Kenya yawatuhumu al-Shabaab kwa mashambulio ya mwisho wa wiki

Na Julius Mokaya mjini Nairobi

Aprili 03, 2012

  • 16 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Viongozi wa Kenya waliwashutumu al-Shabaab kwa mashambulio mawili yaliyolenga kanisa na mgahawa katika eneo la Mombasa Jumamosi (tarehe 31 Machi), wakilaani vurugu na wakiapa kuwakamata mara moja.

  • Maofisa wa jeshi la polisi Kenya wakiweka lindo huko kaskazini mashariki mwa Kenya. Serikali ya Kenya imeongeza usalama katika maeneo ya utalii kwa kipindi cha sikukuu ya Pasaka. [Stringer/AFP]

    Maofisa wa jeshi la polisi Kenya wakiweka lindo huko kaskazini mashariki mwa Kenya. Serikali ya Kenya imeongeza usalama katika maeneo ya utalii kwa kipindi cha sikukuu ya Pasaka. [Stringer/AFP]

“Tutatumia rasilimali zote zilizopo kuondoa kundi hili la kigaidi,” alisema Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya George Saitoti mjini Mombasa wakati akiwafariji waathirika katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Pwani. “Wakenya wawe na tahadhari wakati wote. Hatutachoka kuwasaka watu hawa hadi tuwamalize. Wameangamiza nchi yao na sasa wamekuja hapa kuharibu uchumi wa Kenya.”

Mtu mmoja aliuawa na 33 kujeruhiwa katika mashambulio ya Jumamaosi. Shambulio la kwanza lilitokea saa 12:30 njioni, likilenga mkusanyiko wa wakristo katika eneo la wazi la mkusanyiko wa maombezi huko Mtwapa, takribani kilometa 10 kaskazini mashariki mwa Mombasa. Shambulio la pili lilipiga baa huko jirani na Tanonoka ya Kenya kama saa 1:00 jioni hivi.

Mlipuko huo umetokea kipindi cha chini ya mwezi baada ya shambulio lingine la mlipuko katika kituo kikubwa cha nchi cha usafirishaji wa umma na chenye watu wengi huko Nairobi, ambapo watu tisa waliuawa na 60 kujeruhiwa. Jeshi la polisi na Serikali ya Kenya pia waliwalaumu al-Shabaab kwa mashambulio haya.

Waziri alisema serikali itawalinda Wakenya na wageni kutokana na al-Shabaab, ambao amesema wanataka kuiharibu Kenya.

Waziri Mkuu Raila Odinga amewahakikishia tena watalii na raia kuwa serikali imeimarisha Usalama. Akiongezea kuwa wanaoshirikiana na washambuliaji watakamatwa.

“Polisi wetu wamegundua ushahidi muhimu sana, ambao hatuwezi kuuzungumza hadharani. Wanatumia vielekezo vizuri sana wakati wakijaribu kuwakamata wale wote walio nyuma ya vitendo hivi vya kutisha,” alisema Odinga, ambaye pia alitembelea maeneo yaliyodhurika na kuwatembelea waathirika hospitalini.

“Kenya iko salama. Hakuna atakayewatishia watalii. Waendelee kuja Kenya na serikali itawalinda,” aliviambia vyombo vya habari.

Msemaji wa Waziri Mkuu, Dennis Onyango, aliiambia Sabahi kuwa maofisa zaidi wa usalama wamepelekwa Mkoa wa Pwani kuimarisha usalama kwa kipindi ncha sikukuu ya Pasaka, kwa kuwa Mombasa ni sehemu kuu ya kusherehekea sikukuu nchini Kenya.

"Waziri mkuu ameagiza polisi na mawakala wengine wa usalama kuendelea na kasi ya kuimarisha usalama katika maeneo yote ya pwani na maeneo mengine ya nchi ambayo yanaweza kuwa yanalengwa na magaidi," alisema.

Mara baada ya viongozi wa ngazi za juu kuwalaumu kikundi kilichoshirikishwa na al-Qaeda kwa mashambulio, al-Shabaab walituma ujumbe katika akaunti yao ya Twittter wakitahadharisha mashambulio zaidi nchini Kenya kwa kuwa Jeshi la Ulinzi la Kenya linaendelea na shughuli zake nchini Somalia.

Zoezi la Linda Nchi la Kenya limefanikiwa kuwang’oa al-Shabaab kutoka Somalia Kusini tangu mwezi Oktoba, kufuatia mfululizo wa mashambulizi na utekwaji uliofanywa na wanamgambo wa al-Shabaab katika maeneo ya pwani ya Kenya. Utekaji ulifanywa zaidi kwa watalii wageni. Mwezi huu wanajeshi wa Kenya walishirikiana na majeshi ya AMISOM.

"Wananchi wa Kenya lazima watambue kwamba vikundi vingi vya Kenya vinaendelea kuwadhulumu Waislamu wa Somalia wasio na hatia, vichache vinatafuta maeneo ambayo wakenya wapo; na zaidi vinavyopinga wanavyojisikia Waislamu wa Somalia, zaidi sana vinabana maisha ya Wakenya yatakavyokuwa," kundi la wanajeshi lilitahadhalisha. "Hii ni sheria ya kutoa adhabu inayostahili. Usalama wenu unategemea usalama wetu. Ni vita ya muda mrefu na Wakenya ni lazima wasipate matarajio ya matokeo mazuri wala matumaini ya ushindi."

Sheikh Juma Ngao, mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Waislamu la Taifa, amelaani mashambulio hayo kuwa si ya haki na ni kinyume na Katiba ya Kenya.

"Huu ni uvunjaji wa haki za watu wengine kukusanyika na kuabudu. Ni kitendo cha kinyama na ni lazima kilaaniwe "aliiambia Sabahi. "Katiba inatuhakikishia na kulinda haki ya kila mtu na inapaswa kuheshimiwa. Serikali inapaswa kuwashughulikia kikamilifu wale wote waliohusika na mashambulio bila kujali imani zao."

Siku ya Jumatatu, hospitali kuu ya Mkoa wa Pwani ilitangaza kwamba watu waliojeruhiwa katika mashambulio walikuwa salama.

"Ninaweza kuthibitisha kwamba takriban watu 20 kati yao, wameruhusiwa na waliobaki wanaendelea vizuri. Hata yule mvulana mdogo ambaye hali yake ilikuwa mbaya ametolewa nje ya kitengo cha kuhudumia wagonjwa mahututi na atahitaji tu mtaalamu wa macho kumfanyia upasuaji moja kati ya macho yake," Dk. Maurice Simuyu, mkurugenzi wa tiba wa hospitali ya mkoa aliiambia Sabahi.

Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Pwani Aggrey Adoli aliiambia Sabahi kwamba vifaa vyenye mlipuko vilivyotumika katika mashambulio na askari wanajaribu kutafiti iwapo kuna kundi jingine la magaidi lililoshiriki katika mashambulio.

"Tunaendelea na uchunguzi na wanamgambo wa al-Shabaab ni mojawapo ya vikundi vya magaidi tunavyovichunguza," alisema. "Uchunguzi wetu wa awali unaonyesha kwamba kilichokuwa kikitumika katika mashambulio kilikuwa kikitoa milipuko, lakini bado tunaendelea kutafiti kuwa kilikuwa ni kifaa gani na uhakika wa chanzo chake."

Alisema pia kwamba usalama umekuwa pia ukiimarishwa katika maeneo muhimu kama vile kampuni iliyopo Mombasa ya Kenya Petroleum Refineries, Ltd.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 17)

Dislike_icon(4)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • tracy. R
    April 26, 2012 @ 02:46:33PM

    Uongozi wa Mungu ni bora zaidi sio tu kwa kushinda ugaidi bali pia kwa kujenga Kenya iliyo bora zaidi.

  • MIRRIAM KIARIE
    April 19, 2012 @ 05:48:56AM

    Watu hawa wanapaswa kujua kuwa kuna Mungu anayeishi ambaye ni wa haki na usawa kwa watu wake wote. Kwa hivyo ni wakati sasa wa kutafakari na kukumbuka madhara yote waliyoyasababisha kwa watu wengi wasio na hatia kila pahali. Mungu wazindue na uwafanye wafahamu kila wanachokifanya.

  • anne njoki
    April 19, 2012 @ 05:47:42AM

    Tusaidieni kwa swala, ili tuweze kuushinda ugaidi

  • DAVI
    April 18, 2012 @ 09:25:14AM

    Kwa nini watu wanafikiri kuwa al-Shabaab sio binadamu, ambapo majeshi ya Kenya yanafyatulia risasi chochote wasichoweza kukidhibiti. Ushauri wangu kwa askari wa Kenya ni kuondoka kutoka waliko al-Shabaab na ardhi ya Somalia. Si kila siku tunakuwa wakombozi. Hatuna ulazima wa kuteseka kwa ajili ya watu wanaopenda maisha yao katika mapamabano. Kwa hivyo, ikiwa kuna watu wema nchini Somalia, wako wapi?

  • emalingati
    April 18, 2012 @ 09:11:32AM

    Tufanye kama Wamarekani, hakuna kupatana na al-Shabaab, daima.

  • KINYUA FRESH
    April 16, 2012 @ 10:15:46AM

    TUFANYEKAZI ZAIDI YA KUWAMALIZA AL-SHABAAB

  • VICTOR
    April 16, 2012 @ 10:13:48AM

    KAZI NZURI KWA KENYA KULETA AMANI

  • samuel
    April 14, 2012 @ 06:13:16AM

    Wote walaaniwe na waingizwe motoni na sio peponi na bikra 20, huo ni upuuzi tu.

  • hash
    April 11, 2012 @ 12:35:14PM

    Kazi nzuri

  • misheck kariuki
    April 10, 2012 @ 08:55:03AM

    Wakenya wanatakiwa wawe na tahadahri muda wote na kila pahali. Waepuke maeneo yenye watu wengi na watoe taarifa polisi mara moja juu watuhumiwa wanaotuliwa shaka.

  • Duncan Otieno
    April 10, 2012 @ 08:48:49AM

    Kile ambacho al-Shabaab wanakiamini, hakioneshi kumpenda wala kumjali Mwenyezi Mungu ambaye sisi tunaamini ni mkubwa. Ikiwa tunataka isiwe hivyo, itakuwa Mwenyezi Mungu ni muuaji na gaidi, kitu ambacho hakistahiki kuunganishwa na Mwenyezi Mungu ambaye ni muumbaji na hawezi wakati wowote kukiharibu kile ambacho anachokiona ni kizuri.

  • James Kuria
    April 9, 2012 @ 12:34:00PM

    Wakati huu ambapo nchi yetu inakabiliana na maadui zetu al-Shabaab, lazima Wakenya wakubali ushauri wa kuepuka maeneo ya msongamano. Ikiwa ni vigumu kufanya hivyo, basi wawe walinzi na kukitilia shaka kitu chochote ambacho si cha kawaida. Pia, watafute ushauri juu ya vipi kuwatambua watu ambao ni wanamgambo. Na zaidi, Wakenya waendelee kuwaombea KDF katika wakati huu mgumu na pia kwa kazi nzuri iliyofanywa.

  • Abdulwahab Ali
    April 6, 2012 @ 11:54:41AM

    Maoni yangu ni kuwa hakuna popote katika Koran Takatifu kunakohalalisha uuaji wa watu wasio na hatia, na kuna aya ya Koran Takatifu ambapo Mwenyezi Mungu anasema “usichome Nyumba ambapo Jina la Mwenyezi Mungu linatajwa.” Kile wanachofanya al-Shabaab ni DHAMBI KUBWA. Al-Shabaab sio Waislamu wazuri, wanapaswa kutubu kwa Mwenyezi Mungu kabla hawajafa.

  • dave
    April 6, 2012 @ 11:05:10AM

    Tafadhali tusaidieni kwa sala, ndizo zinazoweza kuushinda ugaidi.

  • Niine Farah
    April 5, 2012 @ 05:24:16PM

    Hilo lilitokea usiku niliondoka kule. Na kawaida watu wa vikosi vya usalama wanapoteza wakati katika sehemu wanazoishi Wasomali. Hapana, watu wa usalama wawaangalie Waislamu wa Kenya kwa sababu Wasomali nchini Kenya ni watu wa amani. Kama wanataka vita wasingeondoka Somalia. Ninawahurumia watu hawa wasio na hatia wakati ningewaambia watu wa usalama, wanaume na wanawake, wasiwaogope Wasomali. Miezi hii polisi sio wabaya sana kama walivyokuwa kabla. Pengine katiba mpya itafanya jambo zuri na nilipiga kura ya ndio wakati mimi ni Mkenya wa uongo.

  • Kris Wamapesa
    April 5, 2012 @ 11:13:01AM

    Wakati umefika kwa viongozi wa Kenya kutambua umuhimu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya kama kikosi cha kimataifa chenye utaalamu na uaminifu ambacho kimezifunika serikali zenye nguvu ulimwenguni kwa mbinu na utaratibu wao wa kulimaliza genge la al-Shabaab. Hongera Kenya. Mungu Mwenye uwezo awe mwongozo na nguvu zenu.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo