Vikosi vya Umoja wa Afrika vikikaribia ngome kubwa kabisa ya al-Shabaab karibu ya Mogadishu

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Februari 16, 2012

  • 60 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Muungano wa vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika vilipiga hatua kubwa baada ya mapambano makali yaliyotokea Jumanne (tarehe 14 Februari) katika viunga vya magharibi na kusini ya Mogadishu, kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa Somalia na makamanda wa Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia.

“Vikosi vya taifa vyenye silaha, vikisaidiwa na vikosi vya Umoja wa Afrika, viliweza kusonga mbele kuingia katika ngome za kikundi cha waasi cha al-Shabaab -- kilichoungana na al-Qaeda – huko kwenye eneo la Elasha na ushoroba wa Afgoye,” alisema Kanali Abdullah Osman, kamanda wa kikosi cha pili cha Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia.

“Operesheni hizi hazitosita. Tutaendelea mpaka tukamate makambi muhimu ya ulinzi ya watu wenye msimamo mkali katika eneo la Elasha na ushoroba wa Afgoye, mpaka tutakapowatoa al-Shabaab kutoka eneo hilo," Osman aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi.

Naye Kamanda wa vikosi vya AMISOM Brigadia Audace Nduwumunsi alisema,” AMISOM iliendesha operesheni iliyofanikiwa dhidi ya magaidi wa al-Shabaab katika viunga vya Mogadishu hapo Jumanne asubuhi. Vilevile tuliweza kudhibiti maeneo ya kimkakati ya kuingilia mji mkuu kwa kusini na magharibi, pamoja na barabara inayoelekea ushoroba wa Afgoye, ambayo ni ngome ya magaidi.”

Nduwumunsi alisema wapiganaji 10 wa al-Shabaab waliuawa, pamoja na askari wawili wa Burundi ambao wanafanyakazi na AMISOM.

Ushoroba wa Afgoye, ulioko kilomita 30 magharibi ya Mogadishu, ni makazi ya watu wengi sana wa ndani waliohama makazi yao, waliolazimika kuyahama makazi yao katika miaka michache kutokana na vita vilivyokuwa vikiendela na hali ya njaa.

Nduwumunsi alisema kuwa kuenea kwa vikosi vilivyoungana kuelekea ushoroba wa Afgoye ni sehemu ya Juhudi za AMISOM za kuiokoa Mogadishu na kupanua zaidi eneo la usalama lililo katika udhibiti wa vikosi vya usalama.

Wakazi wa Elasha wakimbia vurugu

Wakati wapiganaji wakikaribia Elasha, maelfu ya Wasomali waliokimbia makazi yao wanaoishi katika eneo hilo, waliyakimbia makazi yao ya muda.

Saida Abdi, mama wa watoto sita kutoka Elasha, aliiambia Sabahi, “Tuna wasiwasi sana, kwa vile barabara inayoelekea Mogadishu imefungwa kwa sababu ya mapigano na safari za raia kwenda na kutoka Mogadishu zimesimamishwa.”

“Watu walianza kukimbia eneo hilo ili kuepuka mapigano,” alisema. “Wanatumia njia mbadala ili kuweza kufika Mogadishu.”

Naye Ahmed Omar, anayeishi katika makazi ya Kilomita 13, alisema, “Familia nyingi zinazoishi eneo la Kilomita 13, sasa wamekwama na hawawezi kuondoka, kwa vile barabara pekee inayoelekea Mogadishu imefungwa.”

"Tuna wasiwasi kuwa vita vinaweza kufika kwenye maeneo yetu. Tumekwama,” aliiambia Sabahi. Alisema misili kutoka pande zote ilifika eneo lake. Alitoa wito kwa pande zinazopigana kufungua njia ili kuwawezesha raia kurejea Mogadishu.

Raisi wa Somalia ataka marufuku ya silaha isitishwe

Raisi wa Somali Sheikh Sharif Sheikh Ahmed aliutaka Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa hapo Jumatano kuondoa kikwazo cha silaha Somalia tangu mwaka 1992.

Tunaiomba jumuiya ya kimataifa kuondosha marufuku ya silaha iliyowekewa Somalia kwa sababu si haki kuendelea na marufuku hii wakati ambapo tunapigana na al-Qaeda,” alisema katika hotuba kwa kundi la raia waliokuwa wanaandamana karibu na kasri la raisi dhidi ya muungano wa al-Shabaab na al-Qaeda.

“Kuunganishwa nguvu hivi karibuni baina ya al-Shabaab na al-Qaeda kunapelekea kusitishwe kwa marufuku yaliyowekwa juu ya uagizaji silaha nchini Somalia kuwa ni jambo linalohitajika”, alisema. "Tuna mpango wa kujenga na kuvipatia silaha vikosi vyetu vya Somalia, lakini hatuwezi kulipatia jeshi letu la taifa silaha wakati ambapo marufuku ya silaha bado inaendelea.”

“Jeshi la Somalia kwa sasa linakabiliwa na shida kutokana na matatizo ya kiuchumi na upungufu wa silaha," Ahmed alisema. “Al-Shabaab na al-Qaeda wanakabiliwa na vipingamizi vikubwa na makosa mengi nchini Somalia na tunahitaji msaada zaidi ili kuliunga mkono jeshi la Somalia, ili kuimarisha uwezo wake wa kijeshi na kuweza kuwaangamiza al-Shabaab, ambayo imetangaza rasmi kuungana na al-Qaeda katika Pembe ya Afrika.”

Wasomali wapinga dhidi ya al-Qaeda na al-Shabaab

Maelfu ya Wasomali wameripotiwa kujazana mitaani hapo Jumatano usiku kucha hadi Alhamisi katika kupinga muungano wa al-Shabaab na al-Qaeda uliotangazwa wiki iliyopita.

“Hatutaki al-Qaeda! Hatutaki al-Shabaab!” Watu walikuwa wanapiga kelele huko Mogadishu huku wakielekea karibu na kasri la raisi, wakipita sehemu ambazo zililengwa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya al-Shabaab.

“Tumekuja hapa kulaani al-Shabaab kujiunga na al-Qaeda,” Yousif Shedni mwandamanaji anayeandamana karibu na kasri, aliiambia Sabahi. “Tumeishateseka vya kutosha na hatutaki tena. Al-Qaeda na al-Shabaab lazima watuache na waondoke nchini mwetu, vinginevyo watu wa Somalia wako tayari kupambana nao.”

Miriem Tahir, mwandamanaji mwingine, aliiambia Sabahi, “Tunaandamana kuliunga mkono jeshi la Somalia, ambalo linaendelea kupata ushindi dhidi ya adui, pamoja na kuwapinga al-Qaeda na washirika wake wa Somalia. Hakuna mtu anayekubali mchafuko zaidi katika nchi yetu.”

“Nchi hii ni kwa ajili ya Wasomali na wala sio wapiganaji wa kigeni kama al-Qaeda – hatutavumilia zaidi vurugu zao," raisi aliliambia kundi hilo.

Maandamano kama hayo vilevile alifanyika katika mji wa Luuq kwenye jimbo la kaskazini la Gedo, redio ya Somalia ya Bar-kulan iliripoti. Maelfu wa waandamanaji walipiga kelele, “Somalia ni ya Wasomalia”, wakati wakipita katika mitaa ya Luuq.

Inaripotiwa kuwa maandamano yalipangwa na Serikali ya Mpito ya Shirikisho na washirika wao, na yamekuja siku mbili baada ya al-Shabaab nao kukusanyana ili kusherehekea muungano wao na al-Qaeda.

Al-Qaeda ndio kikwazo pekee kinachoikabili amani na maendeleo nchini Somalia, alisema Diyaad Abdi Kalil, ambaye ni afisa usalama, kuwaambia waandamanaji huko Luuq. Aliapa kuwa vikosi vya usalama vitawatoa al-Qaeda nje ya Somalia na kumtaka kila raia kuilinda nchi dhidi ya kikundi hiki cha ugaidi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 163)

Dislike_icon(31)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • supber
    April 3, 2012 @ 02:26:10PM

    Ninawaapiza al-Shabaab na ninawaombea waanguke kwa sababu wanamwaga damu ya binadamu wanaodai kuwa si Waislamu. (Mungu, aliye juu zaidi, katika Koran Takatifu ametuamrisha tusiue binadaamu, wawe Waislamu au wasiwe Waislamu kwa sababu yoyote, isipokuwa katika hali zilizoelezwa katika Kuran)...Ninawaapiza al-Shabaab kwa kufanya vitendo vya viovu kwa jina la dini.

  • axmed jaamac cuweyd (qaasdj)
    April 2, 2012 @ 04:00:25AM

    Kkkkkkkkkkkkkk. Kwa kuweka wazi, ninaishi katika nchi ya jirani, Somaliland na ninaweza kufikiria matatizo ambayo ndugu zangu wa Somalia wanateseka kwayo kwa sasa. Nina picha akilini ya Somalia kuwa nchi iliyotulia na ningependa kuwaomba watu wa Somalia kujiamini wenyewe na kuja na ufumbuzi kutokana na wao wenyewe juu ya matatizo yao badala ya kuwategemea wageni.

  • muna bashe cismaan
    March 31, 2012 @ 07:36:11AM

    Somalia daima haitapata maendeleo, kwa vile Waethiopia wamekuwa maadui zetu na bado wanaendelea kuja nchini kwetu. Ninawataka mjue kuwa daima hawatatuokoa au kutupa ulinzi wowote. Kwa maoni yangu, tuanze kuwapa mafunzo askari wa Somalia na tuvitoe vikosi vyote vya kigeni nchini. Lazima tujitosheleze wenyewe na kujiamini. Ikiwa huwezi kuishughulikia nyumba yako, adui hawezi kufanya lolote kwa ajili yako. Hakuna yeyote katika vikosi hivi vya AMISOM ambaye anatoka nchi ya Kiislamu isipokuwa Djibouti. Hata hiyo Djibouti inafanyakazi kwa niaba ya Ufaransa, hawawezi kumwamini Mwenyezi Mungu. Kama Somaliland, lazima tutatue matatizo yetu chini ya mti, tutatue matatizo yetu na tufanyekazi kwa ajili ya kupata amani.

  • ismaaciil mahamed osman
    March 28, 2012 @ 11:01:18AM

    Mimi ni Ismail Mohammad Osman nafikiri kuwa Somalia itakuwa na amani.

  • mukhtar mohamed
    March 18, 2012 @ 06:52:26AM

    Ninalipenda kituo hiki cha TV, kwa hivyo tafadahalini wasilianeni nami.

  • I D Mamai
    March 14, 2012 @ 08:32:58AM

    Ni bahati nzuri sana kuwa Wasomali wamekuwa na fursa ya kusimama ili kulinda nchi yao kama inavyosemwa, "Safari ya maili nyingi huanza na hatua ya mwanzo". Watu wanaowaunga mkono wameanza hizi hatua za mwanzo nyingi kwa hivyo nyinyi mnahitaji kuingia njiani na kufuata nyayo. Wenzangu, wathibitishieni waasi kuwa hakuna kilichobakia zaidi kwa ajili yao na kwa matendo yao maovu kwa vile wamewafanyeni wafungwa kwa muda mrefu. Kwa hakika hili liliwanyima fursa ya kufaidi hewa ya amani, uhuru na kujichanganya na ulimwengu. Kumbukeni kuwa Mwenyezi Mungu hakuwaumbeni kuwa wafungwa maisha yenu yote.

  • S. Mchillo
    March 12, 2012 @ 10:36:03PM

    Kundelea kwa vikosi nchini Somalia kunapelekea kushindwa kwa al-Shabaab na al-Qaeda. Hakuna nguvu ambayo inaweza kushinda mbele ya upande unaoungwa mkono na umma. Ni kosa kuwataja al-Shabaab kuwa ni Waislamu kwa vile vitendo vyao ni kinyume na imani wanayodai kuhubiri. Kwa imani yangu, al-Shabaab na al-Qaeda ni Mashetani wanaotaka kuuharibu Uislamu na kwa hivyo ni maadui wa imani ya Uislamu kwa hivo wajibu wa kila Mwislamu ni kupambana na majambazi haya.

  • guuthey
    March 11, 2012 @ 06:14:41AM

    Amani iwe juu yenu. Kwanza kabla ya wote ningependa kuishukuru serikali kwa kazi nzuri ambayo imefanya. Pili, wanachama wa al-Shabaab si Wasomali bali wageni walioletwa kuibomoa Somalia. Wanalipwa ili kuendesha vitendo vya kigaidi nchini Somalia na watu wa Somalia lazima wajilinde wenyewe kutokana na maadui kama hao. Ni mama wangapi wanateseka, ikiwa si maadui na wana hamu na Wasomali katika mioyo yao wangewahurumia watu masikini wa Somalia.

  • j.musyoka
    March 10, 2012 @ 12:54:24PM

    Viongozi wa Somalia lazima waache siasa uchwara na kuungana pamoja na kuwaokoa watoto na wanawake wa Somalia kutoka maovu ya vita na ujinga wa kutojua kusoma na kuandika katika karne hii.

  • somalidid
    March 8, 2012 @ 11:57:37PM

    Mnajiongopea wenyewe tu.

  • soomalidid
    March 8, 2012 @ 11:55:07PM

    Daima hamtopata amani wakati mnakataa uwepo wa taifa huru la Somaliland.

  • SACIIDO SIYAAD YALAXAW
    March 8, 2012 @ 09:54:25AM

    Ha! Ha! Ha! Al-Shabaab wanaanguka na lazima tuungane dhidi yao ili tuwadhoofishe zaidi. Wanadhoofika na hawawezi kutudhibiti zaidi. Tuungane dhidi yao kama ndugu na tuwang’oe. Mimi sijui al-Shabaab ni akina nani. Ni kikundi kilichochanganyikiwa kinachojiita vijana lakini ukweli kimeundwa na watu wazee. Ninashangaa kwa nini wanamuita kijana mtu kama Hassan Aweys wakati wanaelewa kuwa ni mzee. Kwa kweli hawajui nini maana ya neno “kijana” wanalolitumia. Ninaiomba serikali kuwafunga jela wale wote wanaowaunga mkono al-Shabaab.

  • Geoffrey
    March 8, 2012 @ 07:33:17AM

    Somaliland ina fursa sawa ya kuwa na AMANI ya kudumu sasa, mara tu watakapokuwa wameshajifunza kutokana na makosa yao ya nyuma. Kumbatieni amani na msimame dhidi ya kile kinachoitwa al-Qaeda na al-Shabaab na kuelekeza nguvu zenu katika kusuluhisha jamuiya kadhaa na kujenga nchi, sasa hiyo itakuwa ni kuvuta hewa ya amani. Kumbukeni, mtu aende Mashariki au Magharibi, nyumbani ni bora zaidi. Wasomali ni wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wazuri. Amkeni enyi watu muuoneshe ulimwengu kuwa KWELI mnaweza. Nyinyi mna baraka zetu na tutawasaidia kwa nguvu zetu zote ndogo. Elekezeni nguvu zenu katika kupata hatima njema. Tafadhalini, watoto wenu wanahitaji amani, mapenzi yenu kama wazazi na inawezekana.

  • Adamhussein
    March 8, 2012 @ 06:32:04AM

    Sisi hatujui kilichoko katika siku za mbele. Tunamwomba Mwenyezi Mungu Atulinde.

  • githaiga
    March 7, 2012 @ 04:43:42AM

    Wafuasi wa al-Shabaab wamebaki kuwa historia, watu kutoka Afrika wanapenda amani na umoja, wengi wameteseka katika mikono ya wanamgambo, ndio maana majeshi ya Ethiopia, KDF na AMISOM wanaelezea mapenzi yao kwa kutumia MILIO YA BUNDUKI kwa maadui wa Somalia. Wakristo au Waislamu, wote wanapenda amani, Wahindu au Wapagani wanahisi kuwa amani ndio muhimu. Kwa nini kuwakandamiza watu wenu wenyewe kwa maslahi ya ubinafsi. Bora kikombe cha maji katika nchi iliyojaa amani kuliko ZIWA lililojaa maziwa katika nchi iliyojaa MILIO YA BUNDUKI. AL-SHABAAB MSIO NA HAYA - MSHINDWE MLIOKOSA THAMANI ZA MAADILI NA DINI-MLIOSHIKWA NA UROHO NA UKOLONI MAMBO LEO – MLIOSIMAMISHWA NA UKOSEFU WENU WA DIRA – MLIOTELEKEZWA NA ALLAH/MUNGU NA WATU – MLIOZUILIWA NA NYAKATI ZINAZOBADILIKA – MLIOGEUZWA MAVUMBI NA LAANA ZA MABABU ZENU – MLIORUHUSIWA KUFA BILA HURUMA – MNAOPIGWA VITA NA UPUMBAVU, UENDAWAZIMU, UKOSEFU WA MAWAZO, UROHO NA UBABAIFU. Somalia inastahiki kuheshimika, siku zenu zinahesabika.

  • sami
    March 7, 2012 @ 02:54:16AM

    Jeshi la Kenya lilikuja Somalia kukisafisha kikundi chenye siasa kali cha kigaidi kinachoitwa al-Shabaab. Jeshi la Kenya limekuwa halifanyikazi ipasavyo kwa sababu bado kuna miji iliyo katika udhibiti wa al-Shabaab, mmoja wao ni Kismayu. Uwezo wa jeshi la Kenya kuwashinda al-Shabaab na kurejesha amani unatiliwa mashaka na watu wengi.

  • saed mohamed Ali
    March 5, 2012 @ 01:36:45PM

    Kwa hali yoyote, kikundi cha al-Shabaab kitashindwa siku hizi mbeleni. Na sisi kama Wasomali, lazima tufikiri namna ya kuijenga upya nchi yetu kwa kuweka amani ndani ya jamii ya Somalia na tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie.

  • khadar
    March 2, 2012 @ 07:20:57AM

    Kwa maoni yangu, AMISOM wamefanya kazi nzuri nchini Somalia. Nafikiri ikiwa watabakia Somalia, wataweza kuichukua nchi yote na huo ni ushindi kwa watu wa Somalia baadaye vikosi vyetu vikabidhiwe udhibiti wa nchi.

  • Abdi Mohamed
    March 2, 2012 @ 03:39:40AM

    Inaweza kuonekana kwa watu wengine kuwa wazo la umoja wa Afrika ni ndoto ambayo daima haiwezi kufikiwa hasa, wakati hali ya kisiasa, kiuchumi na hata kijeshi katika Pembe ya Afrika imekuwa mbaya sana kwa jumla. Pia, machafuko ya nchi za Kiarabu na taathira zake kwa eneo hili kunafanya umoja wa Afrika kuwa kama njozi kutokana na ukweli kwamba kuna mambo mengi yanahitajika ili kuufikia. Kama ambavyo ulimwengu umeshuhudia, kujaribu muungano kupitia Umoja wa Afrika na kuliangalia hili katika mtizamo wa uwezekano wa kupata matokeo, tumeshuhudia maendeleo katika hatua za kiuchumi, maendeleo katika elimu na kwa kipindi cha kuwepo kwake umefanikiwa. Hakuna shaka kuwa ikiwa Afrika itaungana inaweza kufikia kiwango sawa cha maendeleo kama Ulaya kwa sababu Afrika ina kila kitu kinachoweza kuifanya iwe rahisi kwa sababu ina mtaji mkubwa wa watu, na rasilimali za chakula na maji. Ikilinganishwa na Ulaya, Afrika ina rasilimali hizo nyingi zaidi.

  • cabdicasiis muhamed xasan
    March 1, 2012 @ 02:34:31AM

    Ningependa nchi kuwa na amani kwa sababu tutakuwa katika hatari. Nchi yetu itakuwa na amani ikiwa watu wetu wataamua. Nchi yetu inahitaji watu wawe na kazi.

  • Ali Hasssan
    February 28, 2012 @ 04:40:03PM

    Mimi ni Msomali na sina matumaini kuhusu Somalia tokea al-Shabaab iliungana na al-Qaeda badala ya kufikiria vipi kuijenga upya nchi yao.

  • Kasim
    February 28, 2012 @ 04:11:39PM

    Viongozi wa Somalia wasingekubali msaada wa kijeshi bila ya kuuchunguza sana vinginevyo Wamarekani watadhibiti uwanja na bila shaka kuufanya mtumwa uongozi wa Somalia kwa ahadi za silaha na vitu kwa kubadilishana nao kuwa mbele katika eneo la kimkakati.

  • Metho Kilonzo
    February 28, 2012 @ 12:06:21PM

    Saa ya giza zaidi ni muda mdogo kabla ya alfajiri. Tayari mmeishajitolea vya kutosha na amani na mafanikio tayari vipo hapa.

  • Kombe Kombe
    February 28, 2012 @ 08:01:18AM

    Watu wote wa Somalia tunawatakieni kila la heri. Nchi ya Somalia ni yenu kuijenga au kuivunja. Tafadhali tumieni fursa hii ili kuwasafisha wageni moja kwa moja na kwa mwisho.

  • alvin wambua musyoka
    February 28, 2012 @ 07:30:08AM

    Kwa rehema za Mwenyezi Mungu al-Shabaab na al-Qaeda watashindwa

  • sam
    February 28, 2012 @ 05:36:36AM

    Hongera kwa wale askari-askari wetu, sisi tunawasherehekea nyie wanaume. Wafanyeni na wao wasikia maumivu vilevile(al-Shabaab.

  • ABDI BISHAR
    February 28, 2012 @ 04:17:31AM

    Muda wa Al-Shabaab umekwisha. Somalia isubiri amani.

  • Geoffrey
    February 28, 2012 @ 01:46:27AM

    Hawa wanaoitwa wanamgambo ndio chanzo cha mateso ya Somalia, juhudi zote za AMISOM na KDF zikaribishwe na kuungwa mkono kwa sala. TUNAHITAJI AMANI SOMALIA kama ilivyo nchi jirani. Wasomali simamieni kwa AMANI, UPENDO NA UMOJA.

  • abdinuur
    February 27, 2012 @ 11:54:59AM

    Mimi sikufurahi kuhusu ushirikiano baina ya al-Shabaab na Al-Qaeda.

  • maiyo
    February 27, 2012 @ 09:31:55AM

    Ndio, ndugu zetu wa Somalia wanashinda. Tufurahie amani wakati tunamsubiri Yesu, karibuni atakuwa pamoja nasi.

  • Munyao
    February 27, 2012 @ 09:21:22AM

    Somalia ni nchi iliyobarikiwa, lakini al-Shabaab wasichukue fursa ya viongozi wake mbovu. Asante kwa KDF kwa kuanza safari ya kuifanya Somalia kuwa nchi nzuri, ambayo siku za mbele kila mtu hatatamani kuikosa Somalia. KDF wawindeni wahalifu hao na wamalizeni, kwa maana ya kuwamaliza moja kwa moja. Hatutaki kuwasikia tena. Hongera KDF. Mungu awabariki na Mungu ibariki Kenya.

  • kiptoo
    February 27, 2012 @ 04:20:08AM

    Hongera raia wa Somalia na vikosi vya kijeshi mnafanya kazi nzuri. Mwenyezi Mungu awajalie amani

  • jackson mutai
    February 27, 2012 @ 12:42:43AM

    Vita hivi vitaendelea mpaka lini ili Wasomali waweze kurejea na kufaidi amani na maendeleo, badala ya vita?

  • HARRISON
    February 26, 2012 @ 04:36:17PM

    Hongera raia wa Somalia. Mmeonesha ukomavu na mmeonesha kuwa watu mnaopenda amani. Endeleeni tafadhali, endeleeni na moyo wenu wa kuvikataa vikundi viwili vilivyokataliwa ambavyo daima havipendi amani. Mungu ajalie ombi la raisi wenu likubaliwe katika wakati kama huu. Endeleeni akina kaka na dada zangu.

  • njau
    February 26, 2012 @ 03:28:59PM

    Dunia lazima iwaunge mkono KDF na TFG kwa kuiteka Kismayu. Al-Shabaab hawatakuwa na jingine la kufanya isipokuwa kusalimu amri au kujitumbukiza baharini.

  • alice nderui
    February 25, 2012 @ 02:31:55AM

    Kila la heri Wasomali, ardhi ni yenu na sio ya wageni. Amani iwe kwenu nyote. Mungu ibariki Afrika.

  • r onyango
    February 25, 2012 @ 01:37:51AM

    Somalia inapaswa kupata serikali imara muda huohuo. Nilikwepo katika kambi za wakimbizi za ddb na kkm, ambako kuna mateso mengi, watu hawa wanataka kurejea katika nchi yao wanayoipenda. Kuna wengine ambao wangetamani wapate makazi sehemu nyingine lakini ukweli ni kuwa hata uende magharibi au mashariki, nyumbani ni nyumbani.

  • Edwin m. A.
    February 24, 2012 @ 09:16:29PM

    Kila chenye mwanzo huwa na mwisho. Al-Shabaab hatimaye watafikia mwisho wao. Na Jeshi la Ulinzi la Kenya litawafikisha mwisho wao.

  • barnabas kithuure
    February 24, 2012 @ 12:17:25PM

    Al-Qaeda na al-Shabaab ni watu haramu ambao lazima wapigwe kwa rasilimali zote zilizopo ikiwemo kwa mawe.

  • Reuben
    February 24, 2012 @ 10:39:22AM

    Maendeleo mazuri...Vikosi vyetu endeleeni na mwendo.

  • KAREEM
    February 24, 2012 @ 09:04:31AM

    Mwisho wa yote al-Shabaab watashinda.

  • maurice ngochi
    February 24, 2012 @ 12:19:20AM

    Hongereni askari wote. Al-Shabaab wenye msimamo mkali lazima wauliwe hapo hapo. Mungu vibariki vikosi vya Umoja wa Afrika kwa kuwasaidia watu wa Somalia.

  • Ali Ahmed Al-Hameed
    February 23, 2012 @ 04:09:11PM

    Somalia ni mali ya Wasomali. Wao peke yao ndio wenye haki ya kuchagua na kukaribisha marafiki. Mwenyezi Mungu ijalie amani Somalia.

  • teresa wambua
    February 23, 2012 @ 02:48:25PM

    Mpaka sasa kile kimekuwa kinafanywa ili kuwazuwia al-Shabaab kinawafanya Wasomali washushe pumzi na vilevile kwa Wakenya kwa sababu sisi sote tuko kwenye hatari sawa. Hongera kwa askari wa Kenya waliohusika.

  • dickson safari bushasha
    February 23, 2012 @ 05:41:04AM

    Hakuana amani itakayokuja bila ya kumwaga damu. Umoja wa Mataifa lazima uungane na vikosi vya AMISOM katika vita hivi kwa vile ni usumbufu kwa dunia nzima.

  • Olwenyi
    February 23, 2012 @ 03:26:49AM

    “Imeripotiwa kuwa maandamano yaliandaliwa na Serikali ya Mpito ya Shirikisho na washirika wao, na yamekuja siku mbili baada ya al-Shabaab kuandaa mkutano ili kusherehekea kuungana kwao na al-Qaeda”. Mkiwa na AMISOM upande wenu, hamna sababu ya kuandaa maandamano. Wakabiliane na daieni nchi yenu!

  • koli david
    February 23, 2012 @ 12:48:25AM

    Al-Shabaab wanalaaniwa na watu wote kwa kuua ndugu zetu. Al-Shabaab sio watu wa dini, vita hivi sio vya jihadi. Al-shabaab ondokeni kwa ushindi wa kibindadamu. Ondokeni kwa maendeleo ya wote.

  • kioko samson
    February 22, 2012 @ 05:08:27AM

    Njia pekee ya kupata amani nchini Somalia ni kuzilemaza operesheni za wale wanaojiita Al-Shabaab na Al-Qaeda, kwa hivyo jeshi la Somalia linahitaji kuungwa mkono kwa silaha za lazima

  • paul kiptoo
    February 21, 2012 @ 08:37:43AM

    Kazi nzuri akina kaka na akina dada wa Somali. Komboeni nchi yenu nzuri na mrejee katika jamii ya mataifa yenye amani na mafanikio. Al-Shabaab na wafuasi wao lazima watoke Somalia, tunawaungeni mkono. Kikwazo cha silaha kiondolewe ili waweze kuislaimisha nchi.

  • Isdorah atieno
    February 21, 2012 @ 03:18:10AM

    Yote hii ni kwa ajili ya kusali kwa ajili ya nchi zetu mbili ili ziwe na amani.

  • stano
    February 21, 2012 @ 02:33:29AM

    Hatimaye kaka zetu wa Somalia wamegundua gharama za vita visivyokwisha. Simameni dhidi genge hili la kihalifu la kigeni na waondoeni katika nchi yenu inayopenda amani.

  • Faqi yusksel
    February 20, 2012 @ 11:17:34AM

    Vizuri, vikosi vya kulinda amani vya Afrika vimeonesha wazi kusababisha mgogoro na vita visivyokwisha katika eneo hili. Operesheni hii inaweza kusaidia kidogo kuimarisha utawala nchini, hata kama itashindwa kupatikana yote. Inatarajiwa kwa operesheni hii kulinda utawala wa serikali ya mpito ya shirikisho na kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Somalia, kwa hivyo, hii inaweza kuwa na umuhimu mkubwa sana katika vita dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab au wanamgambo wengine wanaopinga utawala wao katika nchi. Zaidi ya hayo, moja ya dhamana za kikosi cha kulinda amani ni kusaidia mashirika ya misaada ili kutekeleza msaada wao muhimu sana katika nchi, kwa njia hiyo, watu wengi wanaotegemea kazi ya misaada, wataweza kupata misaada ya lazima! Vilevile, kikosi cha kulinda amani wanatarajiwa kujenga mpango wa usalama dhidi ya al-Shabaab na washirika wao. Kuwepo kwao ni kuibuka kwa matumaini kwa jamii, vikosi vyao vina nidhamu na vimefunzwa zaidi kuliko kikosi cha taifa cha Somalia. Wako katika ushindani na wanamgambo wenye silaha hasa wale wa al-Shabaab. Kwa sababu hii, raia wengi wana imani na kikosi cha kulinda amani.

  • c/salaan
    February 20, 2012 @ 10:22:19AM

    Al-Qaeda na Al-Shabaab, Mimi ni Msomali ninayeishi ughaibuni muda mrefu na sina matumaini kuhusu Somalia kwa sababu waliungana na Al-Qaeda. Mungu wasaidie Wasomali, popote walipo ulimwenguni. Amani na Baraka za Mungu ziwe juu yenu.

  • kiura ireri
    February 20, 2012 @ 07:36:55AM

    Wakati wa al-Shabaab umefika. Malizeni umwagaji wa damu duniani. Watu hawamjui Mungu.

  • olonyenkare
    February 19, 2012 @ 04:18:57AM

    Hatimae Wasomali wameungana dhidi ya adui yao/zao mmoja. Vilevile ni vizuri kuona mapenzi yanayong'ara katika wanaume na wanawake wetu wanaovaa sare, huku wakifanya kila wawezalo katika midani ya Somalia.

  • Muscab mujahid furtm hord
    February 18, 2012 @ 01:22:15PM

    Majeshi ya Kiafrika yasiyoamini Mungu, wale waasi na vyombo vyao vya habari vya propaganda waliripoti kuwa waliuteka mji wa Mogadishu na usalama ni wa kuaminika. Madai yao yamethibitishwa kuwa ni uongo na mashujaa wanaofuata imani ya Kiislamu. Watu wenye ari walishambulia ngome kadhaa zilizokuwa zinamilikiwa na kundi la wasioamini Mungu ndani ya Somalia katika wilaya za Bar Ubah & Yaqshiq. Watu wasioamini Mungu sasa wameghumiwa kwa mashambulizi haya na wanajiuliza ikiwa mashujaa hawa wana mabawa au walizuka kutoka chini ya ardhi.

  • Omandi
    February 18, 2012 @ 12:57:21PM

    HONGERENI & safi sana kaka zetu wa Mogadishu, na bado tunawataka Wasomali wengi zaidi watoke na kuwakataa wauwaji hawa wasio na moyo kwa jina la al-Shebab/Qaida. Hapa Kenya tunawaunga mkono kikamilifu, kama ambavyo daima tumekuwa tukishangaa kwa nini mnaendelea kuwavumilia wahalifu hawa katika maisha yenu? Mna watoto wa kulisha, kuelimisha na nyinyi wenyewe kujitafutia kazi nzuri za kufanya, kuendeleza nchi yenu na kuishi maisha mazuri. Enyi watu, mnahitaji amani! Msione haya. ITAFUTENI, iendeeni na msikubali kurubuniwa na wahalifu hawa. Miaka yote hii iliyopotea ya kuua Wasomali wasio na hatia, kuwalemaza, kuwatekwa nyara, kubakwa, njaa, maradhi. SIMAMENI & MSEME HAPANA!! KWA MALAIKA HAWA WA VIFO!! HATUTAKI SHEBAB. Hatutaki QAIDA. SASA tunataka amani kwa ajili ya Somalia!!

  • Bitisururu
    February 18, 2012 @ 12:43:07PM

    Juhudi za Wakenya kuisaidia Serikali ya Somalia zimefanikiwa. Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Kenya ameongea juu ya mambo haya katika Bunge la Kenya, ambamo alishughulikia mpango wa kuokoa maisha na mali. Vitendo hivi vilifuata tendo la kikatili la Al-Shabaab la kuteka wataalam wageni na wageni wengine waliokuwa nchini Kenya. Waliamini kwamba ushambulizi huo ulitendwa na kundi la Al-Shabaab la kisomali. Nao hawakupinga mswada huo, hata walipobainisha mashambulizi hayo.Mwenendo wa Wakenya umeupa mfumo wa ulinzi wa Serikali ya Somalia usaidizi mwingi.Wamepigana kwa njia isiyomruhusu yeyote kulala salama.Waasi daima wako tayari kuangamiza yeyote atakayewapinga. Mpango wa ulinzi wa Kikenya umepunguza ugaidi na mauaji katika sehemu za kusini za Jamhuri ya Somalia kwa kiwango kikubwa.

  • makau
    February 18, 2012 @ 04:11:46AM

    Mtu anaweza kushangaa itachukua muda gani Afrika kuzungumzia juu ya al-Shabaab. Serikali zinasema tu kuwa zinaunga mkono AMISOM na Kikosi cha Ulinzi cha Kenya, lakini lazima ziende mbali zaidi ya zoezi hili la mahusiano ya umma. Hebu watoe misaada ya kifedha na watu waliopatiwa mafunzo. Al-Shabaab lazima washindwe kwa haraka kadiri inavyowezekana ili kuanza kuleta maendeleo kwa eneo hili.

  • hillton munene
    February 17, 2012 @ 07:42:37AM

    Ni lazima watoweke kwa sababu ya ukatili wao kwa mbari huko Afrika

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo