Januari 17, 2012
Viongozi wa Puntland wako katika tahadhari ya hali ya juu kufuatia taarifa kuwa al-Shabaab, wanaokimbia magharibi na kusini ya Somalia, wanakusudia kujikusanya huko Puntland, maafisa wa serikali walisema.
Maafisa wanakilaumu kikundi chenye uhusiano na al-Qaeda kwa mauaji ya Dk. Ahmed Haji Abdirahman, mwanazuoni mkuu wa Kiislamu Somalia, mwezi uliopita. Kufuatia mauaji hayo, wanazuoni wengi wa kidini, viongozi wa kikabila na maafisa wa serikali wamezungumzia dhidi ya mafunzo ya siasa kali ya al-Shaabab.
Katika hotuba yake ya kutimiza miaka mitatu ofisini hapo tarehe 8 Januari, Raisi Abdirahman Sheikh Mohamed Faroole aliwalaumu “wageni wanaoivamia Somalia” kwa vita na msimamo mkali unaoikumba Somalia. Alimshambulia Ahmed Abdi Godane kiongozi wa kiimani wa al-Shabaab huko Somalia, kwa kuwa wakala wao. Godane amejaribu kutawala Somalia kwa “kuua watu mashuhuri na kuwapa silaha wauwaji”, wauwaji hao hao ambao walimuua Abdirahman mwezi uliopita, alisema Faroole.
Abdirahman alipigwa risasi mara saba na watu wenye silaha huko Bossaso hapo tarehe 5 Disemba wakati alipokuwa anatoka msikitini karibu na nyumba yake baada ya swala ya asubuhi.
Faroole alisema kuwa viongozi wa al-Shabaab wanatoa rushwa, wanawanyonya na kuwatia kasumba vijana wenye kuweza kudhuriwa zaidi ili wafanye mauaji. Hata hivyo, hivi sasa wanamgambo wa al-Shabaab wanakabiliwa na vita pande nne – kutoka vikosi vya Kenya huko magharibi, Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia huko kusini, Serikali ya Mpito ya Shirikisho huko Mogadishu na vikosi vya Puntland katikati ya Somalia – wapiganaji wa al-Shabaab hawataweza kujificha, alisema.
Taarifa za kiintelijensia zinaonesha kuwa baadhi ya sehemu za al-Shabaab wanaweza kuwa wanaelekea Puntland kujipanga upya, aliongeza. “Wao [wapiganaji wa al-Shabaab], wakifuatana na wake zao, wanadhamiria kunyemelea kwa kujificha katika maeneo ambayo wameishasafishwa,” rais alisema. “Nimeweka vikosi vya usalama katika hali kubwa ya tahadhari na tutawakamata,” aliongeza.
Katika hotuba yake, Faroole alizitaja operesheni za kijeshi zilizofanikiwa ambazo serikali yake ilifanya dhidi ya al-Shabaab, ikiwa ni pamoja na operesheni zilizowekwa za hatua za kiusalama katika miji mikuu ya Puntland zilizopelekea mwaka 2010 kukamatwa kwa baadhi ya ngome za al-Shabaab na askari waasi wa mataifa mbalimbali.
Licha ya mafanikio, Faroole alikubali kuwa bado Puntland inakabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama zinazokuwa zikijengeka kwa miaka kumi iliyopita. Kwa dhamiri hiyo, aliwataka raia, hasa wa Bossaso, kufanyakazi kwa karibu na viongozi na kuripoti shughuli zozote za kutiliwa shaka.
Raisi alisema al-Shabaab in tishio linalolenga wanawake na watoto kwa kujitolea kuwaandikisha watoto bure katika shule za kidini, lakini badala yake wanawapeleka “mahali kusiko na marejeo” mara tu wanapokuwa katika miliki ya al-Shabaab.
Waziri wa Usalama Khalif Isse Mudan, ambaye pia alizungumza katika sherehe ya kutimia miaka mitatu ya utawala wa Faroole, alisema serikali ya Puntland imewekeza rasilimali zake nyingi katika usalama wa jimbo.
“Serikali imewekeza sana katika usalama na imefanikiwa katika kuwatia jela wauaji wa Dk. Ahmed H. Abdirahman. Hivi sasa, kuna kampeni ya kuwasafisha al-Shabaab na wanazuoni wa Kiislamu ambao wanashughulika kikamilifu katika kutoa mahubiri ya mwamko kwa umma huko Bossaso yote, kuujulisha umma kuhusu maovu ya al-Shabaab”, Mudan alisema.
Wanazuoni wa kidini waliitisha mkutano wa siku tatu uliomaliza tarehe 7 Januari, kujadili hali ya usalama huko Puntland na kupanga jawabu zao katika Msikiti wa al-Rawda huko Bossaso. Washiriki wa mkutano kwa pamoja walikikamata kikundi cha mauaji ya watu wasio na hatia na kuonya umma kwa jumla dhidi ya “mafunzo ya al-Shabaab”.
Sheikh Ahmed Abdisamad, mwanazuoni wa Puntland aliyezungumza katika mkutano, alisema kikundi kidogo cha al-Shabaab kiitwacho “Amniyad”kilipata mafunzo mahsusi ili kutisha raia. Njia pekee ya kushinda tisho hilo ni "kuunda mstari wa mbele wa umoja, kimeundwa na kikundi chenye raia na watu wa serikali”, alisema.
Viongozi wa kikabila vilevile waliungana na viongozi wa kidini na wanaharakati wa kijamii katika kampeni za kutoa mwamko dhidi ya al-Shabaab.
Leelkase, mkuu wa kikundi kidogo cha Darood huko Mudug, kilikutana mwezi uliopita katika mji wa Galdogob kuzungumzia usalama katika kanda. Kikundi hicho cha kikabila kilitoa taarifa ya kuwalaani al-Shabaab kwa mauaji ya Abdirahman na umma kukusanya nguvu zao pamoja na serikali na wengine ili kuwashinda al-Shabaab.
Ahmed Harti, kabila katika kanda ya Bari, lilitoa kauli kama hiyo mwezi huu, kwa kupasa sauti ya kuunga mkono kwenye vita dhidi ya al-Shabaab na vikundi vyengine vya kigaidi. Taarifa ilisema kuunga mkono kwao kwa usalama wa Jimbo la Puntland na kwa kuunganisha nguvu ili kuwatoa vijana wanaopotoshwa na al-Shabaab.
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Ninawambia waandishi wa habari mnaochapisha katika tovuti hii, ikiwa mnataka kusema uongo, semeni uongo ulio kweli...hii ni kwa sababu baadhi ya mambo mnayochapisha yanatuvunja moyo tu.
Kwanza, lazima wanazuoni wa Kiislamu wakipinge kikundi hiki cha kigaidi kwa kuitumia dini ya Kiislamu ili kufanya mambo mabaya na wakati huo huo kudai kuwa ni kikundi cha Kislamu kinacho pigana vita vitakatifu kwa niaba yao na pia kuwaiga al-Qaeda na kudai ushindi. Wanazuoni wa Kiislamu kutoka ulimwengu wa Kiislamu lazima watoe hukumu (fatwa) ili kuwapiga marufuku al-Shabaab na kuwaapiza. Ni lazima kwa nchi za Kiarabu kushirikiana na kupeleka majeshi nchini Somalia kupambana na al-Shabaab, kusimamisha sheria na utulivu, kuikomboa nchi, kuwasaidia kijamii na kiuchumi waathirika wa ukame, kufanyakazi jinsi ya kurejesha amani Somalia ili iwe na utulivu tena.