Wachambuzi: Al-Shabaab yawatumia wanawake wa mabomu ya kujitoa muhanga kama kimbilio lao la mwisho

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Aprili 06, 2012

 • 59 Maoni
 • Chapisha
 • Panga upya Punguza Ongeza

Wachambuzi wa Somalia waliiambia Sabahi kuwa shambulio la mwanamke aliyevaa bomu la kujitoa muhanga katika Jumba la Taifa la Maonesho siku ya Jumatano (tarehe 4 Aprili) linaonesha kuwa al-Shabaab wanakabiliwa na tatizo la kuandikisha watu wa kujitoa muhanga kwa mabomu na inawaandikisha wanawake wa mabomu ya kujitoa muhanga kama hatua yao ya mwisho katika kubadilisha mkakati wao wa kigaidi.

 • Maafisa usalama wakitoka nje ya Jumba la Taifa la Maonesho mjini Mogadishu baada ya shambulio la Jumatano la bomu la kujitoa muhanga. [Na Mahmoud Mohammed/Sabahi]

  Maafisa usalama wakitoka nje ya Jumba la Taifa la Maonesho mjini Mogadishu baada ya shambulio la Jumatano la bomu la kujitoa muhanga. [Na Mahmoud Mohammed/Sabahi]

“Inaonesha kuwa al-Shabaab wanakabiliwa na tatizo la kuwashawishi watu kufanya mashambulio ya kujitoa muhanga, na ndio maana wanakimbilia walipuaji wa mabomu ya kujitoa muhanga wanawake katika jaribio lao la kubadilisha mkakati katika operesheni zao za kigaidi,” alisema mchambuzi wa masuala ya kisiasa Yusuf Mohammed, mwanachama wa zamani wa baraza la Muungano wa Mahakama za Kiislamu.

“Njia zinazotumiwa na magaidi zinaonesha kuwa wao [al-Shabaab] ni maadui wa amani na watu wa Somalia,” Mohammed aliiambia Sabahi, na kuongeza kuwa vitendo vyao vinaonesha kabisa wasivyothamini maisha ya binadamu.

Kiasi cha watu sita waliuawa na 10 kujeruhiwa wakati msichana alipolipua ukanda wa milipuko, akimlenga Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali na mawaziri wengine walohudhuria. Washirika hao wa al-Qeada, al-Shabaab walidai kuhusika kwa shambulio hilo.

Shambulio hilo lilikuwa la aina yake lililolenga Jumba la Taifa la maonesho tangu lilipofunguliwa upya mwezi uliopita baada ya miaka 20, alama yenye nguvu ya mabadiliko. Limetokea wakati Mogadishu inashuhudia kuimarika kwa hali ya usalama kutokana na kuondolewa kwa al-Shabaab mwezi Agosti 2010.

“Tendo la magaidi kulenga sehemu zilizojaa wananchi ni ishara kubwa ya udhaifu wao na kukosa kwa uwezo wa kukabiliana na vikosi vyenye silaha katika uwanja wa vita. Haiko wazi kuwa kwa nini wawalenge wananchi bila ya kuchagua,” Mohammed alisema. “Zaidi, mashambulizi ya kujitoa muhanga yanayofanywa na wanawake ni suala geni kwa utamaduni wa Somalia. Kama kuna lolote, basi hili linaonesha kuwa [al-Shabaab] inawawia vigumu kuwaandikisha watu ambao wangefanya mashambulizi ya kujitoa muhanga kwa sababu wanaharibu matumaini na ndoto za watu wa Somalia.”

Hii ni mara ya pili mwanamke kufanya shambulio kama hilo nchini Somalia. Hapo mwezi Juni 2011, Waziri wa Mambo ya Ndani na Uslama Abdishakur Sheikh Hassan aliuawawa katika shambulio kama hilo nyumbani kwake mjini Mogadishu.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Mukhtar Abdinur anasema kilichotokea katika Jumba la Taifa la Maonesho haliwezi kuwa limesababishwa na usalama legelege mjini Mogadishu. “Licha ya juhudi za serikali ya Somalia kuimarisha usalama mjini, magaidi wanajaribu kubadili mkakati wao kwa kuwatumia wanawake wanaojitoa muhanga kwa mabomu; hili ni kimbilio lao la mwisho,” aliiambia Sabahi. Alisema anatarajia kuwa watu wa Somalia watazishinda changamoto hizo katika mapambano yao ya kutafuta amani.

Wanawake huponyoka katika usalama

Maafisa wa usalama wamesema mkosaji wa shambulio hili la kujitoa muhanga alikuwa mwanamke ambaye alidharauliwa na afisa wa polisi. Mohammed alisema, mlinzi katika jumba la maonesho, alisema mshambulizi alisisitiza kuingia katika jumba hilo, akisistiza kuwa alikuwa afisa w apolisi.

“Tulimzuwia, lakini baadhi ya walinzi wa waziri mkuu walituambia tumwache kwa vile alikuwa na kitambulisho cha polisi,” Said aliiambia Sabahi. Alisema alijilipua sekunde chache baada ya Waziri Mkuu kupanda jukwaani kutoa hotuba yake.

Vikosi vya usalama vya Somalia na Umoja wa Afrika ndivyo vilivyokuwa dhamana wa usalama katika jumba la maonesho, wakilazimika kuwakagua wale wanaoingia katika jengo hilo.

“Hatujui vipi alimudu kuingia katika jumba la maonesho kwa sababu kulikuwa na upekuzi mkali wa usalama uliowahusu wageni wote waliotembelea jumba hilo, wakiwemo wabunge mara tu baada ya kuingia katika ukumbi wa jumba hilo, Mbunge Mohammed Omar Dalha aliiambia Sabahi.

Viongozi wa kimataifa walaani shambulio

Jumuiya ya michezo ya Somalia ilipoteza watu wake wawili muhimu sana katika shabulio hilo: Said Mohamed Nur "Mugaanbe", raisi wa Shirikisho la Mpira la Somalia, na Aadan Haaji Yabaroow "Wiish", raisi wa Kamati ya Olimpiki ya Somalia.

Serikali ya mpito ya Somalia, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika walililaani vikali Shambulio hilo.

Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia Balozi Augustine Mahiga alisema, “Hatima ya Somalia haiwezi kufanywa mateka na wachache wenye vurugu ambao wamekimbilia vitendo vya kioga vya kigaidi vinavyowalenga raia wenzao.” Alilitaka taifa la Somalia na viongozi wake kuthibitisha tena wajibu wao wa kuelekea amani na masikilizano.

“Tusiliruhusu tukio hili la kusikitisha kukwamisha maendeleo yanayofanywa nchini Somalia,” alisema. “Kufunguliwa upya kwa Jumba la Taifa la Maonesho ni alama ya mabadiliko ya kweli ambayo yanatokea nchini Somalia: mji huu unajengwa upya, utamaduni unafufuliwa na matumaini yanarejeshwa.”

Brigadia Jenerali Audace Nduwumunsi, naibu kamanda wa Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia, alilieleza shambulio la jumba la maonesho kuwa ni uhalifu wa kuchukiza uliofanywa dhidi ya watu wa Somalia.

“Kwa mara nyingine tena njia za magaidi zinaonesha kuwa ni maadui wa amani na wageni kwa utamaduni wa Somalia. “Kwa shambulio lao hili wanajaribu kukwamisha matumaini na ndoto za watu wa Somalia lakini watashindwa.”

“Kitendo hiki cha kigaidi kinaonesha jinsi gani magaidi walivyochanganyikiwa, kwa vile walishashindwa kwenye uwanja wa mapambano. Kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab kinavuta pumzi zake za mwisho,” alisema Waziri Mkuu Ali, na kuiambia AFP kuwa yeye ndiye aliyekuwa amelengwa katika shambulio hilo.

“Vitendo hivi vya kuchanganyikiwa na vya kizimwi vinavyofanywa na magaidi havitaturejesha nyuma na kutuzuia tusitekeleze majukumu yetu ya kitaifa. Kinyume chake, vinaupa nguvu zaidi uamuzi wetu wa kuwasagasaga magaidi hawa na kuleta amani ya kudumu na utulivu nchini mwetu na kwa ajili ya watu wetu,” alisema.

“Kushambulia jumba la maonesho lilikuwa tendo la kiwoga linalothibitisha ni kiasi gani wamechanganyikiwa,” alisema Raisi Sheikh Sharif Sheikh Ahmed. “Wanajaribu kuzuia maendeleo yaliyokwishafanywa na watu wa Somalia na wanajaribu kuharibu matumaini ya amani na utulivu nchini kote. Serikali ya Somalia inalaani shambulio hili la kinyama na linatoa rambirambi kwa familia za wahanga na tunawatakia wale waliojeruhiwa wapone haraka.”

Ahmed alitoa wito kwa watu wa Somalia kusimama na kuungana dhidi ya wale wanaoua watu Somalia, na kuahidi kuwa watavikimaliza vikundi hivi vya kigaidi karibuni sana.

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

 • Hamse sheikh
  June 17, 2012 @ 05:43:29PM

  Hizi zitakuwa ni tetesi tu. Nina wasiwasi iwapo Mogadishu na maeneo yanayoizunguka yatakuwa ya amani milele mpaka pale watakapokaa pamoja na kutubu kwa Mungu kwa ajili ya dhambi ambazo wamefanya.

 • abuu mucaad
  June 15, 2012 @ 04:34:39AM

  Amani iwe juu yenu. Baada ya maamkizi, ningependa kusema kuwa kila mmoja analitafsiri neno ugaidi kwa njia yake mwenyewe na mimi yangu ni moja katika hizo. Kwa maana yangu mwenyewe, ninafahamu kuwa magaidi ni watu wanaozivamia nchi za Kiislamu na kuua Waislamu. Wewe unamjua nani kama gaidi katika maana yako mwenyewe. Ninafahamu gaidi ni yule anayeupiga vita Uislamu na kuua Waislamu wanaopenda kutumia Sharia ya Kiislamu. Tunaweza kusema nani ni gaidi? Ni wale Waislamu wanaopigana kulinda dini yao kutoka kwa madui au wale wanaouvamia Uislamu? Mimi siwatambui al-Shabaab kama ni magaidi. Al-Shabaab ni kikundi pekee kinachopigana kulinda dini na Wasomali dhidi ya maadui na ikiwa ninaweza kukuulizeni: ndugu zangu, ni nani anakiuka haki za wengine baina ya mvamizi na yule anayeulinda Uislamu na Wasomali dhidi ya uvamizi?

 • abdirisaak cilmi
  June 14, 2012 @ 09:56:23AM

  Uhuru, ubinadamu na jina zuri la Wasomalia, mambo yaliyokua yanajulikana, sasa yote yako katika tishio. Haya yaliongozwa na viongozi wa dini waliotujia kwa jina la Muungano wa Mahakama za Kiislamu. Kikundi hiki kiliundwa na al-Shabaab na wale waliopo serikalini wakiongozwa na Sheikh Sharif. Wakauza bandari ya Somalia kwa Kenya na kila mtu analijua hilo. Wamechanganya maisha na siasa. Sasa wameanza mazungumzo na Somaliland. Wanataka kujua kwa nini Somalialnd inataka kuwa nchi huru? Kwa nini hawasemi tu kuwa Somaliland itambuliwe kama taifa huru?

 • taageer islam
  June 10, 2012 @ 12:46:45PM

  Naweza kuwahakikishia kwamba taarifa niliyosoma katika tovuti ilikuwa na maana ya kuwadhihaki Al-Shabaab. Napenda kukuambieni kwamba si watu pekee tu ambao hufa kwa ajili ya Mungu katika kuilinda dini. Uislamu kama dini iliteremshwa ili kuongoza wanaume na wanawake na kwamba wana wajibu sawa katika kuilinda. Waislamu wote wana wajibu sawa na umoja wetu, bila kujali jinsia,kuilinda dini ni kitu muhimu. Kauli zenu hazitatuvunja moyo na kwa kweli ni wapiganaji wa vita vitakatifu lakini ni bahati mbaya kusikia madai hayo kutoka kwa Waislamu ambao akili zao zimetiwa sumu na bado wanafikiri kwamba wako sahihi. Wengi wenu mmekuwa mkiharibiwa kiakili kiasi kwamba mmefanywa kuamini kwamba Uislamu ni dini ya ugaidi. Magaidi ni wale wanaowatia mawazo ya kubadilisha dini zenu na utamaduni wenu unaohitajika na mpango wa muda mrefu wa miaka 100 ijayo. Ukweli ni kwamba wasiokuwa Waislamu watapata faida ya asilimia 3 ambayo itaathiri kizazi chetu cha baadaye cha Waislamu katika kila kitu kizuri wanachofanya kwa ajili yetu kwa sasa. Al-Shabaab ni kikundi kinachojumuisha watu waliongoka na sisi pia tunaomba kwa Mungu kutuongoza njia iliyo sawa. Napenda kuhitimisha kwamba jamii ya Waislamu inaamini katika maneno ya Mungu (tutailinda dini) na nina uhakika Uislamu utashinda.

 • cabdulaahi
  June 6, 2012 @ 03:44:18PM

  Kabla ya kuzungumzia amani nchini Somalia, kwanza tungeizuia Kenya isinyonye rasilimali katika bahari yetu na kuwafunga wale kutoka Somalia ambao ni tatizo kwa meli kusafiri katika bahari zetu.

 • ali
  June 6, 2012 @ 02:51:05PM

  Ninapenda kuwaomba Wasomali kukaa pamoja na kupatana. Saidieni watu wenu ili kushinda majanga na njaa. Mungu hatawakatalia kile mnachomuomba, kwa hivyo msali, mumuombe amani na mpendane.

 • cabdi cumar
  May 29, 2012 @ 02:15:36PM

  Vipi tunaweza kuielezea vizuri Somalia kama nchi?

 • Raxmo Maxamed Jaamac
  May 29, 2012 @ 01:37:27PM

  Wanahistoria wa Kiislamu wanaiita itikadi hii “Khawariji” kwa maana ya waasi kutoka dini ya Kiislamu. Itikadi hii haifungamani na nchi na wakati maalumu, katika ulimwengu wa Kiislamu lakini popote Waislamu wanapoishi! Wanaishi na kufanya biashara katika Hargeisa. Wanachojali zaidi ni kuona biashara zao ni za misingi ya halali au haramu lakini sio wakweli katika maneno yao na mara moja hubadilika misimamo yao. Ikiwa wanashaka kuwa chanzo cha kazi yao sio cha halali kwa mujibu wa sheria za Kiislamu wanaisamehe. Mfano mzuri wa hili, ni pale mlipouliza mwanachama wa kikundi hiki na familia mbili na aliyetaka kuacha kazi yake kwa misingi kama hiyo, kwa nini hasubiri hadi mpaka apate kazi nyingine? Alinijibu kuwa ana wasiwasi ya mtaji alioanzia biashara alikuwa anafanyakazi katika ushuru wa forodha, kwa hivyo nikamwambia ni Mungu tu anayejua chanzo cha mtaji wa biashara yake na angeendelea kufanyakazi huko, halmuradi tu alikuwa anafanyakazi ya halali kwa biashara yake. Alikataa ushauri wangu na akastaafu kazini!! Nimekuwa nikimuona akifanyakazi katika kampuni chini ya mwezi mmoja. Kwa hivyo, itikadi hii haifungamani na jumuiya moja tu lakini ipo popote katika ulimwengu wa Kiislamu. Ikiwa inaungwa mkono, inakuwa imara na ngumu kuivumilia.

 • ABUBAKAR SHIIKH CUMAR
  May 27, 2012 @ 02:50:14PM

  AMANI IWE JUU YENU. BAADA YA SALAMU, IKIWA NITAELEZA HISIA YANGU, NINGEPENDA KUSEMA KWAMBA TUKO KATIKA TISHIO KUBWA KUTOKA KWA AL-SHABAAB. WATU HAWA WAMEPANDA MBEGU YA UHASAMA KATIKA JAMII YA WASOMALI. HAWA NI VIRUSI NA WATAMUATHIRI MTU YEYOTE ASIYE KUWA NA NGUVU ZA KISASA ZA KUPAMBANA NA VIRUSI. NINGEPENDA KUWAOMBA WAZAZI KUWA MAKINI NA WALE AMBAO WANAWAAMINI KUWAKABIDHI WATOTO WAO KUWAFUNDISHA SHULENI. TUKISHINDWA KUWA MAKINI NA WALE WANAOFUNDISHA WATOTO WETU SHULENI, BASI TUSISHANGAE KUONA WATOTO WETU WANAJILIPUA WENYEWE KATIKA MASHAMBULIZI YA KUJITOA MUHANGA KUTOKANA NA ITIKADI POTOFU YA KWENDA PEPONI IWAPO WATAJILIPUA WENYEWE. SISI KAMA WASOMALI, NADHANI HUU NI WAKATI WETU KUJITETEA WENYEWE KUTOKANA NA VIRUSI HIVI VINAVYOVAMIA WATU WETU NA MALI ZAO...ASANTENI

 • alib yare
  May 25, 2012 @ 08:40:04AM

  Hawa ni mashetani na sio al-Shabaab. Al-Shabaab maana yake ni “kijana”. Hawa waitwe Mashetani, sio al-Shabaab.

 • C/LAAHI MUUSE DARWIISH
  May 18, 2012 @ 09:02:41AM

  Al-Shabaab ni tishio kubwa kwa Somalia. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie kuwamaliza.

 • JAGEM IN KISMAYU
  May 18, 2012 @ 05:43:44AM

  KDF walikuwa hawafanya vizuri zaidi wakati AMISOM ilipoanza operesheni nchini Somalia. HONGERA KWAO.

 • cabdi wahaab
  May 17, 2012 @ 05:14:21PM

  Hakuna shaka kuwa al-Shabaab ni mtandao wa kimataifa wa kigaidi, kwa hivyo Wasomali lazima wawe na tahadhari juu ya kikundi hiki cha kigaidi na wakati huo huo wajaribu kufahamu vyanzo vya mapato, uongozi na itikadi zao. Ikiwa mtaweza kuzielewa hali zote hizi za kikundi nilichokitaja, mtaweza kuelewa pia kuwa al-Shabaab ni sehemu ya vuguvugu la Wanajihadi wa salafi linaloongozwa na kuendeshwa Afghanistani na Pakistani. Wanafadhiliwa na Saudi Arabia ambayo ni nchi ambako hupatiwa mafunzo ili kusitisha urejeshaji amani nchini Somalia. Misheni ya Saudi Arabia ya kukifadhili kikundi hiki ni kukatisha utafutaji na uchimbaji mafuta yaliyogunduliwa kwa wingi nchini Somalia kwa hofu ya kushindana na mafuta yanayozalishwa Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba ya Arabuni. Saudia inajaribu kila inachoweza kukatisha biashara ya baharini ya ulimwengu kwa kuwalipa maharamia wateke nyara meli zinazosafiri baharini.

 • ina muuse
  May 17, 2012 @ 02:22:28AM

  Hii inachanganya sana!

 • axmad
  May 16, 2012 @ 12:22:38PM

  Amani iwe juu yenu. Kila kitu kinachofanywa na Muislamu lazima kitokane na kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu na mila za mtume. Maovu yote haya yanayotokea leo Somalia ni kwa sababu watu wamedharau mafundisho ya kitabu kitakatifu.

 • geele
  May 16, 2012 @ 12:07:11PM

  Amani iwe juu yenu. Ningependa kuwaomba ndugu zangu al-Shabaab waache kupigana na kumwaga damu ya Waislamu wenzao.

 • rashiid
  May 16, 2012 @ 10:43:53AM

  Ni vyema kuwa mlitishwa na tangazo la karibuni la al-Shabaab na huu ujumbe utawasaidieni kuacha kuwakosoa wale walioongozwa vyema na njia za Mwenyezi Mungu. Ikiwa utakosoa jambo la haki au la, wakati utafika watawashindeni kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu.

 • moureen
  May 16, 2012 @ 10:05:59AM

  Hatutaweza kuondokana na watu hawa kwa sababu kichwa kiko Kenya wakati tunapigana na mkia ulioko Somalia. Mtu hawezi kumjua nani ni al-Shabaab kwa sababu Wasomalia wamejazana tele Kenya. Baadhi ya vijana wetu wa Kenya ni wanachama wao. Sababu inayowafanya kujiunga na kikundi ni kuwa Kenya hakuna kazi kule na wanapewa pesa nzuri. Tafuteni suluhisho zuri la kutatua suala hili la al-Shabaab. Kupigana nao hakutasaidia, kwa sababu Wakenya wengi wanakufa kutokana na mashambulizi mengi ya maguruneti.

 • JAMES KARANJA
  May 16, 2012 @ 06:43:19AM

  Haijalishi mbinu gani wanatumia, watashindwa tu.

 • ow malaaqow
  May 15, 2012 @ 12:34:04PM

  Ningependa kupata heshima ya kuwasalimu nyote.

 • Antonio Di Natale
  May 15, 2012 @ 09:34:15AM

  Ninaichukia Mogadishu na al-Shabaab. Ninaitakia Somaliland utulivu wa kudumu.

 • guuthey
  May 15, 2012 @ 08:12:38AM

  Al-Shabaab wanatakiwa waje na suluhisho bora la kudumu la kurejesha amani nchini badala ya kuua watu bila sababu. Hamuogopi laana ya Waislamu mnaowaua bila makosa? Hamuwahurumii Wasomali wenzenu ambao wamekumbwa na majanga au nyinyi ni wanaharamu mlioletwa na vikosi vya kigeni ambavyo havina huruma na jamii ya Wasomali? Mnafikiri al-Shabaab ni jumuiya ya kidini? Kwa ushahidi wa namna wanavyoua kimbari watu wasio na hatia nchini, wanaonekana kutumiwa na wageni waliofukuzwa toka nchini kwao kwa kusababisha matatizo. Mkishindwa kuilinda nchi yenu, wao wataichukua.

 • maxamuud
  May 14, 2012 @ 04:05:29AM

  Amani iwe juu yenu. Ninaweza kuona watu wengi ambao wamechanganyikiwa hapa. Ni bahati mbaya sana kuwa wanajiita kama wapiganaji wa vita vitakatifu lakini hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kusoma vizuri Sura ya Kwanza ya Kuran Takatifu. Hawajui chochote kuhusu dini ya Kiislamu na hawawezi kuwakilisha chama chochote cha Kiislamu.

 • fareerkaygii
  May 14, 2012 @ 03:44:44AM

  Kwanza ningependa kuwasalimu. Pili, al-Shabaab wanadai kuwa wao ni Waislamu lakini bado wanamwaga damu ya Waislamu wengine bila ya sababu yoyote. Tumesikia wapi au kuona Muislamu akihalalisha umwagaji damu wa Muislamu mwengine????!!!!!!!!!!!!!!!!!

 • Jeremy
  May 11, 2012 @ 04:59:18AM

  Al-Shabaab lazima wasafishwe kabisa na tena moja kwa moja.

 • johnson
  May 10, 2012 @ 01:56:40PM

  Al-Shabaab si Waislamu. Ni kikundi cha wahalifu chenye haja ya kuuwa Wasomali na kuwakatalia fursa ya kuishi kwa amani. Wasomali wote waungane dhidi ya genge hili.

 • CABDI
  May 10, 2012 @ 12:34:59PM

  KWA MAONI YANGU, NAHISI WANGEMUOGOPA MUNGU NA KUACHA KULIPUA WATU KWA MABOMU. WASOMALI WANGEVUMILIA MATATIZO YANAYOWAKABILI. AL-SHABAAB IMEUNDWA NA WATU AMBAO NI WAISLAMU NA SERIKALI NAYO YOTE INA WAISLAMU. NINAMWOMBA MWENYEZI MUNGU KUWAPATANISHA WOTE, SERIKALI NA AL-SHABAAB NA KUJENGA MAPENZI YA UDUGU BAINA YAO ILI WAACHE WASIO WAISLAMU AMBAO WANACHUKUA FURSA YA MGOGORO BAINA YAO. PIA NINAMWOMBA MUNGU KUREJESHA AMANI SOMALIA NAKUWAZUIA WASIO WAISLAMU KUINGIA KATIKA NCHI YANGU. AMANI IWE JUU YENU.

 • عبد الله الرفاعي
  May 9, 2012 @ 08:15:50PM

  Mwenyezi wahurumie raia wote na wale wote walioathirika kutokana na vurugu, uhalifu, unyama, ukatili na uovu uliofanywa na vikundi na magengi yanayoharibu utulivu na usalama wa nchi nyingi, ikiwemo Somalia. Nchi hii imeshuhudia kuwepo kwa kikundi cha al-Shabaab. Wamehusudi maisha ya raia masikini wa Somalia, ambao wamekabili changamoto chungu, zinazouma na kuogofya na mashaka. Damu ya watu wengi wasio na hatia imemwagika, na hawakutenda baya lolote, hasa linapokuja suala la mabomu ya kujitoa muhanga ambapo watu wengi wasio na hatia huuawa. Hawa ni wahanga wa operesheni za kigaidi zinazofanywa na al-Shabaab, ambao wametenda maovu mengi, operesheni za kikatili dhidi ya watu wa Somalia. Mwenyezi Mungu wahurumie watu wasio na hatia ambao damu yao ilimwagika na maisha yao kukatishwa na kikundi cha al-Shabaab, wanaolipua mabomu ya kujitoa muhanga! Wanatumia vijana katika kutekeleza operesheni hizo na kuwashambulia raia wasio na hatia. Wanawanyonya vijana kwa kuwajaribu kwa pesa na kuwasukuma katika utekelezaji wa mauaji haya ya kujitoa muhanga yanayopelekea vifo vya watu wengi wasio na hatia. Mwenyezi Mungu walaani, wadhalilishe na kuwatia aibu kwa kuwa wao ndio sababu ya vurugu, uhalifu na ukatili ambao sasa unatokea.

 • kelvin
  May 7, 2012 @ 09:33:20AM

  Al-Shabaab wanapaswa kuweka silaha zao chini na kuipa fursa amani, na wao kuzungumza juu ya uwezekano kuingizwa katika serikali Mpya ya Somalia.

 • mudane cawaadi
  May 7, 2012 @ 03:44:14AM

  Maoni yangu ni kuwa al-Shabaab washughulikiwe katika hali ile ile ambayo wamekuwa wakiitendea jamii, na viongozi wao wapigwe mawe mpaka kufa. Wao waliwaadhibu watu na kuwaita makafiri na kwa maoni yangu, na wao wafanywe hivyo hivyo.

 • Dr:xabuub
  May 5, 2012 @ 05:16:11AM

  Kwa nini nchi nyingine zinakataa kuitambua Somaliland ikiwa imeshaendelea? Ningependa kuwaambia watu mpigane kwa ajili ya eneo lenu na msione haya kulilinda. Huu ndio wakati muafaka, tuliambiwa na Mtume wetu katika hadithi zake, kwa hivyo tutubu na kurejea katika njia iliyonyooka.

 • arafaat c/kariin mead
  May 4, 2012 @ 12:42:25PM

  Ikiwa ninazungumzia al-Shabaab, kama mwanasiasa kijana, ninaweza kusema kuwa ni kikundi kinachotumiwa na kusaidiwa kiuchumi na nchi za kigeni ili kusababisha maangamizi nchini Somalia. Ikiwa Somalia itakuwa na amani katika siku za karibuni, kwa hivyo Burundi na AMISOM itabidi waondoke nchini mwetu.

 • Sheikh bundid.
  May 4, 2012 @ 03:32:41AM

  Nimekuwa nikihubiri juu ya uhalifu wa al-Shabaab na washirika wake tangu mwaka 2008 kupitia vyombo vya habari, baadhi ya Wasomali walikuwa hata wakanikaripia na baadaye kunishutumu na kuniita “mwendawazimu”, sheikh mpumbavu. Kwa kuwa sasa ukweli umejikuja juu, tunaweza kuendelea kuwalaani kila sekunde ili wasafishwe kutoka ardhi yetu. Sheikh Bundid.

 • P K
  May 3, 2012 @ 01:02:16PM

  NISEMAJE: DUNIA INABADILIKA.

 • xuseen muuse shiil
  May 1, 2012 @ 09:12:00AM

  Mimi natofautiana na al-Shabaab na ninaunga mkono jaribio lolote la kuwang’oa kwa sababu nimegundua kuwa hawa sio Waislamu na wameasi kutoka dini ya Kiislamu. Lazima wapigwe na wang’olewe nchini ikiwa kuna haja ya kurejesha amani nchini Somalia.

 • kevin mombasa
  May 1, 2012 @ 06:18:00AM

  Viongozi wa al-Shabaab watumie wake zao na watoto wao kufanya mashambulizi haya ya kujitoa muhanga na sio watoto wa watu wengine. Hata Osama aliwazuia watoto wake wasiingie katika jihadi na aliwahamasisha wakaishi nchi za magharibi. Ni aina gani hii ya watu waoga! Mwenyezi Mungu (Inshaallah) awashinde kama alivyofanya kwa Osama, Zarkawi, Fazool n.k. Kila kitu hutokea kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu!!

 • ismail mohamed ismail
  May 1, 2012 @ 02:56:06AM

  Nchi yetu; Somalia imejaaliwa malighafi ikiwemo mito lakini Wasomali hawajui na hawajali. Zamani Somalia ilikuwa Simba wa Africa lakini sasa imegeuzwa kuwa paka. Wasomali wanazugumza lugha moja na wanafuata dini moja; Uislamu, bado inakuwa shida kwao kupatana wao kwa wao. Sote tuombe kwa Mungu atusaidie kupata ufumbuzi wa matatizo yetu. Asanteni nyote. Kutoka kwa Ismo, nawapendeni.

 • zaki suldan hasan
  April 30, 2012 @ 08:52:19AM

  Nimesikitishwa sana na jambo hili.

 • SALIM
  April 30, 2012 @ 03:31:27AM

  Si ubinadamu kuua watu wasio na hatia wawe Wakristo au Waislamu. Tufikirie kesho ambapo tutasimama mbele ya MWENYEZI MUNGU kujibu maswali magumu kuhusu roho za watu wasio na hatia. Tuendeleze upendo, sio vita...

 • ken tush
  April 30, 2012 @ 03:00:47AM

  Nchi ya Somalia ni nzuri, tajiri na yenye raia wema lakini mpaka pale, watu wa Somalia watakapojua nini wanataka na wakipiganie, wawakabili magaidi bila ya woga au hisani, ndio wakati huo amani na maisha ya kawaida yatakaporejea huko Somalia.

 • Gelle
  April 29, 2012 @ 03:47:03AM

  Watu wa Somalia watafakari pamoja na kufahamu sababu zilizoko nyuma ya mashambulizi haya ya kila siku ya kujitoa muhanga. Kwa nini mashambulizi haya ya mabomu yanafanywa na vijana wadogo wa Kisomali? Nathubutu kusema kuwa kama vijana hawa wangepatiwa fursa za kazi, amali ya kufanya, lazima wangetulia wenyewe. Kwa hali yoyote, serikali na mizizi yake lazima wafanyekazi pamoja mkono kwa mkono na kujaribu kuwaotoa hawa wanaojiita Mujahidina. Wasomali lazima wanyanyue macho yao na kumjua nani ndie adui wao na nani sie.

 • mubarik
  April 28, 2012 @ 02:48:48AM

  Ningependa kuwaamkieni nyote. Ninaunga mkono taarifa hii lakini ningewaomba msiandike habari ambazo hamna uhakika nazo kwa sababu mnaweza kusababisha waomaji. Vyombo vya habari vimetoa aina 18 tofauti za tukio lililotokea. Mwanzo iliandikwa kuwa maafisa wa usalama walichukua fedha kwa kushirikiana na wahalifu, mara nyingine ikaarifiwa kuwa tukio lililotokea lilifanywa na maafisa wa waziri mkuu. Vyombo vya habari viliripoti pia kuwa hili lilipangwa kama ulipizaji kisasi baina ya makabila. Sisi tunajiuliza, ni habari ipi katika hizi ni sahihi na ipi ni ya uongo. Ripoti zinazopingana zinapindisha ukweli wa mambo na kuwaacha wasomaji wanabaika. Ningeviomba vyombo vya habari vya Somalia na waandishi wa habari wasiandike cochote kinachosemwa na watu badala yake wajaribu wanachokisema kiwe kina maana. Yoyote yule aliyelipua bomu la kujitoa muhanga, sisi tunababaishwa na nani aliyesababisha mlipuko. Asanteni.

 • SHARON NTHAMBI MUTINDA
  April 27, 2012 @ 03:25:07PM

  Wasomali wamefurahi sana kuwa na [serikali ya] mpito na kunufaika na nchi yenye amani kama kenya na vita vyake muhimu ambavyo vitaandika historia. Amani itakuja kwa Wasomali na wanasihi kuwashukuru Wakenya kwa vile watafaidika na nyenzo walizonazo na ambazo bado hazijagunduliwa. NAOMBA OPERESHENI ZILETE ATHARI NZURI KWA WASOMALI NA WAKENYA WANAOHUSIKA.

 • Joseph Musoko
  April 26, 2012 @ 06:43:24AM

  Ndio, siku moja mungu ataikomboa Somalia. Muda wake utafika karibuni. Tuwaache WAAFRIKA watubu, waswali na waingilie kati kwa Somalia.

 • [email protected]
  April 23, 2012 @ 05:44:07AM

  Ningependa kutoa rambirambi zangu za dhati kwa watu wote waliofikwa na msiba na ninamuomba Mungu awasaidie kuhimili wakati huu wa majaribu. Pia ningependa kutoa ushauri kwa watu wote wanafanya vitendo hivyo vya uharibifu wawakumbuke ndugu zao waliathiriwa katika tukio hilo.

 • Xaqaaiq
  April 21, 2012 @ 10:51:37AM

  Ningependa kukana habari kuwa wanawake wamekuwa walipuaji mabomu ya kujitoa muhanga kama inavyosemwa hapa na leo na siku za mbele, nitaiambia jamii juu ya uongo unaoandika kuwapotosha Wasomali. Mlipuko huu ulipangwa na serikali ya Mpito yenyewe. Si al-Shabaab wala jamii yoyote iliyodai kuhusika na mlipuko na tunajua kuwa mlipuko ulipangwa na serikali. Hamuwezi kutudanganya zaidi.

 • Dr. Dahir Mohamed Ghedi
  April 19, 2012 @ 03:51:39PM

  Hatuwezi kufumba macho yetu na kudharau haya yanayotokea Somalia. Tunahitaji kuja na mpango wa kutatua mzozo wa Somalia ambao dunia yote inayaushangaa.

 • NiX
  April 19, 2012 @ 10:20:01AM

  Iwe ni al-Shabaab au mtu mwingine yeyote, kikundi au vuguvugu ambalo linalenga kuwakosesha fursa binadamu kama njia ya kuwasilisha kutoridhika au pengine uroho, kuua ni kubaya sana na ni uovu. Fungueni macho, nyoyo na hisia zenu na muijenge nchi hii nzuri ya Somalia. Watoeni na muwashitaki wauwaji hawa, waongo na wezi wa Fahari la Taifa la Somalia. Baada ya yote, wananchi wa kawaida ndio wanaoteseka na wahangaikaji wakubwa.

 • Hibo Najax
  April 12, 2012 @ 04:16:50AM

  Tarehe 12 Aprili 2012 Nimesikitishwa sana na kile kilichotokea kwa sababu ni kitu cha kuhuzunisha na ni tofauti na misiba mingine iliyowahi kusababishwa na al-Shabaab. Al-Shabaab walijulikana tangu mwanzo kuwa walikuwa wanawahadaa wanaume kwa kuwalisha kasumba ya itikadi zao lakini sasa wameanza kuwahadaa wanawake pia. Ninapenda kufikisha ujumbe wangu kwa al-Shabaab wataulizwa mbele ya mwenyezi Mungu huko akhera kwa maovu wanayofanya sasa ulimwenguni. Yeyote anayefariki katika milipuko inayotekelezwa na al-Shabaab ataingia katika pepo ya Mwenyezi Mungu na pia kwa yule anayeuawa kwa mabomu ya kujitoa muhanga kwa sababu alilazimishwa kufanya hivyo na al-Shabaab.

 • axmedrooney
  April 12, 2012 @ 01:21:51AM

  Mungu Asifiwe. Ningependa kutoa shukrani zangu kwa Wasomali hasa maafisa wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho na viongozi wengine wa kijamii popote wanapoishi. Kwa kweli ni hadithi inayo huzunisha sana na ningependa kuyataka mashirika ya usalama ya serikali kuimarisha uchunguzi wa ukaguzi wa usalama kwenye milango ya kingilia uwanja wa ndege. Ukaguzi wa kina lazima ufanywe kwenye milango ya kuingilia viwanja vya ndege kwa kutumia zana za ukaguzi zenye nguvu, ili kuzuia vitendo kama hivyo visitokee tena.

 • Carol
  April 11, 2012 @ 10:24:25AM

  Serikali ya Somalia imepitia wakati mgumu kweli. Kikundi cha kigaidi kinaua wananchi wasio na hatia, watu hawa wanapaswa wajue kuwa zawadi yao ni hapa duniani tu kwa matumizi ya upanga uleule utakaowaua kama mlivyoua....Kwa nini muwatoe watu maisha na si kazi yenu? Ni kazi ya Mungu.

 • nuradin dahir hassan
  April 10, 2012 @ 06:09:41PM

  Mimi siishi Mogadishu lakini kwa maoni yangu, nafikiri mlipuko uliongozwa na AMISOM kwa sababu vikosi vya AMISOM viko Somalia ili kujipatia fedha kutoka Umoja wa Afrika, kwa hivyo, wanaweza kupewa fedha zaidi kutoka kwa al-Shabaab kuliko zile wanazopewa na Umoja wa Afrika. Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari, al-Shabaab walidai kuhusika na mlipuko huo kwa kusema kuwa waliouweka katika pahali pa kimkakati ndani ya jengo wakati serikali inasema mlipuko huo ulisababishwa na mwanamke aliyevaa bomu la kujitoa muhanga. Nani anasema kweli baina ya serikali na al-Shabaab? Nafikiri serikali inasema uongo kwa sababu haiwezi kuwakani serikali ishindwe kujilinda na walipuaji wa kujitoa muhanga kama hao licha ya juhudi za karibuni za kuzidisha usalama. Naamini kuwa wamo baadhi ya watu wa al-Shabaab ndani ya serikali ya shirikisho na iko haja ya kulifanyia uchunguzi suala hili.

 • suldaan
  April 9, 2012 @ 04:36:42PM

  Tahariri hii ni nzuri sana na inafichua ukweli.

 • Abdalla Muse Omer
  April 9, 2012 @ 04:17:15PM

  Amani iwe juu yenu. Ningependa kueleza maoni yangu juu ya al-Shabaab. Kila ambacho watu hawa wanafanya hakina mizizi katika dini ya Kiislamu kwa sababu hadithi za Mtume zinatuambia kuwa Uislamu ni dini ya huruma na baadhi ya ay aza Kuran Takatifu zinapiga marufuku kuuwawa kwa watu wasio na hatia kwa sababu yoyote ile. Uislamu unasisitiza kuishi kwa amani na kusaidiana. Pia Uislamu unatukataza kuwauwa wasio kuwa Waislamu ambao wanaishi na sisi na ambao hawaupigi vita Uislamu. Kwa hivyo al-Shabaab ni mashetani wanaojificha chini ya jina la Uislamu na inatupasa tujikinge dhidi ya vitendo viovu vyenye dhamira ya kuiangamiza jamii isiwepo. Ikiwa al-Shabaab wapo kwa ajili ya kazi njema yoyote inayohusu dini ya Kiislamu, kwa nini viongozi wao hawashiriki katika mabomu ya kujitoa muhanga? Hawafanyi hivyo, na hii inaonesha wazi kuwa sio watu wema. Ningependa kuwatahadharisha vijana wa Somalia popote walipo, dhidi ya itikadi za al-Shabaab za kupotosha zinazohamasisha mauaji ya mabomu ya kujitoa muhanga….(Hutaingia peponi kwa kutekeleza mauaji kwa mabomu ya kujitoa muhanga dhidi ya ndugu zako Waislamu ambao hawakufanya lolote… Mwenyezi Mungu anasema katika Kuran takatifu, “Ikiwa mtu atamuua muamini kwa kusudia, malipo yake ni moto, ambao atadumu huko (milele): Na hasira na laana ya Mwenyezi Mungu zitakuwa juu yake, na adhabu kali sana inatayarishwa kwa ajili yake.” Someni Kuran Takatifu na mufahamu maana yake. Mwenyezi Mungu atuongoze katika njia iliyonyooka. TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AWAOKOE NA AKUONGOZENI KATIKA NJIA ILIYONYOOKA…AMEN

 • حسن عبد الله
  April 9, 2012 @ 10:14:13AM

  Ikiwa tutakiangalia kwa jumla kikundi hiki – Kikundi cha Vijana wa Mujahdina Somalia – tutaona kuwa ni kikundi cha silaha kilichojikita katika maeneo fulani ya Somalia. Pengine wengi wao, au kwa uwazi zaidi, wanachama wanaokiunda, wanatoka katika nchi ambazo kinazidhibiti na wanatumia njia zile zile za kama kikundi chochote cha mapinduzi. Au, kwa kuweka wazi zaidi, wanaimarishwa kwa mauaji na vitendo vya kigaidi na wanatumia mkabala huu wa vurugu ili kufikia malengo yao, iwe lengo hili ni kuidhibiti Somalia au kueneza dini ya Kiislamu miongoni mwa watu wasio Waislamu nchini Somalia, au hata malengo mengine wanayoyatarajia, mpaka pale kikundi cha Vijana wa Mujahdina walipofuata mawazo ya al-Qaeda hivi karibuni, pamoja na tangazo la viongozi wao kuwa wana deni la kulipa kwa al-Qaeda na viongozi wake, na kwamba wanafuata njia moja na wao, au angalau njia zao ni sawasawa. Haya yanayapa umuhimu wa mawazo kwamba hii ndio nia ya kikundi hiki, kudhibiti nchi yoyote kama vile Somalia, kufuatia mkabala wa mawazo ya Kiislamu kwa mtazamo wao wenyewe ambao wangependa kuueneza. Lakini ningependa kusema kwamba mauaji, uharibifu na ugaidi sio jingine lolote bali ni njia chafu za kueneza itikadi na mkabala ambao wao wanaamini kuwa ni wa juu zaidi na ndio ulio sahihi kabisa. Dini ya Kiislamu inataka watu wawe wanavumiliana na kila mtu kuwa na heshima na kufanya mambo kwa wastani, kwa hivyo kuua watu wasio na hatia ambao hawana kosa lolote ni uhalifu mkubwa dhidi ya ubinadamu. Natamani ningejua kikundi hiki kinataka nini hasa.

 • falis
  April 9, 2012 @ 04:31:00AM

  Nimesikitishwa sana na kile kilichoteokea kwa sababu ni kitu kisichoweza kuaminika ambacho hakiwezi kufanywa na mtu mwenye akili timamu. Kwa hivyo, nafikiri walimtuma mwanamke kichaa ambaye ama alikuwa hajui kile alichokuwa anafanya au hajui kabisa thamani ya maisha. Alitumwa na watu ambao ni maadui kwa Wasomali wote, hasa wale wanaoishi nchini Somalia. Watu hawa ambao hawajui maana ya Uislamu na Jihadi (vita vitakatifu) na ambao hawathamini nchi na watu wake. Wasomali wa kweli hawachagui kuvaa ushungi na kuua kwa kujitoa muhanga. Hawa si chochote bali ni watu mmoja mmoja waliokodiwa ambao wana akili pungufu na woga. Tafadhali, msinielewe vibaya ikiwa nimetoa maoni marefu, ni kwa sababu tu nimehuzunishwa na uangamizwaji wa watu wa Somalia.

 • J K SIGEI
  April 9, 2012 @ 02:21:45AM

  Kwa kuwa huu ndio mtindo wao mpya, wanawake hasa kutoka jamii ya Waislamu lazima wachunguzwe kwa kina kutokana na mtindo wa mavazi yao. Si rahisi kujua wamebeba nini.

 • samuel
  April 8, 2012 @ 11:06:03AM

  al - shabab yapaswa kuhafishwa inchini

 • P N Githinji
  April 7, 2012 @ 10:44:27AM

  Somaliland ni nzuri sana, tajiri na inao raia wema lakini haitakuwa hivyo hadi pale watu wa Somalia watakapojua kile wanachotaka na kile wanachopigania, kuwakabili magaidi bila ya woga wala kuwahurumia; ndio wakati huo amani na masisha ya kawaida yatakaporejea Somalia.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo