Aprili 05, 2012
Wachambuzi wa washirika wa a-Qaeda al-Shabaab wamesema kuwa ukosoaji wa hadharani hivi karibuni wa kiongozi wa al-Shabaab Sheikh Hassan Dahir Aweys dhidi ya viongozi wengine wa kikundi na vitendo vyao kunaashiria kukua kwa mgogoro ndani ya uongozi wa kikundi.
Siku ya Ijumaa (tarehe 30 Machi), Aweys, kiongozi wa zamani ya kikundi cha Hizbu Islam, aliwashutumu viongozi wengine wa al-Shabaab kwa kumwaga damu ya Waislamu na kwa kuua wananchi wasio na hatia kwa jina la Uislamu. Alivielezea vitendo vya viongozi wa al-Shabaab kuwa wameenda mbali na Uislamu.
“Ninawaonya kaka zangu wa jihadi katika al-Shabaab kwa jina la Uislamu,” Aweys aliuambia mkusanyiko wa wafuasi wake
Onyo hilo lilikuja chini ya wiki moja kabla ya al-Shabaab walipochukua dhamana kwa shambulio lililoua maafisa wawili wa michezo katika jumba la maonesho huko Mogadishu, na kufuatia kuzuka kwa lawama za wachunguzi wa ndani kwamba kikundi shirika wa al-Qaeda kinaua wananchi wa Somalia wbila ya hukumu za halali katika lamama za vitendo vyao.
Pia, lawama hizo zilikuja baada ya kiongozi wa kigeni wa al-Shabaab, Omar Hammami, anayejulikana kama Abu Mansour al-Amriki, alitoa tarifa kuwa anahofia maisha yake kutoka kwa viongozi wengine wa al-Shabaab kwa sababu ya tafauti za kimkakati na kiitikadi.
Aweys alikuwa akitoa maoni juu ya taarifa iliyotolewa wiki iliyopita na kiongozi wa al-Shabaab, Ahmed Abdi Godane, , anayejulikana pia kama Mukhtar abu al-Zubair.
“Hairuhusiwi kuunda kikundi, chama au chombo chochote kiwa cha silaha au bila silaha katika maeneo yanayodhibitiwa na wanajihadi wa al-Shabaab kwa sababu inachululiwa kama njia ya kuwagawa, kuwadhoofisha na kuwachanachana Waislamu. Kikundi chochote kinachojaribu kuunda muungano mpya au chama kipya ndani ya al-Shabaab kitachukuliwa kama adui na lazima kipigwe vita,” Godane alisema.
Aweys alikuwa kiongozi wa zamani wa baraza la Muungano wa Mahakama za Waislamu, na alikuwa anaonekana kama mmoja wa viongozi wenye itikadi kali wa kikundi. Alichukua udhibiti wa Hizbu Islam mwaka 2009, akiapa kupigana na serikali ya Somalia. Alijisalimisha kwa al-Shabaab mwaka 2010 baada ya kushindwa katika vita vya kuwania madaraka ndani ya kikundi chake, kulikomlazimisha kuunganisha kikundi chake na al-Shabaab na kwa hiari yake kukabidhi silaha.
“Ukosoaji huu hadharani wa Sheikh Aweys dhidi ya viongozi wengine wa al-Shabaab kunaonesha kuongezeka kwa mgawanyiko wa ndani na mzozo miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab, kitu ambacho ni hali ya kuchanganyikiwa,” alisema Abdullahi Sheikh Hassan, mchambuzi wa masuala ya kisiasa kiongozi wa chama cha Muungano wa Amani.
“Pengine lengo la Sheikh Aweys katika kukua kwa mzozo na viongozi wengine wa al-Shabaab lilikuwa kupata fursa ya kutoka na kujiondoa ndani ya kikundi na kuunda kikundi chengine cha wanajihadi kilichojitenga na al-Shabaab, Hassan alisema. “Inawezekana pia alitaka kutuma ujumbe kuwa yuko tayari kuzungumza na kupatana na serikali.”
Ingawaje Aweys aliwahi kukiri hadharani tafauti zake na Godane katika taarifa za nyuma, hii ni mara ya kwanza kuthubutu kukosoa hadharani vitendo vya viongozi wa al-Shabaab, alisema Hassan.
Kwa mujibu wa ripoti kutoaka vyombo vya habari vya Somalia, ugomvi baina ya viongozi wa al-Shabaab umeongezeka tangu Mogadishu ilipokombolewa na majeshi ya Serikali ya Mpito ya Shirikisho pamoja na ya Umoja wa Afrika. troops.
Hassan alisema Aweys alikuwa na fursa ya kuonesha uwezo wake kwa sababu anao wanamgambo kutoka ukoo wake mwenyewe. Godono, hata hivyo, yeye anatoka Somaliland na hawezi kufaidika na kuungwa mkono kikabila kutoka kusini
Katika kuibu vitisho vilivyotolewa na Godane, Aweys alisema, “Huwezi kutishia kuua watu, na hakuna kikundi chcochote chenye haki ya pekee ya kupiganajihadi kwa sababu jihadi wajibu [wa kidini] na si wa kikundi kimoja pekee, kama vile al-Shabaab, kilivyo na haki ya kuchcukua bendera ya jihadi. Kila mtu ananshiriki katika jihadi, iwe mmoja mmoja au katika vikundi, shirika au makabila.”
"Watu wanaogopa kuwakosoa moja kwa moja viongozi wa al-Shabaab kwa sababu ya uuaji wake holela wa wananchi,” alisema. “Mimi siogopi kuwakosoa.”
Mohammed Mustafa, mchambuzi wa mauala ya kisiasa, alisema mvutano miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab umeongezeka tangu kikundi unakiambukiza kikundi kilipotangaza kujiunga na al-Qaeda mwezi wa Februari.
“Tafauti kubwa zinakiambukiza kikundi, lakini mgawanyiko wa ndani ulikuwa juu wakati kikundi kilipotangaza kuungana na mtandao wa kigaidi wa kimataifa, al-Qaeda,” Mustafa alisema. “Ikiwa hii haikuwa sababu, kwa nini Sheikh Aweys hakusema hadharani kabla juu ya mauaji ya wananchi na kuruhusu umwagaji damu wa Wasomali wasio na hatia?”
“Tangu al-Shabaab walipoungana na al-Qaeda, kumekuwepo na ishara zakuongezeka kwa mgawanyiko wa ndani miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab, na mzozo umeongezeka unaelekezwa kwa wale wanaopendelea kuungana na al-Qaeda na wale wanaolipinga hilo,” alisema.
Aweys alisema kuungana kwa al-Shabaab na al-Qaeda hakuwakilishi ukhalifa ambao unapaswa kufuatwa.
"Al-Shabaab na al-Qaeda ni sehemu ndogo tu ya kikundi kikubwa cha Uislamu na itikadi ya al-Qaeda haipaswi kuonekana kama ndiyo itikadi pekee, njia ya haki ya Uislamu,” alisema.
Al-Shabaab hawajawahipo kuwa kikundi kilichoungana kiitikadi, alisema mchambuzi wa siasa Ahmed Abdirahman, kiongozi wa kikundi ambacho kimegawika katika kambi mbili zinazoshindana tangu mwanzo.
Kwa mujibu wa Abdirahman, kikundi cha mwanzo ni al-Qaeda ambao ni wafuasi wa jihadi. Kikundi kidogo hiki kimekuwa kikiongozwa na Godane, ambaye “anatarajia awe kiongozi mkuu wa al-Qaaeda katika mashariki ya Afrika” na ambaye amekuweko nyuma ya muungano huu na al-Qaeda.
Kikundi chengie¡ne, kinachowajumuiya Aweys na afisa wa al-Shabaab Mukhtar Robow, wanasema wanapigna vita dhidi ya “uvamizi wa kigeni”. Kikunf¡di hiki “kinaichukulia Seriklai ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia kuwa imeundewa na vibaraka, lakini pia kinafikiria kuwa inawezekana kuzungumza na kupatana nao iwapo tu vikosi vya kigeni vitaondoka nchini,” Abdirahman alisema.
Ikiwa viongozi kama Aweys na Robow watachagua njia ya mazungumzo, Godane atajishitukia kuwa ametengwa, alisema Abdirahman.
“Bila ya shaka hatakuwa na uwezo wa kuendelea na njia ya jihadi kwa sababu hana uwezo wa kupigana na tayari ameshapoteza wanamgambo wengi wa al-Shabaab wanaotoka makabila ya kusini,” alisema. “Na hili linatokea wakati kuna shinikizo la kijeshi ambalo kikundi kinakabiliwa nalo kutoka pande tatu za mapambano kwa wakati mmoja.”
Msemaji wa serikali ya Somalia, Abdirahman Omar Osman "Yarisow", amemtaka Aweys kuweka silaha zake chini, kuacha kuwaua raia na kujiunga na utaratibu wa kutafuta amani.
“Ikiwa Aweys hataitikia wito huu, atamalizikia kama walivyomalizikia magaidi wengine kabla yake, na ndiyo maana anapaswa kuchagua amani kabla hajachelewa kabisa,” alisema Yarisow.
Hassan hakuondoa uwezekano wa kuwapo mawasiliano baina ya serikali na Aweys katika jitihada za kutafuta suluhisho la amani kumruhusu Aweys kujiunga na utaratibu wa amani baada ya kutangaza kuacha vitendo vya vurugu, kuweka chini silaha zake na kujiengua kutoka al-Shabaab.
“Inafahamika kuwa daima Aweys alikuwa akitafuta kuwa na udhibiti wa kisiasa…lakini al-Shabaab wamezizima jitihada zake,” alisema Hassan. “Sasa anajaribu kujiwasilisha mbele ya watu wa Somalia kama mtu ambaye hakubaliani na sera za al-Shabaab, ingawa mikono yake bado imetapakaa damu.”
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Sielewi kwa nini vita hivi Vitakatifu ni kwa ajili ya nini. Inakuwaje watu wanaweza kuua watu wenzao kwa jina la vita vitakatifu? Na kama vita vingekuwa vita vitakatifu kama wanavyodai, kwa nini basi wanaua watu wasio na hatia? Ni wazi kuwa vita hivi vinashajiishwa na siasa. Na mtu anaweza kushangaa kwa nini wanataka kudhibiti nchi ambayo watapaswa kuondoka serikalini. Hawa hawana hatima na enzi yao inaelekea kwenye maangamizi.Tayari wameshajisafishia njia ya kujimaliza wenyewe.
Amani iwe juu yenu. Kwa maoni yangu, mwanzo nilidhani al-Shabaab walikuwa wanapigana vita vitakatfu lakini niligundua baadaye kuwa vita vyao vilikuwa vya kisiasa na havihusiani vyovyote na dini. Kiongozi wa al-Shabaab; Godane alikuwa na dhamiri ya kuiangamiza Somalia Kusini ili Somaliland ipate uhuru wake na baadaye achukue uongozi wa nchi. Ikiwa ni kweli wanapigana vita vitakatifu, vipi tena wawe wanajihusisha na mizozo ya ndani?. Kulikuwa na ujumbe wa vitisho kutoka viongozi wa kusini kama vile Hassan na Mukhtar Robob kupinga na uhuru wa Somaliland. Ili kuzuia hilo lisitokee, ghafla Godane alitangaza kuishirikisha al-Shabaab na al-Qaeda. Ushirika huu haukukubaliwa na viongozi wote wa al-Shabaab na hii ndio sababu kwa nini kikundi kimekumbwa na migogoro ya ndani.
Wazo lililopendekezwa na ndugu yetu hapo kabla kuhusu mgawanyiko, na haja ya wengine ya kujiunga katika mchakato wa kisiasa kwa masharti kuwa waondokane na mawazo ya itikadi kali za “al-Shabaab”, ni mazuri na natumai kuwa serikali yetu tukufu itawapa fursa ikiwa watarudi nyuma na kujutia matendo yao ya nyuma. Lazima waache mawazo ya itikadi kali kwa sababu Mungu huwakubali kwa masharti kwamba hawarejei tena katika matendo yao mabaya.
Al-Shabaab ni kizazi cha shetani ambacho hakitasalimiaka na moto wa jahanamu baada ya kifo.
Hassan Dahir Aweys na Godane wametenda uhalifu ule ule...Wakati Bw. Aweys alipogundua kuwa hakuweza kupata maslahi yake binafsi, ndipo alipoamua kupingana na washirika wake. Wote wanapaswa kufikishwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu kwa uvunjaji wa haki nyingi za binadamu. Hata hivyo, ikiwa wataepuka kushtakiwa kwa uhalifu waliofanya, watakuwa na kujibu mbele ya Mwenyezi Mungu baada ya kifo. Wote wameshiriki katika mauaji, kuwalazimisha watu kuhama makazi yao na kuwaibia maelfu ya watu, na sasa wanatafuta kimbilio la salama.
Kwa maoni yangu, naamini kuwa Hassan Dahir Aweys hakuwa na haja na jamii ya Somalia moyoni mwake lakini yupo kwa ajili ya kuiharibu jamii ya Somalia kwa kuwahadaa baadhi ya watu kwa kutumia jina la dini na kuwaua watu wengine kwa wengi. Itikadi yake potofu aliyokuwa akieneza kwa muda mrefu haikufanikiwa, iliyopelekea kushindwa kwa al-Shabaab. Ukweli kuwa karibuni alijiunga na vikosi vya al-Shabaab hakukuthibitisha chochote zaidi ya kushindwa kwake; lengo lake pekee ni kukamata utawala, lakini ameshindwa kabisa na muda wake umepita.
Hili ni jambo la busara sana lakini itatubidi tusubiri Hassan atangaze hali yake kwa sababu bado anaonekana hajaamua.
Ni wazi kuwa maafisa waandamizi wa al-Shabaab wanakabiliwa na tofauti kubwa kwa vile wanajihadi wanamaanisha al-Qaeda waliojiunga nao hivi karibuni. Serikali ya TFG mpokeeni kwa mikono miwili Hassan Dahir Aweys kwa kujitoa kutoka al-Shabaab. Hii namaanisha Hassan anataka kuachana na vitendo vyake vya zamani wakati anapoona al-Shabaab inakabiliwa na matatizo mawili makubwa – shinikizo kutoka majeshi ya vikosi vya washirika kutoka pande nyingi kunadhoofisha nguvu za kikundi. Tatizo jingine ni kusema Godene ni kiongozi wa al-Shabaab na amepumzika kusini lakini hana athari yoyote kaskazini au haingilii kwa sababu ukoo wake uko katika eneo lenye utulivu na haruhusu kuingiliwa amani isipokuwa katika eneo la Sool aliua maafisa kadhaa wakubwa wanaotokana na ukoo wa Dhubahante. Lengo la Godene sio jihadi bali anataka kufanya vurugu zisizomalizika katika maeneo ya kusini na kaskazini mwa Somalia. Kuna suali liheshimiwe, kwa nini Godene alianzisha jihadi kutoka maeneo ya Kaskazini.