ahmed Abdi Godane.
Mfululizo huo wa taarifa za vyombo vya habari, hata hivyo unasema kuwa al-Amriki alikuwa hai hapo kabla na alipelekwa Kismayo wiki iliyopita. Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari vya Somalia, alionekana akiwa chini ya ulinzi mkali wa wapiganaji wa al-shabaab huku mienendo yake ikifuatiliwa kwa karibu huku uchunguzi ukiwa unaendelea.
Viongozi wa Al-Shabaab hawajasema lolote kuhusu ripoti hizo hadi sasa. Hatma ya kundi hilo linalopigana Jihadi imeendelea kuwa mada inayogonga sana vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa al-Shabaab imekuwa kimya kuhusu taarifa za kuuawa kwa Hammami kwa sababu kwa sasa hakuna maelewano ndani ya kundi.
"Al-Shabaab wako katika vita vikali [na vikosi vya serikali], lakini pamoja na mapambano hayo walilazimika kuwashughulikia viongozi wao wawili ambao ni Abu Mansour al-Amriki na mwenzie Hasan Dahir Aweys, ambao walikuwa wakiwashangaza wenzao wa kundi hilo kwa matamko yao yenye kushangaza," alisema mchambuzi wa masuala ya siasa Ahmednur Shidane aliiambia Sabahi. "Sasa inaonekana hawataki kutoa matamko yenye mkanganyiko."
Mwezi uliopita, Aweys aliwashutumu viongozi wenzie wa al-Shabaab kwa kumwaga damu za Waislamu na kuwaua raia wasio na hatia kwa jina la uislamu, akimaanisha matendo yanayofanywa na viongozi wa kundi hilo nchini Somalia.
Katika mkanda wa video uliorekodiwa mwezi uliopita, Hammami alitangaza kuwa "maisha yake yako mashakani kutokana na kundi hilo baada ya kuwepo kwa tofauti baina ya viongozi wa kundi kuhusu masuala ya sharia na mikakati."
Kufuatia kutolewa hadharani kwa mkanda huo, al-Shabaab walisema kuwa "wameshtushwa" na kutangaza kuanza uchunguzi mara moja juu mkanda huo ili kujua nani muhusika aliyeutengeneza na nini lengo lake la kuutoa hadharani.
"Inawezekana kweli kuwa suala la al-Amriki halijapatiwa ufumbuzi, na kwa kuwa [viongozi wa kundi wa al-Shabaab] hawataki kukanganyana ndo maana wameamua kukaa kimya hadi hapo watakapokubaliana uamuzi wa mwisho," alisema Shidane.
Mchambuzi mwingine wa masuala ya siasa, Mohamed Abaas, ambaye amekuwa akifuatilia maendeleo ya al-Shabaab, alisema kundi hilo limekuwa kimya kwa sababu bado wanajaribu kupanga namna ya kuishughulikia hali iliyopo sasa.
“Kwangu mimi inaonekana kwamba wana matatizo fulani na ndio maana hawataki kujibu ripoti zinazosambazwa kwenye vyombo vya habari kuhusiana na kifo cha al-Amriki kinachotajwa kutokea kwenye mikono yao,” aliiambia Sabahi.
Abaas asema kimya cha al-Shabaab kinaonesha zaidi namna kesi ya Hammami ilivyo ngumu kuwakilisha uhusiano wa kundi hilo la al-Qaeda.
“Al-Shabaa haijawahi kuwa kimya kwa kipindi kirefu kama hiki huko nyuma. Kesi hii inaonekana kuwa tofauti na nyingine,” alisema.
Abaas alisema kwamba ikiwa kweli al-Amriki aliuawa na wapiganaji wa al-Shbaab, itawakilisha ukweli kwamba kwa mara ya kwanza kundi hilo linamuua mmoja wa viongozi wake waliozaliwa katika nchi za kigeni, jambo ambalo litaongeza shaka kwa wapiganaji wengine wa kigeni na kulisambaratisha kundi hilo.
“Suala la al-Amriki sio tu kitu ambacho al-Shabaab wanaweza kukishughulikia kwa haraka kutokana na cheo chake kikubwa alichonacho katika kundi la al-Qaeda,” alisema.
