Al-Shabaab huwaua raia wa Somalia kwa mashitaka yasiyo halali

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Aprili 04, 2012

  • 7 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wanazuoni wa dini na wataalamu wa sheria wanakishutumu kikundi cha al-Shabaab kwa kutenda uhalifu na kufanya mauaji chini ya “visingizio vya uongo katika utekelezaji wa Sharia za Uislamu”.

  • Mwanamgambo wa al-Shabaab akiwasimamia raia wa Somalia mwezi Februari huko Elasha Bihaya. Imeripotiwa kuwa kikundi hiki huwaua watu hadharani ili kueneza hofu kwa raia. [Na Mohamed Abdiwahab/AFP]

    Mwanamgambo wa al-Shabaab akiwasimamia raia wa Somalia mwezi Februari huko Elasha Bihaya. Imeripotiwa kuwa kikundi hiki huwaua watu hadharani ili kueneza hofu kwa raia. [Na Mohamed Abdiwahab/AFP]

Mashirika ya haki za kibinadamu na wanaharakati pia wazishutumu mahakama za al-Shabaab katika maeneo wanayoyadhibiti. Hukumu hutolewa bila ya kesi halali na katika uvunjaji wa sheria za Somalia na za kimataifa, wanasema.

Mahakama zinazoendeshwa na al-Shabaab zimekuwa zikitoa hukumu zikiwemo za kuua, kupigwa mawe, kuchapwa viboko na ukataji viungo. Kikundi hiki washirika wa al-Qaeda mara nyingi huwapa tahadhari watu dhidi ya kushirikiana na serikali ya Somalia, hata kwa sababu za kawaida, na kuwatishia kuwaua.

Katika miaka mitatu iliyopita, kikundi cha al-Shabaab kimeshaua makumi ya wanawake na wanaume nchini kote kwa mashitaka yakiwemo ya kuisaidia Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia (TFG) na vikosi vya Umoja wa Afrika, au kwa kufanya upelelezi na serikali za jirani.

Katikati ya mwezi Machi, wapiganaji wa al-Shabaab walimuua kijana wa kiume chini ya miaka 20 huko eneo la Galgalato kaskazini ya Mogadishu kwa mashitaka ya kufanya upelelezi kwa vikosi vya serikali ya Somalia.

Al-Shabaab wanafanya mambo kinyume na sharia ya Kiislamu

"Utekelezaji wa hukumu ni suala la taifa lililo halali, na si haki ya kikundi chochote, iwe kinaamua kutekeleza adhabu ya kifo au kinatekeleza vifungu vya hudud,” alisema Sheikh Abdulqadir Somow, msemaji wa Baraza Kuu la wanazuoni wa Ahlu Sunna Wal Jamaa, sehemu ya Shirikisho la Sheria za Sufi nchini Somalia.

Sheikh Somow alisema al-Shabaab wametenda uhalifu na mauaji dhidi ya wananchi wasio na hatia chini ya kisingizio cha mashitaka ya upelelezi. Alisema kutokukubaliana miongoni mwa mahakimu wa Kiislamu dhidi ya watu wanaohukumiwa kwa upelelezi, lakini kuwaua haimo katika sharia ya Kiislamu.

"Kikundi hiki kimefanya zaidi ya uhalifu, na ikiwa utaangalia njia ambayo inaua watu, vitendo vyao havina mashiko ya kisheria, lakini ni kinyume na sharia ya Kiislamu,” aliiambia Sabahi. “Kikundi cha al-Shabaab kinatafuta tu kuwatisha raia wa Somalia kwa hukumu hizi.”

Wasomali wameshitushwa na utekelezaji mkali wa tafsiri za sharia ya Kiislamu. Kikundi kiliwakata vichwa watu kadhaa kwa mashitaka ya kuwa Wakristo, wapelelezi au waasi wa Uislamu. Baada ya kuwahukumu washitakiwa, wanachama wa al-Shabaab huwazika katika maeneo yanayojulikana kama “makaburi ya makafiri”, wakazi wa maeneo amabayo zamani yalidhibitiwa na al-Shabaab walisema.

“Katika miaka mitatu iliyopita, kikundi cha al-Shabaab, ambacho kilikuwa kinaudhibiti mji, walifanya mfululizo wa mambo ya kutisha ambayo yaliwatisha watu wengi mjini, alisema Omar Isac, mkazi wa Baidoa mwenye umri wa miaka 43, ambako karibuni vikosi vya washirika viliudhibiti. "Baidoa ilikuwa sehemu ya utekelezaji wa mauaji, Wanachama wa kikundi cha al-Shabaab wakati mmoja waliwakata vichwa wakazi saba wa mjini kwa mashitaka ya kuwa wakristo na wapelelezi mwezi wa Juni 2009."

Mohamed Hassan, mkazi wa Beledweyne katikati ya Somalia mwenye umri wa miaka 36, ambako vikosi vya washirika viliudhibiti mwaka huu, alisema al-Shabaab walifanya uhalifu mwingi dhidi ya wakazi wa mjini, na mbinu zao dhidi ya raia zimefikia kiwango cha kumuua yeyote waliyeamini alishirikiana na serikali ya mpito au kwa kushutumu sera za kikundi.

“Kikundi cha al-Shabaab kiliwaua wasichana wawili huko Beledweyne mwezi Oktoba 2010 kwa mashitaka ya kuvifanyia upelelezi vikosi vinavyoiunga mkono serikali, na huo ulikuwa uuaji wa kwanza wa aina yake kutokea mjini,” Hassan aliiambia Sabahi.

Hassan alisema kaburi la halaiki lililochimbwa na al-Shabaab liligunduliwa huko Beledweyne likiwa na zaidi wa miili 20 mwezi Januari. “Maiti zilizogunduliwa katika kaburi la halaiki zilikuwa pamoja na wananchi ambao kikundi cha al-Shabaab kiliwaua bila ya kuwashitaki,” alisema.

Somow aliwashutumu al-Shabaab kwa kutenda uhalifu dhidi ya watu wa Somalia chini ya kisingizio cha kutekeleza sharia ya Kiislamu.

Kikundi cha al-Shabaab kilitenda uhalifu kwa jina la Uislamu. Ni bahati mbaya kuwa jina la Uislamu linatumika katika kuwaua Waislamu wasio na hatia, alisema.

Somow alisema al-Shabaab “hawana haki yoyote ya kisheria ya kutekeleza vifungu hivyo, na hawana haki yoyote ya kutoa hukumu za kisheria kwa sababu hiyo ni haki ya kisheria ya viongozi rasmi”.

Al-Shabaab wafanya ‘mashitaka ya kujionesha’

Bashir Ahmed, profesa wa sheria na kiongozi ya jumuiya ya uangalizi wa sheria za nchi, alisema hukumu zinazoamriwa na al-Shabaab zilitolewa wakati wa mashitaka ya kujionesha ambayo yanakiuka viwango vya kimataifa vya sheria na haki za binadamu.

“Mauaji yaliyofanywa na kikundi cha al-Shabaab yalikuwa yanafanywa wakati wa mashitaka ya kujionesha, wakati mashitaka halali hayatolewi kwa washukiwa,” Ahmed aliiambia Sababhi. “Watu waliohukumiwa hawapewi haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hizo au kupinga maamuzi ya kisheria ili kujitetea.”

Alisema kuwa kuwazuia washitakiwa haki ya kukata rufaa juu ya hukumu dhidi yao au kujitetea wenyewe kunaonesha kuwa kikundi hiki hakithamini hata kidogo maisha ya binadamu.

Hassan Abdullahi, anayefanyakazi katika shirika la haki za binadamu nchini, alisema utaratibu wa al-Shabaab ni pamoja na kuwaalika watu kushuhudia mauaji hayo, na kusababisha athari hasi za kisaikolojia kwa watazamaji, zaidi kwa kueneza woga kuliko kutekeza haki.

“Kikundi cha al-Shabaab kinaonesha sehemu kadhaa za miili ya watu waliohukumiwa katika sehemu za umma na kuvitundika kwenye nguzo za umeme ili watu wa kawaida wavione,” Abdullahi alisema. “Mauaji haya na upigaji mawe hufanywa katika maeneo ya wazi yakiangaliwa na maelfu ya watu wanaoalikwa kushuhudia utoaji hukumu huo wakati wanapoufanya.”

Wanamgambo wa al-Shabaab huwalazimisha wakazi kushuhudia mauaji, upigaji mawe na mijeledi, alisema, huku wanatumia vipaza sauti kuwaita watu waje washuhudie.

“Wanamgambo wa al-Shabaab huwachinja wananchi na kuitupa miili yao mitaani au masokoni, na katika kesi nyingine vichwa kadhaa hutupwa mitaani na sehemu nyingine za miili yao kuachwa katika eneo jingine si mbali na kule vichwa vilikotupwa ili kuwatishwa watu na kusababisha hofu katika mioyo ya wananchi,” alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 14)

Dislike_icon(8)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • abudaxdaax
    May 15, 2012 @ 04:56:06AM

    Kwa asilimia 100 ninayakubali na ninayafurahia mafunzo ya Mtume Muhammada S.A.W. Baadhi ya watu wanafikiri kumkata mwizi mkono si jambo zuri; hii ni sharia ya Muumba, iwe ukapenda usipende. Wazinifu tunawapiga mawe wakati wanapofanya uzinifu. Yote haya niliyoyasema yamo katika sharia ya Kiislamu. Sisemi kuwa wanachofanya al-Shabaab ni sahihi, lakini ninazungumzia kuhusu lililo sahihi na kuandikwa katika sharia. Lakini si kila Muislamu lazima afuate dini kwa ukamilifu, kwa wale wanaofikiri kuwa ni dhidi ya haki za binadamu, wajue kuwa hii si dini ya haki za binadamu, hii ni dini ya Mwenyezi Mungu na yeye anafanya anachopenda.

  • Axmed shaakir suldaan xussen muuse
    April 30, 2012 @ 05:46:17AM

    Nadhani ni wakati sasa kufuata mafundisho ya Kuran Takatifu na mila za Mtume wetu (Amani Iwe Juu Yake). Hii ndio njia pekee tutaweza kufanikia hapa duniani na kesho akhera.

  • cabdi yare
    April 19, 2012 @ 04:19:09AM

    Ni nani bora zaidi kuliko yule anayeongoza kwa kutumia sheria za Kiislamu (Sharia)? Unafikiri yule anayeongoza kwa kutumia katiba iliyoandikwa na wasiokuwa Waislamu ni bora kuliko yule anayeongoza kwa kutumia sharia za Kiislamu?

  • calixiiray maydhane rayaale
    April 18, 2012 @ 07:39:24AM

    Ninaunga mkono vikosi vya pamoja vya Misheni ya Afrika na Somalia.

  • salihah
    April 14, 2012 @ 12:25:53AM

    Sheikh Abdulkadir, uko sahihi lakini unawazungumzia nani? Al-Shabaab ni kikundi ambacho kinatumia vibaya na kutoa picha chafu juu ya dini. Tunaitaka serikali iwakamate wanachama wote wa al-Shabaab, wawapeleke mahakani na kuwaadhibu kwa uhalifu waliofanya dhidi ya jamii. Tunajua wana makosa na tulishalisema hili kabla, kwamba hawawezi kutenda haki kwa kuua watu wakati kuwepo kwao sio halali kwa vile hawakuchaguliwa na watu. Kwa kuchukua hali zetu kama mfano, unafikiri hatima yetu itakuwaje ikiwa itaachwa katika mikono ya vikundi vya wapotofu kama al-Shabaab?

  • abdi kuus
    April 5, 2012 @ 12:11:51PM

    Wanachama wa al-Shabaab ni wezi wanaojificha chini ya kisingizio cha dini.

  • ringo
    April 5, 2012 @ 07:03:02AM

    Basi ni vyema lakini habari hii, unahitaji kutoa suluhisho la maana ili kukabiliana na tatizo au kulipunguza kiasi kwamba hakutakuwepo na watu waliojeruhiwa.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo