Al-Shabaab wakimbia, wasema wachambuzi

Mahmoud Mohammed wa Mogadishu amesaidia katika ripoti hii

Aprili 16, 2012

  • 24 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Shinikizo la kijeshi linaoloendelea dhidi ya kundi la al-Shabaab katika maeneo ya kati na kusini mwa Somalia yamewafanya wapiganaji wa kundi hilo lililoungana na al-Qaeda wachanganyikiwe na kutafuta maeneo mbadala ya kujificha, wachambuzi wa Somalia wameiambia Sabahi.

  • Wapiganaji wa al-Shabaab wakitembea katika mitaa ya wilaya ya Daynile mjini Mogadishu mwezi Machi. Wanamgambo hao wamekuwa wakilikimbia eneo la kaskazini kutokana na kuongezeka kwa shinikizo dhidi yao. [Mohamed Abdiwahab/AFP]

    Wapiganaji wa al-Shabaab wakitembea katika mitaa ya wilaya ya Daynile mjini Mogadishu mwezi Machi. Wanamgambo hao wamekuwa wakilikimbia eneo la kaskazini kutokana na kuongezeka kwa shinikizo dhidi yao. [Mohamed Abdiwahab/AFP]

Baada ya kupoteza mfululizo maeneo kadhaa – ya karibuni zaidi yakiwa ni Hudur, Mahas na El Bur – wapiganaji wa al-Shabaab wamekimbilia katika maeneo ya mafichoni kama vile Milima ya Golis ili kujipanga upya, wamesema.

“Hakuna shaka kwamba al-Shabaab wanakimbia. Kundi hilo linadhoofika siku hadi siku kwani wapiganaji wake wamejikuta wakiwa wamezingirwa [na vikosi vya usalama],” alisema Mohammed Hussein, mchambuzi wa masuala ya usalama na kanali mstaafu wa jeshi la Somali.

"Al-Shabaab wamepoteza udhibiti wa sehemu kubwa ya ngome zake katika maeneo ya kati na kusini mwa Somalia katika kipindi cha miezi michache iliyopita; na sasa wanajaribu kukimbia,” alisema. “Sasa hawana njia nyingine isipokuwa kujisalimisha au kuikimbia Somalia.”

Uongozi uliosambaratika

“Wapiganaji wa al-Shabaab na al-Qaeda sasa wamedhoofishwa na wapo katika hali ya majuto,” alisema Waziri Mkuu wa Somalia, Abdiweli Mohamed Ali, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hapo Jumatano (tarehe 11 Aprili).

Ismail Abdullahi, mchambuzi wa siasa katika Kituo cha Masomo ya Pembe ya Afrika, alisema “wapiganaji wa al-Shabaab sasa wamezungukwa kila upande na mbano unazidi kukaza kwa haraka sana.”

Kukosekana kwa hali ya kuaminiana ndani ya uongozi wa kundi hili, ambayo ni matokeo ya kuongezeka kwa tofauti, kumewaathiri sana wapiganaji ambao wanaamua kukimbia, Abdullahi aliiambia Sabahi. “Kila kiongozi kwenye kundi hilo hivi sasa anafikiria mahala pa kukimbilia,” alisema.

Hali ya kutofahamiana ndani ya uongozi wa kundi hilo iliongezeka pale mpiganaji Jihadi aliyezaliwa Marekani, Omar Hammami, ajulikanaye pia kama Abu Mansour al-Amriki, aliyeripotiwa kuuawa tarehe 5 Aprili. Baadhi ya wanachama wa ngazi za juu wa kundi hilo, ambao walifahamu kuhusu mauaji hayo katika mkutano wa viongozi uliofanyika Baraawe, walikasirika na kujiondoa na wapiganaji wao, uliripoti mtandao wa habari wa Gedo Online.

Abdullahi alisema kwamba kwa kuwa viongozi wa al-Shabaab walishindwa kuvuna nyoyo na akili za makabila ya Somalia hapo kabla, viongozi hao hawawezi kurudi kwenye miji yao na kujipanga tena wakiungwa mkono na makabila yao. “Njia pekee waliyonayo ni kukimbilia kwenye maeneo ya milimani kaskazini mashariki mwa nchi,” alisema.

'Tora Bora' ndani ya Somalia

Wachambuzi waliiambia Sabahi kwamba wapiganaji wa al-Shabaab na wanamgambo wa makundi mengine wamejiweka kwenye Milima ya Golis kutokana na mahala lilipo eneo hilo ambalo linatazamana na Ghuba ya Aden na Bab al-Mandeb na kufanana na Tora Bora nchini Afghanistani.

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Abdulqadir Osman, ambae anafuatilia makundi ya Waislamu wenye imani kali nchini Somalia, alisema wanamgambo hao walipanga kutengeneza vituo vya siri na kambi za mafunzo na Milima ya Golis inaweza kutoa ngome ya maficho kwa magaidi. “Maeneo haya yatafaa kwa lengo hili kwa kuwa yana mazingira mazuri kuwafunza wapiganaji Jihadi,” alisema.

Osman alisema wapiganaji wa Milima ya Golis, ambao mwezi Februari walitangaza rasmi kujiunga na al-Shabaab wamekuwa wakifanya kazi katika eneo hili kwa dhamira hiyo hiyo.

“Wametumia fursa hii na ukosefu wa vikosi vya usalama, na hiyo ndiyo sababu viongozi wa al-Shabaab wanadhani kuwa eneo hili la milima linaweza kuwapa sehemu salama wanayoweza kujificha kwa muda,” alisema.

Eneo hilo gumu lenye miinuko si sahihi kwa mapigano ya kawaida ya kivita na huenda ikawa vigumu kwa wanajeshi wa serikali kupenya, wachambuzi waliiambia Sabahi.

“Itakuwa vigumu kwa jeshi lolote kulifikia kirahisi eneo hili na kupambana na wale waliojichimbia huko, kwa sababu ni eneo la milima, lililo na mapango na mizunguko mingi ambayo inaweza kuwa kama sehemu za maficho kwa wapiganaji wenye imani kali,” alisema mchambuzi Dawood Mohammed, profesa wa Chuo Kikuu mjini Mogadishu.

Vikosi vya usalama vyajitayarifa na uingiaji kwa wingi wa wanamgambo

Vikosi vya kanda vya usalama vimekuwa vikijitayarisha na uwezekano wa kuingia kwa wingi kwa wapiganaji wa al-Shabaab wanaokwenda kaskazini wakati kikundi kinaendelea kukabiliwa na ongezeko la shinikizo katika pande tatu za uwanja wa mapambano kutoka Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia na washirika wake.

Hapo Jumapili, baada ya kamati ya usalama kukutana huko Galkayo, Gavana wa Mudug, Mohamed Yusuf Jama, alisema mpaka wa kusini utafungwa katika hatua ya kujikinga ili kuwatoa nje al-Shabaab.

Raisi Sheikh Sharif Sheikh Ahmed aliahidi kuwa serikali ya mpito itaunga mkono operesheni za usalama huko Puntland ili kuwazuia al-Shabaab wasijikusanye upya katika maeneo ya mbali katika taifa lenye utawala wa ndani.

Hapo Jumanne, Raisi wa Puntland Abdirahman Mohamed Faroole alisisitiza kuwa Juu ya jukumu la utawala wake la kuwang’oa al-Shabaab kutoka mipaka yake na kuwazuia wengine wasiingie. “Ikiwa tutahitaji msaada wa kijeshi, tutaomba, lakini ninaamini kuwa majeshi yetu yatazuia uasi huo,” alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 63)

Dislike_icon(10)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • otieno
    May 21, 2012 @ 11:01:13AM

    Wamalizeni al-Shabaab mara moja na moja kwa moja.

  • arafat
    May 18, 2012 @ 02:34:35PM

    Kusema kweli haya nimapigano baina ya Waislamu na Wakristo, vita hivi havina mwisho mpaka jua kutua! Swali ni hili, ikiwa nyinyi ni Waislamu au "Waislamu wa kweli" wa Somalia, sio wale wanaotumia Ukristo kama pesa:- 1. Tunapigana kwa miaka 26-28. Ikiwa serikali hizi za Kikristo zinataka kupatikane amani Somalia, kwa nini wanakuja sasa na sio kabla? 2. Ikiwa ni Waislamu, tangu lini Waislammu na Wakristo wamekuwa kama ndugu? Kwa sababu katika Kuran tunaambiwa kuwa Wakristo ni maadui zetu na pia wanataka kuchoma na kuharibu Kuran Takatifu. Angalieni tafadhali, kinachoendelea katika ulimwengu huu, ikiwa mna akili nzuri ya kufikiri na mnajua zaidi kuhusu dini! Nipeni jawabu zenu, asanteni.

  • Bashar
    May 16, 2012 @ 07:16:59AM

    Mungu akipenda siku moja Somalia itakuwa nchi ya amani.

  • none
    May 13, 2012 @ 04:44:15AM

    Nzuri sana.

  • PATRICK KARANJA MAINA.
    May 10, 2012 @ 09:54:54AM

    Wanamgambo wa al-Shabaab lazima washughulikiwe mpaka watakaposalimu amri lakini kuweni macho na kulipiza kwao kisasi. Kwa maoni yangu sifikiri kama VIKOSI VYA KENYA viko na uwezo wa KUHIMILI vitakapochanganyika na AL-QAEDA.

  • Telesphory Mwadime Kitimo
    May 10, 2012 @ 09:52:36AM

    Hongera AMISOM na washirika kwa kazi nzuri mliyofanya. Natarajia kusikia habari kuhusu ya shule na viwanda ndani ya Somalia. Maendeleo ya Somalia yataimarisha Jumuiya yetu ya Afrika ya Mashariki na kumfanya kila mtu awe na furaha.

  • mohamed khalif
    May 9, 2012 @ 06:05:53AM

    Mwenyezi Mungu akipenda Somalia itakuwa na amani.

  • EZEKIEL MABUKA NYANGOYA
    May 7, 2012 @ 04:17:34AM

    Wanamgambo wa al-Shabaab lazima washughulikiwe bila huruma kwa sababu kikundi hiki sio tu ni tishio kwa Somalia bali pia kinaathiri hali ya uchumi wa nchi jirani. Shughuli za utalii zinasimama kwa sababu ya woga. NINAIPONGEZA SERIKALI YA KENYA KWA KUCHUKUA HATUA KALI DHIDI YA KIKUNDI HIKI CHA KIGAIDI. HONGERA!

  • Harold Kinyanjui
    May 6, 2012 @ 08:25:02AM

    Al-Shabaab wameharibu imani tuliyokuwa nayo vijana wa Kenya kwa kuwapa mafunzo baadhi yao katika itikadi zao zenye mwelekeo wa kurudi nyuma. Kwa nini mtu auwe watu wasio na hatia na kujifanya kiasi cha kuwa yeye ni Mungu?

  • Dickson Kenga
    May 6, 2012 @ 02:19:43AM

    Hongera! Kikundi hiki lazima kimalizwe!!! Lazima amani ipatikane kwa ndugu zetu.

  • Borafya
    May 5, 2012 @ 10:44:45AM

    Habari! Wale ambao mwanzo walijihisi ni mashujaa wa al-Andalus sasa wanakabiliwa na kazi yao isiyo na uhakika ya ugaidi. Ha! Haaa! Wenzangu, mwanzo niliwaambia kuwa KDF hawana kazi ya kucheza na wajibu wao. Wamechelewa sana na bahati mbaya sana, al-Shabaab sasa wanakimbia kunusuru maisha yao.

  • mubaarik bashiir aw cumar
    April 26, 2012 @ 11:53:26AM

    Wanachama wa al-Shabaab wanaandamwa na maslahi yao ya kichoyo na hawana huruma yoyote kwa nchi na wananchi. Bila ya shaka wao ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa Pembe ya Afrika.

  • Bwocha Nyagemi
    April 24, 2012 @ 04:35:27AM

    Kazi nzuri. Swala zangu ni kuwa magaidi watashughulikiwa hadi kifo kitakapowakumba ili Wasomali wenye nia njema waweze kufanyakazi kwa pamoja na kujenga nchi yao. Ulimwengu wote unaelekea kwenye uhuru wa dunia wakati wahuni hawa nchini Somalia wameng’ang’ania kuwatia watu jela ya umasikini wa kudumu na kutokuwa na nguvu na kukata tamaa. Aibu iliyoje! Hongera kwa jeshi la Kenya na AMISOM kwa jumla.

  • Murathi Salesio
    April 23, 2012 @ 11:04:33AM

    Hakuna cha bure, waacheni al-Shabaab wajuwe kuwa habari hizi ni chanya. Wajitayarishe kufa kimya kimya.

  • thouffs
    April 23, 2012 @ 05:06:17AM

    Hii ndio njia ambayo imetarajiwa, nina wasiwasi kidogo tu juu ya hali itakavyokuwa iwapo wapiganaji wa al-Shabaab watapigana vita vya msituni katika Milima ya Golis, vifo vitakuwa vingi sana. Baada ya kusema hayo, heko kwa KDF, askari wa serikali na washirika katika AMISOM.

  • Kabutiei David
    April 21, 2012 @ 11:39:22PM

    Habari hii ni nzuri na tuviunge mkono vikosi vya AMISOM na KDF katika kazi ya kuijenga upya Somalia. Pia ninawataka Wasomali kuungana katika kujenga nchi yao na kuondokana na migogoro isiyo na faida kama vile kukosoana, mapigano ya kikabila na matendo ya uhalifu kwa sababu mauaji au kujaribu kuua kunaharibu utu wenu na maisha kwa jumla. Kwa unyenyekevu achaneni na vikundi vichafu kama vile al-Qaida na al-Shabaab kwa sababu uwezo umo mikononi mwenu kuutumia dhidi ya vitendo vyao vichafu na uharibifu na bila ya hivyo kamwe hamtaweza kuimarisha hali ya maisha nchini kwa sababu ya uharibifu huu wa vikundi kama hivi. Ni suala la kuwa na utawala bora tu na kuungana na mataifa mengine katika kujenga uchumi wa nchi yetu na hatimaye Somalia kuwa pahali pazuri pa kuishi.

  • Evance
    April 18, 2012 @ 09:38:40AM

    Heko kwa kutupashia habari hizi, lakini kile kinachonitia hofu na shaka ni kuwa wanajeshi wa KDF wanaendelea vilivyo na nimefurahia uvumilivu wao, ingawa Wakenya wanaendelea kuteswa kwa kulipzwa na maguruneti katika kila kona ya nchi hii, watu wapoteza maisha yao na waliyo baki wanaachwa kuishi katikati ya hofu na matumaini.

  • Burhaan
    April 17, 2012 @ 07:28:16PM

    Mapinduzi katika nchi za Kiarabu yanawapiga sana watu wenye msimamo mkali, hilo ndilo ninaloona. Agenda ya watu wenye misimao mikali wanatumia tawala zisizokuwa za kidemokrasia katika nchi za Kiislamu kama eneo la kutoa mafunzo na kwa vile mataifa yanabadilika na mchakato wa kidemokrasia unapiga hatua, watu wenye itikadi kali wanapoteza nguvu. Ni hivyo hivyo kwa al-Shabaab kwa vile serikali ya Somalia inajiimarisha zaidi, na hiyo ni hatua ya wenye itikadi kali kukosa pahali pa kutolea mafunzo. Endelea taifa langu, karibuni tutakuwa na pahali miongoni mwa nchi za kisasa na tuwaache al-Shabaab waingie motoni.

  • P Githinji
    April 17, 2012 @ 04:38:25PM

    Kwa hakika, Al-Shabaab hawana faida, na kumalizika kwao ndio njia pekee ya kuwawezesha Wasomali kujua na kuonja utamu wa amani baada ya muda mrefu wa kutokuwepo na serikali. Kila siku tunamuomba Mwenyezi Mungu tunapowaona mnasafiri katika bahari hii iliyochafuka na kuifanya meli ifike katika bahari tulivu siku za mbele lakini karibuni.

  • skimman
    April 17, 2012 @ 12:00:08PM

    Ninaipenda pia, ikiwa viongozi wa Somalia wamekusudia kazi, tena tuone kama si maneno ya kisiasa tu.

  • Dennis Kiprono Kipkalis
    April 17, 2012 @ 11:54:09AM

    Nimefurahishwa sana na juhudi za askari wa KDF wanaopigana na kikundi cha kigaidi. Karibuni kazi yao itazaa matunda ikiwa wataendelea bila ya kuchoka.

  • joachim thuo ahmed
    April 17, 2012 @ 08:13:23AM

    Huu ni wazimu kamili

  • ugaaso
    April 17, 2012 @ 06:39:55AM

    Kwa nini watu wanauwana wao kwa wao? Kwa nini tunasafishana mmoja mmoja tusiwepo? Ni nani anayechochea vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa maslahi yake? Ukabila ni uovu wakati al-Shabaab ni gonjwa sugu lisilo na dawa ambalo linaua watu kwa halaiki. Kwa nini hatujikumbushi mafundisho ya dini, kutatua migogoro na kuzuwia umwagaji damu? Hali hii haivumiliki na kwa hivyo tuungane ili kupambana na dubwana hili - al-Shabaab, kwa sababu hawatambakisha mtu.

  • ben kiprop
    April 17, 2012 @ 03:57:17AM

    Hii ni habari nzuri lakini kwa al-Shabaab acha niwaambieni kuwa Somalia ni ya Wasomali na ni wao peke yao wanaoweza kuifanya itawalike. Jengeni nchi yenu na muache shughuli za kijeshi kwa sababu hazitawasaidia nyinyi wala nchi hata kidogo. Watu wa nje watakuja Somalia kwa ajili ya maslahi ya kiuchumi tu na sio kuwasaidia Wasomali kwa vile ni nyinyi Wasomali ambao mtajenga nchi yenu na wala sio mtu mwengine yeyote. Viikataeni vitendo vya al-Qaeda, al-Shabaab na mambo ya koo ikiwa mnataka kuendelea. Somalia imeshapoteza uwezo wake mkubwa, hakuna haja ya vitendo vya uhalifu. Ikiwa nyinyi watu mnaipenda Somalia. Tafadhalini wasimamisheni al-Shabaab, al-Qaeda na vitendo vyao na muunge mkono shughuli za KDF na AMISOM kwa ajili ya Somalia iliyo bora.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo