Machi 02, 2012
Serikali ya Somalia, mashirika ya haki za vyombo vya habari, na maafisa wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika walilaani mauaji wa mwandishi wa habari Abukar Hassan Kadaf, ambaye alipigwa risasi na watu wenye silaha wasiojulikana nje nyumbani kwake Mogadishu Jumanne jioni (tarehe 28 Februari).
Kadaf alikuwa na umri wa miaka 43 na aliacha mke na watoto wanne. Alikuwa ni mwandishi wa habari wa pili kuuawa mjini Mogadishu mwaka huu.
Akiwa mkurugenzi wa zamani wa kituo cha redio cha Somaliweyn, Kadaf alikuwa anajulikana kama mmoja kati ya watu muhimu sana katika vyombo vya habari na fani ya habari nchini Somalia. Alifanyakazi na mashirika kadhaa ya kijamii na alikuwa mtetezi wa amani.
Kadaf vilevile alikuwa anashiriki kikamilifu katika mashirika ya vijana, ambayo karibuni yaliwahamasisha maandamano mjini Mogadishu kulaani tangazo la muungano baina ya al-Shabaab na al-Qaeda.
“Tukiwa na hisia imara juu ya tukio hili, tunalaani mauaji ya mwandishi huyu wa habari na mkurugenzi wa zamani wa kituo cha radio cha Somaliweyn na tunatoa wito kwa serikali ya shirikisho kufungua mara moja uchunguzi wa kina katika mauaji yaliyofanywa dhidi ya waandishi wa habari ili kuhakikisha kuwa wahalifu wanafikishwa mbele ya sheria na kumaliza kusamehewa,” alisema Mohammed Ibrahim, Katibu Mkuu wa Umoja wa Kitaifa wa Waandishi wa Habari wa Somalia.
“Hii ni moja tu kati ya mfululizo wa ushari dhidi ya waandishi wa habari wa Somalia ambao umekuwa yakitokea,” Ibrahim aliiambia Sabahi. “Huu ni msiba mpya na mwendelezo wa juhudi za kukandamiza uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari huru nchini Somalia. Pia ni ishara ya hatari ambayo inawakabili wanaharakati na wale wanaofanyakazi na vyombo vya habari katika mji mkuu, Mogadishu.”
Ibrahim alisema kila juhudi zinawezekana lazima zifanywe ili kuzuia mauaji ya waandishi wa habari na wanaharakati wa jumuiya za kiraia. Aliyaelezea mazingira ambayo waandishi wa habari wanafanyia kazi, ni ya hatari na yenye ugumu mkubwa sana.
“Tuna wasiwasi mkubwa sana na usalama wa waandishi wa habari,” alisema. “Mpaka sasa, hakuna mtu yeyote aliyefikishwa mbele ya sheria wala kuadhibiwa kwa yale waliyoyafanya, na ndio maana wanaendelea kuua waandishi wa habari zaidi. Hili ni suala kubwa la kuwa na wasiwasi nalo jijini Mogadishu na tunaiomba serikali kuwapatia ulinzi zaidi.”
Shirika la Habari la Mogadishu, ambalo liko mstari wa mbele katika kukuza amani na kutetea haki za waandishi wa habari, vilevile lililaani mashambulizi yanayoendelea dhidi ya waandishi wa habari wa Somalia na kuitaka Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia kulichunguza tukio hili.
Abdullahi Mohammed Hassan, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Habari la Somalia, aliyaita mauaji ya Kadafi kuwa ni “ya kutisha na yasiyokubalika”.
Kadaf aliuliwa karibu na nyumba yake katika wilaya ya Wadajir, kusini mwa mji, ambayo ni mojawapo ya sehemu ya Mogadishu yenye amani na utulivu kabisa. Watu wenye silaha wasiojulikana walimpiga risasi Kadaf nje ya nyumba yake, na kumuua hapohapo kabla ya kukimbia toka eneo la tukio.
Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo na hakuna mtu yeyote mwenye silaha ameishatambuliwa. Afisa polisi Mohamed Abdulkadir alisema mauaji yako chini ya uchunguzi na ripoti ya awali inaonesha kuwa walikuwa washambuliaji wawili, AFP iliripoti.
Naibu Waziri wa Habari, Barua na Mawasiliano Abdullahi Bile Noor aliwashitumu al-Shabaab kwa mauaji ya mkurugenzi wa zamani wa kituo cha redio.
“Serikali ya Somalia inalaani vikali kulengwa kwa waandishi wa habari na inaelezea masikitiko yake makubwa kwa kifo cha Abubakar Kadaf,” Noor alisema.
Aliongeza kuwa al-Shabaab wameamua kulipiza kisasi bila ya kubagua baada ya upotevu wao wa mapambano ya kijeshi ya hivi karibuni. Ushahidi wa hayo, ni mauaji ya waandishi wa habari na al-Shabaab katika muda wa kasoro ya miezi mitatu.
“Kuwalenga waandishi wa habari na kuwatishia hakukuweza kunyamazisha uhuru wa vyombo vya habari nchi Somalia na vilevile hakutasitisha juhudi zetu za kuleta amani nchi Somalia,” Noor alisema na kuongeza kuwa wahalifu wataandamwa na kupelekwa mbele ya sheria kwa gharama yoyote ile.
Kwa mujibu wa watetezi wa uhuru wa Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka, waandishi wa habari 25 wameishauliwa nchini Somalia baina ya mwaka 2007 na 2011.
Salad Ali Jilli, mjumbe wa kamati ya ulinzi ya bunge nanaibu waziri wa zamani wa ulinzi, alisema kwamba uwezo wa vikosi vya usalama kuendesha uchunguzi wa mara moja una dosari. Alisema ilikuwa ni muhimu kuwatambua wale waliohusika na uhalifu na mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa vyombo vya habari na wanaharakati, na kuwapeleka mbele ya sheria.
“Hatuwezi kukubali mauaji yanayoendelea, ambayo yanakandamiza haki ya watu wa Somalia kuishi,” Jilli aliiambia Sabahi. “Na hii ni kweli hususani kwa viongozi wa jamii, na ndio maana tunaitaka serikali na vikosi vyake vya usalama kurudufu juhudi zake katika kuwinda watu wanaohusika na uhalifu huu.”
Somaliweyn kilikuwa kituo cha radio cha kujitegemea kaskazini mwa Mogadishu. Kituo kilivamiwa mwaka 2010 na wanamgambo wa al-Shabaab ambao walibeba vifaa vya utangazaji na kompyuta.
Wenzake Kadaf waliiambia Sabahi kwamba alikuwa na mipango ya kuzindua upya kituo hicho na karibu alikuwa mstari wa mbele katika jamii kwa vile alikuwa anajihusisha na siasa za eneo.
Wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika walilaani kifo cha Kadaf na kuahidi kuvisaidia vyombo vya usalama vya Somalia kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria.
Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika nchini Somalia Boubacar Gaoussou Diarra alisema, “Mauaji ya waandishi wa habari wanaowakilisha sauti za watu...ni uhalifu usiovumilika.”
“Asasi za mpito za shirikisho lazima zirudufu juhudi zao za kumaliza utamaduni wa kutoshitakiwa na kuanzisha mara moja uchunguzi huru ili kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria,” alisema Augustine Mahiga, mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchi Somalia.
Mahiga alisema Ofisi ya Siasa ya Umoja wa Mataifa Somalia ilikuwa tayari kutoa msaada unaohitajika kuhusu hilo.
“Ninatoa heshima zangu kwa waandishi wa habari hodari wa Somalia ambao wanafanyakazi katika hali ngumu sana ili kuweka shinikizo kwa wahalifu hawa wanaojaribu kuwatisha watu wa Somalia,” Mahiga alisema. “Ninatoa wito kwa wale wanaolinda haki za msingi za uhuru wa kujieleza wasirejeshwe nyuma na vitendo hivi vya ugaidi.”
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Miongoni mwa vyombo vya habari vya Kiarabu, kuna baadhi yao viko upande wa magaidi, na vingine ni maadui dhidi yao. Hii inathibitishwa na aina mbalimbali za maoni na tafsiri binafsi zilizopo miongoni mwa watu binafsi na wafanyakazi wenyewe wa vyombo vya habari. Kwa upande mmoja, wako wale wanaoonesha uadui dhidi ya magaidi, wanaopambana nao na kuanika uso wao wa uovu. Kwa upande wa pili, kuna wale wanaopindisha ukweli kwa maneno matamu ya kiitikadi kali ili kuendeleza vitendo vyote vya vikundi vya kigaidi na watu binafsi. Pia wapo wale wanaokuwa katikati na wanajaribu kuripoti matukio kwa ukweli ili kuonesha picha halisi ya matukio. Mimi ninaunga mkono vile vyombo vya habari vinavyosimamia ukweli na haki, vinavyofanyakazi na wale wanaoonewa, kupigania haki zao na kupigana dhidi ya itikadi kali na ugaidi. Chombo hiki cha habari ni kimoja chenye dhamiri ya heshima na fahari. Lengo hili ni kuwaunganisha watu na kuepuka kujenga tofauti baina yao au kudhuriana. Chombo cha habari kina nafasi kubwa sana katika kuwasilisha ukweli wa matukio na kile kinachoendelea kwa watu ambao wanapima kile kinachotokea.
Kikundi hiki kisicho halali kinalenga kila kitu na sio vyombo vya habari tu wakati wakitumia itikadi yao ya uongo ili kushawisha wafuasi wao wenye mawazo machafu ya vilevile. Wanawajaza hofu waandishi wa habari ili waweze kuwashawishi watu wengi zaidi na kueneza itikadi zao potofu. Kikundi cha kigaidi, al-Shabaab ambao ni wahalifu, waliua waandishi wa habari wengi kama inavyoshuhudiwa na ulimwengu. Waandishi wa habari wanalengwa na kuuliwa kama mtu mwengine yeyote na kikundi hiki cha kigaidi, al-Shabaab. Kwa kweli wanafanya hivi ili kuficha vitendo vyao vya kinyama wanaoufanya nchini Somalia. Wanataka waendelee kuchinja watu wasio na hatia na kuwalipua kwa mabomu, bila ya kuonekana na ulimwengu. Kwa sababu hii, wanawatishia na kuwajaza hofu waandishi wa habari wenyeji na wa kimataifa wanaofanyakazi Somalia, kwa hivyo kuifanya kazi ya vyombo vya habari kuwa ni ya hatari.
Mitandao ya vyombo vya habari imechangia sana kwa jamii ya dunia, waandishi wengi wa habari, wenyeji wa redio na wamiliki wa blogu wamepoteza maisha yao kwa sababu tu walikuwa wanaeleza ukweli kwa watu wa kawaida. Ili kuangaza zaidi juu ya siasa kali na uvumilivu, vyombo vya habari lazima viwe waaminifu, vyenye kuheshimika, viwe na uadilifu na wawe wakweli.
Ikiwa unataka ushinde vita dhidi ya mwendawazimu, lazima uwe na wazimu mara mbili ya ule alionao yeye kichwani mwake au ujidai kuwa na wewe unao.
Ni nani zaidi baina ya watu wa Somalia na waandishi wa habari nchini Somalia? Kwa nini hamkupiga kelele kama hizi wakati watu wengine wasio na hati walipokuwa wanasingiziwa na kuwasaidia. kkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkk