Aprili 12, 2012
Wakati uharamia unaendelea kuwa tishio kwa ubaharia huko bahari ya Hindi, unaosababisha hasara kubwa za kiuchumi, serikali kadhaa na waandaa sera wanasema ushirikiano wa kikanda ni ufunguo muhimu katika kushughulikia suala hili.
“Ikiwa kuna wakati wowote kulikuwa na haja ya juhudi za pamoja na ushirikiano, basi juhudi hizo zinahusiana na uharamia,” Waziri wa Ulinzi wa India A. K. Antony alisema hivi karibuni katika kufungua mkutano wa mwaka wa siku mbili katika Shirika la Bahari la India.
Mkutano huo wa washauri mabingwa ulikusanya wazungumzaji kutoka Marekani, Ufaransa, Australia na nchi za Ghuba pamoja na India. China ilijitoa katika mkutano huo wa tarehe 27-28 Februari.
Tangu ilipojiunga na juhudi za kupambana na uharamia mwaka 2008, Jeshi la Maji la India limeziongoza kiasi cha meli 2,000, asilimia 85 kati ya hizo zikiwa na bendera za kigeni, alisema Antony, na kueleza kuridhika kwake kuwa India imechangia katika “juhudi za pamoja za usalama”.
“Lakini changamoto ya uharamia bado halijafanikiwa kikamilifu, na kuna makubaliano kuwa wakati maharamia wanaweza kuidhibiti baharí, ufumbuzi wa kweli uko katika kushughulikia kiini cha sababu, ambazo ni nzito na kwa sasa ziko nchi kavu,” alionya.
Antony alitoa ufafanuzi wa kipengele hicho katika mahojiano kwa njia ya simu iliyofuatia na Khabar South Asia. “Kuna haja ya kung’oa sababu za msingi za uharamia, na kwamba kuna ukosefu wa chakula na njaa katika mataifa ambako maharamia wanaishi,” alisema waziri huyo.
Kwa mujibu wa Kituo cha Kuripoti Uharamia cha Shirika la Kimataifa la Bhari (IBM), tatizo liko zaidi katika njia zipitazo Bahari ya Arabia na Ghuba ya Aden. Ni katika sehemu hii yenye matatizo ya kisiasa, ambako India, China na Japani hivi karibuni zimeongeza ushirikiano wao.
Mataifa hiyo matatu, yanayofanyakazi kila moja likijitegemea katika Ghuba ya Aden, yamekubaliana kubadilishana habari na uratibu juu ya mwenendo wa meli za vita katika ushoroba muhimi yakiwa na lengo la kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mapengo hafifu ya kulinda meli za mizigo.
“Kabla, msafara wa ulinzi [wa India, Japan na China] ulikuwa unafuatana karibu pamoja katika muda mfupi, na kuiacha Ghuba ya Aden bila ya ulinzi kwa sehemu kubwa ya siku,” alisema Msaidizi Mkuu wa Maafisa wa Jeshi la Majini. Monty Khanna aliuambia mkutano huo wa New Delhi mwezi Februari, kwa mujibu wa gazeti la masuala ya kisasa la The Diplomat.
Ghuba ya Aden ni njia ya meli muhimu sana kwa uchumi wan chi hizi tatu. Wizara ya Usafirishaji Baharini imekadiria kuwa India inaagiza kutoka nje kupitia Ghuba ya Aden kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 50, na husafirisha dola za Kimarekani bilioni 60, kila mwaka, gazeti hilo lilisema.
“Mpangilio huu mpya ni bora zaidi,” Khanna aliiambia Khabaar South Asia. “Msafara wa ulinzi wan chi hizi tatu zinazoshirikiana kwa sasa zitaweza kubadilishana zamu ya ulinzi katika eneo lenye hatari zaidi na hatimaye zitaruhusu meli za biashara kupita kwa usalama.”
Kapteni Pradip Kundu wa meli ya biashara MV Karine Bulker aliiambia Khabar kuwa maharamia wa Somalia wamebadilisha tabia zao za uharamia”.
“Hapo kabla, maharamia walikuwa wanazishambulia meli katika bahari za Malacca na Indonesia. Walikuwa wanakamata pesa na vitu vingine vya thamani. Utekaji nyara haukuwa dhamiri yao. Sasa wamebadilisha tabia zao za uharamia. Wanawazuia mabaharia kama mateka na hata kuwatesa.”
India tayari imeshaunganisha nguvu na Ulaya katika kushughulikia uharamia. Kwa kiwango cha juu, mkutano wa EU-India huko New Delhi mwezi Februari, unafanywa kuwa rasmi kwa ushirikiano wake katika Operesheni Atlanta, ambayo ilikuwa operesheni ya kwanza ya jeshi la majini la EU.
Operesheni Atalanta imepeleka baina ya meli tano na kumi nje ya mwambao wa Somalia kuanzia mwaka 2008 ili kufuatana na meli za misaada ya kibinadamu na kuepuka mashambulizi ya maharamia kwa meli za biashara zinazotumia njia muhimu za meli.
EU uliidhinisha hapo tarehe 23 Machi kuruhusu meli zake za kivita kuvipiga vyombo vya maharamia katika fukwe za Somali, na kupanua misheni ya kupambana na uharamia hadi mwezi Disemba 2014.
Muda ulioongezwa wa misheni ya EU katika Pembe ya Afrika utawaruhusu watendaji wa kijeshi kuyapiga magari, bidhaa, boti na mafuta yanayowekwa katika mwambao.
NATO pia ilikubali hapo tarehe 19 Machi kuongeza Ngao ya Operesheni Baharini hadi mwaka 2014, na kusema kuwa juhudi za kimataifa za kudhibiti uharamia zinasaidia kupunguza idadi ya utekaji nyara.
Misheni ya NATO, ambayo inazo meli nne za vita katika bahari za Pembe ya Afrika, zimekatisha wizi na kuvisindikiza vyombo vya Umoja wa Mataifa vinavyopeleka misaada Afrika tangu mwaka 2008.
Maharamia wanaofanya shughuli zao kutoka Somalia walitekeleza mashambulizi 237 mwaka 2011, zaidi ya nusu ulimwenguni kote, kwa mujibu wa Shirika la Bahari la Kimataifa (IBM).
Mashambulizi ya Somalia yaliigharimu dunia karibu ya dola za Kimarekani bilioni 7 mwaka 2011, ikiwa ni pamoja na dola za Kimarekani bilioni 2 katika operesheni za kijeshi, walinzi wenye silaha na vifaa kwa ajili ya kuzilinda meli, kikundi cha Marekani kinachosimamia Uharamia kilitoa tathmini hapo mwezi Februari.
Kwa mujibu ya takwinu za IBM za mwaka 2012, ambazo zilisawazishwa tarehe 19 Machi, kwa sasa maharamia wa Somalia wanashikilia vyombo 13 na mateka 197.
Lakini licha ya idadi kubwa ya matukio ya kiharamia mwaka 2011, utekaji nyara ulipungua mwaka huo hadi kufikia matukio 28, kutokaa 49 mwaka uliopita.
“Idadi kamili ya uharamia wa Somalia ungeweza kuwa mkubwa zaidi kama isingekuwa ni kwa juhudi za vikosi vya majeshi ya majini vya kimataifa,” IBM ilisema katika taarifa yake ya mwaka 2011.
Uharamia umeharibu tasnia za uvuvi na utalii katika nchi nyingi na taathira zake zimezidi mara tatu kuliko ilivyotarajiwa. Mkurugenzi wa Baraza la Mambo ya Ulimwengu lililoko India Vijay Sakhuja aliiambia Khabar kuwa uharamia umekatisha uwezo wa wanasayansi wa India kufanya utafiti wao wa pepe za monsuni katika Bahari ya Hindi.
“Suala hilo linaweza kusababisha matatizo wakati uchumi wa nchi unaelekea kutokana na mwenendo wa pepo hizo za msimu,” alisema.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Uhalamia ni tatizo kubwa katika kanda hii ya EST AFRICA inatupasa kuangalia chanzo cha tatizo sio kuangalia uhalimia tu nionavyo uhalamia unafadhiliwa na nchi za maghalibi kwa maslah yao binafs na kuweka hali za nchi zinazochipukia kiuchumi kuwa katika wakati mgum zaidi
Inafurahisha sana muonekano wa kila upande.