Muungano wa al-Shabaab na al-Qaeda unajaribu kunyanyua ari -- wachambuzi

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Februari 13, 2012

  • 86 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wachambuzi wa kisiasa wa Somalia wanasema tangazo la kuungana baina ya kikundi cha al-Shabaab na al-Qaeda kunafuatia kupoteza kwao fedha na vifaa kunakovikumba vikundi vyote viwili, na kutapunguza kuungwa kwao mkono kwa al-Shabaab miongoni mwa Wasomali.

  • Wapiganaji wa al-Shabaab, amabo sasa wamejiunga rasmi na al-Qaeda, wakifanya mazoezi ya kijeshi kwenye kijiji huko eneo la Lower Shabelle mwezi Februari 2011. [Na Abdurashid Abdulle/Shirika la Habari la AFP]

    Wapiganaji wa al-Shabaab, amabo sasa wamejiunga rasmi na al-Qaeda, wakifanya mazoezi ya kijeshi kwenye kijiji huko eneo la Lower Shabelle mwezi Februari 2011. [Na Abdurashid Abdulle/Shirika la Habari la AFP]

Katika ujumbe wa video uliotumwa katika majukwaa ya wenye misimamo mikali wiki iliyopita na kiongozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri, alitangaza kuwa kikundi cha al-Shabaab kimeungana na al-Qaeda. Tangazo hili lilikuja zaidi ya miezi minane baada ya al-Shabaab kuapa utii wao kwa kikundi hiki cha kigaidi.

"Al-Shabaab hakitafaidika na kujiunga kwao na vikundi vya kimataifa vya ugaidi kama vile al-Qaeda na atakae faidika pekee katika shughuli hii ni al-Qaeda,” alisema Noor Ahmed, brigadia mstaafu wa jeshi la Somalia. “Hatujui kama ikiwa al-Shabaab wanataka kujiunga katika uwanja wa kimataifa wa jihad ili kushiriki katika jukwaa la kimataifa kama njia yao ya kupata fedha na kuungwa mkono zaidi.”

Ahmed aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi kuwa kuna “makumi ya wapiganaji wa kigeni” katika jeshi la al-Shabaab. “"[Al-Qaeda] wanawahitaji ili kuweza kupeleka wapiganaji hao katika nchi za magharibi ambako walitoka ili kuanzisha mashambulizi ya kigaidi huko.”

Al-Shabaab watapoteza ‘nyoyo na akili’ za Wasomali

Omar Tahir, mkurugenzi wa Kituo cha Maafikiano na Majadiliano ambaye pia ni mtaalamu juu ya vikundi vya Kiislamu huko Somalia, aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi kuwa uongozi wa al-Shabaab umegawika katika kambi mbili.

Alisema kundi la kwanza linajumuisha viongozi wanamgambo wa kikabila kama vile Hassan Dahir Aways na Mukhtar Robow, vilevile anayejulikana kama Abu Mansour. Kundi la pili linaongozwa na wenye msimamo mkali ambao wameathiriwa na al-Qaeda kama vile Mukhtar Abu al-Zubair, kiongozi wa al-Shabaab na Ibrahim al-Afghani.

“Katika miezi michache iliyopita, kulikuwa na mgogoro baina ya vikundi hivi viwili... Lengo la mgogoro huu ilikuwa jukumu la wapiganaji wa kigeni katika kikundi pamoja na namna gani ya kuishughulikia al-Qaeda,” Tahir aliiambia Sabahi.

“Mrengo wenye msimamo mkali zaidi [wa al-Shabaab] unaoongozwa na Abu al-Zubair, ambaye alitaka kujiunga waziwazi na kivifaa na al-Qaeda, kwa hivyo kuifanya Somalia sehemu ya kuanzishia jihadi ya kimataifa, alifanikiwa katika vita vyao vya ndani miongoni wa viongozi wa al-Shabaab,” alisema. “Ama kwa mkondo wenye msimamo wa wastani unaoongozwa na Abu Mansour pamoja na Sheikh Aways, ambao wote wawili walitaka kufuata siasa za wastani katika kushughulika na ulimwengu wa nje pamoja na itikadi inayokubalika kuliko kuwa na uhusiano kamili wa vifaa na al-Qaeda, hawa walishindwa mapambano.”

Tahir alisema mrengo wa wastani walikuwa wanatafuta kuonesha picha ya taifa la Kiislamu la Somalia linaloongozwa na al-Shabaab.

Mchambuzi wa kisiasa Mohamed Abdul Razzaq alisema kwamba ushirikiano wa moja kwa moja wa al-Shabaab na al-Qaeda utaharibu kuungwa mkono kwa kikundi hiki miongoni mwa Wasomali.

“Al-Shabaab watapoteza umaarufu baada ya kujiunga na al-Qaeda," Abdul Razzaq aliiambia Sabahi. “Licha ya ukweli kwamba kikundi hiki kilikuwa kinafuata itikadi ya al-Qaeda, itapoteza nyoyo na akili za watu wa Somalia baada ya kujiunga na al-Qaeda na kikundi hakitoweza kuwa ushawishi mitaani ili kuvutia waungaji mkono wapya.”

Jaribio la 'kukuza ari'

Al-Shabaab ilithibitisha utii wao kwa al-Zawahiri mwezi Juni mwaka jana pale aliposhika uongozi wa al-Qaeda baada ya kifo cha Osama bin Laden. Hili lilichukuliwa na wasimamizi wa usalama kama mwanzo wa uanachama wa al-Shabaab na ule wa mtandao wa kimataifa wa kigaidi wa al-Qaeda.

Siku ya Jumatatu (tarehe 13 Februari), al-Shabaab ilifanya mkusanyiko huko Elasha Biyaha ili kuonesha kuunga kwao mkono al-Qaeda katika Rasi ya Arabuni (AQAP).

"[Al-Shabaab] nchini Somalia imejiunga moja kwa moja na kaka zao wa al-Qaeda, jambo linalomaanisha kuwa sisi ni sehemu yao,” msemaji wa al-Shabaab Sheikh Ali Mohamud Rage alikariririwa na Redio ya Somalia ya RBC akisema.

“Tutafanyakazi na kaka zetu wa AQAP huko Yemen, Saudi Arabia na kwengine ulimwenguni na sisi ni sehemu yao,” alisema. “Sisi ni tawi la AQAP lililopo Somalia.”

Maandamano kama hayo yalifanyika huko Afgoye, Merka na Lafoole, ambako maafisa wengine wa al-Shabaab walitoa wito wa kukabiliana na vikosi vya Serikali ya Mpito ya Shirikisho (TFG) na Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia, kituo hicho cha redio kiliripoti.

Wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema maandamano kama hayo yanaweza kuwa ni jaribio la kupandisha ari ya al-Qaeda na al-Shabaab, kufuatia kupoteza uwezo wa vifaa na fedha kulikovikumba vikundi vyote viwili.

“Al-Shabaab siku zote wamekuwa ni washirika wa al-Qaeda, alisema mchambuzi wa kisiasa Abdul Rashid Ishaaq. “Vilevile, uongozi wa al-Shabaab umekuwa ukipokea amri na miongozo kutoka kwa al-Qaeda kwa muda mrefu, bila ya kutaja ushauri na mafunzo kutoka kwa wajumbe wa mtandao wa kimataifa. Al-Shabaab vilevile wanatumia mbinu za kigaidi za al-Qaeda kama vile mashumbulizi ya muaji, mabomu ya magari na mengineyo.”

Ishaaq aliiambia Sabahi, "Tangazo hili jipya, kwa maoni yangu binafsi, ni juhudi tu za kupandisha ari kwa vikundi vyote viwili kwa sababu hatua hii inakuja wakati mabapo vikundi vyote viwili -- al-Shabaab na al-Qaeda – vimeshuhudia mikwamo mikubwa kutokana na kuondokewa na makamanda wao wakubwa katika miezi 10 iliyopita.”

Uwanja mpya wa vita juu ya ugaidi

TFG ilisema katika taarifa hapo Jumatatu kuwa kuungana kwa vikundi viwili hivi kunathibitisha kuwa vikosi vya serikali na AMISOM vimekuwa vikipigana na al-Qaeda nchini Somalia kwa muda wa miaka mitano iliyopita.

“Vilevile tunaamini kwamba muungano wao utaongeza hali ya kutokuwepo usalama nchini Somalia, Afrika Mashariki na duniani kote, na kwamba Somalia iko katika hatari ya kuwa kiini cha al-Qaeda katika Afrika Mashariki,” taarifa ilisema. “Serikali ya Somalia haitaichukilia kirahisi hatari kutoka muungano wao rasmi na tutapeleka nguvu zetu zote pamoja na watu wote kuwa katika hali ya tahadhari kubwa ili kukabiliana na hatari inayoweza kutokea kwa usalama wa Somalia na eneo la Afrika Mashariki.”

"Tunawataka vijana ambao wamepotoshwa na al-Shabaab kuacha kufanyakazi nao kwa vile ni wazi kwao kuwa kikundi hichi kimeonesha uhalisia wao kwa kuungana na kikundi cha kimataifa cha uhalifu cha al-Qaeda,” TFG ilisema, na kuongeza kuwa waasi wa al-Shabaab tunawapa siku 15 “kuweka silaha chini na kufuata njia ya amani”.

AMISOM ilisema kuungana kwa vikundi viwili kunawakilisha changamoto mpya kwa misheni ya usalama katika eneo hili.

"Al-Shabaab walichukua chapa ya al-Qaeda kwa vile haikuwa sehemu ya Somalia bali sehemu ya al-Qaeda, alisema msemaji wa AMISOM Meja Paddy Akunda. “Tulilijua hilo na tunamtaka kila mtu kuchukua tahadhari zaidi kwa sababu sasa tunapigana na al-Qaeda. Huu ni uwanja mpya [wa vita] dhidi ya ugaidi.”

Akunda aliitaka jumuiya ya kimataifa kuthibitisha haraka wajibu wake kwa Somalia ili isiwe maficho salama kwa ugaidi wa kimataifa.

"Sote tunajua kuwa al-Qaeda wanawaunga mkono al-Shabaab na kwamba itikadi yao sio Somalia na siyo ya Kiislamu, bali itikadi ya al-Qaeda na sasa iko wazi,” alisema Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali. Alisema muungano wa al-Qaeda na al-Shabaab “sio jambo la kushangaza, kutokana na uhusiano imara baina ya wawili hawa.”

Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Somalia ilieleza wasiwasi wake kuhusu hatua inayofuatia ndani ya Somalia baada ya al-Shabaab kujiunga na al-Qaeda.

"Uamuzi wa al-Shabaab kujiunga na al-Qaeda ni tishio kwa hatima ya nchi ya Somalia, alisema Sheikh Bashir Ahmed Salad, mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Somalia. “Mfumo wa kijamii wa Somalia na maumbile ya watu wa Somalia haiendani na maelekezo ya al-Qaeda, kwa hivyo, yeyote ambaye anajaribu kuiweka nchi ya Somalia katika bango la al-Qaeda halizingatii hili.”

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 139)

Dislike_icon(30)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • said juma
    February 2, 2013 @ 12:29:55PM

    makafiri kuuwawa ni haki na mimi naunga mkono vikundi vyote vya kiislam ambavyo wanapigana kwa ajili quran iwe ndio hukmu katika dunia, hakun agaidi wala nini, kilichopo ni vita takatifu baina ya waislam ambao wanata qurani iwe hukmu na makafiri ambao hawataki jambo hilo, na quran haina shaka mda umefika kuhukumu hata kama makafiri hamtaki jambo.

  • Muhammad Haji
    July 13, 2012 @ 12:57:08AM

    Sababu ambayo inawezekena ilivipelekea vikundi hivi viwili ilikuwa ni kuimarisha na kupanua mtandao wa al-Qaeda. Huu ungekuwa mpango kwa ajili ya al-Qaeda kugeuza nadhira zao kutoka wao wenyewe kwa ajili ya kikundi kingine kidogo, al-Shabaab, ili waweze kufanya mashambulizi yao ya kigaidi. Al-Shabaab kwa upande mwingine walihisi ni chagua rahisi zaidi la kupata silaha mpya na mabomu, ambazo zingetumika kwa ajili ya kupigana na majeshi ya Umoja wa Afrika yanayoizunguka Kismayo. Kama viwanja vya ndege vya Mogadishu na Kismayo visingedhibitiwa, vikundi hivi vya kigaidi vingeendelea kupata fedha kutoka kikundi kuu, kwa hivyo kufanya kuwa ngumu zaidi kupambana na ugaidi Somalia.

  • Nuuradiin34@hotmail..com
    July 12, 2012 @ 07:02:21AM

    Huku al-Qaeda wakiwa wanachanika vipande vipande taratibu, utaratibu wao wa kujipatia fedha ikiwa inafifia kidogo kidogo, jambo linalowafanya wawe wametishika na kufilisika. Mambo haya yakiwa katika akili zao. Inawabidi watafute njia zaidi ambapo wanaweza kuweka mikono yao. Kwa hivyo kuanza kuwalenga raia wa hadhi ya juu. Mara tu wakishawazuia mafichoni wananchi hawa, ndipo watadai kiwango kikubwa cha fedha. Pia watazitishia familia za wananchi hawa ili wasiwahusishe polisi. Vinginevyo watawaua mateka wao. Hii ndio njia pekee ya kikundi cha kigaidi kinaweza kujipatia pesa zaidi. Sababu nyengine kwa nini al-Qaida wanawalenga raia ni kuwa wamegundua kuwa serikali haiku tayari kutoa pesa za kikomboleo kwa vikundi vya kigaidi. Kila ambapo serikali inaahidi kutoa pesa kwa vikundi hivi, kwa kawaida serikali hupata njia ya kuwagundua wamejifcha wapi, na kuwaweka kizuizini. Hii inatoa wito wa kuchukuliwa hatua za muhimu kutoka kwa vikundi hivi, ili vijiweke mbali na shughuli zozote za serikali, na kuwa na uwezo wa kusimama kwa miguu yao wenyewe.

  • salama
    July 12, 2012 @ 04:52:29AM

    Baada ya kuona dalili za mapema za kupotea kwao, al-Shabaab waliamua kuwakumbatia al-Qaeda, ili waweze kupata msaada kutoka kwao. Kwa kuwa al-Qaeda ni kikundi kinachoongoza cha ugaidi kinachojulikana ulimwenguni kote na wamekuwa wamehusika katika mashambulizi mengi ya kigaidi, hivyo al-Shabaab walitaka kupata mwongozo kutoka kwao [al-Qaeda]. Kwa kuunganisha vikundi viwili, hilo lingewafanya wawe na nguvu zaidi na al-Qaeda ingeifadhili al-Shabaab kama kawaida, kwa hivyo wangeweza kusimama tena wenyewe.

