Machi 20, 2012
Baada ya vikosi vya jeshi la Kenya kuanzisha Operesheni Linda Nchi mwezi Oktoba kuwatoa al-Shabaab nje ya Somalia, msemaji wa jeshi hilo Meja Emmanuel Chirchir alianza kutumia mtadao wa kijamii, Twitter, kutuma taarifa zinazojiri kuhusu mapigano na dhamira ya Kenya.
Ingawa tayari al-Shabaab walishakuwapo kwenye mtandao kuitia matangazo yao ya redio na televisheni, walianza kutumia Twitter mwezi Disemba, mara kadhaa kupingana na taarifa za Chirchir, wakati mwengine kumtaja yeye moja kwa moja.
Sabahi ilikutana na Chirchir kujadili kujadili misheni ya Kenya nchini Somalia, ambayo karibuni iliungana chini ya usimamizi wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somali na nafasi ya mitandao ya jamii katika kupambana na ujumbe wa al-Shabaab.
Sabahi: Unaweza kutoa tathmini kwa ufupi juu ya operesheni ya Jeshi la Kenya nchini Somalia dhidi ya al-Shabaab?
Major Emmanuel Chirchir: Jeshi la Kenya limefanikiwa katika kiwango cha siasa za kilimwengu kuupa sura mpya mtazamo juu ya Somalia katika mkakati wa kuleta amani, ukifuatiwa na mchakato wa kisiasa katika maeneo yaliyokombolewa kutoka al-Shabaab. Mchakato huu wa kisiasa ndio umekuwa mafanikio muhimu hadi sasa. Kwa watu wa Somalia kwenye maeneo yaliyokombolewa, tumefanikiwa kuwapa matumaini mapya kwamba sasa hakuna tena wasiwasi wa ugaidi. Wasomali wa kwenye maeneo hayo wamekuwa wakijishughulisha na harakati zao za kiuchumi bila ya khofu kwmba faida itachukuliwa na kundi ambalo haliekezi kwao.
Kwa upande wa Kenya, jeshi letu limeweza kurudisha heshima ya mipaka yake na kuondosha kitisho kilihowekwa na al-Shabaab. Mtandao na vikundi cha al-Shabaab nchini vimekandamizwa kwa kiwango kikubwa kupitia Operesheni Linda Nchi, na kuruhusu watu kutembea kwa uhuru ndani ya nchi yao.
Sabahi: Umekuwa ukitumia Twitter kutoa taarifa zinazojiri katika operesheni ya usalama ya jeshi la Kenya. Unaweza kutuambia nini kilichsababisha hatua hii, nani unayekusudia kumfikia, na nini unatarajia kukipata kwa taarifa zako kwenye Twitter?
Chirchir: Al-Shabaab imejikita kwenye ulimwengu wa mtandao, ambako imesambaza ajenda yake. Nyingi ya taarifa zao zimefumwa kipropaganda ili kuwajengea picha ya uhalali.
Kwa kwenda kwenye jukwaa hilo hilo, jeshi la Kenya limeweza kuitangaza ajenda yake. Nyingi ya taarifa za jeshi hilo zinahusu mafanikio yake kwenye uwanja wa vita, ambayo yameonesha namna al-Shabaab ilivyo dhaifu, wakiwa hawana na ustadi wa mapigano. Tumetumia jukwaa hilo hilo la al-Shabaab kuihujumu ajenda yao. Kujitwalia nafasi na nguvu kwenye ulimwengu wa mtandao kulikuwa jambo muhimu katika mapigano yetu na adui
Walengwa walikuwa ni jamii ya Kisomali, hasa iliyo nje ya nchi hiyo, kwani Somalia ni jamii ya kutumia maneno ya mdomo, ambapo taarifa husambaa haraka kupitia mazungumzo. Walengwa wengine walikua ni watu wa Kenya. Uungwaji mkono kutoka kwa Wakenya umekuwa muhimu sana na matumizi ya mitandao ya kijamii yanaongezeka. Kutumiana taarifa kupitia njia hizi, ukiwemo mtandao wa Facebook, kumekuwa na matokeo mazuri kwa jeshi la Kenya.
Walengwa wengine ni pamoja na al-Shabaab wenyewe ambapo huwa tunatangaza mafanikio yetu na kuzigonga akili za wapiganaji wao pigo moja ya jengine. Kupitia waandishi wa habari, tumefanikiwa kuufikia ulimwengu mzima kwa kutumia anwani yetu ya Twitter.
Sabahi: Kwa makisio, unatumia muda gani katika Twitter kwa siku?
Chirchir:Kawaida muda wote niko kwenye Twitter. Ninaingia saa 12:00 asubuhi kuona kile kilichotumwa na al-Shabaab na nini lengo lake, ambalo huwa linatayarisha ujumbe wangu kwa siku hiyo. Ninakwenda kulala usiku wa manane baada ya kuangalia uchukuliaji wao na ule wa waungaji wao mkono. Ujumbe wangu aghlabu huwa na taariya za yanayojiri kwenye uwanja wa mapambano na kupingana na taarifa zozote mbaya. Ninatumia muda mwingi katika mtandao.
Sabahi: Mwezi wa Disemba, al-Shabaab vile vile walifungua akaunti ya Twitter. Baadhi ya waangalizi wanahisi kwamba matumizi yao ya Kiingereza kunaonesha In December, al-Shabaab also opened an account with Twitter. Some observers feel their English tweets indicate that al-Shabaab wanajaribu kuvutia wasomali wanaozungumza Kiingereza, na sio lazima wawe Wasomalis. Unafikiri nini kuhusu hili?
Chirchir: Uchambuzi huo ni sahihi kwa vile imewapa mafunzo watu kutoka sehemu mbalimbali, wakiwemo raia wa Uingereza. Watu hao wanajiunga na kundi hili wakiwa na nguvu na vipaji vyao, ambavyo haraka huvitumia katika mapambano. Uchaguzi wa Kiingereza kama lugha ya mawasiliano kimsingi unakusudia kupata wasomaji dunia nzima.
Sabahi: Unaweza kutupa mfano wowote wa ujumbe wa Twitter ambao al-Shabaab waliuchapisha na kuja kuthibitika kuwa ni uongo?
Chirchir: Kulikuwa na ripoti kwamba ndege ya jeshi la Kenya iliangushwa ambayo haikuwa kweli. Al-Shabaab pia walisema kwamba waliiharibu meli ya jeshi la majini la Kenya, ambayo ia haikuwa kweli. Kumekuwa na uongo mwingi tu.
Sabahi: Kwa tathmini yako zipi ni faida na udhaifu wa kutumia mitandao ya kijamii kuwataarifu watu juu ya hali ya vita?
Chirchir: : Kwa ujumla mitandao ya kijamii ni njia nyepesi ya kutawanya taarifa; njia za kizamani zinadakia habari. Kwa mfano, wengi katika watu wanaotufuatilia kupitia Twitter ni waandishi wa habari, na taariza za yanayojiri kwenye mapambano huwasaidia vyombo vya habari kuandaa ripoti zao. Pia huwaruhusu waandishi wa redio kuwahi haraka kurikodi tukio, waandishi wa magazeti kuweka nafasi na mapema, na kadhalika.
Sabahi: Kwa kiasi gani kujiunga al-Shabaab na Shabaab al-Qaeda kumeathiri juhudi za mitandao ya kijamii na operesheni za kijeshi
Chirchir: Hatujahisi mabadiliko yoyote yale. Kitendo cha jeshi la kenya kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii kumeleta wafuatiliaji makini ambao wanakuwa haraka kuonesha jitihada zisizo matunda za al-Shabaab na kuwajulisha wengine. Kwa hivyo, taarifa za al-Shabaab zinakuwa hazina mafanikio.
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
Watu watano walikamatwa siku ya Jumanne mjini Dar es Salaam wakiwa na vifaa vya kulipua katika mi...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliwataka wabunge kuweka kando madai yao ya kuongezwa mishahara kwa ...
Majeshi ya serikali ya Somalia waliwaua wanamgambo tisa wa al-Shabaab wakati wa mapambanao hapo J...
Mtu asiyejulikana alimpiga kwa risasi na kumuua ofisa wa kitengo cha usalama cha kijeshi huko kas...
Muungano wa Jubilee tawala cha Kenya kilichukua uongozi wa kamati mbili muhimu za bunge Ijumaa (t...
Chama cha Wafanyabiashara na Asasi ya Chakula na Kilimo ya Umoja wa Mataifa vinatoa mafunzo kwa w...
Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi aliwahamiza waandis...
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Athari iliyowekwa nchini Somalia na KDF sio ndogo kwa kipimo chochote. Dunia yote itashukuru sana kwa kitendo hiki.
Sifa kwa vijana wetu wa KDF walioko Somalia. Kismayo itaanguka pamoja na al-Shabaab. Ulimwengu huu hauna nafasi kwa ugaidi na mafundisho yao ya uovu.
Asanteni sana komredi, endeleeni.
Hongera kwa vikosi vyetu vya KDF, vimefanya kazi nzuri.
Jeshi la Kenya limeweka alama bila ya kujali ni kidogo kiasi gani katika kuweka amani na kusaidia katika misafara ya kibinadamu inayosafirisha misaada. Somalia ni nchi kubwa na jeshi la Kenya haliwezi kufikia eneo lote lililoko katika udhibiti wa kikundi cha kigaidi ili kuongeza uwezo wake. Inaohitaji msaada kutoka nchi nyengine na Umoja wa Mataifa.
Ni kwa sababu gani unafikiri kuwaua watu wengine.