Abaas anasema si rahisi kwamba al-Amriki aliuawa. Alisema katika kesi kama hizo, kama ile ya Ahmed Keyse, kiongozi wa kundi hilo mzaliwa wa Somlaia ambaye ndani ya kundi hilo alituhumiwa kwa ujasusi, kundi hilo lilichukuwa mwaka mzima kabla ya kumnyonga.
“Suala la al-Amriki litakuwa linahitaji uchunguzi kama huo,” alisema.
Dahir Hussain, mshiriki mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Mogadishu, anasema kuwa kuuawa kwa wanachama wa kigeni na viongozi wa kikundi kunaweza kuwa pigo kubwa kwa al-Shabaab.
“Ikiwa mauaji ya Abu Mansour al-Amriki na al-Shabaab ni kweli, hilo litakuwa pigo kubwa kwa uaminifu wa kikundi, ndani na nje ya nchi. Hili pia linaweza kupelekea kutokuwa na uwiano ndani ya kikundi na mambo muhimu kwa siku za mbele,” aliiambia Sabahi.
Ikiwa Hammami aliuliwa na al-Shabaab, viongozi wengine wa kigeni ndani ya al-Shabaab wataogopa kufikwa na majaliwa kama hayo, Hussain alisema.
“Kwa muda mrefu sasa, kumekuwepo na dalili ya mgogoro wa kutoaminiana baina ya viongozi wa Somalia katika kikundi kwa upande mmoja na wapiganaji jihadi kutoka al-Qaeda wanaopigana miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab kwa upande mwingine,” Dahir alisema. “Tukio hili hata hivyo, litakuwa na athari kubwa juu ya hatima na majaaliwa ya wapiganaji jihadi wa kigeni nchini Somalia na kutapelekea kuharibika kwa uhusiano wao, pamoja na kupungua kuaminiana baina ya pande hizo mbili.”
Kimya cha wafuasi wa al-Amriki katika uongozi inawezekana kinatokana na “kufuatia kwa machafuko” baada ya habari hizo kujulikana, alisema Abdirahman Abdullahi, mtafiti juu ya masuala ya al-Shabaab na makamo mwenyekiti wa Kituo cha Vyombo vya Habari Somalia mjini Mogadishu.
Abdullahi aliiambia Sabahi kuwa hali ya kutoaminiana ambayo inaitawala al-Shabaab inawalazimisha viongozi wake kujilinda wenywe kwanza kwa sababu hawawezi kuwaamini viongozi wanaowazunguka.
“Inawezekana kuwa kila mmoja wao anaweka kadi zake karibu na kifua, kwa vile kitendo chochote cha ghafla kuhusiana na [tuhuma za] mauaji ya al-Amriki kinaweza kulipiza kisasi cha haraka kutoka kwa kiongozi wa kikundi, Ahmed Abdi Godane ambaye, inaaminika kuwa ndiye mwenye nguvu zaidi katika uwanja huu,” alisema. “Hii ndiyo sababu kiongozi yeyote mfuasi wa Hammami anakuwa na tahadhari kubwa kabla kusema chochote ambacho kinaweza kuchukuliwa kama ni ukosoaji kwa kikundi au uwezekano wa uasi dhidi ya viongozi wa juu.”
Omar Jama, mchambuzi wa masuala ya kisiasa, amasema tukio hili linawakilisha bua linaloweza kuvunja mgongo wa al-Shabaab.
"Al-Shabaab wanaweza kushinda matukio yatokanayo na mauaji [yanayodaiwa] ya al-Amriki, lakini hawataweza kuepukana na kuibuka kwa tofauti na migogoro ambayo itakuwa imetokana na [ripoti za] kifo chake.
"Kikundi cha al-Shabaab kiko katika uchungu wa mwisho wa kukata roho na inaonesha kana kwamba kiko hatua za mwisho za kuporomoka, hasa baada ya uondoaji na uuaji miongoni mwa uongozi wa kikundi kutangazwa hadharani,” Jama alisema. “Al-Shabaab wanashuhudia mgawanyiko wa ndani na wamekuwa wakidhoofika kijeshi huku wakikabiliwa na tatizo la kukosa ari….inapoteza mengi ya maeneo kila siku. Kutokana na kushindwa kijeshi hivi karibuni na migogoro mfululizo, al-Shabaab wako ukingoni mwa kifo.”
Wakati huo huo, Serikali ya Mpito ya Shirikisho ilisema katika taarifa hapo Jumatano (tarehe 18 Aprili) kuwa “inaendelea na juhudi za kuchukua hatua kali za kuharibu ngome za magaidi nchini kote, pamoja na kuimarisha juhudi zake za kupambana na ugaidi.”
Serikali iliseme al-Shabaab wanakabiliwa na mgawanyiko baada ya vifo vya viongozi wao muhimu katika vita vya karibuni.
Meya wa Mogadishu Mohamed Ahmed Nur alitangaza kuwa serikali ya Somalia italipa hadi dola 500 kwa yeyote atakayetoa habari kuhusu mahali walipo viongozi wa kikundi.
“Ninauahidi umma zawadi za vitu kwa habari zozote juu ya maficho ya milipuko. Pia, mtu yeyote atakayetoa habari kuhusu nyumba ambazo wanachama wa al-Shabaab wamejificha zawadi itatolewa – dola 100 kwa mwanachama wa kawaida na dola 500 kwa maafisa wa juu wa kikundi,” Nur alisema.
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Somalia kutangaza zawadi kama hiyo kwa ajili ya kupata habari.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Al-Shabaab walale mahali pema.
Uislamu kama Ukristo ni jumuiya ya kidini yenye mafundisho yanayounga mkono amani na maelewano. Wahalifu kama al-Shabaab wapo kwa maslahi yao binafsi na hawafanyi hayo kwa nia ya pamoja. Jeshi la Kenya lingefikiria kuwabana wanaoleta fujo na sio washutumiwa tu kwa vile mara nyingine huhisi Waislamu wote wanaleta fujo ni jambo ambalo sio kweli. Ninaunga mkono hatua ya jeshi la Kenya kupigania amani nchini Somalia.
islam inaudhi bana watuachie...
Jaribio hilo la al-Shabaab sio la busara kwa sababu wanasababisha vifo vingi vya watu kwa nini wasichukue hatua dhidi yao au wanaogopa kuchukua hatua kwa nini wasiombe msaada wa kuwamalizia mbali?
Al-Shabaab lazima waelewe kuwa siku zao zinahesabika. Vitendo vyao vyovyote vitawagharimu sana.
Umesema kweli Mutanga. Ninaweza kuona kutokana na maoni yako kuwa wewe ni msomi. Kama ingekuwa kila asiye Muislamu anafikiri kama wewe, tungekuwa na dunia iliyo bora zaidi.
Mnafanya kazi nzuri lakini ili kuepuka msionekane kama chombo cha propaganda kwa ajili ya Serikali ya Mpito ya Shirikisho, kuna haja ya kupatikana maelezo kutoka kwa watu au mashirika huru juu ya mada yoyote inayojadiliwa. Mngeweza kuwahamasisha wafuasi wa al-Shabaab (ikiwa mnaweza kuwafikia) ili nao watoe mawazo juu ya suala hilo hilo, ili muwe na habari yenye uwiano. Pia mnaweza kuimarisha uhariri, ili muweze kutoa makala yenye athari na kipaji cha matumizi ya lugha na uwasilishaji wake.
Uislamu ni dini ya AMANI NA KUISHI PAMOJA NA BINADAMU WOTE, KWA KUVUMILIANA. Sioni chochote cha Uislamu katika mashambulizi ya kigaidi kwa wananchi wasio na hatia na utekaji nyara wa watalii nchini Kenya. Kwa hivyo al-Shabaab ni kampuni kubwa ya kihalifu YENYE AJENDA YA KUJIDAI, BASI. Lengo ni kukamata nguvu za kisiasa na utazipata kwa kumwaga damu. Ninaliunga mkono jeshi la Kenya ambalo lazima litarejesha demokrasia na haki za binadamu kwa raia wa kawaida wa Somalia kuamua hatima yao. Lakini mtakapowamaliza al-Shabaab, hatutaki muache ombwe, wekeni misingi ya kidemokrasia ili kuweza kujitawala wenyewe.