  • ibrahim hussein
    June 12, 2012 @ 07:09:05AM

    Osama bin Laden aliuawa na majeshi ya Marekani mwaka jana na kumalizika uongozi wake wa kundi la kigaidi katili kabisa katika Mashariki ya Kati. Kifo cha kiongozi huyu hakitakibadilisha kikundi chenye siasa kali kwa sababu kikundi hiki kimegawanyika katika vikundi vidogo vidogo vya ugaidi ambavyo bado vinafanya shughuli zao za kigaidi. Kitu pekee ambacho kinaweza kubadilika ni kwamba hakutakuwa na mpango mkubwa wa mashambulizi kama yale ya 9/11 ambayo yalihitaji fedha zaidi na kundi lenye umoja zaidi. Vikundi vidogo vidogo vimegeukia katika mahitaji yao ya kichoyo ya fedha na vimekuwa vikifanya shughuli za kigaidi ili kuhakikisha kuwa vinapata fedha. Sababu ya hili ni kwamba watu ambao walikuwa wanafadhili kikundi hiki wamejiondoa zamani kwa sababu kikundi chenyewe kimegeuka kutoka "dhamira" yao ya awali. Kiongozi ambaye alichukua nafasi baada ya bin Laden hana tena udhibiti wa kundi zima na wengi wao wanafanya kazi kama askari wa kukodiwa kwa ajili ya mshahara kwa kumfanyia kazi mtu ambaye anaweza kujaza fedha mfukoni mwake. Mwenyezi Mungu awasaidie waislamu wote kuwaondosha na magaidi.

  • Karuri
    May 19, 2012 @ 06:20:31AM

    KENYA IMEYATAKA, ACHA SASA YAWAFIKE.

  • Rashid Athumani
    May 10, 2012 @ 02:37:01AM

    Tumejiuliza sisi wenyewe kwa nini kuna ugaidi? Lazima tufikirie mara mbili.

  • joseph mwangi wairimu
    May 10, 2012 @ 12:28:01AM

    Watu lazima waungane ili kummaliza adui huyu kwa msaada wa Umoja wa Mataifa kwa kutoa habari kwa viongozi wa maeneo wanaowaamini.

  • Sahro maxamad
    May 9, 2012 @ 12:31:43AM

    Ushirika wa al-Shabaab na al-Qaeda ni mafanikio kwa watu wa Somalia na jumuiya yote ya Kiislamu. Ninaweza kusema kwamba muungano wa vikundi viwili hivi utapelekea kukombolewa kwa Somalia na ulimwengu wa Kiislamu kwa jumla. MWENYEZI MUNGU AKIPENDA.

  • peter
    April 8, 2012 @ 02:26:44PM

    Watu hawa lazima watokomezwe ulimwenguni kwa hatua zozote zilizopo.

  • shaaban mwanza
    March 27, 2012 @ 04:38:57AM

    AL-SHABAAB ni sawa na MUNGIKI ambapo tofauti ni rangi na kabila tu, wanachotaka ni kutengeneza utajiri tu katika vita hivi kwa kuua watu wasio na hatia ulimwenguni kote.

  • Ilyas
    March 24, 2012 @ 11:50:47PM

    Al-Qaeda ni kikundi cha kigaidi kinachopatikana Iraki na Afghnistani na wanafuata aina ya itikadi ya Kiislamu ambayo watu wengi wanawaona kama ni yenye kujipinga na kupotosha. Kanuni za Kiislamu zinaeleza wazi kuwa usiwadhuru binadamu wenzako.

  • polyn
    March 24, 2012 @ 05:39:55AM

    Yaani naipenda hii. Hatua inayofuatia iwe ni juhudi za kumuua au kumkamata kiongozi wa al-Shabaab na kwa hivyo kikundi kitatawanyika moja kwa moja. Hatimaye Somalia na dunia kwa jumla itakuwa na amani. .

  • maxamed xuseen
    March 22, 2012 @ 01:29:57PM

    Nafikiri al-Shabaab wanapoteza imani kwa watu wa Somalia, ambayo zamani walikuwa nayo.

  • FELIX GAYAH
    March 22, 2012 @ 08:01:53AM

    Taifa letu Kenya litakabiliwa na mashambulizi kadhaa kwa vile al-Shabaab, al-Qaeda na Wanajamhuri wa Mombasa (M.R.C.) wanaoibuka wanatiwa moyo na kitu kimoja, wote wanadai kuwa wakombozi wa Uislamu. M.R.C ni kikundi kinachoibuka ambacho kinauwezo wa kungana na vikundi vyengine vyenye itikadi kali kwa vile wanahisi kuwa masuala yao ni muhimu sana na hayawezi kushughulikiwa na viongozi wadogo katika serikali kama vile mawaziri na mameya. Wanaonekana kutaka taifa lililo huru. Ndoto yao hii haiwezi kufikiwa kwa kuungana na zaidi ya kikosi kimoja chenye nguvu kama vile al-Qaeda na al-Shabaab.

  • David kibet
    March 22, 2012 @ 02:47:49AM

    Wanamgambo wa al-Shabaab ni kikwazo kikubwa katika Pembe ya Afrika na kwa watu wa Somalia. Kikundi hiki lazima kisimamishwe ili kuwaruhusu watu wananchi wa Somalia kuishi kwa amani na majirani zao. Al-Qaeda wanataka kuwaunga mkono al-Shabaab ili Somalia iwe uwanja wao wa mafunzo.

  • Name removed for offensive content
    March 21, 2012 @ 08:17:12AM

    Wanamgambo wa al-Shabaab walikuwa tawi la Muungano wa Mahakama za Kiislamu. Uliundwa ili kupambana na Ethiopia na serikali ya mpito ya Somalia. Mahubiri yao yanazungumzia juu ya jihadi ya kimataifa. Walisema hawana uhusiano na al-Qaeda. Ni viongozi wao wanaotaja haja ya kuunda serikali imara ya Kiislamu chini ya sheria za Kiislamu, ile ambayo haina uvunjaji moyo, ambayo itatafsiriwa na Waethiopia na Wamarekani. Al-Shabaab waliwashambulia wananchi wa Somalia na wanaamini kuwa watu sio waaminifu wa desturi za Kiislamu.

  • KENNETH
    March 21, 2012 @ 06:30:54AM

    KDF LAZIMA IWAAMBIE WAKENYA UKWELI KWA NINI WAMEAMUA KUJIUNGA NA AMISOM. NI KWA KUWA AL-SHABAAB WAMEWAZIDI NGUVU AU NINI? MEJA CHIRCHIR, TUELEZE.

  • antony
    March 21, 2012 @ 04:34:14AM

    Al-Shabaab lazima wauliwe.

  • axmed sulayman
    March 19, 2012 @ 12:49:59AM

    Tangu Bin Laden alikuwepo Sudan, kikundi cha al-Qaeda kiko Somalia kutokana na kuwekwa kwa kambi za kuwapa mafunzo katika eneo hili. Aidha, Somalia ni moja ya sehemu ambazo kikundi kinalenga maslahi ya Marekani yaliyoko ndani na nje ya Somalia na uwepo wake nchini Somalia unakiruhusu kikundi hiki kuingia katika nchi zote za Afrika. Kutojitangaza Somalia yenyewe na muingiliano wake baina ya vikundi na hali ya vurugu ambazo zinatokea Somalia kuliwaruhusu al-Qaeda kuingia na kujipanga kirahisi…

  • kiprono yegon
    March 18, 2012 @ 09:58:33AM

    Ni kitu kizuri kwa umoja wa Wamarekani na dunia kujihusisha na kupambana na kikundi cha kigaidi. Kufuatia muungano wa hivi karibuni baina ya al-Qaeda na al-Shabaab itakuwa umwagaji damu katika nchi zinazopambana dhidi ya kikundi cha kigaidi hasa Kenya ambao kwa zaidi ya miezi minane wanapigana nao nchini Somalia. Kwa kuwa imechaguliwa sasa kwa njia moja au nyengine, kunaweza kuokoa mengi ikilinganishwa na shambulizi la mwisho la kigaidi katika kituo cha mabasi cha Machakos; kama Kenya isingekuwa dhidi ya kikundi cha kigaidi isingeweza kupoteza watu wake. Ingawaje kupigana nao kulikuwa na dhamiri ya kuondosha ugaidi, Wakenya wasio na hatia wawanapaswa kuilaumu serikali yao kwa kutokuwa imara katika kuweka usalama kwa vile walilitarajia hilo. Kwa kuyalaumu mataifa ya dunia wanatarajiwa kupambana na watu hawa na kupeleka majeshi ya kimataifa kukipiga, kuwaua na kuangamiza kikundi cha kigaidi.

  • abbas faiq
    March 17, 2012 @ 06:16:38PM

    Kila kikundi cha vijana na al-Qaeda nchini Somalia vinashuhudia kupungua sana kwa uwezo wao wa kijeshi na kuongezeka kwa upungufu wa matendo yao na maeneo ambayo mwanzo vilikuwa vimeenea, ambapo kikundi cha vijana badala ya kudhibiti ardhi kubwa ya kusini mwa Somalia isipokuwa maeneo ya mji mkuu Mogadishu, sasa iko chini ya udhibiti wa serikali ya mpito.

  • Nimo
    March 17, 2012 @ 06:08:46PM

    Somalia inachukuliwa kama makazi salama kwa al-Qaeda na inawapa uhuru wa kutembea kwa vile inayo maeneo mengi ya misitu tofauti na sehemu kubwa ya ardhi wazi za Somalia.

  • wadani fuaad
    March 16, 2012 @ 09:50:04PM

    Al-Qaeda wanachukua fursa ya umoja huu ili kueneza mawazo yao miongoni mwa aina tofauti za vijana. Aidha, kikundi cha vijana tangu mwanzo kilikuwa kinaunga mkono al-Qaeda katika vipengele vya kifikra na mkabala wa kijeshi na kujihesabu wenyewe kuwa washirika wa al-Qaeda na wala sio tawi la kikundi kikuu. Kikundi cha vijana kuungana na al-Qaeda kunaifanya Somalia ifuate tabia za kundi la al-Qaeda katika uhalisia wake na itapeleka operesheni zake za kijeshi Ethiopia, Kenya, Uganda na Djibouti ambazo tayari zina majeshi yao nchini Somalia.

  • adan
    March 15, 2012 @ 04:51:40AM

    Ingawaje tangazo la ushirikiano baina ya al-Shabaab na al-Qaeda lilikuja wakati ambapo vikundi vyote viwili vilikabiliwa na upotevu mkubwa wa mali na nyenzo nyingine, tunaweza kusema kuwa suala hili linapunguza sana heshima ya al-Shabaab katika jamii ya Somalia, na kwa sababu hii watawapoteza watu wao wengi wanaowaunga mkono. Kiongozi wa al-Qaeda alitangaza kuwa walifanya ushirikiano na al-Shabaab miezi 8 kabala ya kikundi hiki kuapa kuwa kitakuwa kitiifu kwa al-Qaeda. Ikiwa tutalichambua hili tunaweza kusema kwamba al-Shabaab hawatafaidika na chochote kutokana na ushirika huo na al-Qaeda na ni al-Qaeda ambao watapata faida zote. Hatujui kuwa al-Shabaab wanafanya ushirikiano huu na Al-Qaeda ili kushiriki katika vita vitakatifu vya kimataifa ili kupata fedha na kuungwa mkono. Nafikiri al-Qaeda wana haja ya wapiganaji kumi wa kigeni wanaopigana na al-Shabaab ili wawapeleke nchi za magharibi ambako walitoka ili watekeleze mashambulizi ya kigaidi.

  • Ahmed
    March 14, 2012 @ 08:21:23PM

    Marekani ilipanga kupeleka vikosi vyao vya usalama ndani na katika nchi nyingi za Kiislamu ili kumsaka Osama Bin Laden, mmoja wa viongozi wakuu wa al-Qaeda. Mwaka jana walimuua nchini Pakistani. Baada ya hilo yote yakaana kwa kueleza kuwa sasa al-Qaeda hawawezi kuwa na nguvu sana kama ilivyokuwa wakati wa Osama Bin Laden. Mawazo hayo ni kweli vilevile; wanamgambo wengi wa al-Qaeda walipoteza maisha yao. Katika miaka ya karibuni habari za kutisha ni kuhusu al-Qaeda. Sasa hawana tena nguvu mikononi mwao na wanapata misaada michache kutoka vikundi vya wanamgambo wengine lakini sasa vilevile wanaendelea kuwa wanaoogopwa sana.

  • Abdirahman
    March 14, 2012 @ 06:38:46PM

    Al-Qaeda na al-Shabaab wana mawazo sawa lakini wako tofauti katika operesheni zao, wanawalenga watu tofauti: al-Qaeda wanavyowalenga watu wa dunia yote na, kwa upande wa pili, al-Shabaab wako eneo la Somalia tu.

  • abdiazeez
    March 13, 2012 @ 01:18:06PM

    Ningependa kusema kuwa wanajidai ni Waislamu lakini ni wanafiki. Nashangaa wakati ninajua kuwa hamumwamini Mungu badala yake mnawaogopa Wamarekani na watu wa Ulaya. Lazima mfanyekazi ngumu ya kutenda haki ili mpate pepo ya Mwenyezi Mungu mbele ya safari na muondoe itikadi za Kimarekani katika akili zenu. Huu ni wakati tunaotarajia mfanyekazi sana na muwe watu wa Mungu katika kila kitu tunachofanya kuliko kutafuta raha za kidunia. Kwa hivyo ninawaomba muwaunge mkono wale wanaopigana kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu ya Kiislamu.

  • Abdullahi
    March 11, 2012 @ 09:28:53PM

    Athari za mauaji ya kiongozi wa Al-Qaida ni kutawanya shirika hilo, kwa sababu wao hufuata maelekezo kutoka kwa viongozi hawa. Wakati viongozi huuawa au hata kufungwa, basi ina maana kwamba kundi litachukua muda zaidi wa kujipanga wenyewe kwa mara nyingine tena, hivyo majeshi ya kupambana na hao uweza kuchukua faida ya machafuko ya kumaliza kundi hilo.

  • mohamed ciilqabe
    March 11, 2012 @ 09:21:10PM

    Wakati ilipodhihirika kuwa al-Shabaab wanafuata itikadi sawa na al-Qaeda. Usawa huu katika itikadi zao ulioneshwa na uhusiano wa karibu wa vikundi viwili hivi hadi kufikia hatua ya al-Shabaab kutangaza kuiunga mkono al-Qaeda na kupandisha bendera yao nchini Somalia. Ikiwa vikundi viwili hivi vitaachiwa kufurahia uhusiano huu wenye nguvu, kwa hivyo hakuna shaka kuwa siku za mbele Somalia itakuwa eneo salama la kujificha al-Qaeda. Ikiwa tutachambua zaidi usawa wao, tunaweza kusema moja kwa moja kuwa al-Qaeda ni kundi mama la al-Shabaab.

  • ahmedmatter
    March 11, 2012 @ 10:02:54AM

    Kwangu mimi inaonekana kuwa viongozi wa al-Shabaab wanataka kuwatia moyo askari wao na waogopewe na TFG na AMISOM, kwa hivyo tunatumai kuwa al-Shabaab watavunjwavunjwa.

  • Don
    March 10, 2012 @ 04:23:55PM

    Don, mtu mmoja mwenye hekima alisema…”Kitu pekee cha muhimu kwa uovu kushinda ni kwa mtu mwema kutofanya lolote. Ninashangazwa sana na jinsi gani mashehe na maimamu wamekuwa woga katika kukikataa kikundi hiki cha uovu ambacho kinayachafua mafunzo ya Kuran na kuutukana Uislamu kwa kueneza uovu. Wako wapi viongozi wakweli, imara na wanaoheshimika kusimama na kuwakataa? Au wao pia wanaogopa?” Au wako pamoja na hawa waovu kwa siri ambao wanawateka vijana wa kiume kinyume na hiari yao, kama LRA, kwenda kupigana kwa ajili yao. Faraji anatoa maoni mazuri ambayo yanapaswa kusomwa na kila mtu anayehusika. Waacheni watu wafuate akili zao. Waacheni watu wachague vipi wanataka kuabudu. Mwenyezi Mungu ni mkubwa wa kutosha wa kuamua na kusimamia shughuli Zake mwenyewe. Tafadhalini, mwacheni Yeye!

  • Ojukwu
    March 10, 2012 @ 06:01:33AM

    Mara moja Sulman Rushdie alichapisha kitabu kinaitwa “Aya za Shetani”, na karibu auliwe. Ni mafundisho ya aya kama hizo za Kuran ambazo zinawafanya watu vipofu na kuua watu wengine kwa jina la dini. Mungu ni upendo na daima hakuruhusu katika maamrisho yake binadamu mmoja kumuua mwengine kwa jina lake, daima; huyo hawezi kuwa Mungu. Ni shetani tu anayeweza kufanya hivyo. Ikiwa bado kuna watu wanaoamini mafundisho hayo ya chuki, mauaji n.k., kwa hivyo kaka na dada zetu mnamwabudu shetani bila ya kujua. Tafadhali kiruhusu kitabu hiki (Aya za Shetani) kichapishwe mtandaoni ili kaka na dada zetu waone nuru kwa kukisoma na waweze kujibainisha wenyewe na dini ya kweli ambapo watu wanaishi katika amani, mapenzi, umoja na udugu kwa kusaidiana katika kumwabudu MUNGU wa kweli wau upendo.

  • Saddam
    March 10, 2012 @ 03:58:58AM

    Nadhani huu ni ujanja tu wa kuongeza nguvu na kujenga hofu na hisia ya ujinga kwa majeshi ya Kenya na AMISOM pia kuwazuia kufanya kazi zao za kurejesha amani na utaratibu katika taifa kubwa la Somalia lisilofuata sheria. Lakini majeshi ya Kenya pamoja na washirika wao wamefikia pahali lazima wamkamate nyati pembe na Mwenyezi Mungu awape msaada wanaohitaji katika kutekeleza kazi hii, kwa sababu ni watoto na wanawake tu wa Somalia wanaoteseka katika mikono ya “al-Shabaab” wakatili.

  • sam maenda ong'ondi
    March 9, 2012 @ 12:56:15PM

    WAKATI UMEFIKA SASA KWA SOMALIA KUWA NA AMANI KAMILI BAADA YA KUWA TULIBOMOLEWA BOMOLEWA.

  • GEOFFREY
    March 9, 2012 @ 06:36:51AM

    Itikadi yao (al-Shabaab) sio kufika popote, ni upotezaji tu wa wakati, mali na maisha ya watu wasio na hatia, jambo ambalo halikubaliki kwa Mwenyezi Mungu ambaye wanamwamini.

  • jera
    March 9, 2012 @ 06:00:04AM

    Maoni yangu juu ya habari hii, mnapaswa kufikiri kabla ya kuamua kitu.......!

  • Sangaka
    March 9, 2012 @ 03:41:09AM

    Wapigeni kwa nguvu ng'ombe hawa. KDF endeleeni, endeleeni, bila woga.

  • anyona caleb
    March 9, 2012 @ 12:31:12AM

    Wacha watu wetu wasonge mbele

  • stephen wabuti
    March 8, 2012 @ 06:58:32AM

    Kwa mawazo yangu, ikiwa itawezekana, ulimwengu wote ungeangalia upya shughuli zote zinazofanywa na haya yanayoitwa “Madrasa”. Hii nchi ni kitovu cha ugaidi wa vichekesho. Viongozi wa Kiislamu ambao wako dhidi ya ugaidi lazima waamke na kuanzisha jumuiya ya kimataifa iliyokuwa haina ufisadi na wala kupendeleana ili kuangalia na kuthibitisha shughuli za misikiti. Makanisa nayo yasipuuzwe vilevile.

  • KEVIN
    March 8, 2012 @ 02:53:56AM

    AMANI ITALETWA NA MUNGU TU. WAKATI UMEFIKA TUNALIA KWA BWANA. SASA MPANGO ULE HAUKUFANIKIWA. JIUNGE NA MIMI.

  • peter
    March 7, 2012 @ 11:03:22PM

    Wanyama hawa wanaoitwa al-Shabaab na al-Qaeda wawaache watu wema wa Somalia kufaidi nchi yao pia wao wenyewe. Al-Shabaab ni kikundi kidogo tu. Unganeni na Wasomali wengine kujenga nchi yenu. Nguruwe wapumbavu.

  • Kimario Leons Ngalai
    March 7, 2012 @ 09:58:26AM

    Wanachama wote wa al-Shabaab lazima watimuliwe na jumuiya za kimataifa.

  • maxamed abdikariim
    March 7, 2012 @ 03:06:55AM

    Al-Shabaab ni umoja ambao uko nje ili kuitisha jamii na Uislamu haumaanishi ugaidi. Baadhi ya watu walifananisha woga wao kwa Al-Shabaab na ule wa kumwogopa Mwenyezi Mungu. Wanasali kutokana na woga wao kwa Al-Shabaab na hivyo ni vibaya kweli kweli.

  • lenny
    March 7, 2012 @ 02:36:49AM

    Hawa al-Shabaab si kwa ajili ya dini, ni kwa ajili ya watu wanaotaka kujitajirisha kutokana na vita hivi. Wanaelewa kuwa mara tu amani itkaporejea Somalia watakuwa hawana biashara. Wahalifu wa kweli wala hawako Somalia, wametuma watumishi wao kuwafanyia kazi chafu. Heshima kwa KDF, watawasafisha majambazi hawa kwa vyovyote itakavyokuwa. ENDELEENI KDF ENDELEENI, mnanifanya nijivunie kuwa Mkenya. Poteleeni mbali al-Shabaab! Poteleeni mbali al-Qeada.

  • faraji abasi
    March 7, 2012 @ 01:42:25AM

    Itikadi inayofuatwa na Al-Qaeda inatofautiana na kanuni na sheria halisi za Kiislamu. Kwa mfano, mauaji ya watu daima yamepigwa marufuku kwa Waislamu wote. Mtume mwenyewe (S.A.W.) alipendelea upunguzaji wa ufuasi wa njia ya Jihad; naye alishadidia kwamba mauaji hayawezi kuleta usafi. Uislamu ni dini ya amani, siyo dini ya vurugu. Mungu alishadidia jambo hili katika agizo lake la kwamba Waislamu washiriki katika mazungumzo badala ya kuwalazimisha wafuasi wa dini zingine kukubaliana nao. Kanuni halisi ya Uislamu inatambua mazungumzo na inaahidi thawabu mbinguni kwa wale wanaofuata mwenendo wa maafikiano. Aidha, Mtume (S.A.W.) hakushindilia mafunzo ya Uislamu kwa wale wasio Waislamu. Mbali na haya, Mtume (S.A.W.) aliwashangaza na kuwavutia wale wasio Waislamu kwa utulivu wake na mapendeleo yake ya amani. Yale mashirika ya siasa kali ya Kiislamu kama Al-Qaeda, yanayodai kufuata Uislamu wa Sunni, Sharia madhabuti na msimamo mkali wa Kiislamu, yanapendelea siasa kali. Yanatangaza na kueneza mafunzo bandia yanayoendeleza ugaidi kote duniani na kuonyesha picha ya Uislamu kama dini ya vurugu na ukatili.

  • paul kamau
    March 6, 2012 @ 08:59:03AM

    Nyinyi vijana hamko makini kuhusu kila kinachoendelea nchini Somalia wakati ambapo KDF imepata hasara kubwa lakini wanaficha ukweli. Sasa wanautaka Umoja wa Mataifa kuleta askari zaidi ili kuwasaidia, vinginevyo watasafishwa ndani ya muda mfupi sana.

  • paul
    March 6, 2012 @ 08:53:30AM

    Ni magaidi gani hawa unaowakusudia? Una maana kupigana na uvamizi wa nje ni sawa na ugaidi? Usiwe mpuuzi kijana, hawa Wasomali wanapigana kwa ajili ya nchi yao sawa na njia ile Wakikuyu walipigana kwa ajili ya ardhí yao katikati ya Kenya. Hawakuitwa magaidi bali Maumau, kwa hivyo suala kubwa ni lipi hapa? Ng’ombe mpumbavu.

  • yusuf ,Tanzani
    March 6, 2012 @ 02:42:36AM

    Samahani, mimi sizungumzi kuhusu al-Shabaab au kikundi cha Kiislamu, lakini hii ni habari kwa Waislamu wote duniani. Mwenyezi Mungu alisema hivi dhidi ya wale wasiokuwa Waislamu. Kwa nini, kwa sababu hawamwamini Mwenyezi Mungu. Watu wote wasiokuwa Waislamu wako dhidi ya Waislamu. Vipi tutakuwa marafiki wao wakati wao ni maadui kwetu? Tuache njia hii ya unafiki na tuwaambie ukweli. UN, UNHR wako dhidi ya Kurani na sheria ya Kiislamu, na walitulazimisha kufuata katiba iliyotungwa na mwanadamu. Sisi hatukuumbwa na mwanadamu bali tumeumbwa na Mwenyezi Mungu, lazima tufuate sheria yake ambayo ni Kurani.

  • moses sonko
    March 5, 2012 @ 08:17:33AM

    Vyovyote watakavyojaribu itathibitika kuwa wamefeli kabisa kwa sababu hawajui wamejichanganya na nani.

  • flora
    March 5, 2012 @ 05:38:37AM

    Hiki ni kikundi cha wanamgambo ambacho lazima kiondoshwe.

  • nicholas tukero
    March 5, 2012 @ 12:57:30AM

    Hawa watu wapuuzi wasiokuwa na kazi lazima watafutwe kabla hawajasafishwa.

  • ALFA
    March 4, 2012 @ 01:44:26PM

    WAPIGENI KWA NGUVU…HATA WAJIITE JINA GANI…

  • SHEBA
    March 4, 2012 @ 11:17:59AM

    Kinachoendelea Somalia si vita baina ya Waislamu dhidi ya wavamizi Wakristo, bali ni kitendo cha mataifa jirani, yanayotishwa na mashambulizi ya vurugu za ugaidi wa kimataifa. Mantiki ya suala hili linahusiana na: ikiwa tutakalia makalio yetu, silaha za kutisha ambazo zinatandazwa na vyombo vya Marekani, maslahi ya Israili na Ndege za Abiria karibuni sana na wala sio mbali zitatufika na kutuaibisha kwa kuchanganya damu zetu na za mama na watoto wetu. Kwa hivyo, kwa nini tusikutane na watu wasiofaa katika jamii wanaotafuna bangi (au chochote kila kinaweza kumfanya mtu mzima kujilipuwa mbele ya wanawake na watoto? Dawa za kulevya: basi) nje uwanjani. Wanatumia jina la dini katika mchezo kwa sababu jambo la kwanza, ufahamu wa akili zao juu ya Mungu katika utakatifu wa maisha ni ajinabi kwao.

  • Kenneth kiruai
    March 4, 2012 @ 07:53:01AM

    Hicho kitu kinachoitwa al-Shabaab kitashughulikiwa ipasavyo pale tu watakapozibiwa njia zao za kujipatia mapato.

  • abdirahman
    March 4, 2012 @ 05:41:45AM

    Kwa maoni yangu, kushuka kwa ushawishi wa al-Shabaab kulianza kabla ya tangazo la al-Zawahiri la kujiunga kwa al-Shabaab katika mtandao mkubwa wa al-Qaeda. Hili linaweza kuwapandisha ari kidogo, lakini hakuwezi kubadilisha ukweli kuwa nyota ya al-Shabaab imezimika na lugha yao tamu ya dini sasa haifai tena. Hata hivyo, kubadilisha huku kwa mikakati na mbinu kunakofanywa na al-Shabaab na kushuka kwa thamani kwao katika nyanja za umma hakuna maana kuwa watapotea, kwa usiku mmoja, katika uwanja wa siasa za Somalia, kinyume chake, wataunda mabomu yao ya kiuaji na kuanza operesheni za kupiga na kukimbia katika sehemu za kitaifa isipokuwa, vya Serikali ya Mpito ya Shirikisho ianzishe vyombo vya kiintelijensia na usalama vinavoweza kubaini mashambulizi ya siku za mbele ya al-Shabaab.

  • eliteelite
    March 3, 2012 @ 08:24:51AM

    Al-Shabaab inapawsa kusisitisha upuuzi wao

  • omo
    March 3, 2012 @ 05:41:43AM

    Mateke ya mwisho ya farasi anayekata roho............

  • FREDRICK WANYONYI
    March 3, 2012 @ 05:04:02AM

    Fikiria vikundi vya wanamgambo wa al-Shabaab na al-Qaeda, tayari wamesababisha mateso kwa raia wa Somalia, wakiwemo watoto, vijana na wazee, fikiria watu wa Somalia wanaokufa kwa njaa wakati wakikimbia vikundi hivi, ooooh Mungu wetu wa peponi, wahurumie akina kaka na dada zetu wa Somalia ili siku moja waweze kufaidi amani katika nchi yao wenyewe. Tungependa kuona watoto wanaenda shule na wanaume na wanawake wanafanya shughuli zao katika nchi yao. Wakimbizi wote wanaoishi nchini Kenya waweze kurejea nchini kwao kwa sherehe, kwa shangwe na furaha. Mungu rejesha amani Somalia, watu wako wameishateseka sana katika mikono ya wahalifu wa kimataifa. Ooooh YESU, wewe ni mponyaji na mwenye huruma!!!!!!! Mwana Mfalme wa AMANI!!! AMEN.

  • kennedy chesoni
    March 2, 2012 @ 07:38:50AM

    Kila kitu kina muda wake na kule muda unapita na kufanikiwa kwa wengine.

  • david kyalo
    March 2, 2012 @ 07:34:31AM

    Jina lolote watakalojiita, tunawatwanga!!

  • Muema Al muthui
    March 1, 2012 @ 03:09:20PM

    Hii haiongezi chochote. Ushirika wa al-Shabaab na al-Qaeda umekuwepo kwa muda mrefu na unajulikana.

  • kipyegon koech wesley
    March 1, 2012 @ 08:27:56AM

    Hizi habari mpya ni kabambe, Ahsante.

  • Elder john Ogando
    March 1, 2012 @ 12:09:00AM

    Tunasali ili kurejeshwa amani Somalia. Kuingilia kati kwa Mungu kutavifanya vikundi vyote kuweka silaha zao chini na kudai amani. Shetani ashindwe kwa jina la Bwana wetu.

  • munyasia
    February 29, 2012 @ 11:29:46PM

    Vitendo vya hivi karibuni vilivyofanywa na al-Shabaab vinamaanisha mateke ya mwisho ya farasi anayekufa na karibuni wataadhibishwa ili kuwajibika maovu yao.

  • ok
    February 26, 2012 @ 02:50:52PM

    Yote ni kweli

  • Hassan Ibrahim
    February 26, 2012 @ 01:47:20AM

    Wale wanaoshikilia itikadi za msimamo mkali wanaamini kwamba al-Shabaab wanasababisha matatizo ndani ya Somalia, hata hivyo, kuna sheria kali na zisizokubalika zilizowekwa na wengine. Al-Shabaab ni kikundi cha kweli cha Kiislamu ambacho kinapewa tafsiri mbaya ya dini ya Kiislamu na tatizo sio kutokuwa na uweledi kuhusu Uislamu na kutofahamu ujumbe wa Kiislamu. Watu wanasema vibaya juu ya al-Shabaab kwa sababu (watu) wao hawaifahamu vyema dini. Al-Shabaab wako sahihi kwa mujibu wa dini ya Kiislamu na kila Muislamu anatarajiwa afanye hivyohivyo kwa ajili ya dini. Waislamu wanaacha dini yao kwa kushabikia itikadi za kigeni zilizopandikizwa kwao na watu wasioamini.

  • Halimo Harbi
    February 25, 2012 @ 03:04:49AM

    Al-Shabaab na al-Qaeda wanauhusiano wa karibu sana. Al-Shabaab wameonesha wazi kuwa ni tawi la al-Qaeda. Kuuliwa kwa kiongozi wa al-Qaeda kulikuwa na taathira kubwa kwa al-Shabaab. Kuuliwa kwa kiongozi wa al-Qaeda kumepelekea uamuzi wa kuua wafanyakazi wa mashirika ya misaada na askari wa misheni ya kulinda amani waliopelekwa Somalia. Al-Shabaab vilevile wametaja malengo mengine ni kulipiza kisasi kwa kuuliwa kwa viongozi wa al-Qaeda katika maeneo ya milimani Pakistani. Vilevile hii inaonesha kuwa kulikuwa na vitisho kwa maisha ya bibi yake Obama mwezi Mei mwaka jana. Bibi yake Obama anayeishi Kenya vilevile aitishiwa na al-Shabaab baada ya kuuliwa kwa Osama huko Abbottabad Pakistani. Kulikuwa na kilio cha haraka kwa usalama katika mji wake. Ni muhimu kwa al-Shabaab wawepo chini ya viongozi wa serikali ili kusitisha vitisho vyao kwa raia wa Somalia au wananchi nyingine. Majaribio yoyote lazima yafanyike ili kuhakikisha kuwa al-Shabaab hawawezi kuendesha vitisho vyao popote ulimwenguni vya kulipiza kisasi kutokana na mauaji ya Osama.

  • yasmin said elemanih
    February 21, 2012 @ 03:20:57AM

    Nzuri sana

  • pwk
    February 20, 2012 @ 09:22:43AM

    Wote Al-Qaeda na Al-Shabaab ni genge la wahalifu wenye kiu ya damu wanaofurahi katika kueneza machungu na huzuni kwa watu wao wenyewe. Haiaminiki kwamba mtu kwa jina la Mungu atalichukulia hii kuwa ni kazi ya kidini kuua watu wasio na hatia. Ni Mungu gani huyu anayefurahia damu ya wanawake na watoto wasio na hatia, na bado mnatutaka tuwafuate? Tafadhali, tunaweza kutumia akili zetu na kubadilisha hii imani ya kiajabu. wahome

  • hanad maxamed
    February 19, 2012 @ 06:25:53AM

    Amani iwe juu yenu. Kwanza, ikiwa nitazungumzia juu ya umoja baina ya vikundi viwili vya Kiislamu; Harakat al-Shabaab al-Mujahideen na Al-Qaeda, hii ni habari ya kukaribishwa. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, kama ningekuweko Somalia, ningeungana nao lakini kwa bahati mbaya hivi sasa ninaishi katika mji mkuu wa Sweden. Ninawatakia Al-Shabaab wadumu milele na daima hawataanguka.

  • Robert
    February 18, 2012 @ 07:18:10AM

    Al-Shabaab wanafikiri kwa kuungana kwao na Al-Qaeda kutawafanya wawe imara. Mimi nafikiri watakuwa dhaifu zaidi na zaidi kutokana na muungano wao huu. Vilevile, muungano wao ni ishara ya kushindwa kwao na inachoonesha tu ni kuwa walishagundua kuwa hawana matumaini yoyote ili kuweza kuishi huko mbeleni katika jamii ya sasa ya Somalia.

  • ernest fred
    February 18, 2012 @ 04:59:06AM

    KARIBUNI HIVI TUTAIKAMATA KISMAYU NA IKIFANYIKA HIYO TUTAWAONA WAKIANGUKA

  • wanjosh
    February 18, 2012 @ 03:44:23AM

    Al-Shabaab, Al-Qaeda au vyovyote wawavyo, ni vikundi vilivyoundwa na baadhi ya watu, sio na Mungu au dini katika nyoyo zao, bali makusudi ya kibinafsi kabisa. Kurubuni akili dhaifu kumekuwepo kwa muda mrefu ambapo makusudi ya ubinafsi yanafungwafungwa katika lugha tamu fasaha za kulinda "nchi", "dini", "mbari", "kabila" yetu n.k. Watu wengi hatia hupoteza maisha yao bila ya kuwa na hatia yoyote wakati wale walioanzisha wanafaidi ngawira. Katika kikundi cha al-Shabaab, tunaona kundi la vijana masikini likiongozwa na baadhi ya walokole wa "dini" wanaoanzisha vita dhidi ya watu wasio na hatia. Imedhirika kwa wale wanaoweza kuona kwa nyuma ya pazia kuwa vtendo kama hivi havina uhusiano wowote na dini. Jukumu kubwa la Waingereza (raia, sio serikali)wamekuwa wakichukulia vita dhidi ya al-Shabaab kumekuwa suala la kushangaza. Kifurushi cha milipuko kilichoonekana ndani ya nyumba ya mwanamke Muingereza huko Mombasa vilevile kimezua maswali mengi yasiyopata jibu. Waafrika tunapaswa kufumbua macho yetu. Nchi za Magharibi taratibu zimeanza kupoteza mashiko yake katika bara hili na tunaweza kufanya chochote ili kubakisha umuhimu wake. Hii ni pamoja na kurudi nyuma katika mbinu zake za kizamani za kusababisha migongano pale inapobidi.

  • Sabasi omaoro
    February 18, 2012 @ 03:23:42AM

    Vikosi vya kimataifa vinavyopambana na al-Qaeda vingefungua sehemu Somalia na kutenga rasilimali zaidi ili kuviunga mkono vikosi vya AMISOM, TFG na Kenya ili kuwapiga magaidi.

  • Ayanna
    February 16, 2012 @ 11:14:48AM

    Habari zinazoihusu Somalia zinaweza kuwachanganya watu kwa sababu ya matumizi ya maneno tofauti ili kuelezea aina mbalimbali za migogoro ambayo inatokea hapa. Hii inaendelezwa na Serikali ya Mpito ya Shirikisho na Umoja wa Mahakama za Kiislamu. Vita hivi baina ya makundi mengine na historia za nyuma, mabwana wa vita, nchi majirani, Marekani na wageni wengine walio nyuma ya vita vitakatifu. Marekani inauchukulia Umoja wa Mahakama za Kiislamu kama magaidi kwa sababu ni wasaliti, na kutokana na hili, habari za Marekani kuhusu yale yanayotokea Somalia zinatilia mkazo zaidi katika kupinga ugaidi.

  • Bado
    February 16, 2012 @ 11:05:47AM

    Mashirika ya kiutu yamejaribu juu chini kukomesha kundi la wanamgambo la Al-Shabaab. Wameungana na Serikali ya Shirikisho ya Somalia kupambana na hili kundi la wanamgambo waasi ili kudumisha amani. Muungano wa Afrika umetuma walinzi wa amani elfu sita wa dharura mara moja kuokoa maisha na mali nchini Somalia. Makundi yaliyo dhidi ya Al-Shabaab yameunga mkono serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Somalia kupambana na hawa waasi. Mojawapo wa vikundi vinavyounga serikali mkono ni Hizbul Islam. Hili ni kundi la wanamgambo lenye nguvu lililo tayari kujitolea kupa nchi yao msaada wa kiutu. Wamejitolea kukabiliana na hili jeshi haramu na kumaliza ugomvi na kurejesha usalama kwa watu wa Somalia.

  • omoke1
    February 16, 2012 @ 07:51:57AM

    Al-Shabaab wana vikundi ambavyo havimtambui Mungu na ni vya kishetani kwa hivyo haviwezi kudumu sawa na Al-Qaeda. Wote ni magaidi na wauaji wa wananchi wasio na hatia na Mungu hataki hivyo, kwa hivyo lazima watakufa/watamalizika. NCHI ZOTE ZINAZOMWOGOPA MUNGU UNGANENI NA KUSAIDIANA MPAKA TUWAMALIZE al-Shabaab/al-Qaeda. MUNGU AWABARIKI WOTE.

  • Adimu
    February 15, 2012 @ 01:22:31PM

    Tanzania, kama mojawapo ya nchi zilizo karibu na Somalia, ina wasiwasi juu ya usalama wake kutokana na kundi la wanamgambo la Al-Shabaab. Wakimbizi wengi kutoka Somalia walihamia nchini humo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Somalia. Tisho la Al-Shabaab limepanda tangu viongozi wa wanamgambo hao watishe vita dhidi ya wale watakaojaribu kuingilia kati. Kutokana na tukio hilo kuna wasiwasi kuhusu usalama wa watu, nchi na mali. Hakuna ajuaye ni lini au wapi ambapo waasi wa Al-Shabaab watavamia. Jambo hili limewabidi walinda usalama kuwa macho na kusimama imara wakati wowote. Wakifanya hivi, watapunguza tisho la Al-Shabaab na, hatimaye, watafaulu dhidi ya maadui wao.

  • abdul shire
    February 15, 2012 @ 12:38:59PM

    Kama kawaida, ni kikundi cha vijana kinachotumia dini kama pumbazo, wenye wazimu wa madaraka na katika mtindo wa kijambazi. Katika historia yote, kulikuwepo vikundi vya vijana kama hiki vyenye asili tofauti za kidini na kilikuwa na sifa kama hizi, kwa hivyo, hiki hasa hakiwezi kutenganishwa na Waislamu. Miaka michache iliyopita, Wakristo walikuwa wamezoea kuua wanawake hasa wale waliokuwa wanashutumiwa kwa jicho baya (uchawi) au waliogundulika kujihusisha na tabia chafu, aina zote hizi za uhalifu zilikuwa zinatendwa kwa kisingizio cha dini. Ni bahati mbaya kuwa katika karne ya 21, vikundi vidogo vya wajinga kutekeleza vitendo vya kinyama katika hali ileile lakini vyombo vya habari ulimwenguni vinavyopuuza kabisa 24/7.

  • emmanuel wanyama
    February 15, 2012 @ 07:28:26AM

    Nimependa hii

  • Edwin Oduor
    February 15, 2012 @ 07:12:25AM

    Bila ya shaka kuungana na magaidi hakutawasaidia al-Shabaab kwa sababu hawana umaarufu miongoni mwa umma wenyeji wa Somalia.

  • osman E. Awaleh
    February 15, 2012 @ 03:13:08AM

    Somalia ni kama keki iliyokwishaokwa na kila mtu anataka kuchukua kipande chake. Sio tu kwa nchi za Ukanda huu bali pia al-Qaeda. Vikundi vyote hivi vinavyogombana vinaathiriwa na misingi ya kikabila, isipokuwa wachache wanaounga mkono itikadi ya kimataifa ya al-Qaeda, na hawa bila ya shaka watashindwa, kwa sababu hawana msingi wa kuungwa mkono na makabila au hata maoni ya watu walio wengi ndani ya al-Shabaab kama vile Dhahir Aweiys na viongozi wengine wenyeji. Kwa hivyo, Muungano wa al-Shabaab na al-Qaeda hauna faida yoyote.

  • peter mburu
    February 15, 2012 @ 01:53:49AM

    Kila mmoja lazima apinge vitendo vya vurugu vya al-Shabaab bila ya kujali dini yake. Vita dhidi ya ugaidi lazima vienee pande zote ili kuwa na dunia isiyokuwa na magaidi,,,,

  • Mohamed Jama Ibrahim
    February 14, 2012 @ 08:29:51AM

    Makala haya ni maoni tu, lakini tunapaswa kujiuliza sisi wenyewe ni kitu gani kitazuka kutokana na muungano walioutangaza. Kwa maoni yangu ni kuwa hii italeta faida kubwa kwa Al-Shabaab ambao watapata mafunzo, jeshi na fedha kutoka kwa Al-Qaeda Mkuu. Hii pia ni kuvunja moyo hali ya balaa na ukosefu wa haki kwa washirika. Sijui kuhusu wale waliosema baadhi ya maelezo katika makala, lakini wanasahau au wanakataa kuwa watu wa Somalia ni asilimia 100 Waislamu na kamwe hawatakubali kutawaliwa na Ukristo ulioletwa na vibaraka weusi wa Wakristo weupe ili kutawala watu Waislamu popote walipo. Kwa mtazamo wa kijeshi, muungano huu [wa al-Qaeda na al-Shabaab] utakuwa nguvu zitakazoshinda Wakristo na washirika wao katika Pembe ya Afrika. Ni ushindi kwa Waislamu, na kushindwa kwa hasara kwa Wakristo na jamaa zao. Shukurani kwa Mwenyezi Mungu.

  • Feynuus
    February 14, 2012 @ 05:57:49AM

    Wanamgambo wa Somalia walikuwa tawi la Umoja wa Mahakama za Kiislamu. Uliundwa ili kupigana dhidi ya Ethiopia na Serikali ya mpito ya Somalia. Mahubiri yao yanazungumzia juu ya jihadi ya kimataifa. Walisema hawana uhusiano na al-Qaeda. Ni viongozi ndio wanataja dhamiri yao ya kuunda serikali imara ya Kiislamu inayofuata Sharia; serikali ambayo iko huru na isiyovunja moyo, ambayo ingeweza kutafsiriwa hivyo na Waethiopia au Wamarekani. Al-Shabaab waliwashambulia raia wa Somalia na waliamini kuwa watu hawako wakweli katika kufuata mila za Kiislamu.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo