Januari 31, 2012
Uharamia wa Somalia umeharibu sana hali za kiuchumi na kijamii katika eneo hilo, hasa katika shughuli za biashara kwenye bandari ya Berbera, maafisa wa ubaharia na biashara wameeleza.
Naibu Mweneyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Somalia Mohamed Shukri Jama alibainisha njia mbili ambazo biashara imeathiriwa bandarini.
“Kwanza, kiasi cha shehena kimeongezeka sana. Kwa mfano, bei katika bandari ya Berbera ni mara mbili zaidi kuliko za Jibuti,” aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi. “Pili, meli kubwa za kuaminika hazitaki au zinasita kusafirisha bidhaa kupeleka bandari ya Berbera; na ikiwa moja itaonekana, bei wanazotaka ni kubwa zaidi kuliko huko nyuma.”
“Vipengele viwili hivyo vinatoa changamoto kwa bidhaa za walaji zinazoingia katika bandari ya Berbera kuwa za ushindani sana kwenye soko,” Jama alisema. “Hivi sasa, kuna wasafirishaji wawili wa Somaliland ambao mzigo wao wa saruji zimekwama Pakistani kwa miezi mitano iliyopita kwa sababu hawajaweza kuusafirisha [mzigo] kuuleta Berbera.”
Yusuf Ismail Ali, mkuu wa Wakala wa Ubaharia wa Tawfiq na wakala wa meli zinazotia gati katika bandari ya Berbera, alisema tatizo jingine ni kuwa meli za mizigo zinazotokea Dubai, Kuwait na Oman zinaweza kuwa katika hatari kubwa kwa uharamia, hasa wakati huu ambapo maharamia wameenea hadi bahari za kimataifa.
Alisema kuongezeka kwa kiasi cha shehena kumepunguza idadi ya meli zinazotaka kusafirisha mizigo huko Berbera, hasa zile za kutoka Brazil, India na Bangladesh zinazosafirisha sukari na mchele.
“Kwa sababu ya kuongezeka kwa bima, meli za mizigo zimepandisha kiasi cha shehena, kwa hivyo mzigo wa tani 14 zilizokuwa zinasafirishwa kwa meli moja sasa zinasafirishwa kwa kutumia boti ndogo 14, jambo ambalo hupandisha kiasi cha usafirishaji,” Ali aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi.
Naibu Mweneyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Somalia alielezea namna gani gharama za uharamia zinawagusa walaji.
“Wafanyabiashara wataongeza katika bidhaa gharama za matumizi, halafu juu hapo kuongeza faida halisi,” Jama alisema. “Kwa hivyo, kuongezeka kwa gharama za usafirishaji kumekuwa na athari kubwa kwa bei katika soko, hasa kutokana na kiasi hicho.”
Ongezeko kubwa katika bandari ya Berbera, ambayo ni bandari kubwa zaidi kaskazini mwa Somalia, zinaonekana katika sehemu zote za uchumi wa Somaliland.
“Kodi zinazotozwa katika bandari ni chanzo kikuu cha mapato kwa serikali na zinaathiri bajeti ya mwaka ya matumizi. Kila wakati ambapo bidhaa zinazotozwa kodi zinapoongezeka, vilevile mapato ya serikali huongezeka. Kinyume chake, kila ambapo bidhaa zinazotozwa kodi zinapopungua, mapato ya serikali vilevile hupungua,” Jama alisema.
Biashara pia zinahisi maumivu ya kupungua kwa mahitaji ya walaji na kupungua kwa bidhaa kutokana na bei kubwa sana za bidhaa, Jama alisema, na kuongeza kuwa taathira za uharamia kwa uchumi ni nyingi na “tatizo kubwa”.
Fatima Hussein, ambaye ana duka la bidhaa huko Hargesia, alisema yeye na wateja wake wanahisi taathira za kupanda kwa bei.
“Wateja wanalalamika kila mara bei za bidhaa zinapopanda, na wengine wanaondoka na hawataki kurejea tena kwa sababu hawawezi tena kuzimudu na inakuwa ngumu kununua bidhaa,” alisema.
Alisema baadhi ya bidhaa zilizokuwa zinauzwa ndani ya miezi mitatu sasa zinabaki katika mashubaka kwa miezi tisa au zaidi.
Somaliland imekuwa ikilenga katika juhudi za kuzuwia shughuli za uharamia kwa kuendesha na kuhukumu kesi za uharamia wenyewe. Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Sahil Osman Ibrahim Dahir aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi kuwa tangu mwaka 2008, viongozi wameishaendesha kesi 80 za uharamia.
Ripoti ya karibuni kutoka Shirika la Bahari la Kimataifa liligundua kuwa kesi za jumla za uharamia katika bandari za Somalia ziliongezeka kutoka 219 mwaka 2010 hadi 237 mwaka 2011, hata hivyo idadi ya utekaji nyara uliofanikiwa imepungua kutoka 49 hadi 28, kwa sehemu kubwa kutokana na juhudi za vikosi vya kimataifa vya usalama.
Hakuna bandari nyingine iliyoathiriwa vibaya sana na uharamia kuliko bandari ya Berbera, alisema naibu mkaguzi wa bandari ya Berbera Omar Abokor Jama.
“Tunacho kikosi imara sana cha bandari kinachofanya doria katika mwambao wetu, kuilinda dhidi ya shughuli za kiharamia zenye dhamiri ya kuzizuwia meli,” aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi. “Hakuna hata meli moja inayoelekea bandari ya Berbera iliyotekwa bado, isipokuwa MV Juba XX, iliyokuwa inasafirisha mzigo wa mafuta kwa ajili ya shirika la mafuta la Red Sea Petroleum. Ilitekwa nyara kando ya mwambao wetu, na ilipopelekwa Bossaso, tulifanya makubaliano ya kuachiliwa kwake kupitia mbinu za kijadi za Kisomali, kwa sababu Wasomali hawawezi kuwekana mateka kwa sababu ya kuheshimiwa kwa mila za Kisomali.”
Mkaguzi wa bandari alisema vikosi vya bandari vya Somalia haviongozi meli, bali hutumia mfumo wa rada kudhibiti mzunguko wa maili 90 za mwambao.
Afisa wa Chama cha Wafanyabiashara alisema jumuiya ya kimataifa lazima ione kila Berbera inachofanya ili kulinda mwambao na kuutofautisha na bandari nyingine za Somalia. Alisema meli zinapaswa kuhamasishwa kuleta bidhaa katika bandari ya Berbera.
“Ikiwa meli zingekuwa zinatekwa nyara na kufunga gati kando ya mwambao wetu, ikiwa tungekuwa tunatoa usalama na kuwaficha maharamia, kwa hivyo tungechukuliwa kama sawa na Somalia, vyenginevyo tusichukuliwe sawa na wao,” Jama alisema.
Somaliland inatayarisha sheria dhidi ya uharamia inayopanga kuwahukumu maharamia bila ya kuangalia utaifa wao, ikiwa pamoja na wale wanaojihusisha na kuupatia fedha uharamia.
“Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Madawa na Uhaini (UNODC) inaunga mkono sheria hii na imesaidia Wizara ya Sheria [ya Somaliland] katika kuandaa muswada,” mwakilishi wa UNODC wa Somaliland Mohamoud Abokor aliuambia mtandao wa habari wa Sabahi.
Abokor alisema sheria dhidi ya uharamia, ambayo iansubiri kupitishwa na bunge, inaeleza kuwa maharamia wawekwe jela zilizojengwa kwa ajili ya wafungwa kutumikia vifungo vya muda mrefu.
Alisema programu za kuwarejesha katika hali ya kawaida, kutoa ushauri nasaha, mafunzo ya amali na programu za elimu rasmi zinatolewa kwa matumaini kwamba baada ya kumaliza vifungo, maharamia wawe ni watu wenye mchango kwa jamii.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Uharamia ni shughuli ambao hauwezi kusimamishwa. Nakusudia kusema kuwa hakuna mtu anayeweza kuzuwia mlo wa mtu mwengine.
Al-Shabaab wanaendesha mashambulizi ya mauaji na uhalifu ndani ya Somalia. Uhalifu huo ni pamoja na kuteka nyara meli katika bahari ya Hindi, kuua watu wasio na hatia na kushambulia mataifa jirani yenye amani kama vile Kenya na Uganda. Uhalifu huu unaweza kuainishwa kuwa dhidi ya ubinadamu na unalaani. Uhalifu huu unatendwa dhidi ya watu wa Somalia na serikali ya mpito. Magaidi wanataka wapewe haki za kisiasa na sauti katika vipi serikali inaendeshwa wakati kuna sera ya kimataifa ambayo serikali haiwezi kujadiliana na magaidi kwa hiyo wanawapiga watu wasio na hatia. Hii siyo sawa na kikundi cha magaidi kinakosea sana. Kitu ambacho wanapaswa kufanya ni kujaribu majadiliano kwa njia ya amani na kuacha kushawishiwa na watu wa nje ambao wana sababu zako kando.