Aprili 16, 2012
Wakati maadhimisho ya pili ya jaribio la mauaji ya aliyekuwa Balozi wa Uingereza nchini Yemen Tim Torlot yakikaribia, familia ya muuaji wa bomu la kujitoa muhanga Othman Ali Noman al-Selwi inaendelea kuteseka na dhiki za kijamii na kifedha.
Baba yake Ali Norman al-Selwi, mkarandasi wa ujenzi, aliuza majengo mawili aliyokuwa anamiliki na familia yake kuhama mara kadhaa ili kuepuka usumbufu kutoka kwa jamii.
Kwa majonzi na huzuni kubwa, al-Selwi aliiambia Al-Sorfa, “Tangu mwanangu alipolipua bomu la kujitoa muhanga, sijawahi kujua kiwango chochote cha furaha.”
“Niliuza nyumba zangu mbili, na kama nisingekuwa na kazi ndogo ndogo za ujenzi, nisingekuwa na kazi yoyote,” alisema.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari hapo tarehe 26 April 2010 bomu hilo, al-selwi alielezea mwisho ambao alijichagulia kuwa ni “majaliwa ya kufedhehesha” na kuwataka vijana wa Yemen “wasizamishwe katika kutenda matendo ya kigaidi”.
Motaz Adnan, mweye umri wa miaka 30, aliiambia Al-Shorfa vipi tukio hilo liliilazimisha familia ya majirani zake kuhamia mbali na ilipokuwa inaishi.
“Kama familia ile ingebakia eneo hilo, ingekabiliwa na usumbufu, hasa kwa vile jamii ya Yemen inakataa matendo ya kigaidi. Watu wangejaribu kuwatupia lawama wazazi wa Othman kwa madai ya kumpuuza mtoto wao au kwa baadhi ya matendo ya kulalamika,” Adna alisema.
Miezi saba iliyopita, al-Selwi alipokea kukubaliwa na viongozi wa usalama wa Yemeni na Uingereza kuyapata mabaki ya mwanawe, ambayo yalikuwa yamezuiwa na Uingereza mpaka hapo uchunguzi wao juu ya vifaa vilivyotumika katika ulipuaji wa bomu utakapokamilika.
"Niliuza mali yangu yote baada ya tukio lile kutokana na shida za kijamii na za kifedha tulizokuwa nazo na kulipia gharama zilizotokana na ufuatiliaji wa kesi ya mwanangu na katika juhudi za kuupata mwili wake ili kuuzika,” al-Selwi alisema.
Hali ya kifedha ya al-Selwi kuanzia hapo ilikuwa mbaya sana na haimruhusu kutayarisha mazishi au kuzuru mwanawe, alisema.
Wanaojitoa muhanga kwa mabomu ‘si mashahidi wala mujahidina’
Nchini Yemeni, wanaojitoa muhanga kwa mabomu wanachukuliwa kama watu wanaojiua wenyewe, sio mujahidina. Na wakati mabaki yanashughulikiwa kwa mujibu wa mila na kumalizia na ibada za sala na mazishi, maafikiano miongoni mwa wanazuoni ni kuwa watu wanaojiua kwa kujitoa muhanga hawawezi kuchukuliwa kama ni mashahidi.
“Wale wanaofanya mauaji kwa mabaomu ya kujitoa muhanga si mashahidi wala mujahidina. Walipotea njia ya kuelekea peponi kwa kufanya vitendo hivyo vya kigaidi,” Sheikh Jabril Ibrahim, mkurugenzi mkuu wa mahubiri na mwongozo katika Wizara ya Wakfu na Mwongozo, aliiambia Al-Shorfa.
“Kwa hali yoyote, wanaojiua kwa mabomu ni Waislamu na watoto wa Waislamu, kwa hivyo, swala hutolewa kwa niaba yao ma wanazikwa kama Waislamu wengine,” alisema.
“Mtume alisema kuwa yule anayekufa chini ya bendera ya ujinga na kuuliwa, kifo chake ni kifo cha kijinga [jahiliyyah]. Wanaojiua kwa mabomu wanapigana chini ya bendera ya ujinga,” alisema Ibrahim.
“Hakuna kikundi wala upande bali Mwenyezi Mungu, mwenye haki ya kuwaweka katika daraja la ushahidi juu ya [muuaji wa kujitoa muhanga] au mtu mwingine yeyote, kwa vile kitu kama hicho ni kupingana na [uwezo wa juu wa] Mungu, aliongeza.
Uislamu ni dini ya upendo na amani na hata kuwakaribisha watu waingie katika Uislamu hakutakiwi kutumike nguvu, alisema.
Vikundi vingine vinatafuta kutumia sharia za Kiislamu ili kuhalalisha vita “ili kupata malengo yao”, Ibrahim alisema.
Kwa hali yoyote ile, alisema, “Uislamu unaweka wazi kuwa wanawake, watoto, wazee, hata miti na wanyama vinatakiwa visiingizwe katika vita. Uislamu unapiga marafuku kuwaua watoto wanaoshiriki katika vita, tofauti na matendo ya baadhi ya vikundi ambavyo kwa makusudi huua wananchi kwa mabomu ya kujitoa muhanga ambapo wanawalenga Waislamu kwenye barabara za umma, karibu na mashule na viwanja vya umma.”
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Wakati familia inapogundua uhalifu wa mmoja wa wanafamilia wake kuelekea imani ya upatanisho, na hili liko wazi kwa kuepuka jamii na watu wa kulipa kisasi, hasa baadhi ya wanasayansi au baadhi ya watawala, kugundua tabia hizo kwa kutokuwepo nyumbani kwa muda mrefu na kujifunga na kikundi kikundi kidogo cha marafiki wenye mawazo sawa pamoja na mikutano, na mazungumzo katika njia ya siri, wanajamii waliobakia katika hali hii, lazima wamjadili kwa pamoja, bila ya majivuno, lakini kwa misingi ya kuwa wote wanamtakia mema na mabadiliko. Kwa hivyo, wanaweza kumfanya akatae shutuma na kuweka wazi ukweli. Siku moja ataweza kurekebisha na kuwa sawa na hali yake. Lakini wale ambao wangependa kusema na hawawezi kuvumilia kuingiliwa na hawataki kuwasikiliza, hivyo ni bora kutoshiriki, kumtakia mema na kuwa na uvumilivu juu ya madhara yake kama njia walizokuwa wafanya Mitume. Mikutano hiyo inapaswa kuendelea kwa muda ili kuhakikisha kuwa kijana hatarejea katika imani zake za zamani, na ni bora kuhamasisha matumizi ya vilabu, shule na sehemu za kujiburudisha. Familia na jamii lazima ziwe na uvumilivu na kuwatunza zaidi watoto wakati wanashugulikia masuala yao wenyewe.
Naamini kuwa yeyote anayefuata mkabala wa kigaidi na kushirikiana na magaidi hana hisia wala maadili. Hii ni kwa sababu mtu kama huyo anajifikiria mwenyewe tu, na hana dhamira kwa chochote zaidi isipokuwa nia yake mbaya na kutovumilia wengine anaobeba moyoni mwake. Mtu kama huyo hana dhamira kwa familia yake, mama na jamaa zake, na haangalii hatari ambazo anaweza kuhusika nazo akifuata njia isiyo sahihi. Pia hazingatii sifa mbaya ambazo zinaweza kuiathiri familia yake kama matokeo ya matendo yake ya kigaidi. Majirani wanaopoteza familia zao kutokana na ugaidi wataidharau familia yake, kwa sababu mtoto wao anaweza kuwa mmoja wa waliohusika na mauaji ya mtoto au wanafamilia yao. Hii itaifanya familia ya gaidi kukejeliwa kwa muda mrefu na watu wengi wataidharau. Kwa hivyo, kila kijana lazima amwogope Mungu na lazima azingatie maslahi na heshima ya familia yake. Asiondoshe jicho juu ya kile walichomtendea na kumkuza, badala ya kuwasaliti kwa kufuata njia ya uovu inayopelekea kujiangamiza wenyewe. Kwa hivyo, vijana wasijihusishe na njia zenye taathira hasi kwa familia zao, kwa kuelewa kuwa tunaishi katika jamii ya mashariki inayoshikilia mila, na tunapenda kusikia hadithi za familia na marafiki wanaotuzunguka. Vijana lazima waheshimu familia zao na majirani. Na wawaheshimu wale waliowalea. Lazima wawe mbali kutokana na mambo mabaya yanayoweza kuathiri familia na heshima zao.
Wazazi wanapaswa kuendeleza wajibu wao kielimu na mafunzo kwa watoto wao. Wanapaswa kujua wanayoyapenda, mawazo na matarajio yao ili kuwahamasisha mambo mazuri na yenye manufaa yaliyomo katika nafsi zao. Wakati huo huo, serikali inapaswa kuchukua jukumu jengine. Lazima ielewe thamani ya vijana na nafasi yao katika ujenzi wa nchi. Lazima tuwatunze na kuwapa wanachohitaji kama vile maisha salama na ya kutulia, wapatiwe fursa za ajira na kuyafanya maisha yao yawe rahisi. Hili lina nafasi kubwa katika kupata matarajio na ndoto za vijana. Kunawasaidia wajitenge na mawazo machafu, vitendo vya kukithiri na kujiweka mbali na njia iliyonyooka. Wanazuoni na watu wa dini pia wana wajibu katika kuonesha ukweli juu ya ugaidi, lazima watoe ushauri kila mara kwa vijana wetu kuhusu uhalifu na mawazo ya kigaidi ambayo yako mbali na mawazo ya dini ya Kiislamu, na hayana uhusiano wowote na Uislamu. Haya yanaweza kufikiwa kupitia mahubiri ya dini na programu za TV. Mambo kama hayo lazima yajadiliwe na sio kupuuzwa.
Mtu anayefanya uhalifu kama huu wa kutisha huwa hajali matokeo ya vitendo vyake; bila shaka matendo yake yameiathiri familia yake mwenyewe, ukoo au kabila na mila na kanuni zake. Vitendo vyake ni dhidi ya Sharia, sheria na mila zote za familia katika eneo au nyanja za kimataifa. Sheria za Kiislamu zinazuwia vitendo hivi; shairi linasema, "Taifa linadumu pamoja na maadili yake...lakini ikiwa maadili haya yatapotea, taifa nalo hupotea."
Watoto wadogo lazima wafundishwe dhana na imani za Kiislamu zinazokubalika kwa mujibu wa viwango vya kanuni za Kiislamu. Lazima wafundishwe matendo ya ibada na tabia njema. Utaratibu wa Mungu katika maisha ya sasa ya mwanadamu yanawakilisha moyo wa uaminifu ambao Mungu alimuumba binadamu. Ili kutekeleza Utaratibu wa Mungu katika dunia hii, hiki ndio kitu cha mwanzo katika maisha ya binadamu duniani; ni suala ambalo vizazi lazima vikuzwe katika mafundisho ya familia juu ya mila za Uislamu unaochukuliwa kama kilango cha usalama kwa jamii ambayo ndani yake hali za mtu mmoja mmoja na jamii kwa jumla zinaimarika, na ambazo zinapelekea kunawiri kwa usalama. Athari zake haziwezi kuondoshwa kirahisi, kinyume chake; na ndio maana tunapata usalama na utulivu kwa vizazi vyetu vinavyojihisi viko salama, kuamsha hisia na vinavyoweza kulinda haki na kurejesha haki za waliokandamizwa, pamoja na hisia zao na uangalifu wao kwa roho za binadamu.
Kuwepo kwa mtu anayejitoa muhanga kwa mabomu katika familia bila shaka kunaathiri hadhi ya familia katika jamii inakoishi, kuna athari za kisaikolojia na kijamii. Jamii inawaangalia wauaji hawa wa kujitoa muhanga kwa jicho la kutoridhika nao. Familia hufanikiwa na hadhi nzuri na kufungamana na maadili ambayo huwarejeshea faida na huwapa heshima miongoni mwa familia nyingine. Kwa hivyo, kiongozi wa familia lazima awaangalie watoto wake, ili asitokee hata mmojamiongoni mwao kuyakosea maadili yake au kuwa na tabia za kikatikama vile mashambulizi ya kujitoa muhanga ambayo hayafaidii na kuwadhuru tu watu wasiio na hatia ambao hawahusiki na mizozo baina ya makundi tafauti, bila ya kujali hadhi au uzawa wao, au hata nafasi zao miongoni mwa wengine. Sisi kama jamii au watu mmoja mmoja katika familia hizi iko haja ya kuendelea na muonekano na hadhi yetu miongoni mwa makabila jirani bila ya kumwaga damu, ili tusiangukie katika makucha ya uhalifu, au ili tusije kutakiwa kuwarejesha wale wale tuliowashambulia.
Ikiwa kuna mabadiliko katika akili za mtu kutoka mtu mwema na kuwa gaidi, itakuwa ni jukumu la wazazi kwa sababu sisi kama wazazi tunaweza kuisawiri njia ya mtoto. Na ikiwa akili ya kawaida ya mnyama inaweza kuwatunza watoto wake, kwa nini sisi kama wazazi tusiweze? Pole kwa familia lakini kwa kweli ni kosa lao. Mwisho wa yote MwenyeziMungu anaweza kutusaidia katika kuwatunza watoto wetu.
Hakuna mwenye nguvu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kwa kweli sijui niseme nini! Mwenyezi Mungu azirehemu roho za mashahidi waliouliwa na zimwi hili. Mwenyezi Mungu awaweke peponi. Ama kuhusu baba wa mhalifu huyu, angetubu na kujiweka huru na makosa ya mwanawe, inaonesha yeye hahusiki na vitendo vya kigaidi vya mwananwe. Dini na sheria havimhukumu baba kwa matendo ya mtoto wake. Lakini kuna kipengele kimoja ningependa kuzielezea familia na wazazi katika nchi zote za Kiislamu, Uislamu ni dini ya uvumilivu, na masheikh wote na watu wa dini lazima wawe wavumilivu kama ilivyo dini yao. Wazazi wasipeleke watoto wao kusoma kwa walimu wa dini wenye msimamo mkali. Mimi kama baba, lazima niulize kwanza iwapo Imamu wa msikiti ni mtu mwenye msimamo mkali au mtu wa wastani, ni zipi dhana zake, kwa sababu mwalimu na wahubiri wanaowaongoza watoto wetu wanaweza kuwaathiri, kuwafanya wafanye mambo mema na wawe wa manufaa kwa jamii. Lakini wahubiri wenye msimamo mkali wanawaelekeza watoto wetu kuzimu na kuwageuza zana za uuaji. Wakati huo huo, ninaiomba serikali kuikagua misikiti; lazima kuwepo na uongozi fulani wenye dhamana ya ukaguzi huu ili misikiti isiwe vituo vya watu wenye msimamo mkali. Asante ndugu na samahani kwa hadithi ndefu!