Kikundi cha Mawasiliano cha Kimataifa Somalia kusifu maendeleo

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Februari 08, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wachambuzi wa kisiasa na viongozi wa jumuiya za kiraia wa Somalia waliyakaribisha mapendekezo ya Kikundi cha Mawasiliano cha Kimataifa Somalia, ambacho kililaani vurugu za al-Shabaab na kutoa wito kwa vyama vya kisiasa kusuluhisha tofauti zao.

  • Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa Somalia ya UN, Augustine Mahiga (kulia), aliwa na Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari huko Mogadishu tarehe 24 Januari [Na Stuart Price/AU-UN IST/ Shirika la Habari la AFP]

    Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa Somalia ya UN, Augustine Mahiga (kulia), aliwa na Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari huko Mogadishu tarehe 24 Januari [Na Stuart Price/AU-UN IST/ Shirika la Habari la AFP]

Wakati wa mkutano wake wa mwisho, kilichofanyika Jibuti tarehe 6-7 Febuari, Kikundi cha Mawasiliano kilisifu mafanikio ya kijeshi ya hivi karibuni ya Misheni ya Umoja wa Afrika ya Somalia (AMISOM), vikosi vya serikali ya Somalia na washirika wao dhidi ya kikundi cha al-Shabaab.

Kikundi cha Kimataifa cha Mawasiliano Somalia vilevile kilitoa wito kwa kumaliza kwa kipindi cha mpito Somalia kama ilivyopangwa mwezi wa Agosti. Kilitoa wito wa kutatuliwa kwa matatizo ya kisiasa katika Bunge la Somalia, na kuvitaka vyama vya kisiasa vya Somalia na viongozi kupanua majadiliano ili kuruhusu maamuzi ya kisiasa ya baadaye kukusanya msaada kadiri inavyowezekana.

Kikundi kilisema Mkutano wa London kuhusu Somalia hapo tarehe 23 Febuari ni fursa ya kuzingatia jitihada juu ya amani na utulivu huko Somalia.

“Tunashuhudia maslahi ya kimataifa na ya kikanda katika suala la Somalia baada ya kipindi kirefu cha kutojali wakati ulitakiwa kutafuta suluhisho kwa mzozo wa Somalia,” alisema mchambuzi wa kisiasa Abdul Razaq Ali.

Ali alitoa wito kwa kutekelezwa kwa haraka mapendekezo ya Kikundi cha Mawasiliano. Alsema mkutano wa London na Mkutano wa mwezi Juni huko Istanbul unafaa kwa jitihada za kuongeza faida na kujitayarisha kwa mwisho wa kipindi cha mpito.

Ni wajibu wa Wasomali, kwa kuelekea uhamasishaji huu wa kimataifa na ni maslahi kwao kuchangamkia fursa hii ya sasa,” aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi.

“Maslahi ya kimataifa katika suala la Somalia ni mahitaji, sio utashi, kwa sababu ya kutokuwepo kwa usalama Somalia kunageuka kuwa tishio sio tu kwa Somalia, bali kwa nchi zilizopo katika eneo hili na vilevile ni tishio kwa amani na uslama wa kimataifa,” Ali alisema. “Uharamia na ugaidi upo na inahitajika kutafuta suluhisho la hali ya kutokuwepo kwa usalama katika nchi.”

Naye Tahir Hussain, msaidizi wa mkuu wa kitivo cha sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Mogadishu, aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi, “Somalia sasa iko katika njia panda wakati inapomaliza Mpango na kukabidhi madaraka ya kisiasa kwa fani, na kumalizika kipindi cha mpito.”

“Kutokana na migawanyiko na migogoro ya sasa katika bunge la Somalia, bila ya kusahau hali ya kutokuwepo kwa serikali iliyoungana na taasisi imara za serikali, itakuwa vigumu kutekeleza jukumu kuu [za lazima kwa] utekelezaji wa Mpango,” alisema.

Mchambuzi wa kisiasa Abdul Wahab Ahmed alisema hatua inayofuata itakuwa muhimu sana katika vipengele vya hatima ya kisiasa ya nchi. Alisema mabadiliko makubwa yatatokea kabla ya mwezi wa Agosti, kama vile kuandika katiba mpya ambayo itamaliza kipindi cha mpito na kuwezesha ukabidhianaji wa madaraka.

“Sasa Somalia inapita katika hatua mpya na matumaini kwa hatima ya watu wa Somalia ni makubwa,” Ahmed aliuambia mtandao wa habari wa Sababhi. “Viongozi wa Somalia lazima waelewe umuhimu wa hali ya sasa ili waweze kuiongoza nchi kutoka katika kikwazo [iliyomo sasa] na kuendelea na mpito wa kisiasa ambao utapelekea kufikia mwisho wa kipindi cha mpito.”

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari wa Somalia Mohammed Ibrahim alikaribisha Kikundi cha Mawasiliano kulaaniwa kwa vurugu na kukua kwa mashambulizi dhidi ya waandishi na taasisi za habari nchini Somalia. Alisema hii inaonesha kukua kwa mwamko wa jumuiya ya kimataifa na viongozi wa Somalia juu ya hatari zinazowakabili waandishi wa habari wa Somalia.

"Kwa mara ya kwanza, Kikundi cha Mawasiliano cha Kimataifa kilichukua msimamo imara kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari na hatari zinazovikabili vyombo vya habari," Ibrahim aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi. “Kikundi vilevile kililaani vikali sana aina zote za vurugu na ugaidi unaofanyiwa waandishi wa habari wa Somalia na taasisi za habari na kuwataka viongozi kuacha kuwasamehe na badala yake kuwashitaki wale wanahusika na uhalifu.”

Katika mwisho wa taarifa yake, Kikundi cha Mawasiliano kiliwataka al-Shabaab na vikundi vyote vyenye misimamo mikali nchini kuachana na vurugu na kujiunga na mchakato wa kuleta amani. Vilevile Kikundi kiliwataka wafadhili kuiunga mkono AMISOM na kusaidia kuimarisha uwezo wa vikosi vya Serikali ya Mpito ya Somalia.

Vilevile kikundi kilikaribisha kufunguliwa kwa Ofisi ya Kisiasa ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia huko Mogadishu na kuelezea matumaini yake kwamba mashirika mengine wabia watafuata mfano na kufungua ofisi zao nchini.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo