Februari 23, 2012
Mlipuko mkubwa unaolenga kambi kubwa kwa watu wasio na makazi ndani ya nchi (IDPs) huko Mogadishu umeeneza hofu kubwa miongoni mwa wakazi wake na kuchochea wito kwa serikali kuongeza ulinzi wa makambi hayo.
Ingawaje hakuna upande uliodai kuhusika na shambulio hilo, hili ni shambulio la pili mwaka huu lililolenga kambi ya wakimbizi, Serikali ya Somalia imetuwahumu al-Shabaab kwa kulenga IDPs kama ishara ya uwezo unaopunguza kwa kikundi kupambana na jeshi la Somalia na Vikosi vya Umoja wa Afrika.
Mlipuko ambao umetikisa kambi ya Badbaado Jumatatu (tarehe 20 Februari) ulimuua si chini ya askari mmoja wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho (TFG) na kuwaacha watu wengi wakiwa wamejeruhiwa. Kambi inayoendeshwa na serikali ni kambi kubwa kuliko yote kwa wakimbizi katika mji mkuu huo na ni makazi kwa watu wanaokadiriwa kufikia 30,000 ambao wamekimbia ukame na njaa.
Mashuhuda walioshuhudia kwa macho waliambia Sabahi kuwa mlipuko ulitokana na bomu la kufukia ardhini lililotegeshwa ndani ya kambi hiyo. Vyanzo vingine vya habari vilithibitisha kwamba mlipuko huo ulilenga askari wa TFG wanaowajibika kuwalinda IDPs wakati walipokuwa kwenye doria ya kawaida ndani ya kambi hiyo.
Mwezi Januari uliopita, mlipuko katika kambi ya Siliga huko Mogadishu uliua watu sita na kujeruhi watu watano muda mfupi baada ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wa kimataifa kutembelea eneo la mgawanyo wa chakula katika kambi hiyo. Mashambulizi ya mabomu yalifuatia siku chache baadaye, ikiua watu tisa katika kambi hiyo na wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Wakazi wameelezea hofu na wasiwasi kufuatia mlipuko katika kambi ya Badbaado.
"Hatujui ni kwa nini tunalengwa,” alisema Fatima Nour, mama wa watoto sita anayeishi kambini.
"Hatujui kama hao wanaotushambulia wanafanya hivyo kwa kuzingatia kwamba kambi hii inasimamiwa na serikali. Kama wanataka kuvilenga vikosi vya serikali, basi hii sio kambi ya jeshi kwa ajili ya vikosi vya serikali bali ni kambi kwa ajili ya wasio na makazi, walio katika mazingira magumu na watu wasio na hatia waliokimbia njaa na ukame,” aliieleza Sabahi.
Nour alitoa wito kwa serikali kuilinda kambi.
Kwa mujibu wa makisio ya Umoja wa Mataifa, watu wasio na makazi zaidi ya 185,000 wanaishi Mogadishu, wamesambaa kote kwa muda na kujazana makambini.
Licha ya tamko la Umoja wa Mataifa kwamba njaa Somalia imekwisha, watu wengi wasio na makazi Mogadishu wanasita kurejea katika majumba yao kwa sababu al-Shabaab imeweka vikwazo vikali katika kazi za mashirika ya kimataifa ya misaada. Kundi linalohusiana na al-Qaeda limeyapiga marufuku mashirika mengi ya kimataifa kufanya kazi katika maeneo wanayoyadhibiti.
"Hatuwezi kurejea katika majumba yetu kama wapiganaji wa al-Shabaab wanaendelea kuzuia misaada kufika katika maeneo wanayoyadhibiti,” alisema Amina Hassan, ambaye alitafuta hifadhi Mogadishu na watoto wake saba, wakikimbia ukame na njaa mwaka jana.
Aliieleza Sabahi, "Tunapendelea kukaa hapa Mogadishu ili tuweze kupata chakula badala ya kurejea vijijini kwetu bila ya msaada wowote.”
Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanawaomba viongozi wa serikali na vikosi vyao vya usalama kuwalindawWatu wasio na makazi na kuimarisha ulinzi katika makambi.
Abdul Fattah Mahmoud, kiongozi katika asasi isiyo ya kiserikali wenyeji inayofanya kazi ya kuwalisha watu wasio na makazi huko Mogadishu, alisema, “Serikali inapaswa kutoa ulinzi na kuwalinda watu wasio na makazi wanaokusanyika kwa makundi kuelekea Mogadishu. Tunaomba ongezeko la vikosi maalumu ili kulinda [vizuri] watu wasio na makazi na jitihada za misaada.”
Mwezi Septemba uliopita, serikali iliunda kikosi maalumu kinachoundwa na muungano wa polisi, jeshi na vikosi vya usalama ili kuwalinda watu wasio na makazi wanaoishi makambini na kulinda jitihada za misaada ya kibinadamu.
"Kutoa ulinzi kwa watu wasio na makazi na makambi hakuko katika kiwango kimoja kama kilivyokuwa miezi kadhaa iliyopita, hii ndiyo sababu serikali inapaswa kuimarisha hatua za ulinzi katika makambi yaliyopo katika mji,” alisema. “Hii itarekebisha mazingira ambapo kuna ukosefu wa usalama ambao, matokeo yake, unazuia usambazaji wa misaada katika baadha ya makambi”.
Alisema serikali imeelekeza jitihada zake katika kambi ya Badbaado peke yake wakati makambi mengine yameachwa bila ulinzi.
Moalem Abdullah Ali, Mkuu wa wilaya ya Dharkenley, ambako kambi ya Badbaado inapatikana, alimwambia Sabahi kwamba vikundi vya kijeshi vya serikali kwa sasa vinashughulikia zoezi la usalama kuwakamata wote watakaohusika na mlipuko. Alisema huu ulikuwa ni mlipuko wa kwanza wa aina yake kuillenga kambi ya Badbaado.
Ali alisema kwamba majeshi ya ulinzi na polisi walishitakiwa kwa kuilinda kambi iliyofunga eneo baada ya mlipuko kwa ajili ya kutafuta waliofanya kosa hilo.
Serikali ya Somali iliwalaumu wanamgambo wa al-Shabaab kwa kushambulia makambi ya IDP kutokana na vikundi vya wanajeshi kupunguza uwezo wa kukabiliana na majeshi ya Somalia na majeshi ya Umoja wa Afrika. Serikali ilisema watu wenye msimamo mkali sasa wanashambulia watu wasiokuwa na ulinzi na watu waliokosa makazi.
"Baada ya kushindwa mara kadhaa kuwadhuru wakazi wa Mogadishu, kutokana na uangalifu na uthabiti wa shughuli za kuzuia ugaidi kwa huduma ya kiintelijensia ya Somalia, [Wakala wa Usalama wa Taifa la Somalia], al-Shabaab (al-Qaeda Somalia) wanaonekana wamebadilisha mashambulizi kwa wale ambao serikali ya Somalia na jumuiya ya kimataifa wamekuwa wakisaidia kuokoa maisha yao," Kaimu Waziri wa Habari, Posta na Mawasiliano ya simu Abdullahi Bile Noor alisema katika taarifa yake siku ya Jumanne.
"Kama hawajali maisha ya waislamu wenzao wenye shida wa Kisomali, swali ni kwamba nani atafuatia katika mashambulizi?" aliongeza.
Noor alisema serikali imelaumu shambulio, waliloliita "la kikatili na sio la kibinadamu".
"Serikali inashughulikia kuimarisha ulinzi katika makambi ya IDP kwa kupeleka zaidi majeshi ya polisi ili kuokoa maisha ya watu wasio na makazi wanaoishi pale," alisema.
Katika maelezo yaliyorushwa hewani na Redio Mogadishu tareha 17Februari, ofisa mwandamizi wa al-Shabaab Fuad Mohamed Khalaf, anayejulikana pia kama Shangole, aliwashambulia katika himaya ya wakimbizi wa muda zinazodhibitiwa na kundi hilo.
"Ni wazi kutokana na vitendo vyao, mbili ya tatu ya Wasomali ambao wamekua wakiishi chini ya sheria yetu wamekimbilia katika maeneo yanayodhibitiwa na makafiri. Waamini wachache ambao wapo chini ya vitisho vya kudumu wamebaki hapa," alisema. Alisema wakimbizi wangetoroka kwenda maeneo yenye udhibiti wa al-Shabaab kama vile Marka au Baidoa.
"Wale waliohama wataishia jehanamu," aliwaonya.
Baidoa, ambayo zamani ilikuwa kambi kuu ya al-Shabaab, iliangukia kwa majeshi ya serikali ya Somalia na Ethiopia siku ya Jumatano.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Mimi nafikiri al-Shabaab wataishia kushindwa kwa sababu walikuwa dhaifu tangu mwanzo na sasa wamevuta macho ya ulimwengu wote. Wamekwisha.
Inahabarisha sana na ni sahihi, endeleeni na kazi nzuri. Asanteni sana.
Huu ni uendawazimu, vipi watu hao wanaweza kuchukuliwa kuwa wabinadamu.