Al-Shabaab wako katika ukingo wa kushindwa, wasema wachambuzi

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Februari 27, 2012

 • 115 Maoni
 • Chapisha
 • Panga upya Punguza Ongeza

Mfululizo wa vipingamizi vya kijeshi na kupoteza viongozi wao wakuu kumewadhoofisha al-Shabaab huko Somalia, maafisa wa serikali na wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema.

 • Polisi na askari wa Kenya wakiwalinda watuhumiwa wa al-Shabaab katika jela ya muda ya Mogadishu hapo tarehe 21 Februari. [Na Abdurashid Abdulle Abikar/AFP]

  Polisi na askari wa Kenya wakiwalinda watuhumiwa wa al-Shabaab katika jela ya muda ya Mogadishu hapo tarehe 21 Februari. [Na Abdurashid Abdulle Abikar/AFP]

Wakiwa wamebanwa katika pande tatu za mstari wa mbele kutoka kwa vikosi vya kikanda na majeshi ya Somalia, kikundi kilikabiliwa na pigo jeigine kubwa hapo Ijumaa (tarehe 24 Februari), ambapo iliripotiwa kuwa shambulizi la anga liliua baadhi ya wanamgambo wa kigeni wanaopigana pamoja na kikundi kilichoungana na al-Qaeda huko Lower Shebelle.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, mwanamgambo aliyejulikana kwa jina la Mohammed Sakr aliuwawa,pamoja na wanamgambo wengine wawili wa kigeni. Vyombo vya vya habari vya Somalia vilvile vilimtaja Mkenya, Sheikh AbubakarHaji Ahmed, na vilevile inawezekana Mmisri mmoja ameuliwa, ingawaje kiwango cha ushiriki wao bado hakiko wazi.

Al-Shabaab iko njiani kuelekea kushindwa,” alisema Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohammed Ali katika hitimisho la Mkutano wa London kuhusu Somalia hapo Alhamisi, na kuongeza kuwa atakaribisha mashambulizi “yaliyolengwa” dhidi ya ngome za al-Shabaab na wanachama wa al-Qaeda nchini Somalia.

“[Wanamgambo] wamepoteza mioyo na akili za watu wa Somalia, na ndio maana wanapoteza maeneo siku baada ya siku na tunatarajia kuwa kikundi cha waasi wa al-Shabaab kitakosa wanamgambo ndani ya muda wa mwezi mmoja,” Ali alisema.

Wachambuzi wa masuala ya usalama na siasa wa Somalia wanasema mashambulizi ya anga dhidi ya viongozi wa al-Shabaab, kambi za kigaidi na wanachama wageni wa al-Qaeda kunasaidia kukidhoofisha kikundi.

“Wapiganaji wa kigeni kutoka al-Qaeda walikuja Somalia ili kudhoofisha usalama na kuichafua nchi yetu na eneo zima na kujenga maeneo salama kwa ajili ya magaidi nchini Somalia kutoka ulimwenguni kote,” mchambuzi wa usalama Somalia Bashir Mohammed aliiambia Sabahi. “Na hii ndio maana tunakaribisha mashambulizi ya anga dhidi yao.”

Mohammed alisema vifo vilivyoripotiwa vya wapiganaji wa kigeni katika shambulizi la anga hapo Ijumaa na kabla ya hapo kifo cha Bilal al-Berjawi, kiongozi muhimu wa al-Qaeda katika Pembe ya Afrika, kunathibitisha pigo baya kwa al-Qaeda na washirika wao katika Pembe ya Africa.

Kutekwa kwa Baidoa ni mafanikio katika kupambana na al-Shabaab

Shambulio la anga la Ijumaa lilikuja siku mbili baada ya vikosi vya serikali na washirika wao wa Ethiopia walipoidhibiti Baidoa – moja kati ya ngome kubwa za kimkakati kusini mwa Somalia.

Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia (TFG) ilitangaza katika tarifa kuwa kukombolewa kwa mji wa Baidoa kunawakilisha mwanzo wa mwisho wa kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab.

Wachambuzi kadhaa walisema al-Shabaab wamekabiliwa na mfululizo wa kushindwa na vipingamizi mfululizo katika uwanja wa vita ndani ya miezi michache iliyopita na kwa sasa wako katika ukingo wa kushindwa kabisa.

Kwa sasa al-Shabaab wanakabiliwa na operesheni kubwa za kijeshi mfululizo katika sehemu tatu za mstari wa mbele,” mchambuzi wa masuala ya kisiasa Ahmed Warsame aliiambia Sabahi, “Mashambulizi matatu ya Kenya, Somalia na Ethiopia ili kuwapondaponda waasi wa Al-Shabaab kumeanza kuleta matunda na kikundi kinavuta pumzi zake za mwisho kabla udhibiti wa kijiografia haujapotea.”

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Abdirahman Omar alisema kukombolewa kwa Baidoa, ambayo ni mji wa tatu na mmoja kati ya miji muhimu sana kusini mwa Somalia, ni kipingamizi kingine kwa al-Shabaab.

“Hivi karibuni al-Shabaab wamekuwa katika hali ya kurudi nyuma, lakini kukamatwa kwa Baidoa na miji mingine miwili kusini magharibi mwa nchi bila ya kuwa na upinzani mkubwa ni ishara kwamba al-Shabaab wanadhoofika na kwamba hawawezi kuhimili tena kutokana na kusonga mbele kwa majeshi ya Somalia na washirika wao wa Ethiopia,” Omar aliambia Sabahi.

Omar alisema kuwa vipingamizi mfululizo vinavyowakabili al-Shabaab – Mogadishu, Beledweyne, Baidoa na sehemu nyingine kusini mwa Somalia – ni ishara ya kupungua nguvu za kikundi cha wanamgambo.

“Hatua hii imeonesha kuwa al-Shabaab wanafifia na wako njiani kushindwa. Hatua hii itawatenga na kukaza fundo katika kikundi, na kupanua njia kwa kupotea kabisa kwa al-Shabaab,” alisema.

Naye Daud Makran, mchambuzi wa masuala ya kisiasa Somalia na mhadhiri wa chuo kikuu, vilevile alisema kuondoka kwao Baidoa kunaashiria kuwa kikundi kinadhoofika sana.

"Al-Shabaab kuondoka kwao Baidoa bila ya kupigana, ni ishara ya kuwa kikundi kinapungua uwezo wao wa kijeshi na hata kushindwa kwao kijeshi,” aliiambia Sabahi. “Inaonekana kwamba al-Shabaab wameshindwa na hawawezi tena kuidhibiti kampeni ya kijeshi ya vikosi vya washirika.”

Makran alisema anatarajia mafanikio zaidi ya washirika wa kijeshi. “Binafsi ninafikiri kwamba vikosi hivi vya washirika hivi karibuni vitachukua maeneo zaidi kati na kusini mwa Somalia,” alisema.

Baidoa 'iko huru kutoka makucha ya wenye msimamo mkali'

Abdifatah Mohammed, gavana wa jimbo la Bay, ambako Baidoa ndio mjii wake mkuu, na ambaye anaongoza vikosi vya serikali vilivyoiteka Baidoa kwa msaada wa vikosi vya Ethiopia, aliapa kuendelea na kampeni dhidi ya al-Shabaab.

"Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitatu, wakazi wa Baidoa wamekuwa huru kutoka makucha ya watu wenye msimamo mkali baada ya kuudhibiti mji,” alisema.

“Sasa tunapanga kufuata mabaki ya kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab ambao waliukimbia mji kabla ya kuwasili kwa vikosi vyetu,” Mohammed aliiambia Sabahi. “Tutaendelea na kampeni ya kijeshi dhidi ya al-Shabaab kwanza kuelekea katika mji wa Burakaba na baadae tutaelekea miji iliyobakia katika eneo hili. Kampeni hii itaendelea mpaka tulikomboe eneo lote kikamilifu. Tutawasaka magaidi popote walipo mpaka tuwaondoe kabisa.”

Hata hivyo, al-Shabaab, wakataa kuipoteza kwao Baidoa.

"Kuondoka kwetu Baidoa kulikuwa mpango wa mbinu ili kubadilisha mkakati wa kijeshi,” alisema msemaji wa kijeshi wa al-Shabaab Abdul Azziz Abu Musaab. “Vita dhidi ya vikosi vya serikali [ya Somalia], Ethiopia na Kenya vitaendelea kwa nguvu zaidi kuliko huko nyuma.”

"Wanajihadi waliondoka bila ya kupigana,” Abu Musaab aliiambia Radio Al-Andalus, ambayo inaendeshwa na al-Shabaab. “Sasa tunayazunguka maeneo ya mji na tunaahidi kuyateka tena maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na Baidoa, ambalo ni kaburi kwa wavamizi na washirika wa wanamgambo wa Somalia.”

Abu Musaab alisema kupoteza Baidoa hakuna maana kuwa al-Shabaab imeshindwa kijeshi.

Wapiganaji wa al-Shabaab wakimbilia Yemen

Maendeleo ya kijeshi yamekuja wakati ambapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kwa kauli moja kuongeza idadi ya majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia kwa zaidi ya askari 17,000. Ongezeko hili linadhamira ya kuongeza shinikizo la kijeshi dhidi ya al-Shabaab na kuongeza kuunga mkono serikali ya Somalia. Vilevile unaipa nguvu Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia (AMISOM) ili kuendesha mashambulizi dhidi ya al-Shabaab.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikubali kuipatia AMISOM helikopta tisa, pamoja na helikopta tatu za mashambulizi. Baraza vilevile liliahidi kutoa msaada wa vifaa kwa vikosi vya AMISOM ili kupanua misheni yao nje ya Mogadishu. Kabla ya hapo, uongozi wa AMISOM ulikuwa unaishia ndani ya mji mkuu tu.

Kamanda wa AMISOM Meja Jenerali Fred Mugisha aliwaambia waandishi wa habari Mogadishu hapo Alhamisi kuwa al-Shabaab iko njiani kuanguka na idadi kubwa ya wanachama wake, hasa wa kigeni, wanakimbilia Yemen kwa njia ya bahari.

Mugisha alisema kuwa muda wa kuwashinda al-Shabaab unategemea nia ya jumiya ya kimataifa kuvisaidia vikosi vya AMISOM na serikali ya Somalia.

“Ikiwa tutapata tulichoomba katikavipengele vya kuzidisha idadi ya wanajeshi na kupatiwa helikopta na vifaa vyengine muhimu ili kuendesha misheni, hii ina maana kwamba kushindwa kwa al-Shabaab hakutachukua muda mrefu,” Mugisha alisema.

“Tunashuhudia kuanguka kwa ndani [kwa al-Shabaab] na kwamba inawezekana kuwa kikundi hiki kitaanguka hivi karibuni,” alisema.

Mugisha alisema kiasi cha wanachama 300 wa al-Shabaab walikimbia Somalia na wanaelekea Yemen, kitu alichokitaja kuwa ni “ishara ya kushindwa”.

"Natumai kuwa Wasomali wanafahamu kuwa al-Shabaab, ambao kinawataka watoto wawe kama mabomu [ya binadamu] lakini wakati joto linapopanda, wanaikimbia Somalia. Tumaini langu ni kuwa wataondokana na wazimu huu,” alisema.

Wengine wasema tishio la al-Shabaab bado halijamalizika

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wameonya kuwa kushindwa kijeshi karibuni hakuna maana kuwa kikundi kimemalizwa moja kwa moja.

“Hakuna shaka kuwa al-Shabaab wamedhoofika sana katika kipindi cha nyuma na kwamba kikundi kinakufa na kupoteza uwezo wake kijeshi,” mchambuzi wa masuala ya kisiasa Abubakar Ali aliiambia Sabahi. “Hata hivyo, hii haina maana kuwa kikundi hiki kimefikia hatua ya kuwa kinakimbia nchini.”

Ali alisema wapiganaji wanaweza kuwa wanakwenda Yemen ili kuungana na al-Qaeda katika Rasi ya Arabuni

“Nafikiri kwamba kikundi kitaendelea na uasi wake kwa namna moja au nyingine na inawezekana wakataendelea na mashambulizi ya kigaidi, ya kupiga na kukimbia, vilevile kutega mitego zaidi kuliko zamani,” Ali alisema.

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

 • SAM BISAULE
  September 27, 2012 @ 08:48:51AM

  NINAUNGA MKONO KAMILI KDF NA MAJESHI MENGINE KWA SABABU NDIO DAWA PEKEE KWA WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB. WANAJESHI ENDELEENI!

 • john andati
  April 16, 2012 @ 02:26:32AM

  Hawa ni wauwaji, wanaua kaka na dada zetu, lazima wasafishwe.

 • douglas mugambi
  April 14, 2012 @ 12:24:38PM

  Nadhani vita hivi dhidi ya al-Shabaab ni sawa. Ulimwengu uungane kuwasaidia watu wa Somalia ambao kwa miongo miwili hawajaona amani. Kwa majeshi ya Kenya nchini Somalia na AMISOM ninasema hongera. Kazi nzuri imefanywa tunaposikia wapiganaji hawa wanatorokea Yemen

 • NICOLE
  April 14, 2012 @ 02:07:51AM

  Wauweni al-Shabaab kutoka pande zote. Wasafisheni kutoka uso wa dunia. Iokoeni nchi yangu na majangili hawa, rejesheni amani, kuishi pamoja na mafanikio katika nchi yangu. Rejesheni maadili ya Kiislamu. NATANGAZA KIFO KWA MAGAIDI

 • ANTONY G. THUMI
  April 13, 2012 @ 08:47:45AM

  Sisi majirani wa Somalia hatutarajii kuwa nchi za nje watakuja kuisadia, ni wajibu wetu kuungana na kuwasaidia kukisafisha kikundi kilichopigwa marufuku. Ninawaunga mkono askari wa KDF wanaofanyakazi Somalia na ninawapa heshima wale waliopoteza roho zao njema katika juhudi zao za kuikomboa Pembe ya Afrika. (MIMI NI ASKARI, NINGEPENDA NINGESHIRIKI KATIKA OPERESHENI HII - NINAWAOMBEENI MAFANIKIO KOMREDI)

 • g.kimani
  April 12, 2012 @ 10:43:42AM

  Hakuna mtu mwenye haki ya kulazimisha imani zake kwa watu wengine kama ambavyo al-Shabaab wanafanya, wameisukuma Kenya ukutani. Lazima awepo mtu afanye kile ambacho KDF inafanya. Endeleeni KDF endeleeni

 • moses
  April 11, 2012 @ 10:16:17AM

  Al-Shabaab ni maadui wa taifa linalopenda amani kama Kenya, lazima waangamizwe kutoka uso wa dunia hii.

 • Khadan Mohamed ibrahim
  April 11, 2012 @ 04:25:36AM

  Ninaamini juu ya kutoua watu wasio na hatia, lakini wakati wa utawala wa Muungano wa Mahalama za Kiislamu kila pahali palikuwa na amani, hakukuwa na mauaji, utekaji nyara, unywaji wa ulevi. Nafikiri kitu kilicho nyuma ya vita hivi ni kutoka nchi za Magharibi. Ikiwa hakuna mkono wa nje unaoingilia kati Somalia kungekuwa na amani.

 • Tonito
  April 10, 2012 @ 07:08:20AM

  Ni nzuri kwetu zote kuwa kikundi hiki cha mauaji kinakufa. Kitu muhimu sana ni kwa AMISOM kupewa kila kinachohitajika ili kumaliza kazi. Askari wa Kenya msilale kazini, baadhi ya al-Shabaab wanaweza kuwemo nchini kwa ajili ya kushambulia.

 • melvin kimtai
  April 10, 2012 @ 03:52:01AM

  Mimi napenda kuuliwa kwa al-Shabaab. Nzuri, kikosi cha ulinzi cha Kenya karibuni kitaungana nanyi. Tutaendelea kusali kwa ajili yenu. Nafikiri serikali ingeandaa sherehe za kuwashukuru watakaporejea nyumbani. Ninawapedeni nyote.

 • mohamed
  April 9, 2012 @ 07:01:04PM

  Siwaungi mkono al-Shabaab na siwaelewi sana, lakini naelewa kuwa wanapigania maslahi yao ya kisiasa kama vile USA au kikundi kingine chochote au taifa…Uislamu ni dini ya amani ambayo haihamasishi vurugu, kwa hivyo hili linawaondoa al-Shabaab kuwa ni mujahidina.

 • richard ogutu
  April 9, 2012 @ 04:04:24AM

  Al-Shabaab wawe sahihi au la, wanaoweza kujibu ni watu wa Somalia pekee. Kuwepo kwa watu wa Somalia katika kambi za wakimbizi kunaelezea kiasi gani kikundi hiki kimekuwa kikatili kwa watu wa Somalia. Kwa kuongezea hayo, sasa [al-Shabaab] wanaingia katika nchi jirani kama Kenya kuua na kuteka nyara watu wasio na hatia. Bado unataka tuamini kuwa wako sahihi? Watu wa Somalia wameshateseka sana tangu kuondoka kwa Said Barre mwaka 1991 na kwa hivyo lazima ulimwengu mzima uungane kuisaidia Somalia ipate uhuru wake.

 • EMIRGUNGHO
  April 7, 2012 @ 04:13:25AM

  Al-Shabaab wanaua Waislamu, wanawakata viungo, wanawabaka wanawake wa Kiislamu, wanawaibia Waislamu wenzao...n.k. Vipi tena wanauongopea ulimwengu kuwa wanapigania Uislamu? Hawa ni kizazi cha vurugu! Lazima washughulikiwe kama walivyo. Kwa wale ambao bado wanawaunga mkono makafiri hawa- (Al-Shabaab), lazima waelewe kuwa mchezo umekwisha! Ni suala la wakati tu na hakutakuweko tena na al-Shabaab!

 • Wamunyai
  April 5, 2012 @ 03:38:33PM

  Ni bahati mbaya kuwa baadhi ya Wasomali wasiojua wanachokifanya wamehadaiwa kushiriki katika mabomu ya kujitoa muhanga badala ya kusubiri kuona Somalia huru na iliyokombolewa katika siku za karibuni. Kiasi gani inavunja moyo kwa binadamu wenzao.

 • Winnie
  April 5, 2012 @ 10:20:23AM

  Tuwakabidhi askari wote katika mikono ya Mungu. Na tumwache MUNGU kutoa hukumu yake.

 • Julius
  April 5, 2012 @ 08:57:23AM

  Alshabaab – Lazima waende, tumechoka nao.

 • julie israel kenya
  April 4, 2012 @ 08:28:10AM

  Hongera KDF kwa kazi nzuri.

 • Coolins
  April 3, 2012 @ 10:16:45AM

  Watu hawa lazima washughulikiwe ipasavyo! Maisha ambayo yamepotea chini ya uangalizi wao hayahesabiki. ENDELEENI KDF / AMISOM, msimuache hata mtu mmoja ambaye anajihisi ana haki ya kuua kwa jina la Mungu. Al-Shabaab ni kikundi kisicho na HAJA/MAANA ambacho lazima kimalizwe!!

 • CLEMENT ODERA
  April 3, 2012 @ 09:56:50AM

  Hatuhitaji kuona uwezo wa al-Shabaab unavyoendelea kwa matukio ya karibuni ya ushirikiano wa kitaalamu na al-Qaeda. Usalama lazima uimarishwe na kitu chochote kisipewe nafasi hata iwe ni usiku wa manane au saa za asubuhi kweupe.

 • EZRA KIRUI
  April 3, 2012 @ 04:42:36AM

  KENYA NI NCHI YA AMANI AMBAPO HATUWEZI KUWARUHUSU WAGENI KUHARIBU HESHIMA YETU KWA KUUA WATU WASIO NA HATIA NA WATU WAZURI. NINAMUUNGA MKONO GK WETU KWA KUVIWEZESHA VIKOSI KWENYE MPAKA WA KENYA. VIKOSI VYA KENYA ENDELEENI NA ONGEZENI NGUVUZENU. KILA LA HERI.

 • aluoch
  April 2, 2012 @ 05:50:04PM

  Wanamgambo wa al-Shabaab hawafanyi lolote jema kwa Waislamu na waacheni waape ikiwa katika kikundi chao cha uasi hawauwi Waislamu. Waweke silaha chini, kwa kufanya hivyo mwanguko wao utakuwa taratibu na watatambuliwa kama mashujaa wa vita. Somalia imeshateseka sana na mtu yeyote wa dini hawezi kuwaona watoto wa Mwenyezi Mungu wanachinjwa na askari hawa wa Mwenyezi Mungu.

 • douglas mutai
  April 2, 2012 @ 03:49:16PM

  Hakuna chochote cha kidini katika kila kitu ambacho mashetani hawa wanafanya kwa binadamu wenzao. Waacheni Wasomali wafurahie amani kama nchi nyingine za Kiafrika. Ninawapongeza askari wanaoufanyia ubinadamu hisani nchini Somalia kwa maisha yao. Sala zangu ni kuwa Wasomali warejee nchini kwao na kusaidia kulijenga taifa lao lililo chanikachanika. Kwa wale waliofunikwa na koti la damu kwa kisingizio cha dini, ni shetani tu anayefurahia wakati damu ya binadamu inamwagika. Al-Shabaab ni wakala wa shetani.

 • wanjohi
  April 2, 2012 @ 01:27:20PM

  Nzuri

 • Alan Kibe
  April 2, 2012 @ 02:00:30AM

  Inasemekana wanakimbilia Yemen, jumuiya ya kimataifa iangalie hatua hii, kabla hawajawa kitu kingine. Vinginevyo, heshima kwa majeshi ya Kenya, Somalia na Ethiopia kwa kutekeleza wajibu wenu.

 • odanga
  April 2, 2012 @ 01:57:43AM

  Al-Shabaab ni kikundi cha kigaidi kinachohatarisha uwepo wa binadamu na kwa hivyo lazima kiondolewe. Mtu yeyote mwenye uhusino na al-Shabaab lazima aondolewe kabisa.

 • SAM K
  April 1, 2012 @ 01:00:08PM

  Inasikitisha kuona kaka na dada zetu wanauliwa kama wanyama, kama tendo lile lililotokea katika nchi yetu wenyewe kwenye kituo cha mabasi cha Machakos. Hao wanaoitwa al-Shabaab na wenzao na WAHUNI wengine wanaweza kuwa walitokea Eastleigh au Somalia, wakatuibia maisha ya ndugu zetu wasio na hatia ambao walikuwa wamejitayarisha kwenda kuwaona jamaa zao au mikoani wakaishia katika vifo vya ajabu. Hongera jeshi la Kenya na majeshi mengine ya Afrika kwa kuyasafisha kikamilifu mabaki ya viumbe hawa hatari kutoka sayari hii.

 • Jonnie Tai Kiboi
  April 1, 2012 @ 10:13:50AM

  Al-Shabaab wanapaswa washughulikiwe bila huruma. Bila shaka wang’oeni ndani ya Somalia na kuwazamisha katika Bahari ya Hindi.

 • Najib
  April 1, 2012 @ 09:01:22AM

  Al-Shabaab ni ndugu zetu katika Uislamu. Wako kule kutetea dini ya Mwenyezi Mungu, ambayo wengine walikuja kuibomoa kutoka kiini chake. Ninapenda kusisitiza kuwa, al-Shabaab wataendelea kuweko kule na Mwenyezi Mungu ndiye atakayeleta ushindi wa mwisho kwa hali yoyote, bila ya kujali vipi Marekani, Uingereza, Makafiri wote na wanafiki wote wanaungana pamoja.

 • MAGONDU
  April 1, 2012 @ 06:21:46AM

  Watu wa kawaida wa SOMALIA wanapenda amani. AL-SHABAAB ni kikundi cha vijana waliokosa makazi ambao hawana hata usaidizi wa watu wazima; wanachofanya kwa jina la dini ni wendawazimu tu, kwa mfano, kuua wanafunzi wa udaktari ambao ni WASOMALI NA WAISLAMU kunahusiana vipi na kutimiza wito wa jihadi? Ninaomba na ninamatumaini kuwa kikundi hiki kugharikishwa kutoka uso wa dunia hii haraka iwezekanavyo. IDUMU SOMALIA

 • Abdulghani
  April 1, 2012 @ 01:40:23AM

  Kila kitu kina muda wake, ndivyo ilivyo, na huu ni muda wa amani kwa kaka na dada zetu wa Somalia. Tunawaombeeni iwe ni amani ya kudumu. Mwenyezi Mungu akipenda.

 • mahamad
  March 31, 2012 @ 04:40:00PM

  Kila mtu wakiwemo Wasomali wenyewe wameshachoshwa na misimamo mikali ya al-Shabaab. Wameyapiga marufuku mashirika ya misaada nchini wakati watu wanakufa kwa shida. Wameua waandishi wa habari amabo walitarajiwa kuwa hawako upande wowote katika mzozo huu. Wamefanya ukatili, mateso na mauaji dhidi ya wananchi safi kwa kuiunga mkono tu serikali ya Somalia au kufanyabiashara pamoja nao. Al-Shabaab wamepoteza nyoyo na akili za kila mtu aliyekuwa uti wao wa mgongo, kwa hivyo wanakabiliwa na kushindwa karibuni.

 • Evans Metet
  March 31, 2012 @ 10:15:54AM

  Tunajivunia KDF na AMISOM. Wanafanya kazi nzuri sana na sisi tutaendelea kuwaunga mkono kwa sala zetu. Asanteni

 • Mohamed
  March 31, 2012 @ 03:20:23AM

  Ni bahati mbaya kwa watu kufuata kama vipofu na kama wajinga kutumia maneno yaliyoundwa na tamaduni za kimagharibi zinazokufuru dini kwa kufanya ushetani na kuanzisha vita kwa Uislamu na Waislamu. Kikundi cha Vijana ni Waislamu na wanaweza wakatenda mabaya. Ni busara kwa Waislamu kuwaunga mkono ndugu zao waliowakosea kuliko kupigana sambamba na ukafiri unaoenezwa na mawazo ya Kizayuni ambayo lengo lake la mwisho ni kuufuta Uislamu na Waislamu, lakini kwa hakika hawawezi. Mpende msipende, hivi ni vita vya kilimwengu na vitaendelea mpaka ulimwengu wote utakapotawaliwa na Uislamu na Waislamu.

 • Parkire Evans
  March 30, 2012 @ 04:13:58PM

  Inasemekana kuwa ikiwa huwezi kuwa penseli ya kuandikia furaha ya mwingine basi kuwa kifutio cha huzuni zake. KDF ni [kama] kifutio kwa watu wa Somalia, hongera, hongera, hongera.

 • mathew kamuri
  March 30, 2012 @ 03:23:17PM

  Tungependa kusikia Somalia yenye amani.Muacheni adui ashindwe kwa jina la Bwana, Amen. Sisi Wakenya tumelipa gharama ya kutosha katika vita hii. Hongera majeshi ya Kenya, tayari mmeshafanya kazi nzuri, tunajivunia nyinyi. Endeleeni na moyo huohuo. Tunawaombeeni usiku na mchana. Mungu awabariki nyote.

 • Rotich Kipyego Mastio'ny
  March 30, 2012 @ 10:57:17AM

  Ishara ya kushindwa kwa al-Shabaab ni ishara ya kazi nzuri ya AMISOM na KDF na sisi tunawapongeza. Mungu aibariki kazi ya mikono yao.

 • Anthony
  March 30, 2012 @ 10:10:52AM

  Ninajivunia KDF kwa yale waliyofanya kama ya kujivunia, lakini musiwachukulie al-Shabaab bure bure tu. Hawa ni kama zimwi linaloangalia kipi kinaendelea na wanajua wakati gani wa kushambulia na kuonesha uwezo wa Marekani na Uingereza vipi mambo yanapaswa kufanywa.

 • Caroline
  March 30, 2012 @ 07:02:50AM

  Penye nia pana njia, watu wa Somalia wameshateseka kwa muda mrefu. Mungu atawafungulia Alfajiri Mpya. Al-Shabaab ni kama MUNGIKI nchini Kenya.

 • KEVIN MOMBASA
  March 30, 2012 @ 04:38:24AM

  VITA DHIDI YA AL-SHABAAB SI VITA VINAVYOHUSU DINI KWA SISI WAKRISTO KWA KUWA NI VYA AL-SHABAAB LAKINI KWA KUWA WAO NI KAMA MKONO UNAOWASAIDIA KUWATESA WASOMALI KUTOKA KWA WAFANYABIASHARA HAWA MABWANA NA VIKARAGOSI WAO WAOVU WAARABU AMBAO WANATUMIA DINI ILI KUIBA HAKI NYINGI, HADI SHULE NZURI NA HOSPITALI NA MAISHA KWA JUMLA. SISI WAKENYA TUNAWATAKA WASOMALI WOTE WAREJEE NA KUFAIDI NCHI YAO KATIKA AMANI ILI KUSAIDIA KUJENGA MASHULE NA MAHOSPITALI NA KUREJESHA MILA ZILIZOPOTEA ZA KISOMALI NA UTAMADUNI WA MAPENZI YA UKARIMU NA URAFIKI.

 • wangui njeri
  March 29, 2012 @ 01:10:37PM

  Mimi nina matumaini mema kwamba mwisho wa yote, jeshi la Kenya na vikosi vya Umoja wa Mataifa vitaweza kurejesha utulivu nchini Somalia. Ni kazi nzuri ambayo vikosi vinafanya kwa sababu sifahamu kwa nini watu wengi wateseke kutokana na maslahi ya watu wachache. Nikiwa mtaalamu wa makosa ya jinai, ninaunga mkono vita dhidi ya al-Shabaab. Kuheshimu ubinadamu na kufuata utawala wa sheria ni suala linalosisitizwa ulimwenguni kote, Somalia lazima isaidiwe katika kutimiza ndoto hii.

 • Dun
  March 29, 2012 @ 08:00:51AM

  Hakuna kitu kitakachodumu milele, na hawa wako ukingoni mwa kutokomea. Hongera KDF, AMISOM, Seriklai ya Mpito.

 • Nzamba
  March 29, 2012 @ 07:37:01AM

  Wasafisheni, hawana haki ya kuishi

 • Henry N. Onsando
  March 28, 2012 @ 07:09:17AM

  Asanteni kaka na dada wa Somalia mnaopenda amani kwa ushirikiano wenu na jumuiya ya kimataifa. Jeshi la makabwela halistahili huruma. Tuko tayari kuanzisha sera ya "kuchoma mazao na majumba", kutoka upande wetu, ili kuwajua mashabiki wao miongoni mwetu. Kamwe hataweza kujikusanya tena na kutishia amani yetu.

 • Mohammed
  March 28, 2012 @ 02:35:39AM

  Al-Shabaab ni kikundi kilichoundwa na vijana wa Kiiislamu wanaotaka kuitawala nchi kwa kutumia Sharia (Sheria ya Kiislamu) kwa mujibu wa kile wanachodai. Msiwarukie.

 • DOMINIC ROTICH
  March 27, 2012 @ 09:52:48AM

  Ninajiunga na orodha ya wale wanaoiunga mkono KDF kwa lengo la kuwasafisha al-Shabaab kwa vile ni wauwaji katika uso wa dunia. Hawa ni watu waovu wanaotumia Uislamu ili kuharibu utu. Tunahitaji amani nchini Somalia haraka iwezekanavyo.

 • Ezekiel Luley
  March 26, 2012 @ 11:26:58PM

  Bila ya shaka AMISOM inahitaji msaada ili kuling'oa genge hili ili kuwaruhusu watu wa Somalia wawe katika amani na kuunda serikali imara.

 • Eduh K.
  March 26, 2012 @ 11:04:06AM

  Ilichukua muda mrefu sana kabla ya kuona nuru upande wa pili wa shimo, lakini ni hakika sana, huu si mwanga wa uongo! Magaidi wanavuna shinikizo kutoka vikosi halali. Si busara kutuma hapa maoni ya kuwahurumia al-Shabaab kwa sababu hatimaye itawabidi mzibe nyuso zenu ardhini kabla ya mwisho wa mwaka: wakati huo al-Shabaab watakuwa wanaoza katika makaburi ya historia.

 • Mhina Mpeho
  March 26, 2012 @ 07:15:26AM

  Enyi al-Shabaab, MWENYEZI MUNGU hakubali mambo mnayofanya, maumbile yatawaambieni karibuni kuwa mkabidhi silaha zenu kwa uongozi ili kulinda amani.

 • Timo
  March 26, 2012 @ 06:29:07AM

  Huu ni wakati kwa Somalia kupata amani ya kudumu na kuendeleza taifa leo. Endeleeni vikosi vya Somalia na KDF.

 • amisi
  March 26, 2012 @ 02:45:27AM

  Wakati tunasherehekea ushindi huu unaokuja hivi karibuni, SERIKALI YA KENYA lazima ifikirie KULIPULIWA KWA MABOMU KITUO CHA MABASI CHA MACKAKOS. Kwa nini kupigana na al-Shabaab ndani ya Somalia bila ya kuwafuata kule Eastleigh Kenya kwa vile ninaamini kwa wale walioko Eastleigh wanaandikisha na kuwapatia mafunzo al-Shabaab nchini Kenya na baadaye kuwapeleka Somalia. Pia ninaamini kuwa si al-Shabaab peke yao nchini Somalia, lakini chochote kinachoendelea katika siasa za Kenya ni aina fulani ya al-Shabaab. Wanasiasa wa Kenya wajipangeni na kukumbuka haki za watu waliopoteza makazi yao kabla BWANA MUNGU hajawaadhibuni nyote kwa kile mnachowafanyia watu WAKE. Wakenya, kuweni binadamu kiasi cha kutosha na mjue kuwa sote NI SAWA mbele ya MUUMBA WETU ambaye ni mwenye haki na mkweli.

 • Mukuru
  March 22, 2012 @ 10:30:17AM

  Wajaaliwe watokomezwe kutoa uso wa dunia.

 • Elmi
  March 20, 2012 @ 06:21:37AM

  Al-Shabaab, kuliko kikosi kingine chochote, ndio adui mkubwa wa watu wa Somalia. Kwa kuwang'ang'ania mabwana wao Waarabu wanaharibu utamaduni wa Somalia. Hebu fikiria Msomali anajiita Abu Saida. Aibu zenu! Al-Shabaab wameuvamia msitu wa Somalia ili kulisha njaa za nchi za Kiarabu za Ghuba ambazo zina makaa ya Somalia. Siku moja Al-Shabaab watalazimika kujibu maswali kwa watu wa Somalia, sio tu kwa kuwasababishia vifo na kuuchafua utamaduni wa Somalia lakini pia kwa kuharibu mazingira ya Somalia. Napenda kuvishukuru vikosi vya Wakenya, Warundi, Waganda na Waethiopia pamoja na Somalia kwa kuwapa fundisho al-Shabaab ambalo daima hawatalisahau. Uishi Udugu wa Afrika.

 • moses kaituko
  March 20, 2012 @ 03:53:01AM

  Vidole juu kwa KDF na vikosi vingine vishiriki vinavyopigana pamoja nao. Mimi ninajivunia nyinyi. Endeleeni na wala msirudi nyuma hadi mwisho. KILA LA HERI VIJANA.

 • FREDRICK WANYONYI
  March 20, 2012 @ 12:57:03AM

  Al-Shabaab lazima wapeperushwe nje ya Somalia moja kwa moja. Fikiria walisababisha hasara kubwa kwa maisha ya kaka na dada zetu wa Somalia. Baadhi ya al-Shabaab wanakimbilia Yemen na watu wa Yemen wanaopenda amani lazima wawabainishe na kuwakabidhi kwa uongozi husika bila ya kuchelewa kwa sababu wanaweza kuingia kirahisi na kuisababisha Yemen matatizo tena.

 • Denis Kimani
  March 19, 2012 @ 06:59:07PM

  @iddy abu wao - Mimi ni Mkristo na ninaweza kuwaambieni kuwa hakuna sehemu ya Adolf Hitler inaeleza kuwa alikuwa Mkristo. Yeye alikuwa pagani ambaye hakuhusiana na chochote cha Ukristo. Alijaribu kuwamaliza Wayahudi wote ambao walikuwa wameanzisha msingi ambao Yesu Kristo alikuwa amezaliwa na kukulia nao katika kueneza Injili ulimwenguni – Kwa hivyo maoni yako yanapotosha. Ni watu waliopagawa wanaoua wananchi wasio na hatia kwa jina la Mwenyezi Mungu au kwa jina la Allah lakini hatupaswi kutoa hukumu hivihivi tu dhidi ya kila Mkristo au Muislamu. Sisi Wakristo tunaamini katika amani na tunaheshimu dini nyengine na tunawachukulia marafiki zetu Waislamu kuwa ni ndugu zetu. “Waliobarikiwa ni wapatanishi wa amani, maana hao wataitwa wana wa Mungu.” Mahtayo 5:9.

 • Ombeni Mhina
  March 19, 2012 @ 08:58:01AM

  Al Shabaab wamekuwa mwiba kwa wapenda amani duniani kote, majeshi ya Kenya yameanzisha ukombozi kwa Somalia hatimaye kwa ulimwengu mzima, hebu Polisi wa Dunia Marekani aingize baraka zake ili kazi ikamilike haraka kabla ya kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo

 • Ombeni Mhina
  March 19, 2012 @ 08:41:38AM

  Al-Shabaab ni ubinadamu, tafahali hakuna dini inazungumza vitu vibaya kwa wengine. Rejeeni kwa ALLAH, fikirieni juu ya wengine

 • Dancan oloo
  March 19, 2012 @ 06:39:02AM

  Ninawaunga mkono kikamilifu majeshi ya Kenya kwa kazi yao nzuri na ninauliza kwa nini hawaendi Kismayu na kuiungua kabisa mpaka iwe majivu?

 • francis
  March 18, 2012 @ 08:16:10AM

  Wauwaji wa al-Shabaab wangekuwa wameshasafishwa zamani sana kama ingekuwa vikosi vya Kenya vingejiunga na Ethiopia katika shambulizi lao la mwanzo.

 • Abdulkadir
  March 17, 2012 @ 06:13:12PM

  Kikundi cha vijana kinakabiliwa na matatizo makubwa kuhusiana na muonekano wao mbele ya macho ya Wasomali kutokana na mauaji wanayofanya na kwa mashambulizi yanayofanywa dhidi ya wananchi na malengo mengine yasiyo halali. Kikundi cha vijana kilipiga mabomu sherehe ya mahafali ya wanafunzi wa Chuo cha Afya, jambo lililopelekea kuanguka kwa muonekano wao katika macho ya watu. Baada ya miaka miwili kupita ya tukio lile la kutisha, kikundi kikaanza na ulipuaji mbaya sana wa mabomu ya kujitoa muhanga katika historia ya Somalia ambapo wanafunzi walikuwa wakisubiri kupata misaada ya kusoma nje. Shambulio hili baya na kuongezeka kwa hasira za wananchi dhidi ya kikundi cha vijana kumeharibu kile kilichobakia katika muonekano wao kiasi kwamba hawawezi tena kujisahihisha.

 • Denis Kimani
  March 17, 2012 @ 08:16:38AM

  @iddy abu wao - Mimi ni Mkristo na ninaweza kuwaambieni kuwa hakuna sehemu ya Adolf Hitler inaeleza kuwa alikuwa Mkristo. Yeye alikuwa pagani ambaye hakuhusiana na chochote na Ukristo. Alijaribu kuwamaliza Wayahudi wote ambao walikuwa wameanzisha msingi ambao Yesu Kristo alikuwa amezaliwa na kukulia katika kueneza Injili ulimwenguni – Maoni yako ni hoja ya uongo. Ni watu waliopagawa wanaoua wananchi wasio na hatia kwa jina la Mwenyezi Mungu au kwa jina la Allah lakini hatupaswi kutoa hukumu dhidi ya kila Mkristo au Muislamu. Sisi Wakristo tunaamini katika amani na tunaheshimu dini nyengine na tunawachukulia marafiki zetu Waislamu kuwa ni ndugu zetu. “Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.” Mahtayo 5:9.

 • Ondiwa Mahmoud
  March 17, 2012 @ 06:11:03AM

  Al-Shabaab ni sawa na nambari 666 au 999 ambazo zinafananishwa na shetani. Waacheni washindwe na wasafishwe ulimwenguni, ili tuweze kuishi kwa amani kama peponi.

 • shegow
  March 16, 2012 @ 09:57:50PM

  Hali ya kidini ndio dhamiri kuu ya vikundi vyote vya Kiislamu vyenye silaha popote pale, kupitia operesheni za kujitoa muhanga kwa lengo la kutikisa utulivu, kueneza hofu na kudhoofisha udhibiti wa taifa hadi kuanguka kwake kabisa… Vikundi vyote hivi vinavyochukulia kuimarisha wito wa Sharia ili kufikia utawala au kuibua wito wa (upinzani) silaha kama njia ya kudhibiti, kushawishi na ukorofi, lakini hatimaye wanatimiza mradi wao na ikiwa watashinda, ulimwengu wa Kiislamu utageuka kuwa mataifa madogo kama lilivyokuwa taifa la Al-Andalus katika siku za mwisho za utawala wao.

 • joseph
  March 16, 2012 @ 09:39:26AM

  Hii ni habari nzuri. Nimeipenda.

 • Joash Hongo
  March 16, 2012 @ 04:25:32AM

  Hakutakuwa na pepo kwa al-Shabaab ndani ya Afrika yote kwa jumla.

 • kahuni
  March 16, 2012 @ 04:08:34AM

  Yatakuwa mafanikio makubwa kwa majeshi ya nchi tatu kuwashinda al-Shabaab, hili litaitaka jumuiya ya Kiislamu Afrika kukataa matumizi ya dini zao kwa misingi ya kuwashajiisha kujiunga na vikundi vya kigaidi kama vile al-Shabaab. Hili linaweza kufanyika kwa kubadilisha njia yao ya kumwamudu Mungu. Wakati umefika kwa Waafrika wawe wastaarabu na wakimbie kutawaliwa na vita.

 • David Githenya
  March 16, 2012 @ 03:20:09AM

  Al-Shabaab wako chini ya nyazo za Kenya. Hawana akili na wamedhoofika. Tunawaombeeni WaSomali.

 • Sam Bisaule
  March 15, 2012 @ 08:44:41AM

  UUNGWAJI MKONO KAMILI kwa operesheni za kijeshi dhidi ya WAPIGANAJI JIHADI wa al-Shabaab ambao wanaingilia amani ya kila nchi, "Wang'oeni al-Shabaab na iokoeni Somalia."

 • Major John
  March 15, 2012 @ 05:33:35AM

  Ina tia kichefuchefu na inanikasirishwa kwa vile utendaji wa udugu huu: Hivi MUNGU aliamrisha watu wauwe Waislamu wenzao kwa jina la dini?

 • Timoo
  March 15, 2012 @ 04:14:24AM

  Ni busara kuona kwa njia hasi kila kinachoendelea Somalia baada ya miaka 20 ya uchafu na uozo. Vizazi vimepoteza maisha yao, jamaa, mali na kupoteza utu wao. Tuwaachie ndugu zetu Waislamu waelewe kuwa hili halihusiani na imani, Halihusiani na dini, ni kuhusu nchi ambayo huko nyuma ilikuwa inajivuna lakini imevunjika vipande vipande kwa mapigano ya ndani yasiyo ya lazima, yakichochewa na mabwana wa vita waroho chini ya jina la jihadi ya kidini ili wahurumiwe na umma usio na hatia. Vikosi vya KDF na UNISOM hongera kwa kuendelea kuwavamia al-Shabaab mpaka mlete amani katika nchi ambayo zamani ilikuwa nchi kubwa na muirejeshe kwa wananchi wake ili waweze kuiendeleza kwa ajili ya watoto wao na kwa mafanikio ya watoto wao!

 • maxamuud maxamed muuse
  March 15, 2012 @ 03:47:10AM

  Mimi nafikiri ni sawa kabisa kuwang’oa al-Shabaab kutoka Somalia.

 • Kubasu Gabriel
  March 15, 2012 @ 03:39:31AM

  Nzuri! Hauwezi kufikia malengo ya maendeleo tuliyojiwekea ikiwa majirani zetu al-Shabaab nchini Somalia bado ni tishio. Askari wa Kenya wanafanya kazi nzuri sana na lazima tuwape msaada wanaohitaji. Afrika ya Mashariki, tunakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinaturudisha nyuma, tunaweza kuongeza tatizo jingine lolote katika haya tuliyonayo.

 • FRANCIS MAINA KURIA
  March 15, 2012 @ 02:20:32AM

  Kamanda mkuu wa vikosi vya Kenya yuko salama kiasi gani? Viongozi wetu wako salama kiasi gani? Kiasi tuko salama kwa jumla? KULIPULIWA KWA MABOMU KITUO CHA MABASI CHA MACHAKOS [ni ugaidi au vurugu] - tunaweza kuamini kuwa kikundi cha al-Shabaab kilihusika? - ni kuongezeka kwa vikundi makini zaidi vya ugaidi? - vimekuzwa ndani ya nchi au vinasaidiwa na vikundi vingine imara zaidi vya kigeni kutoka nje kama vile BOKO HARAM? - Ni uhusiano mubwa wa washukiwa wakuu na Uislamu na ushirikiano wao wa kikabila. - Inawezekana kuunganisha hili na uchaguzi mkuu ujao? - Wanafaidika kutokana na misaada ya fedha kisiasa? - Tuwasaidie polisi kwa kukata vitendo vyao vya kiuaji toka shinani. Tunaweza kufanya hivyo kupitia vyombo vya habari vya jamii! Niko pamoja nanyi. NIKO TAYARI KUWA AJENTI WA CHINI KWA CHINI NDANI NA NJE YA NCHI [kwa malipo, bila ya shaka]

 • JACKY
  March 14, 2012 @ 11:02:58AM

  IKIWA MWENYEZI MUNGU NI MUUAJI TENA KWA NINI AKAWAUMBA WAISLAMU? MIMI NINAMWAMINI BWANA WA ISRAELI AMBAYE ALITULETEA MWANAWE MWENYEWE NI YESU ATAKATEWAPELEKA KWENYE HUKUMU WOTE WANAOTENDA VITENDO VYA AL-SHABAAB LAKINI MJUWE KUWA MTOTO WA BINADAMU YUKO KARIBU. TAHADHARINI!!!!!!!!!!

 • galexis
  March 14, 2012 @ 09:21:27AM

  Heshima sana kwa wale wanaopigana na al-Shabaab. Kikundi hiki kimeshaua maelfu ya watu wasio na hatia ambao ninaamini kuwa huo sio msingi wa mafundisho ya Kiislamu. Kwa mara moja na moja kwa moja, kikundi hiki cha kigaidi kinachojishirikisha chenyewe na al-Qaeda kinahitaji kusagwasagwa...heshima sana kwa Jeshi la TFG, heshima sana kwa Jeshi la KDF, heshima kwa Jeshi la Ethiopia.......heshima sana kwa AMISOM.

 • gatune
  March 14, 2012 @ 05:35:00AM

  Lazima wang'olewe moja kwa moja. Hongera majeshi ya Somalia na washirika wenu. Amani ndani ya Somalia sio muhimu kwao tu bali kwa dunia nzima na hasa kwa nchi jirani.

 • Jacob.
  March 13, 2012 @ 10:00:07AM

  Vikosi vya Kenya kwa kushirikiana na Ethiopia na Uganda wametufanya tuwe wakubwa. Wakati wanaendelea kuwamaliza magaidi ndani ya Afrika, sisi tukumbatie amani na umoja ndani ya Afrika na tusikubali kutawaliwa tena. Al-Shabaab wameitawala Somalia kwa muda mrefu. Watu wanaishi kwa woga wa kuuliwa na kila aina vitendo visivyo vya kibinadamu. Ndugu zetu kutoka upande wa pili wa imani waungane nasi kuhakikisha kuwa kuna amani kamili katika nchi jirani.

 • geoffrey
  March 13, 2012 @ 05:53:03AM

  Amani haiji katika sinia la fedha. Mtu lazima apigane kwa ajili yake. Hongera KDF.

 • j.ariek
  March 13, 2012 @ 03:52:04AM

  Tusali kwa familia zilizopoteza jamaa zao katika vita na fidia zitolewe mara moja.

 • حسين الذهبي
  March 12, 2012 @ 11:41:29PM

  Kudhoofika hivi karibuni kwa waasi wa kikundi cha al-Shabaab kunaonesha kwamba majeshi ya Afrika vimefanikiwa kuwashughulikia magaidi na kwamba majeshi hayo yanawasaka siku hadi siku. Majeshi ya Afrika yamewamaliza wengi wa magaidi hawa na wamewashinda magaidi mmoja mmoja na vikundi viovu ambavyo vimekuwa vikihusika na hujuma, uharibifu wa mali, upigaji mabomu, mauaji, utekaji nyara, wizi na kuvunja uhusiano baina ya Wasomali. Kwa hivyo, asante kwa wanajeshi hawa, magaidi waoga walioua na kuwahamisha watu wengi, wameondolewa. Tunatumai kuwa hali itabakia kuwa ya salama, ya utulivu na isiyo na vitendo vya vurugu, uhalifu, hujuma au madhara. Mungu akipenda, na shinikizo hili linalowekwa mfululizo kwa watu wachache waliobakia na kwa wanachama waasi wa kikundi cha al-Shabaab ili kumaliza vitisho vyao moja kwa moja.

 • bamtush
  March 12, 2012 @ 12:31:16PM

  Wauweni, wauweni, hawastahiki chochote zaidi ya kifo. Al-Shabaab ni aibu kwa Afrika.

 • SELESTINE KATO
  March 12, 2012 @ 08:22:28AM

  Hongera kwa hatua lakini chanzo chake cha amani ni Bwana wetu Yesu Kristo

 • wesley kiboigot
  March 12, 2012 @ 03:45:45AM

  Amani nchini Somalia ni furaha kwa watu wa Somalia. Jamhuri ya Somalia yenye amani inakaribishwa na ulimwengu wote. Mapigano yote yanaweza kusitishwa na watoto wadogo kukua kwa amani. Al-Shabaab, wekeni silaha chini, ipeni amani nafasi na vikosi vya kigeni ondokeni. Ni dua yangu tu.

 • Nasori
  March 12, 2012 @ 03:22:35AM

  Dunia nzima inaelewa hali ambayo Somalia inateseka kwa miaka mingi. Kwanza umasikini na ukosefu wa ajiri na pili wanamgambo wa al-Shabaab; vitu viwili hivi ndio sababu ambayo taifa zima la Somalia linateseka. Al-Shabaab ni kikundi cha kigaidi cha al-Qaeda kilichoko katika eneo la Somalia kwa kueneza vitendo vyao vya kigaidi. Itikadi kubwa ya al-Shabaab ni kutangaza jihadi dhidi ya maadui wa Uislamu na kuwatoa nje ya nchi za Kiislamu.

 • HAAJI ALI
  March 11, 2012 @ 03:56:43AM

  NYIE WATU, LAZIMA MJUE KWAMBA, WASHINDI WA MWISHO NI AL-SHABAAB AMBAO WANAPIGANIA JINA KUBWA LA MWENYEZI MUNGU AWE MKUBWA ZAIDI. MWENYEZI MUNGU ALIAHIDI MAFANIKIO, KWA HIVYO MSICHEKE SASA, WAKATI UTAFIKA KARIBUNI. UISLAMU NDIO UTAKAOSHINDA NA KUTAWALA DUNIANI HUMU. MWENYEZI MUNGU AKIPENDA.

 • SAGERO OGUTA ZEDEKIAH
  March 10, 2012 @ 12:08:13PM

  Hongereni ndugu zangu wa Somalia, mmetufanya tujisikie salama dhidi ya vitisho.

 • kabai geoffrey
  March 10, 2012 @ 04:49:29AM

  Heshima sana kwa KDF.

 • ALI MOHAMMAD
  March 10, 2012 @ 02:45:21AM

  Al-Shabaab wanapigana JIHADI. Kenya na nchi nyengine zina maslahi mengine nchini Somalia lakini sio amani. Wakati wa utawala wa mahakama za Kiislamu, Somalia ilikuwa nchi ya amani lakini nguvu za magharibi, Kenya na Ethiopia zilipinga utawala huo kwa sababu hawakutaka UISLAMU utawale Somalia, lakini ninasema vita hivi vitashinda mapambano, UISLAMU utatawala tena mtake msitake.

 • Francis K
  March 10, 2012 @ 01:45:26AM

  Utulivu wa Somalia ni maendeleo mazuri kwa Pembe ya Afrika na hata kwa amani ya dunia. Tuviunge mkono vikosi vya KDF na AMISOM kwa njia zote. Hongera vikosi vyetu! Hongera Serikali zetu za Afrika! Hongera Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

 • NTABO
  March 9, 2012 @ 03:12:09PM

  Huu ni wakati wa kuikomboa Somaliland kutoka kwa shetani. Ninawaunga mkono kwa dhati majeshi ya KDF na AMISOM kwa jumla kwa kazi nzuri iliyofanywa.

 • abuorgn
  March 9, 2012 @ 01:25:10AM

  Jumuiya ya kimataifa huwa inachukua muda mrefu sana kutekeleza mipango yake. Al-Shabaab walikuwa wang'olewa mara tu pale walipoanza kuonekana kuwa ni tishio. Hata hivyo, heshima zote kwa majeshi ya Kenya.

 • jumba hudson
  March 8, 2012 @ 03:29:03AM

  Hongera ndugu zetu wanaofanya kila wanaloweza ili kukisafisha kikundi cha al-Shabaab nchini Somalia. Asanteni kwa uzalendo wenu. Mwenyezi Mungu awapeni nguvu zaidi za kuishinda al-Shabaab na awajaze baraka zake njema.

 • gabbhs
  March 7, 2012 @ 03:16:44AM

  Al-Shabaab ni kondoo tu wasio na mchungaji. Wangeweza kuunda jeshi imara na lenye dhamira ya kuilinda nchi yao inayosumbuliwa na umasikini badala ya kupigana katika vita vya kipumbavu kwa jina la “Allah”.

 • Sinyomah Luwawilo
  March 6, 2012 @ 08:56:33AM

  Nafikiri habari hii ni nzuri kwa watu wote wanaopenda mafanikio na maendeleo. Watu aina yao HAWAHITAJIKI hata kidogo. Asante sana kwa wote wanaoweka juhudi zao kuwezesha kusafishwa moja kwa moja kwa al-Shabaab ndani ya Somalia kwa faida ya Afrika na Dunia kwa jumla!!! Mungu Ibariki Afrika!

 • Leonard G Maina
  March 5, 2012 @ 08:50:15AM

  Wakristo, Wayahudi, Waislamu na waamini wote wanaoshikilia heshima na utakatifu wa maisha ya binadamu lazima washikane mikono ili kuwaangamiza wale wanaotumia jina la Mwenyezi Mungu huku wakitenda uhalifu wa kishetani dhidi ya binadamu wenzao wasio na hatia. Wale wanafuata imani ya Kiislamu kwa ukweli lazima wawaangamize wanamgambo magaidi wa al-Shabaab kwa upiganaji wa jihadi. Mungu wa Ibrahim, Isa na Yakubu si mwoga. Hahitaji binadamu ambao nao watakufa ili kupigana kwa niaba yake. Ni upuuzi mkubwa kwa binadamu yeyote kushikilia dhana kuwa anaweza kuanzisha vita kwa jina la Mwenyezi Mungu. Ushindi dhidi ya wapiganaji hawa ni wa wazi. Ni suala la wakati.

 • JOSEPH
  March 5, 2012 @ 08:38:17AM

  Al-Shabaab wanapoteza makamanda wao wakuu wengi, lakini lazima tuwe na tahadhari sana kwa vile wanaweza kuamua kulipiza visasi na kusababisha hasara kubwa. Hongera majeshi yetu kwa kufanya kazi nzuri sana.

 • fadd
  March 4, 2012 @ 10:11:02AM

  sio siri makala hii ime nikosha sana.wakenya wajipange sawasawa kuwazibiti kikamilifu hao al shababab wasiyo kuwa na huruma na roho zawatu.

 • langat josphat5
  March 2, 2012 @ 04:32:25AM

  Magaidi wa Kiislamu wako katika hofu kubwa..NINAPENDA NINAPOSIKIA KUWA NYUKI WA KIMAREKANI WANAWATAMBAA. nyuki hawa wameua viongozi wengi wa al-Qaeda kuliko mfano mwengine wowote..kwa hivyo endeleeni kuwapa kipigo cha nguvu. Hongera vilevile kwa askari wetu wa Kenya, Uganda na Ethiopia mnaowapiga magaidi.

 • Yusuf Abdihakim
  March 2, 2012 @ 03:50:54AM

  Majeshi ya kulinda amani katika Misheni ya Umoja wa Afrika Somali yameonesha kushughulika sana na dhamiri ya kuwaangamiza al-Shabaab na hii ni kazi ngumu sana. Baraza la Usalama hivi karibuni liliamua kuongeza idadi ya majeshi ya Misheni ya Umoja wa Afrika ili waweze kuzuia kikamilifu ongezeko la mashambulizi ya al-Shabaab. Wakati kukiwa na wasiwasi kuwa Umoja wa Afrika hauichukulii kazi hii kwa makini ingawaje uwezo umo mikononi mwake, hakuna budi kuthamini kwamba idadi ya maeneo yenye amani katika Mogadishu imeongezeka. Hii ina maana kwamba uamuzi wa kuongeza majeshi kwa kweli sio lazima. Pia, kukataa kwa al-Shabaab kuwa wamepoteza maeneo mengi kwa majeshi ya AMISOM vilevile kunapunguza sifa madai ya ushindi ya UA. UA unahitaji kufanya mambo mengi ikiwemo kujipanga upya na kuongeza majeshi yake ili kuwashinda al-Shabaab kwelikweli. Ni muhimu kutumia mikakati mipya ambayo ni ya kisasa ili kuvishinda kabisa vikundi hivi ambavyo vinadhibiti sehemu kubwa ya Somalia.

 • jomo
  March 1, 2012 @ 02:21:52AM

  Wasaudia lazima wasitishe kuwapa fedha hawa wahabi

 • Stanley
  March 1, 2012 @ 02:20:56AM

  Baadhi ya wahusika wakubwa wanataka kuwaonea watu maskini kwa kutumia dini kama kisingizio cha kuiba rasilimali yenye thamani ya Somalia. Mimi siamini kuwa Uislamu unaunga mkono vurugu na mauaji. Nendeni Wasomali, nendeni Wakenya, nendeni Waethiopia, na tuwasafishe hawa wanaofanyia mzaha wa Imani kutoka kwa majirani zetu. Somalia lazima iwe huru na al-Shabaab!!!!

 • abjad huwaz
  February 29, 2012 @ 02:39:22PM

  Ni habari za kawaida tu. Sioni chochote kisichokuwa cha kawaida

 • Jumba
  February 29, 2012 @ 01:50:09PM

  Inahabarisha. Tafafadhali endeleeni kutuletea habari. Al-Shabaab walipaswa kupigwa mabomu jana kwa sababu wale ni vichaa wasio na sababu. Wanapigania kitu gani? Wanapigana kwa faida ya nani? Umoja wa Afrika lazima uanze kuwa wakali na katika hali kama ya Somalia, lazima wapeleke majeshi sio tu kwa kulinda amani bali kuwezesha kuwepo kwa amani. Hongera kwa askari wetu kutoka Kenya, Ethiopia na nchi nyingine ambazo wapo Somalia ili kuhakikisha kuwa hakuna hata mwanachama mmoja kichaa wa al-Shabaab anatoroka.

 • OMI
  February 29, 2012 @ 10:01:38AM

  Waangalizi wa Haki za Binadamu wanapaswa kukiangalia kikundi cha al-Shabaab

 • benson kiprotich
  February 29, 2012 @ 09:12:02AM

  Mimi ni katika wale wenye mawazo ya kuwa askari wa Kenya waweko Somalia ili kuikomboa Somalia kutokana na wanamgambo na kujaalia amani. Kwa hivyo dua yangu kwa vikosi vya Kenya ni kuwashinda al-Shabaab

 • Hassan yusuf
  February 29, 2012 @ 09:00:30AM

  Vikosi katika uwanja wa mapambano vinafanya kazi inayokubalika na lazima viongeze nguvu katika kukimaliza kikundi hiki ambacho sio cha kibinadamu hata kwa wale wenye imani moja na wao –kwa waislamu wenzao. Mwenyezi Mungu si muuaji bali mwenye amani. MUNGU BWANA wa Abraham na Isa na Yakubu, wahukumu al-Shabaab ipasavyo. Mungu Akupelekeni katika mikono ya maadui zenu na awalete katika mwanguko wa milele baada ya kilio cha watu wasio na hatia kufika masikioni Kwake. Kwa VIKOSI vinavyopigana dhidi ya al-Shabaab, sema “EWE BWANA WA ISRAELI NI MOTO WETU” AMEN. Mimi niliingia katika Ukristo baada ya kugundua unyama ambao ningelazimishwa kufanya haukuwa kwa matakwa ya Mungu na sasa niko huru.

 • franc
  February 29, 2012 @ 07:29:31AM

  Al-Shabaab bado ni tishio kubwa kwa amani na utulivu wa kanda na lazima washughulikiwe kikamilifu

 • iddy abu wao
  February 29, 2012 @ 07:27:41AM

  MIMI SIAMINI KUHUSU KILE NYINYI WATU MNASEMA JUU YA AL-SHABAAB KUWA HAMNA CHOCHOTE CHA KIISLAMU NDANI YAKE, KWA SABABU “LORE NKUNDWA” MUASI KATIKA DRC HAKUWA MUASI WA KIISLAMU, HITLER YULE MJERUMANI VILEVILE INAMHUSU IKIWA MTAKUBALI KUWAITA WAKRISTO HAWA WAWILI KUWA NI MAGAIDI, KWA HIVYO MKUMBUKENI KUWA VILEVILE TUNAVYO VIKUNDI VYA KIGAIDI KATIKA UKRISTO LAKINI MIMI, SIKUBALIANI NA MATOKEO HAYA.

 • Felix Ngotho
  February 29, 2012 @ 07:13:31AM

  Kazi nzuri iliyofanywa na KDF. Hongera na endeleeni na utii wenu kwa Kenya. Tunasali kwa ajili yenu, nyie ni watu wetu.

 • Titus Iguria
  February 29, 2012 @ 06:16:19AM

  Hii inaonesha kuwa ni habari chanya na yenye uwiano sana kwa eneo zima na hususa kwa Somalia. Al-Shabaab au AL vyoyote vile lazima washindwe na wafadhili wao wa kijeshi lazima waelewe kuwa eneo hili si uwanja wa kutupia mabaya na maovu ya jamii kama vile al-Qaeda. Mungu Ibariki Afrika!!

 • King Mike
  February 29, 2012 @ 05:23:09AM

  Nimependa habari hii. Imeonesha kwa undani hali halisi ya vita dhidi ya genge la ugaidi (Al-Shabaab), na nina hisia kali kuwa ni suala la wakati tu kabla halijamalizika kwa unyonge kabisa. Ruhusuni iwepo amani katika Pembe ya Afrika.

 • fredrick
  February 29, 2012 @ 04:37:41AM

  alshabaabu bure kabisa

 • alex muhanji
  February 29, 2012 @ 04:15:56AM

  Na mimi pia nitakuwepo huko ili kuwaangamiza bila kujali kitakachotokea. Nitailinda nchi yangu niliyozaliwa. Ninaahidi nitafanya.

 • kirui Bernard
  February 29, 2012 @ 02:54:15AM

  Ninaunga mkono kikamilifu wanajeshi wa Kenya nchini Somalia kwa sababu ulimwengu wote unataka Somalia iliyo huru na isiyokuwa na magaidi, ili isonge mbele sawa na taifa jingine lolote la Afrika.

 • obinge
  February 29, 2012 @ 12:02:54AM

  Al-Shabaab ni tishio ambalo lazima lisafishwe kutoka uso wa dunia.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo